I ran into this piece from RAIA MWEMA, and demonstrated what has been gross incompetence of our media. Its absurd that this kind of journalism is allowed in our society and yet we expect that somehow Democracy will save us. 

Share it with other folks, and whoever knows Ulimwengu's address feel free to forward to him also.

Thuwein

Kikwete na Porojo za Kujivua Gamba

Na Mwandishi Maalumu(You can not publish article with this amount of allegations without revealing the author)


NI vigumu kuamini kwamba rais wa nchi anaweza kuhusika na mchezo mchafu kama huu wa kuwabagua wananchi wake kwa misingi ya dini zao, lakini matukio ya hivi karibuni yanathibitisha hilo.( How? Show us the causality)

Baada ya uchaguzi mwaka jana na hasa tukio la Arusha la Watanzania kupigwa na polisi kwenye maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na kisha harufu ya udini kuibuka, baadhi ya Waislamu wachache wenye mtazamo mkali walianza kuzunguka nchi nzima wakitoa mahubiri ya chuki. (Dates, Names,  what exactly did they say? At least have a source)Mkutano mmoja ulifanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na inadaiwa ulipata baraka za Kikwete (How can we believe u?). Baadhi ya mikutano hiyo ilijadili masuala tata, na baadhi ikaibuka hata na mapendekezo ya ajabu ukiachilia yale ya muda mrefu kama vile kudai Mahakama ya Kadhi na Tanzania kuingia kwenye Jumuiya ya Kiislamu Duniani (OIC).

Madai mengine yalihusu malalamiko kwamba Wakristo wamekuwa wakipendelewa tangu enzi za ukoloni na kwamba ingawa Waislamu ni wengi zaidi Tanzania, lakini hawana nafasi nyingi za madaraka. Madai mengine yaliyotolewa ni kwamba Wakristo wana shule na mahospitali lakini Waislamu hawana, na kwamba serikali hutoa fedha kuzisaidia hospitali za Wakristo na walimu wa kufundisha shule za Wakristo, lakini Waislamu wanaachwa hivi hivi tu.

Baadhi walifikia hata hatua ya kumlaani Mwalimu Nyerere na kusema kwamba hastahili kuitwa Baba wa Taifa; bali anastahili kuitwa Baba wa Kanisa Katoliki. Baadhi yao, akiwemo kigogo wetu, hawamwiti Mwalimu Nyerere kwa hadhi yake iliyozoeleka ya Baba wa Taifa, na badala yake humwita Mzee Nyerere.(We need dates of the events, and names of attendees. At least a background interview. You can’t just throw allegations with NO evidence. WaTanzania sio wajinga hivyo).

Kwa ufupi, kuna imani kubwa miongoni mwa Watanzania kwamba utawala wa Rais Kikwete unalea udini (Do u have a scientific poll to back this up? ), na asipokuwa makini nyufa hii yenye msingi wa kidini inaweza kupanuka na kuutia dosari umoja wa kitaifa tulionao ambao misingi yake si udini.

Geresha ya  kujivua gamba

Pamoja na kubadili safu ya uongozi mjini Dodoma, CCM pia ilitangaza kwamba wanachama wake watatu wanaotuhumiwa kwa ufisadi wajiondoe wenyewe; la sivyo wataondolewa kwa nguvu. Wanachama hao wanatajwa kuwa ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, na wabunge wawili, Andrew Chenge na Rostam Aziz. Ni kweli matajiri hawa hawapendwi na Watanzania wengi isipokuwa pengine wa majimboni mwao tu.
Lakini pia watu hawa watatu wana sifa nyingine: Kwamba ndio tishio pekee na la kweli dhidi ya mpango wa Kikwete wa kusaka mgombea urais wa mwaka 2015 ambaye ni Mwislamu (This is unprecedented. You are accusing the head of state of being mdini, but you are not telling us readers how u have arrived to this conclusion?)

Wanaotaka kumweka Lowassa kwenye urais mwaka 2015, si tu wanakwamishwa na tuhuma hizi zinazomwandama na hatihati hii ya kung’olewa CCM, lakini pia wanakwazwa na Kikwete mwenyewe. Inadaiwa kwamba, kwenye mbio za urais za 2015, tatizo la Kikwete kuhusu Lowassa si kwamba anakabiliwa na tuhuma za ufisadi; bali kwamba si Mwislamu. (You are supposed to quote your sources on this sentence. How can we believe u?)

Kundi hili la kina Lowassa inaaminika lina urafiki wa karibu na Makamba ambaye inadaiwa kuwa agenda yake kubwa kwa mwaka 2015 haikuwa udini; licha ya kuwa naye amesikika mara kadhaa akilumbana na maaskofu; bali yeye (Makamba) ana ndoto ya  mwanae (January) aje kuachiwa urais mwaka 2025 na kundi hili(Now you can read people’s dreams too? How can a respectable news as Raia Mwema publish this nonsense?). Makamba hutamba kwamba mwanae anafaa kuwa kiongozi, na hakuna ubishi kwamba alihakikisha mwanae anapata ubunge, uenyekiti wa kamati ya Bunge, na kisha kuingia kwenye Sekretarieti ya CCM.

