Kibopa nambari moja duniani Bill Gates na mai waifu wake Melinda  Gates leo wametembelea kituo cha utafiti cha Ifakara tawi la Bagamoyo kuangalia shughuli za utafiti wa chanjo ya Malaria unaofanywa na kituo hicho. Bill na Melinda Gates wametoa msaada kwa dola bilioni 10 kusaidi mapambano dhidi ya Malaria na ugonjwa wa Trachoma hivyo ni wadau muhimu hapa nchini na wanastahili heshima zote, japo mwenyewe hapendagi kuuza sura wala kujulikana kuwa yupo mahali. Globu ya Jamii kama kawaida yake ya kuwa mbele hatua kumi katika habari inakupa taswira za  Bill Gates na mai waifu wake akiwa na watafiti na wafanyakazi wa Kituo Hicho.
Bill Gates akiwa na wafanyakazi wa Ifakara Health Institute kituo cha Bagamoyo
Bill Gates akiongea na watafiti na wafanyakazi wa kituo hicho
Bill na Melinda Gates wakiweka sahihi kitabu cha wageni Bagamoyo leo
Bill na Melinda Gates wakipata maelezo juu ya tafiti za Malaria kituoni hapo
Bill Gates akipiga stori na watafiti na wafanyakazi wa kituoni hapo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2011

    MWANDISHI WETU ALOCHAPISHA HII TAARIFA FUATILIA VIZURI HUYU BWANA SIE TENA TAJIRI NR MOJA DUNIANI .....KASHAPIKULIWA ZAMANI TU

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 29, 2011

    Bill Gates siyo kibopa nambari moja duniani, ni nambari mbili. Nambari moja ni Carlos Slim Helu wa Mexico.
    Thanks.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 29, 2011

    jamani hiyo ela nimeshindwa kupiga hesabu ina maana ni Tshs 15,500,000,000,000 au nisaidieni

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 29, 2011

    michuzi dola bil.10 ni sahihi umeichukua hiyo? ni nyingi si mchezo
    labda itakua ni million 10 na sio bil,

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 29, 2011

    Hawa jamaa kutalii majumba yao unahitaji helicopter dadadeki!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 29, 2011

    Katika watu nisiowaelewa ulimwenguni nadhani huyu naye yupo, Jamaa huwa yupo yupo tu na yeye anajichanganya kokote pale bila kujali ni kundi la watu gani. Kaka mimi napiga Kazi Mall nilikuwa napiga stori na tajiri mmoja lakini sikumjua kabisa baadae wafanyakazi wenzangu ndio wananiambia na jamaa alikuwa anaijua Tanzania balaaa

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 29, 2011

    Zitumieni hizo pesa za msaada kwa malengo mliokusudia
    Ili wengine waje na matokeo yaonekane inshallah
    Kila la kheri kituoni hapo
    Mpili Rama Mpili

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 29, 2011

    Ni kweli Bill Gates ni kiboba #2 duniani. Hii imetokana na yeye kugawa pesa nyingi kusaidia maskini tofauti na kibopa #1 Carlos Helu Slim(Lebanese Mexican Billionaire). Carlos yeye amesema sio Santa Clause so hataki mambo ya kugawa pesa zake kwa maskini. Anadai yeye anaanzisha kampuni ambazo zinatoa ajira kwa maskini. Hivyo ndio anavyosaidia maskini na sio kama Bill Gates.

    Eniwei, Bill Gates nae ni bepari mzuri sana msiomuone yuko simple simple. He is one of the Greediest Capitalist just like Gordon Gecko.

    Long Live Free Market Capitalism!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 29, 2011

    wabongo bana teh teh teh wanabishana eti huyu sio tajiri namba moja sasa hata akiwa tajiri namba 10 unafikiri ni suala la mchezo gates ana mihela sio mchezo na nashindwa kuelewa hao waandalizi wa shughuli hiyo yani walishindwa kuweka kiti hapo wanapotia saini ili waweze kukaa bongo juwa ni kali sana mtu anaweza kuanguka kuweni wastaarabu mnapokea milioni 10 dolla mnashindwa kumkaribisha mtu kwenye kiti huyo mtu hata obama mwenyewe anampatia heshima sababu sio mtu wa kuchezea

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 29, 2011

    Na huyo Carlos Slim hafui dafu kwa Hosni Mubarak, na wote wawili wamepata pesa kwa njia chafu. Hivyo tukiangalia tajiri zaidi ya wote duniani ambaye amepata mali yake kwa njia safi anabakia kuwa Bill Gates. Isitoshe Carlos huwa hatoi misaada ya kijami japo wananchi wa Mexico wana shida balaa, jamaa anakula pesa zake bila kuwasaidia wananchi wenzake hata senti moja year-in-year-out. Bill Gates juu!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 29, 2011

    ziende na zanzibar hizo bilioni

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 30, 2011

    Mbowe nae ageiga Bill Gate kwa kutoa magari yake bure kwa CHADEMA!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...