Naibu Waziri wa TAMISEMI,Mh. Agrey Mwanry (mwenye suti) akiwa amesimamia kuwekwa chini ya ulinzi vijana watatu aliowakamata ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja kwa kosa la kula maembe kwenye gari na kutupa maganda barabarani.kushoto ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, Zuberi Mwombeji

Na Woinde Shizza - Globu ya Jamii,arusha

NAIBU Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Agrey Mwanri ameuagiza uongozi wa halmashauri ya jiji la Arusha ,kuhakikisha kwamba jiji hilo linakuwa safi muda wote ikiwa ni pamoja na kuwakamata na kuwafungulia mashtaka wale wote wanaojihusisha na utupaji ovyo wa taka ngumu.

Mwanri alienda mbali zaidi kwa kuwataka viongozi hao kuandika barua za kujiudhulu mara moja iwapo shughuli ya kutunza mazingira katika mji wa Arusha zimewashinda.

Aliyasema hayo mjini hapa baada ya kuwakamata na kuwaweka chini ya ulinzi vijana watatu aliowashuhudia wakila maembe ndani ya gari aina ya Fusso na kutupa maganda ovyo katika barabara ya uhuru mjini hapa.

Alisema kwamba inatia aibu kwa jiji la Arusha ambalo linavitega uchumi vingi na linaingiza wageni wa kila aina wakiwemo mashuhuri kuona linatoa harufu mbaya za taka taka ngumu huku zikizagaa ovyo barabarani bila kuchukua hatua yoyote.

"Hivi nyinyi viongozi mnafanya nini kama hamuwezi kazi ya kuung’arisha mji?? andikeni barua mjivue gamba, wenzetu wa Moshi kwa nini wamewashinda?? nendeni kwa mkurugenzi wa Moshi,Mama Kinabo mkajifunze usafi" alisema Mh. Mwanry na kuongeza

"Haitapendeza kuona mgeni akitembea huku akiwa ameziba mdomo na kitambaa kutokana na harufu mbaya ya uchafu ,hii hatuwezi kuivumilia hata kidogo ,mwambieni na Mkurugenzi wetu kuwa nitatuma wasaidizi wangu waje wafuatilie hatua mlizozichukua’’alisema Mwanri alipokuwa akiwaeleza baadhi ya viongozi wa Manispaa hiyo waliofika eneo la tukio.

Aidha aliwataka viongozi hao wa Manispaa kutumia askari wao kukamata mtu yoyote atakayeonekana kutupa taka ovyo na kuwatoza faini za papo kwa papo,hali ambayo alisema itakomesha uchafu ndani ya jiji hilo .

Mwanry aliamuru vijana hao akiwemo dereva na gari hilo, kuwekwa ndani katika kituo cha polisi na kufunguliwa mashtaka .

Hata hivyo alimwagiza mkuu wa polisi wa wilaya (OCD) Zuberi Mwombeji kuhakikisha kuwa vijana hao hawaachiwi bila kulipa faini kwa mujibu wa sheria za manispaa hiyo na kuonya kwamba iwapo wataachiwa kiujanja ujanja ,taarifa zifikishwe kwake ili achukue hatua zaidi za kinidhamu dhidi ya wahusika.

Hata hivyo baadhi ya wananchi walimweleza wazi, Naibu Waziri huyo kwamba ,uchafu uliokithiri katika jiji la Arusha unatokana na uzembe wa viongozi wa manispaa hiyo kwa kushindwa kusimamia kikamilifu uzoaji wa taka ngumu zinazolundikana maeneo mbali mbali kwa muda mrefu na kujikuta zikioza na kutoa harufu kali.

"Mheshimiwa Waziri uchafu huu unasababishwa na viongozi wa manispaa ,kwanza gari lao la taka huwa linamwaga uchafu ovyo barabarani,halafu wao wenyewe ni wachafu hawazoi uchafu uliopo kwenye masoko ukiingia sokoni unaweza kutapika’’alisema mwananchi mmoja kwa niaba ya wenzake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Nina walakini na huu uamuzi wa kibabe.Hivi kweli mh waziri,nguvu na muda uliotumia kuwakamata kuita waandishi eti vijana watatu wametupa maganda ya maembe hivi kweli ni sawa?