Aidha, mtoto huyo wa Makamba pia anaelezwa kuwemo kwenye kundi linalowaunga mkono watuhumiwa hawa wa ufisadi ambalo lina idadi kubwa ya wabunge na viongozi wa CCM wa ngazi za wilaya, mikoa na taifa. Hii ndiyo sababu tangu CCM ilipoanza kushambulia mafisadi hadharani, yeye amepotea jukwaani!( Have u reach to him and ask for him to comment? That is how professional journalists operates. You just made up your own reasons as if January do not exist.)

Kimsingi, kuna kutofautiana kati ya Makamba na Kikwete kuhusiana na nani awe rais mwaka 2015 na kuhusu nini wafanyiwe hawa watuhumiwa wa ufisadi. Hivyo; tangazo la kujivua gamba pamoja na kutajwa kwa watuhumiwa hao ambao Kikwete mwenyewe aliwapigia kampeni mwaka jana kwenye uchaguzi wa wabunge, ni geresha tu. Ukweli ni kwamba Kikwete alikuwa anaunda timu itakayomrithi mwaka 2015.

Kimsingi, hadi sasa Kikwete ameshawaacha ‘wabaya’ wake wote nje ya Kamati Kuu ambao ‘dhambi’ yao kuu ni kuutaka urais wa mwaka 2015. Watu hao ni pamoja na Membe na Andrew Chenge ambaye anamtaka Lowassa.

 Kwa ufupi, janja hii ya Mwenyekiti Kikwete ya “kujivua gamba” ililenga katika kuwaengua wale wote wanaoweza kumsumbua kwenye suala la urais wa mwaka 2015; ingawa pia ni kweli kwamba ukiuangalia juujuu utaona kuwa mpango huo wa “CCM kujivua gamba” unalenga katika kupunguza nguvu za  CHADEMA kwa kuirejeshea CCM mvuto wake wa zamani.
Vyovyote vile; hakuna ushujaa wala maamuzi magumu yaliyofanyika Dodoma. Ulikuwa ni ‘usanii’ tu, na ndiyo sababu hakuna kiongozi wa CCM anayepigia kelele kung’olewa chamani mafisadi zaidi ya kijana Nape na Katibu Mkuu mpya, Wilson Mukama ambao, hata hivyo, nao wamefungwa “gavana” hivi karibuni kuhusu kulipigia debe suala hilo. Hata Chiligati aliyejitokeza mwanzoni kuhubiri nia ya kuwavua uongozi wa CCM kina Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge, sasa naye ameingia mitini!( Sources?)

Kauli ya Joseph Butiku
Labda nigusie pia kidogo kuhusu malalamiko ya Joseph Butiku aliyoyatoa katika mahojiano na gazeti la Raia Mwema, hivi karibuni, kwamba viongozi wa CCM wamemwachia Mwenyekiti Kikwete mzigo wa kupambana na mafisadi.
Mimi nadhani madai hayo ya Butiku ameyatoa bila kujua ukweli wa mambo. CCM haiko kwenye mapambano na mafisadi; bali Mwenyekiti Kikwete ndiye anapambana na maadui zake kwenye kinyang’anyiro cha kutafuta mrithi wake kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015; ila tu amepata bahati kwamba watu hao hao ndio wanaolalamikiwa kwa ufisadi. Ni bahati tu ya mtende iliyotoa fursa ya ‘usanii’ huu  kuchezwa! (Last election was a referendum on corruption more than anything. But you seem to disagree. You argument is “luck”. You know we can reach conclusion to every issue by attributing it on luck)

Aidha, kelele za CCM kupitia kwa Nape kwamba kuna vyombo vya habari, viongozi wa Upinzani na viongozi wa dini ambao wamepangwa kuwatetea mafisadi na kuishambulia familia ya Kikwete, ni janja ya kuwatangulia mbele ili wakisema jambo, wananchi waambiwe: “Si tulisema, mnaona sasa!?” 
Hata hivyo, inafahamika kuwa makundi haya matatu ndiyo yako mstari wa mbele kupinga ufisadi na udini unaosambazwa na Kikwete na watu wake, hivyo lolote litakalosemwa halitakuwa geni; bali ni muendelezo unaofahamika. Pengine CCM haijui kuwa wananchi wanajua kinachoendelea. (WaTanzania are not stupid, ofcourse they know what is going on. You writing this piece betting on fact that WaTanzania hatujui kinachoendelea. You are betting on our ignorance)

Wagombea wa Kikwete 2015

Kwa kufuatilia mambo ya kisiasa yanavyokwenda na jinsi Rais Kikwete anavyoendesha mambo yake, kuna majina mawili ya watu wanaotajwa ambao angependa wachukue urais na umakamu wa rais wa Muungano mwaka 2015. Hii inatokana pia na imani yake kwamba Katiba mpya haitabadili mfumo wa sasa. (Now you can also predict people’s beliefs. Sources mzee, at least one source to come on the record. How can we believe u)
Sababu kubwa ni mbili: Kwanza, kutekeleza ahadi yake ya siri kwamba hawezi kuacha nchi kwa Mkristo (This is very dangerous. You are being irresponsible with your words throwing allegations like this one. SOURCES??) na pili, kuhakikisha uongozi mpya unamlinda yeye na familia yake dhidi ya misukosuko ya hapa na pale ambayo kawaida kote duniani hutokea mtu akishaacha urais. Hakika, naye hatapenda kushambuliwa kama inavyotokea kwa Mkapa.

