Bsi Mauzo na Masoko wa Tanzania Standard Newspapers , Bi. Christina Gareja ( kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Bwana , Isack Zongela na Bi harusi , Roina Ndaga , mara baada ya kumeremeta kwao wikiendi hii kwenye Kanisa la Tanzania Assemblies Of God ( Goshen Christian Center) , Kilakala Mjini Morogoro ukumbi wa Social Education Centre

Bi harusi , Roina Ndaga akiongoza kuimba wimbo wa ‘ mke mwema’ uliotungwa na kwanya ya Goshen Sound , ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa kwaya hiyo ya Kanisa la Tanzania Assemblies Of God ( T.A.G) ( Goshen Christian Center) , Kilakala Mjini ni mara baada ya kufunga ndoa Mei 14, mwaka huu huku Bwana harusi , Isack Zongela, akifuatishia wimbo huo wakati wa sherehe ilifanyika katika ukumbi wa Social Education Centre wa Mjini Morogoro, Zongela ni Mfanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali , Tanzania Standard (Newspapers) Ltd , (TSN) akiwa ni Mwakilishi wa Mkoa wa Morogoro , na Bi harusi mbali na cheo hicho pia ni Mwalimu wa Shule ya awali ya Kanisa hilo.
Mfanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali , Tanzania Standard (Newspapers) Ltd , (TSN) Makao Makuu ( watatu kushoto) Jitihada Kitundu akiweka saini kwneye kadi maalumu ya watumishi wa TSN , kulia kwake ni Meneja Mauzo na Masoko wa TSN , Christina Gareja na wapili ( kushoto) Meneja wa Rasilimali watu wa TSN , wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa sherehe ya harusi hiyo
Meneja wa Rasilimali watu wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali , Tanzania Standard (Newspapers) Ltd (TSN) Dailynews , Sundaynews, HABARILEO na HABARILEO JUMAPILI akisoma maelezo mafupi kabla ya kukabidhi risiti ya fedha iliyotolewa zawadi kwa bwana harusi , Isack Zongela, mfanyakazi na mwakilishi wa TSN Mkoa wa Morogoro ( hayupo pichani) sambamba na zawadi nyingine za wafanyakazi wa Ofisi ya Mkoa baada ya kumeremeta na Bi Roina Ndaga. Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii, mji kasoro bahari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...