Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Halima Dendego akiangalia Tella ya matrekta madogo yaliyonunuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kwa matumizi ya Halmashauri hiyo lakini yalibaikika kuwa hayana viwango vya ubora na kukidhi mahitaji ya matumizi.Halmashauri hiyo imesababisha hasara ya Mamilioni ya Fedha kwa kununua Trekta hizo ambazo hazina viwango vya ubora.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilosa , akiangalia matrekta madogo na zana zake kwenye jengo la Ujenzi Wilayani humo ambayo hayana ubora na viwango.
inakuwaje haya ma trecta yame lala ?wakati wana nchi wanayaitaji sana .
ReplyDeletetutafika kweli ?
mdau paris
Jamani muyarejeshe haraka huko yalikotoka. Hizo ni fedha zetu sote walipa kodi.
ReplyDeleteAu mumeshakatiwa 30%.
Walionunua wamechukuliwa hatua gani? Hizo nyumba zao walizojenga zichukuliwe ziuzwe hela irudishwe.
ReplyDeletena huko walikonunua kulikua hamna contract? Ni heri waingie gharama ya kuyarudisha huko yalikotoka.
Bongo tambarare...nani wa kumlaumu? Baba, mama, watoto nao wote wachakachuaji nai wakumwambia mwenzake stop...
Du, kweli kazi bado tunayo! Lilikuwa ni wazo la nani kununua hayo ma-toy? na akina nani wakapitisha na kuhakiki hayo malipo jamani???????????? Nasikia hasira sana kwa vitendo kama hivi!!!
ReplyDelete