Baada ya kufanikiwa kuwaengua pembeni Lowassa na Membe (Prof. Mwandosya kanusurika?) ni nani, basi, ambaye Kikwete anamtaka kwa urais wa 2015 na atachezaje karata zake kuhakikisha jina la mtu huyo linapeta?
Ili watu hao wawili anaowataka wakubalike, inaaminika kuwa Kikwete atatumia mtindo ule ule wa funika kombe mwanaharamu apite. Atawapendekeza kwa kutumia vigezo vinavyoficha ukweli (Now umekuwa Mnajimu. You can predict the future). Kutokana na hali ya kisiasa itakavyokuwa, anaweza kusema: “Jamani ni zamu ya wanawake sasa, tusitawale akina baba tu, nchi yetu wote.”

Iwapo wazo hili litakwama, basi, Kikwete anaweza kusema hivi: “Jamani sasa wenzetu wa Zanzibar nao, miaka 20 imepita, tuwape nao nafasi jamani.” Msemo huu, hata hivyo, hauna mashiko iwapo Katiba haitakuwa na agizo hilo; kwani upande wa Upinzani unaweza kuweka wagombea wote wa Bara.
Mbinu hiyo Kikwete ameshawahi kuitumia kwenye kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana ambapo alimpendekeza kijana wa Visiwani, na pia aliitumia kwenye kupata jina la mgombea wa uspika. Anaamini kuwa mbinu hiyo itasaidia kufunika hoja yake ya udini isionekane, na hivyo kufanikisha kupata rais Mwislamu.

Asha-Rose Migiro na Dk. Mwinyi

Katika miaka ya karibuni Kikwete amekuwa na mahusiano ya karibu ya kikazi na mwanamama mmoja ambaye kila baada ya miezi michache hufika Ikulu, na kisha picha nyingi hupigwa kuonesha kwamba wawili hao wanaelewana na wanashirikiana kisiasa pia.

Huyu ni mwanamama ambaye ni mmoja wa wanasiasa wachanga waliofaidika na vyeo vya uwaziri wa Kikwete mwaka 2005. Aidha, pale Tanzania ilipopewa mwanya wa kutoa jina la mwanamke wa kushika nafasi ya juu kimataifa, Kikwete hakusita kumtaja mwanamama huyu.

Nafasi hii ilikuwa baada ya Tanzania kufanya kampeni kubwa barani Afrika kuunga mkono jina la Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini, Ban ki-Moon, kwenye kugombea nafasi ya ukatibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Mwanamama huyo pia ana kisomo kizuri kinachokubalika na kinachoweza kuwaaminisha watu wanaotaka kuuliza maswali kuhusu uwezo wake kiutendaji wa kuiongoza nchi yenye matatizo ya uchumi na yenye mipasuko kibao kama Tanzania. Mwanamama huyo ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro ambaye anaelezwa kuanza kujiandaa kurejea nyumbani Tanzania siku si nyingi.

Kwa upande wa Zanzibar, ni waziri mmoja kijana ambaye urafiki wake na Kikwete huwashangaza viongozi wengine wa Zanzibar; mathalani jinsi wanavyosalimiana kama watoto wa mjini. Katika mtandao wa YouTube Watanzania waliweka picha ya video ya Kikwete akisalimiana ‘kishkaji’ na waziri huyu kwenye Uwanja wa Amani, Zanzibar siku ya Januari 12, mwaka huu. Picha hiyo iliibua gumzo kubwa (What is your point?? What do u want us readers to take away from this useless paragraph? President and his minister wanasilimiana kishkaji, so what?)

Hivi karibuni Waziri huyu alipokabiliwa na msukosuko wa kutakiwa na wananchi kwamba ajiuzulu ambao kimsingi ulisababishwa na utendaji dhaifu wa Jeshi la Wananchi uliochukua maisha ya watu kwenye milipuko ya maghala ya silaha, alikataa na Kikwete hakusema kitu. Huyu ni Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussein Mwinyi.

Hitimisho langu
Inaaminika kuwa hao wawili ndio chaguo la Kikwete katika mbio za urais za 2015, na chaguo lake hilo linachagizwa zaidi na dini zao (How did you arrive to this conclusion? Throughout this piece, you have not convince us readers to buy on your accusation that our President is a religious fanatic) badala ya vigezo vya jumla vya sifa ambazo Watanzania wote tunataka mtu anayetaka kuwania urais kuwa nazo.