    Mbaya zaidi mh wewe umekuwa polisi ukawakamata,pili ukawa hakimu ukatoa hukumu walipe faini,yaani yote hayo yamefanyika bila kufuata taratibu.Watu wanaiba mabilioni na nchi inajua haiwafanyi kitu.

    Halmashauri ndio chakachukua tender za usafi hawachukuliwi hatua..Kwanini hawa vijina wasingepewa nafasi ya kujitete kwa kitendo walichofanya?

    ReplyDelete
  2. watanzania kweli mnashangaza lipijema kwenu nyie niugomvi tu na serikali yenu tuuuuuu kila siku tunawashangaa sana sisi tunavyoishi kwa shida tunaipenda kweli hiyo tabu ambayo nyie mnaiona mbona hamna aibu?mungu awape nn nyie?hamieni kwetu somalia du watu waajabu kweli sijawahi ona duniani

    ReplyDelete
  3. Sasa wafunguliwe mashitaka kwa sheria ipi?au kiongozi yoyote wa sirikali ya ccm anaweza sema ufunguliwe mashitaka na polisi wakakamata watu bila hata ya kuwa na kifungu cha sheria?acheni kuwaonea wananchi wanaolipa kodi kuchangia mishahara yenu nyie viongozi..mbona kuna uchafu mwingi tu ndani ya hiyo ccm yenu na bado mnafumbia mambo?waelimisheni wananchi juu ya umuhimu wa usafi na viongozi wa miji wafanye kazi yao ya kuweka miji safi sio kukaa bar siku nzima(najua michuzi utanibania hii comment ila sawa tu)

    ReplyDelete
  4. Ndaki, hawa wamekamatwa, ushahidi, mashahidi, na vizibiti vipo kwahiyo wamehukumiwa faini maana wanachafua mazingira na hata wenyewe kwenye picha wanaona haya. Kwahivyo haina haja ya kwenda mahakamani kwa makosa kama haya ni faini papo hapo. Unaowashukia kuiba mabilioni ni kuwa hakuna ushahidi wa maneno yako, inabidi upatikane ushahidi, mashahidi na vizibiti ndio kesi ihukumiwe. Haki haipatikani kwa jazba bali kwa busara la sivyo Tanzania itageuka Tunisia, Rwanda, Libya, Misri na Yemen. Je utafurahia kuona wanafamilia wako wamefikwa na matatizo kwa kisingizio cha demokrasia?

    ReplyDelete
  5. Wewe Edwin Ndaki ni katika wale ambao hawajali usafi wa Mazingira na wanaona kutupa mataka ovyo barabarani ni sawa tu. Sheria ipo na faini yake ni Sh. 50,000 kwa hivyo Mh. Mwanri hakukosea.

    Tena tunatamani na viongozi wengine wangekuwa kama yeye kwani ni aibu kwa mtu kutupa taka ovyo barabarani. HONGERA SANA NA UKIWANONA WENGINE UWAKAMATISHE MPAKA WAKOME. NA HATA HAPA DAR ES SALAAM UKIWAONA WAKAMATISHE MPAKA WAELEWE.

    ReplyDelete
  6. Kaka Edwin tutibu jipu na baadae tutibu kansa. Tupige vita uchafu kwa wakati huu tulionao na suala la tenders litashugulikiwa kwa nguvu ama udhaifu wake. Nimependa utaratibu wao-atleast kuwa na clean city.

    Utaratibu wa fine nk nadhani wanayo sheria ndogo kufanya hivyo.
    Kaka tupende usafi nyumbani kaka na ni heri iwe kwa miji yote Tanzania. Ni bora kujenga utamaduni huo.

