WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
Kwa kushirikiana na
TAASISI YA BENJAMIN WILLIAM MKAPA HIV/AIDS
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS inatekeleza Mradi wa kuimarisha mifumo ya huduma za afya ( Health Systems Strengthening) kupitia ufadhili wa Mfuko wa Duniawa kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria - Mzunguko wa 9 ( Global Fund Round 9). Baadhi ya malengo ya mradi ni pamoja na; kuongeza wataalam wa afya, ili kuimarisha huduma za UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na huduma nyinginezo, katika Halmashauri zilizopo maeneo yenye uhaba mkubwa wa watumishi kutokana na changamoto ya mazingira yake.
Baadhi ya malengo ya mradi ni pamoja na kuimarisha uwezo wa vyuo vya mafunzo ya afya, kwa kuvipatia wakufunzi zaidi, ili kuhakikisha kuwa uzalishaji wa wataalam wa afya unaongezeka zaidi nchini. Katika kutekeleza azma hii, BMAF wanatoa tangazo la nafasi za kazi kwa waalimu 137 wa vyuo vya Afya, kama ifuatavyo:
| ||
CHUO | KADA | IDADI |
| Nurse Tutors | 4 |
| Nurse Tutors | 5 |
| ||
| Medical Doctors Assistant Medical Officers (AMO) | 4 3 |
| Medical Doctors Asst Medical Officer (AMO) | 4 2 |
| ||
| Medical Doctors Medical Specialist | 4 1 |
| Nurse Tutors | 6 |
| Medical Doctors Asst Medical Officers (AMO) | 2 3 |
| Nurse Tutors | 5 |
| Nurse Tutors | 3 |
| Nurse Tutors | 6 |
| ||
| Nurse Tutors | 4 |
| Nurse Tutors | 5 |
| Medical Doctors Specialists | 4 2 |
| Nurse Tutors | 5 |
| Nurse Tutors | 3 |
| Nurse Tutors | 4 |
| Dental Surgeons | 2 |
| Medical Doctors | 3 |
| Nurse Tutors | 3 |
| ||
| Medical Doctors | 6 |
| Medical Doctors | 1 |
| Asst Medical Officers | 2 |
| Medical Doctors | 6 |
| Nurse Tutors | 2 |
| Nurse Tutors | 3 |
| ||
| Nurse Tutors | 2 |
| Medical Doctors | 4 |
| Nurse Tutors | 6 |
| ||
| Medical Doctors | 3 |
| Medical Doctor | 1 |
| Medical Doctor Asst. Medical Officers | 2 3 |
| ||
| Nurse Tutors | 3 |
| Medical Doctors | 2 |
| Nurse Tutors | 4 |
Izingatiwe kwamba:
- Ajira ndani ya mradi huu itatolewa kwa mkataba wa miaka miwili. Kwa wale wote watakaofanikiwa kumaliza vipindi vyao vya mikataba, wataajiriwa katika utumishi wa umma.
- Watumishi waliopo katika ajira ya utumishi wa umma au katika Taasisi/Vyuo vya mashirika ya dini (FBOs) hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi.
- Mishahara itatolewa kwa mujibu wa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Na. 1 wa mwaka 2009 kulingana na sifa na ujuzi wa mtumishi husika pamoja na maslahi mengineyo yaliyobainishwa katika mradi.
- Kwa taratibu za Serikali, wataalamu wenye umri chini ya miaka 45 wanashauriwa kuomba zaidi, na watakuwa na fursa kubwa ya ajira yao kuingia serikalini kwa masharti ya kudumu na pensheni. Kwa wataalamu wenye umri zaidi ya miaka 45 au waliostaafu, maombi yao pia yatashughulikiwa na ajira ya serikali itakuwa kwa mkataba.
Maombi yote yaambatanishwe na:
- Barua ya maombi ya kazi, ikipendekeza Halmashauri 3 mwombaji anayopendelea kupangwa kazi, na pia aonyesha ridhaa ya kujiunga na utumishi wa umma, baada ya mkataba wa miaka miwili kumalizika.
- Nakala ya cheti cha Taaluma na cheti cha kidato cha 4 pamoja na cha 6 (iwapo anacho), na viwe vimethibitishwa na Hakimu au Wakili.
- Picha mbili (2) – saizi ya Pasipoti na maelezo binafsi (CV), ikionyesha umri, anuani kamili na namba ya simu ya kiganjani, pamoja na anuani/ namba ya kiganjani ya wadhamini wako.
Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe 15 Juni 2011
Maombi yote yatumwe kwa:
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, S.L.P. 9083, DAR ES SALAAM.
Tangazo hili linapatikana pia katika tovuti za:
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...