Hata hivyo, napenda nieleweke kwamba sina tatizo na rais ajaye kuwa Mwislamu au Mkristo; ilimradi tu awe ni kiongozi hodari, mchapakazi, mwadilifu na mwona mbali. Angalizo langu ni kwamba rais huyo ajaye asitafutwe kwa msingi wa dini yake; bali kwa vigezo hivyo vya ubora.

Nasisitiza hivyo; maana Watanzania katika ujumla wao  hawajali dini ya mtu ila uadilifu na uchapakazi tu, lakini viongozi wetu ndio wenye matatizo ya udini. Na kwa hakika, Kikwete analo tatizo hilo.

Nihitimishe kwa kusisitiza kwamba wajibu wa wana-CCM ni kukisafisha chama chao kwa uaminifu na werevu, na kisha kuachia demokrasia iamue nani awe mgombea wa CCM mwaka 2015. CCM na Kikwete wawe waangalifu na dhana hii ya “sasa ni zamu yetu kutawala” ili Tanzania isitumbukie kwenye matatizo yanayosikika kwenye nchi zingine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2011

    Hayo ni magazeti ya CHADEMA ambayo yanatumika kuichafua CCM na kuifagilia CHADEMA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2011

    Ilo toleo la Raia mwema lina nakala nyingi tu, kulikoni kuichagua hii tu?. Wanazuoni walisema "ukitupa jiwe gizani na ukisikia kilio ujue limempata muhusika". Inawezekana nakala hii ujumbe wake umekugusa sana wewe muhusika. Pili kwa uwelewa wangu nakala za news papers haziitaji source/references nyingi kama mtoa hoja anavyotaka. Ukumbuke hii ni nakala just for weekly news paper na sio academic paper ambayo inaandaliwa kutolewa kwenye academic arena.Hoja yako haina mshiko. Tatu yalioandika humo sio mageni kwa watanzania,wengi tunaelewa mambo yanavyokwenda hapo Ikulu, na na jinsi JK anavyo-promoti udini- Raia mwema wamesaidia tu kuweka record na kuwapa taharifa watanzania wengi zaidi.Pole sana Dr kwa kuguswa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2011

    sasa hivi tunataka wakristo wampigie kura mkristo na waislam halikadhalika tuone nani atashinda ugonvi uishe

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli hadhi ya gazeti imeshuka kutokana na kuwa na wahandishi ama elimu yao kwa ujumla ndogo au kuna kundi la watu linawapa upofu. kwa kweli tuhuma alizotoa huyu mhandishi ni nzito na ilipaswa wizara husika ichukue hatua kwani kauli kama hizi hazijengi bali zinabomoa. Tukumbuke mauaji ya wenyewe kwa wenyewe kule Rwanda yalichagizwa zaidi na aina hii ya uandishi. Mimi kama Mtanzania nimeguswa sana na habari hii na kuona tunapoelekea sasa na huu tunaouwita uhuru wa habari sipo. Narudia tena waziri husika anatakiwa achukue hatua ya kukemea suala hili na si kusubiri mpaka mambo yanaharibika.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2011

    Wewe naona ni mwanafunzi wewe. Endelea na masomo yako usipoteze muda wako ku "track change"! makala za magazeti. CCM ina matatizo, Serikali ina matatizo na ndio maana Tanzania inaendelea kupeta kwa umasikini. Upendeleo wa kidini na kifamilia kwenye uongozi wa chama, serikani, mashirika na sekta nyingine upo sana na ndio maana majina ni yale yale tunaendelea kuyasikia siku hadi siku. Watu wanarithishana. Lets stop hitting around the bush with words. We need changes in this country!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2011

    Nashangaa uandishi kama huu unachukuliwa kama uandishi! Unapomtuhumu Rais wa nchi kwa kuwagawa wananchi kwa misingi ya udini bila ushahidi ni kufanya hicho hicho unachomtuhumu Rais. Mimi ni mkristo. Sioni Rais kuwa mkristo inanisaidia nini mimi. Aidha sioni uislam wa Kikwete umewakandamiza vipi wakristo. Hebu msituharibie nchi kwa ujinga wa kuchimbua hisia zakugawanya watu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2011

    Tunajua Ulimwengu haijali CCM. Lakini hata nchi yetu haijali pia? What a pity? How irresponsible?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2011

    ujinga tu hapa...mna interests zenu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 05, 2011

    Wewe uliyeleta na ku comment hii article ndo mbaya zaidi. Kwanza umeileta hapa ili isomwe na watu wengi ambao pengine wasingeusoma ujumbe wa huyu mwandishi. Pili inavyoonesha wewe ndo mdini zaidi, hivyo wote wawili hovyo. Ungewasiliana na gazeti husika na si kuonesha kwamaba unaweza kiingereza. Huoni hata aibu, mwenzeko kaandika kwa kiswahili wewe unaandika kwa kiingereza za kukatika katika. Hata hivyo katoa maoni na mtazamo wake na itabaki hivyo. Mwisho walisema wahenga kuwa ''lisemwalo lipo kama halipo laja''.Mkuu michuzi jihazali na watu wa namna hii wanaharibu umaarufu wa blog yako na mchango wako kwa jamii.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 05, 2011

    Idiot...wewe mwenyewe hujasema ni nani una akili kweli?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 05, 2011

    Mwandishi wa makala hii amemkosea Raisi wa nchi kwa kumlisha maneno.Aina hii ya waandishi wasiozingatia miiko ya uandishi ni hatari.Nakubaliana na mkosoaji(kwa maandishi mekundu).