    Suala la kuita waandishi nk ni demo kaka. I dont see anything wrong with that. Tuombee miji yetu iwe kama mamtoni. Na watu wawe na culture ya usafi

    Do you know that Dar-es-salaama ni jiji la 12 kwa uchafu duniani?
    Angalia http://www.forbes.com/2008/02/24/pollution-baku-oil-biz-logistics-cx_tl_0226dirtycities_slide_15.html

    ReplyDelete
  7. Eti kama hawawezi kazi ya kuung'arisha mji waandike barua ya kujivua gamba!!! Ha ha ha... Ila waziri naye vp? Badala ya kuwachimba biti halmashauri kwa uzembe wao,eti yeye anaanza kukamata watupa maganda ya maembe!! Kama vp na yeye ajivue gamba tu...

    Mfumbuzi
    Mashariki ya mbali.

    ReplyDelete
  8. Hongera kwa kuchukua hatua kama hiyo. Nchi hii inahitaji viongozi wenye mamlaka na Dar ni aibu tupu! Natamani wawepo wengi kama huyu!

    ReplyDelete
  9. safi sana MH.MWANRY hakuna kitu kinaniudhi kama kumkuta mtu mzima anatupa taka hovyo na jiji la Arusha ni chafu sana na watalii ni wengi alivyofanya MH ni sawa kabisa iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia ya kutupa taka hovyo hiyo ni safi kabisa uchafu unaharibu sifa ya jiji hii iendelee isiwe nguvu ya soda nataka Arusha pawepasafi kama moshi big up MH

    ReplyDelete
  10. Eeeeeeeeeeh,eeeeeeh,Tanzania oyeeee? Wote wana makosa kama ifuatavyo; kuua mende kwa rungu na simba kwa fimbo is fun. Hata kama wamechafua mazingira haisababishi kuwapotezea muda na kuacha kudeal na waosha magari na kondakta wanaowaua watz kwa uendeshaji mbaya na leseni wanazo anapaswa akafuatilie leseni zinavyotoka rather than kudeal na watu wanaotuliza njaa zao kwa maisha ya mtz kupanda na kumwezesha kushindia embe more than African food. Nilitegemea awape wafiwa pole atembelee majeruhi eti ana deal na wala maembe, tatizo lingine wananchi hawajui sheria wanapaswa kuelimishwa na ni aibu kuanza kuwaelimisha kwenye maembe badala ya katiba ya nchi na sheria yake then tuendelee na usafi maana viongozi niwachafu kuanzia rohoni then na nchi au mazingira yakiwa machafu si ajabu. Mungu+Rushwa=uongo. Acheni kuabudu wakati Mungu hapendi mfanyayo au badilikeni tuone Imani yenu kwa matendo. Na nyie watu wa Arusha wenzangu iweni usafi but in the other way kama mnakatwa kodi chafueni ili badala ya kula hizo kodi zenu zifanyiwe kazi. Ningetamani kusikia umewatembelea majeruhi na kuwapa pole wafiwa na kuwanyang'anya leseni madereva feki

    ReplyDelete
  11. Good Job

    ReplyDelete
  12. Hata mie namsifu kwa hilo. Wadau muelewe kuwa wenzetu Moshi na Arusha wameweka sheria ya utupaji taka ovyo. Ukikamatwa unatupa taka hovyo unalipa faini ya shilingi 50,000. Ona miji yao ilivyokuwa safi. Dar na ninyi muige jiji liwe safi. Muache uswahili.

    ReplyDelete
  13. Maganda ya embe jamani ni BIO-DEGRADABLE MAANA YAKE NI KWAMBA YAKIOZA YANAKUWA SEHEMU YA UOTO. BORA ANGEKAMATA WANAOTUPA CHUPA ZA PLASTIKI NA MIFUKO.

    HAO WATU NI KUWAONEA TU KWANI NCHI NZIMA WATU WANATEMBEA HUKU WANAKULA MAHINDI NA KUTUPA MAGUNZI.

    TAFUTENI MAFISADI ACHENI KUPOTEZA NGUVU KAZI YA POLISI

    ReplyDelete
  14. Agrey utanafuta cheap popularity weye,kama mji mchafu mkurugenzi wa manispaa anafanya nini hapo??fukuza kazi weka kichwa mupya. Akili kidogo NGUVU nyingi,mtupa maganda mtaani anakamwatwa kwa SMG,wakati almashauri zote watu wanakwiba mnabaki kuwachekea na kuwahamisha vituo vya kazi tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...