Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es salaam Rose Lamosai(kulia) akitoa utaratibu wa kuendesha uchaguzi wa viongozi wa TUGHE kwa wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo jana jijini Dar es salaam. Mwingine ni Afisa Tawala wa Wizara hiyo Mussa Varisanga (kushoto)
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Tawi la TUGHE wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na michezo Peter Singano (kulia) akikabidhi vitendea kazi jana jijini Dar es salaam kwa Mwenyekiti mpya wa Tawi la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa TUGHE Dkt Magreth Mtaki (katikati). Anayeshuhudia ni Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es salaam Rose Lamosai(kushoto)
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na michezo Peter Singano (katikati) akiwashukuru wafanyakazi wa Wizara hiyo jana jijini Dar es salaam kwa ushirikiano waliompa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita akiwa Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Wizara hiyo. Kulia ni Mwenyekiti mpya wa Tawi la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa TUGHE Dkt Magreth Mtaki na na Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es salaam Rose Lamosai(kushoto)
Mwenyekiti mpya wa Tawi la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa TUGHE Dkt Magreth Mtaki (kulia) akiwashukuru wafanyakazi wa Wizara hiyo kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti wao jana jijini dar es salam kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Wengine ni msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia nia Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es salaam Rose Lamosai(katikati) na Afisa Tawala wa Wizara hiyo Mussa Varisanga (kushoto).
Baadhi ya viongozi wapya wa TUGHE wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo waliochaguliwa jana jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari.
Baadhi ya wafanyakazi na wananchama wa TUGHE wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo wakiwa katika mkutano wa uchaguzi wa kuchagua viongozi wapya wa TUGHE Tawi hilo jana jijini Dar es salaam.
Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...