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 05, 2011

    Bwana Thuwein wasikupe tabu hao RAI MWEMA, walishawahi kukiri kwenye moja ya makala zao kuwa wanatumiwa kama propaganda machine, rejea makala hii hapa chini JK NAYE NI KAMA MWINYI TU,
    Raia Mwema Octoba 31, 2007

    Masikini Mzee Ali Hassan Mwinyi!

    Ncheme, nchicheme? Oktoba 31, 2007

    TUNGEKUWA tumejaaliwa uungwana na Mwenyezi Mungu, nasi tukawa ni watu wa kukiri makosa yetu na kisha tukawa na moyo wa kutaka radhi wale tuliowakosea, basi Watanzania wengi tungekuwa tumekwisha kuunga ujumbe wa watu wasiopungua 500 kwenda kuanguka chini ya miguu ya Mzee Ali Hassan Mwinyi huku tukimwomba atusamehe kwa makosa makubwa tuliyomtendea.
    Ujumbe huo ungepaswa uongozwe na wahariri na wasanifu wakuu wa tahariri katika magazeti ya miaka ya mwanzo ya 1990, kwa sababu sisi ndio hasa tulikuwa msitari wa mbele katika kutenda makosa hayo dhidi ya mzee huyo ambaye tulimbatiza jina la “Mzee Ruksa”.
    Kosa kubwa tulilotenda dhidi ya Rais huyo wa Awamu ya Pili ilikuwa ni kumhusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi, hata kuwafanya wasomaji wa magazeti yaliyochapishwa wakati huo, waamini kwamba kilichokuwa kikifanyika Ikulu ulikuwa ni uharamia wa hali ya juu.
    Sasa tunajua kwamba yote haya hayakuwa kweli. Haiwezekani kusema kwamba Mzee Mwinyi hakuwa na dosari, kwani kusema hivyo ni kumwondoa kwenye kundi la binadamu.
    Alikuwa na dosari zake na udhaifu wake, na hayo bado anayo hadi leo, kwa ilivyokuwa wakati akiwa Ikulu. Lakini pia ni kweli kwamba sehemu ya udhaifu wake ilitokana na wema na upole wake katika mazingira ya “manyang’au” aliowaamini na ambao hawakusita kuutumia upole wake na jina lake kufanya walivyotaka kwa kumsingizia yeye.
    Leo hii sote tunajua kwamba tulimwonea sana Mzee Mwinyi kwa kumbebesha mambo yasiyokuwa yake. Na wala si yeye peke yake aliyekumbwa na uonevu huo bali pia mkewe, Bi Sitti Mwinyi, ambaye naye alihusishwa na kila aina ya maovu kutokana na uvumi ulioenezwa na baadhi ya vyombo vya habari.
    Baadhi tutakumbuka pia kwamba Mzee Mwinyi aliwahi kulalamika hadharani kwamba uvumi ulikuwa umeenezwa kuhusu yeye kumwoa kigori mdogo kwa kumfanya aache shule… kila aina ya uvumu na uzushi. Mzee huyu muungwana alivumilia, akavuta subira, akasamehe. Haishangazi kwamba amebaki kuwa kipenzi cha Watanzania kutokana na upole, unyenyekevu na uadilifu wake.
    Tunajua sasa kwamba, ingawaje vitendo vya ufisadi vilitendeka chini ya uongozi wake, yeye mwenyewe binafsi hakuhusika moja kwa moja.
    Baada ya Mzee Mwinyi kuondoka madarakani ndipo nchi hii imepata bahati mbaya si tu ya kuendelea kuelemewa na vitendo vya ufisadi katika safu za uongozi, bali pia mkosi wa kuwa na ‘kiongozi’ mkuu anayesimamia ufisadi huo kwa kushiriki yeye mwenyewe binafsi kuunda kampuni ya biashara na kuisajili rasmi kwa anwani ya ofisi ya umma, na hata kujihaulishia umiliki wa kampuni ya serikali na kuiandikisha kwa jina lake na familia yake na maswahiba zake.
    Tumshukuru Mungu tunayo Katiba inayoweka mipaka ya mihula ya uongozi, la sivyo baada ya mihula mitano tungeikuta nchi imehamia bara jingine kwa jinsi tamaa za wakuu zilivyozidi na jinsi matumbo yao yalivyo na nafasi za kujaza.
    Kisha tumshukuru Mzee Mwinyi kwa uungwana wake, na mwisho tumwombe radhi kwa jinsi tulivyomdhalilisha.

    Copyright 2007, Raia Mwema Publications All rights reserved.

