Mwamvita
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Ijuma hii itajumuika pamoja na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla ya chakula cha usiku pamoja na burudani ya muziki katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba chakula hicho ni sehemu ya utamaduni wa kampuni hiyo wa kuimarisha mahusiano na wadau wake mbalimbali ikiwemo Bunge na Serikali pamoja na kutambua juhudi za wadau hao katika maendeleo ya taifa na watu wake.

"Tumekuwa na utamaduni wa kuandaa hafla za aina hii wakati wa Bunge ila ya mwaka huu mambo yatakuwa mazuri na ya aina yake ikilinganishwa na tulizowahi kufanya miaka ya nyuma na kwa mantiki hiyo kauli mbiu ya mwaka huu ni "More Than Ever Before" na tunamaanisha"Alisema Mwamvita.

"Vodacom Tanzania inakwenda Bungeni mjini Dodoma ikiwa na sura mpya kufuatia mabadiliko makubwa katika muonekanao wake wa rangi na kauli mbiu ambayo sasa ni "kazi ni kwako" na hivyo tunataka kuwadhihirishia waheshimiwa wabunge upya wetu katika kila jambo tunalolifanya si tu katika utoaji wa huduma za mawasiliano ya mkononi nchini"Aliongeza Mwamvita

Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda anatarajiwa kuongoza hafla hiyo itakayohudhuriwa pia na Spika wa Bunge Mama Anne Makinda, Kiongozi wa Kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe pamoja na wabunge wakiwemo mawaziri na naibu mawaziri watakaojumuika na viongozi wa Vodacom Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Dietlof Mare.

Mwamvita alisema anatambua kuwa wabunge kwa sasa wapo katika kazi nzito ya kujadili bajeti ya Serikali kazi ambayo Vodacom inaitambua na kuiheshimu na hivyo pamoja na mambo mengine bado suala la kuwaandalia hafla za aina hiyo nalo lina sehemu yake ili kuwapatia fursa ya kukutana nje ya mazingira ya kazi.

"Kwa niaba ya Uongozi wa Vodacom na wafanyakazi wake napenda kutumia fursa hii kwa heshima na taadhima kuwakaribisha waheshimiwa wabunge wote kujumuika pamoka katika usiku wa Vodacom na Bunge utakaoburudishwa na Mwanamuziki Banana Zorro, Diamond pamoja na Bi. Shakira ikiwa ni kuendeleza mahusiano mema yaliyopo yenye azma ya kujenga taifa lenye maendeleo makubwa katika nyanja ya mawasiliano ya simu za mkononi."Amesema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2011

    Haya makampuni yanaandaa chakula kwa wabunge kwanini? Itabidi tuangalie sheria zetu. Hii ni lobbying yaani wabunge wanapigwa mamisosi na burudani halafu kesho watasema nini kuhusu kampuni husika kama kitu kama kutolipa kodi kikitokea?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2011

    Ndugu wananch, ghafula hii ya chakula cha usiku kuandaliwa na Vodacom kwaajili ya wabunge inaonyesha ni jinsi gani kampuni kubwa zina jidhatiti katika kujenga mahusiano ambayo yataleta ugumu inapofika wakati wa kuleta sheria za mabadiliko katika nyanja za mawasiliano. This is absolutely wrong and needs to stop NOW!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2011

    Hii siyo takrima hii? Kesho nani ataisema vibaya Airtel au Zantel? Nani atakemea high rates za mobile internet? Nani atatetea ongezeko la corporate tax za mobile phone companies?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...