Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Ali Saidi Manya ambaye pia ni Diwani wa kata ya Lizaboni (pichani ) amefariki dunia leo katika Hospitali ya Misheni Peramiho.

Taarifa za Msiba huo zimetangazwa na naibu Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Mariam Dizumba na kupokelewa kwa mshtuko mkubwa na wakazi wa manispaa ya Songea na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.

Naibu Meya Dizumba amesema mazishi ya Mstahiki Meya Ali Saidi Manya yatafanywa nyumbani kwake Lizaboni Manispaa ya Songea Siku ya Jumatatu Tarehe 1 Agosti 2011.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...