    NA HAO NI RAIA MWEMA KATU HAWAKUFUNGUA MIDOMO ENZI YA MKAPA BALI KUMPAMBA KWA MAPAMBIO LAKINI ENZI YA MWINYI WALIMCHAFUA TANI YAO KISHA WAKAJA KUMUOMBA RADHI, NA JK NAYE KAMA MWINYI TU, SASA SIJUI HUYU WATTASINGIZIA WAMETUMWA NA NANI?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 05, 2011

    Why and how can a blind man blame someone who has got sight? You are generalizing that "watanzania sio wajinga" how did you reached to this conclusion? What are the basis of your conclusion. How did you manage to post this unworthy analysis in MICHUZI? Issa why are you allowing these types of analysis?

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 05, 2011

    kumekuwa na kundi kubwa la hawa wanaojiita waandishi wa habari (wengi hawana sifa za uandishi wa habari) hapa tanzania kutia choko choko za udini kutoka pande mbili za kiislamu na kikristo. Mbali ya mfano ulioletwa hapa leo ni yule mwandishi wa mwanzo ku-suggest kuwa ule uchomwaji wa vibanda huko zanzibar ni kwa sababu za uzanzibari na ubara pamoja na udini ilhali wenye vibanda waliochomewa vibanda wanaotoka bara ilikuja kujulikana baadae kuwa ni wachache na wengi ni watu wa asili ya zanzibar.

    Magazeti mengi naona hapa tanzania wana lengo moja tu wanataka yale yaliotokea burundi, rwanda na kwengineko na tanzania yatokee. Hawatawacha tabia hii hadi pale patakapo waka moto nchini. Wenye kumbukumbu watakumbuka ni waandishi wa habari ndio waliosababisha kuvunjika kwa jumuia ya mashariki ya awali.

    Enyi mnaojiita waandishi wa habari ilhali hata hamjui kanuni za uandishi wa habari endeleeni tu na fitina zenu za kutaka watanzania wachukiane na kuuana lakini mkumbuke yakiaanza hayo ni damu nzito itawajaa mikononi mwenu daima.

    Mpenda salama

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 05, 2011

    Mwandishi yeye ndo mdini, ameonaje au amejuwaje huo udini, anaweza kuuthibitisha mahakamani?

    Ndo maana kila siku nashauri kuwa ianzishwe sheria kikatiba itakayodhibiti ubaguzi ili sheria itawale na sio mawazo na mapenzi ya watu. Nahisi hii hseria haitaanzishwa maana kutokuwepo kwake kunawanufaisha kadhaa. Na wakidhuriwa na udini watatumia midomo na magazeti. Haisaidii. Sheria, sheria, sheria!!!!!!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 05, 2011

    asante kwa kunihabarisha. mi niko mbali na sijasoma raia mwema. ila am into the writer's arguments not your mr analyst! wewe lazima utakuwa umetumwa either na waislamu au jk.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 05, 2011

    Jamani sisi wakristo tunatia bidii sana kwenye masomo. Mkumbuke sisi wakristo utamaduni wetu uko karibu sana na wamagharibi. Wenzetu utamaduni wao uko karibu na uarabuni. Nchi za magharibi wanapenda elimu. Nchi za uarabuni ni madrasat na biashara. Hicho ndicho kilichowaathiri waisilamu.

    Halafu ugaidi ndiyo umewaharibia kabisaaa. Majina yetu wakristo yanahusishwa na mambo mazuri ya amani. Nidyo maana sasa vijana wote wa kiislamu huku ulaya wamebadili majina na wanatumia majina yetu ya kikristo.

    Wakulaumiwa ni nyinyi wenyewe waislamu na mtazamo wenu kwenye elimu. Msitafute mchawi mwingine.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 05, 2011

    Huu ni mfano mzuri wa jinsi gani maadili ya uandishi yalivyoporomoka na kuishia kuwa ushabiki wa kisiasa. Nashukuru kwa huyu mdau kuchukua muda kukosoa jarida hili.Wananchi hatuambiwi ukweli, bali tunachonganishwa na hawa waandishi bila ya sababu za msingi. Athari za kuchemsha damu za wananchi bila ya kuwa na ushahidi wa kinachoandikwa sio tu kwamba ni character assassination kwa wale wanaoandikwa, bali inajenga chuki ambayo itafika mahali haiwezi kuzuilika na kuleta maafa katika jamii. Watanzania inabidi tukemee kwa nguvu zote makala zote kama hizi ambazo hazitoi ushahidi wowote wa kile kinachotajwa.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 05, 2011

    ANON WA SUN 05, 07;22:00 KAMA USEMAYO YANA UKWELI BASI NUSU YA WATANZANIA WANGEKUWA WAMEELIKA KAMA MNAVYOSEMA NUSU NI WAKRISTO. LAKINI NIKIANGALIA WATZS HUKO VIJIJINI WENGI HAWANA ELIMU SASA HUO MKAZO WA WAKRISTO KWENYE ELIMU UNAMNUFAISHA MKRISTO YUPI? AU UNATAKA KUTWAMBIA KUWA WAKRISTO NI WACHACHE SANA MANAKE MAJORITY HAWAJASOMA NA WASOMI NI MINORITY.

    Sometimes msiwe mnakurupuka na baseless arguments elimu iko kila sehemu sio magharibi tu hana uchina na sehemu nyingine za Asia kuna elimu, hata kwetu Afrika ipo elimu. Na kama wasomi wenyewe wa kikristo ni wa aina yako basi hiyo elimu yenu ina mushkeli haijaweza kukuelimisha unaingia class room kukariri kisha unapewa cheti basi umemaliza na kwa aina yenu ya wasomi ndio maana nchi imeshindwa kuendelea kwenye nyanja zote.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 05, 2011

    KAMA NI KUJIBU BASI TUJIBU HOJA ZOTE AMBAZO TUNA MASHAKA NAZO KUWA HAZINA UKWELI AU ZA KUCHAFUANA.
    KUANZIA SASA KILA MTANZANIA MWENYE NIA AANZE KUJIBU NA KULETA HAPA BLOG YA JAMII, TUTAFIKA???

    WATANZANIA TUMECHOKA SASA NA UBISHI WENU HUSIO NA MAANA, UNATAKA USHAHIDI GANI TENA WEWE ULIYE LETA HII HUITAYO HOJA YA HAJA??

    NAOMBA MUWE WAKWELI NA TUACHE UNAFIKI, MATATIZO GANI AMBAYO YAMEANDIKWA AMBAYO HAYAPO NA HAYANA UKWELI??

    IMEFIKA WAKATI TUKAWEKA UTAIFA MBELE NA SIO MATUMBO MBELE, TUFIKIRI KWA KUTUMIA VICHWA NA TUTEMBEE KWA KUTUMIA MIGUU, TUSIBADIRISHE UTARATIBU HUU.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 05, 2011

    wewe Anonymous wa jun 05.07;22;00pm2011 umemaliza kila kitu uliyosema inaukweli kwa asilimia mia moja sina zaidi

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 06, 2011

    vyuo vikuu uarabuni ni vizuri zaidi ya hivi vyenu watanzania, halafu angalia wahadhiri kama kina ninyi mmo.

    Hizi kauli za kufanya madrasa kila siku kisingizio cha kunyimwa kazi na elimu ya juu zitaisha lini. hakuna hata data inayosapoti misemo hiyo.

    Mbona shule za msingi tuna uwiano sawa? kama tungekuwa hatutaki shule hata hiyo ya msingi tungesienda!!!!!

    hao jamaa wanaofata majina ya kikristo ni kwa sababu ya kukwepa ubaguzi. halafu we jamaa hujasoma.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 06, 2011

    Michuzi,

    Pamoja na kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakiiba kazi zako na kuweka kwenye blog zao Uchwara. Mimi nimekwazika kwani nilitaka ni-print comments halafu nikiwa kwenye foleni kwani napenda kusoma article yote kabla ya kutoa comment zangu. Hivyo naomba uniwekee print ili niweze soma article hiyo kabla ya kuandika maoni. Vile vile naomba uwaambie wandishi wenzio kuwa kuna mtu mmoja sikumbuki ni nani alisema. "Daktari akikosea anaua mtu mmoja, Dr. wa mifugo akikosea anaua mfugo husika. Lakini Mwandishi akikosea anaweza kuua taifa". HIVYO JAMANI MUWE MAKINI mtatupeleka kwenye VITU %$£^&*&((£"!"^*(() zenu

    Observer

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 06, 2011

    MIE NADHANI HUO NI MPANGO MAALUMU WA CHADEMA PAMOJA NA WAPAMBE WAO, KAMA MWANDISHI ANALAUMU KUHUSU UDINI WA JK MBONA HAJIULIZI MTU ALIYESOMEA UPADRI TU ANAPIGIWA DEBE KUWA RAISI WA NCHI KAMA INGEKUWA MTU KASOMEA USHEKHE TU NA AKATAKA KUGOMBEA URAISI MAGAZETI YOTE YANGEMBEZA NA KUMADHALILISHA, LAKINI NASHANGAA HOJA ZA BAADHI YA WAISLAMU KUHUSU UPENDELEO KWA WAKRISTO MBONA ZINATOLEWA KWA USHAHIDI WA VITABU TENA VIMEANDIKWA NA VIONGOZI WA KANISA HATA YEYE NYERERE ALISHAKIRI KINACHOFANYIKA NI PROPAGANDA KAMA ZA VYOMBO VYA HABARI VYA ULAYA VINAVYOANDIKA KUPENDELEA MAMBO YAO NA HATA TZ VYOMBO VYA HABARI VIMESHATEKWA NA HAO WALIOPENDELEWA KWA MUDA MREFU MIE NAONA KATIB AIJAYO IWEKE WAZI MIPAKA YA KUGAWANA MADARAKA NA UONGOZI LA SIVYO NCHI ITACHAFUKA WATU HAWEZI KUNYAMAZISHWA KWA PROPAGANDA

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 06, 2011

    Nadhani ni vyema kujadili hoja ya msingi badala ya kuleta mambo kama ya udini. Mchambuzi katutahadharisha kwamba waandishi wanapaswa kuwa makini katika uandishi wao wa makala kwa kuhakikisha kuwa na taarifa sahihi zenye ushahidi kuliko kuweka dhana zaidi ambazo zinaweza kusababisha mchafuko katika nchi yetu.
    Hao wanaosema kwamba wakristo wamesoma ni vema kuangalia upya kisomo chao kwani kwa muda mrefu nchi inaendan kombo ikiwa na wasomi hao ambao wanashindwa kutoa miongozo sahihi.
    Madrasaah nayo ni shule, mtu aliyepita masomo hayo na akafunzwa elimu hiyo vizuri naye ameelimika na ana mchango wake katika jamii kwani anachangia kuweka maadili ya wananchi na kuweza kufanya wananchi wakawa watu wema.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 06, 2011

    Mimi naona kuwa huyo aliyejiita mpembuzi ameleta hasira zake tu hapa hakuna la maana alilonipatia. Kwanza kanikera kwa kiingereza chake hicho katikati ya kiswahili, na hapo naelewa alichosema, je wale ambao hawakuweza kujua kasema nini si ndio kawajeruhi hisia kabisa? Kama hauamini kuwa ni mgomvi; angali pale ambapo pametolewa maelezo ya ushahidi anaonyesha kukasirika kabisa (rejea habari ilosema mambo ya you tube). Mimi naamini kuwa serikali haina dini ila nakubali kuwa watu wake wanazo dini, basi huenda kweli kuna udini serikalini kupitia watu wake! Ushauri wa bure; tuziache dini nje ya ofisi zetu, tukitoka maofisini tuzipitie na kwenda nazo majumbani kwani nyumbani bila dini nako hakutafaa! Mniwie radhi kama nilikaribia kuchafua hiyo hali ya hewa nayoisema mjomba Michuzi.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 06, 2011

    jamani lisemwalo lipo na kama halipo laja, na msimkemee sana huyu aliyetoa maelezo hayo, ukweli mkubwa upo ndani yake na sio uongo lakini kwa vile siye watanzania ni wafinyu wa akili basi lazima tuone ni uongo kila kinachoelezwa na watu, kwani huyu mwandishi ameshatafakari kwa muda na kuyaona haya ndio maana akaitoa yeye sio mwehu wala mwenda wazimu, kulikuwa na mambo ya mahakama kadhi na aliahidi kusaini kipindi chake cha mwisho kwani huo sio udini? kulikuwa na oic aliwaahidi waislamu kuwa atasaini kipindi chake cha mwisho huo sio udini?basi ninachotaka kusema ni ukweli kwamba urais wa kikwete ni wa kutisha na kusambaratisha wananchi na akitaka kujua dunia inakuwaje asaini hizi kalabrasha za dini aone, asifanye watu vipofu atakufa pamoja na uzazi wake wote, hakuna wajinga nyie ambao hamjaelewa hili linaloendelea nyamazeni wananchi wa leo sio wapumbavu au wajinga sasa wameshaelewa kila kitu kinachoendelea ktika nchi yao. cha muhimu kikwete afanye kazi iliyomweka madarakani na sio udini, kwani yeye sio rais wa wakristo au waislamu tu, ni wa wote, kwani sikuwahi kuona baba anayebagua watoto wake. tumeshtuka jamani, nyie mlolala na kumlaumu mwandishi hamjatambua hilo. sasa eleweni yaloandikwa ni ya kweli tupu.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 06, 2011

    hizi makala,ukizisoma, unaziacha,tafsiri unayo mwenyewe.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 06, 2011

    I can bet you with 100% certainty kwamba huyu aliyelalamika na kucopy hii article kutoka Raia mwema ni mwislamu au yuko kwenye circle ya CCM... Ambayo maana yake, so you feel offended.

    Kama wewe unajua au unakosoa mwandishi, kwanini usi-counterattack na article yako tena ukawatumia raia mwema na ukaweka jina lako na utajibu one paragraph after the other?

    Hakuna lolote nyie puppet tu wa CCM, na ndo mmetufanya watu tumeamua kuishi nje ya nchi kwasababu mnaozesha nchi na ufisadi.



    Seriously, inasikitisha saana na inachefua kwasababu nobody is ready to lead but rob the nation.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 06, 2011

    wazazi wangu walinipeleka shule nitoe giza machoni pangu mbele ya ulimwengu! niwe na uwezo wa kutafakari na kupambanua mambo kwa mapana yake! swala si kwenda shule; hiyo shule imekusaidiaje? you need to be wise! you need to distinguish reality from emotions! think broadly! but siku zote usiwe mtumwa wa fikira! mi napenda mawazo huru but sipendi hii kauli ya WATANZANIA HAWAPENDI OR WANAPENDA HIKI! CAUSE mi nakua mtanzania na napenda or sipendi wao wanayo suggest! but good people haki ya kikatiba naiona hapa!

    "struggle is my life, will struggle till the end of my days!" Nelson Mandela

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 23, 2011

    The way you think aof the Problem is the problem....lakini katika hili mkosoaji na ndiye anaonekana kuwa ndiye problem zaidi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...