Mratibu wa Promosheni ya Mchongo, inayoendeshwa na Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Essy Ogunde, akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo itakayodumu miezi mitatu ambayo washiriki watajishindia zawadi mbalimbali, likiwamo gari aina ya Toyota Vitz kwa upande wa magazeti ya michezo,Bingwa na Dimba na Toyota Suzuki kwa Gazeti la Mtanzania. Promosheni hiyo ilizindulia katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Sinza Kijiweni, Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Masoko na Usambazaji, Grace Kassella.
Meneja Masoko na Usambazaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Grace Kassella, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Promosheni ya Mchongo, inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu, ambako washiriki watajishindia zawadi mbalimbali, zikiwamo gari aina ya Toyota Vitz kwa upande wa magazeti ya michezo, Bingwa na Dimba na Toyota Suzuki kwa Gazeti la Mtanzania. Promosheni hiyo ilizinduliwa jana katika Ofisi za Kampuni hiyo, zilizopo Sinza Kijiweni, Dar es Salaam.

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ni New Habari (2006) ambao ni watengenezaji wa magazeti ya Bingwa, Dimba, Mtanzania, Rai na The African, imezindua promesheni iliyopewa jina la Mchongo ambayo itampa msomaji wa magazeti yao matatu kujishindia zawadi ya gari na nyinginezo.

Akizungumza katika uzinduzi wa promosheni hiyo, Makao Makuu ya Kampuni hiyo, Sinza Kijiweni, jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Usambazaji wa New Habari, Grace Kasella, alisema promosheni hiyo itawahusu wasomaji wa magazeti ya Bingwa, Dimba na Mtanzania.

Alisema kuwa wasomaji wa Bingwa na Dimba, watashindania gari dogo aina ya Vitz lenye thamani ya Sh milioni 8.5, wakati wale wa Mtanzania watawania gari aina ya Suzuki Vitara yenye thamani ya Sh milioni 14, katika droo kubwa itakayofanyika baada ya miezi mitatu, ikitarajiwa kumalizika Oktoba mwaka huu kwenye ofisi za kampuni hiyo.

“Zawadi hizo za magari pamoja na nyinginezo kama fulana, runinga, kofia, mipira na nyinginezo zitakazokuwa zikitolewa katika droo ndogo za kila mwezi, zina thamani ya Sh milioni 36,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Usanifu Kurasa wa kampuni hiyo ambaye ndiye msimamizi wa promosheni hiyo, Essy Ogunde, alisema msomaji wa magazeti hayo, ataingia kwenye promosheni hiyo kwa kujaza kuponi inayopatikana kwenye magazeti hayo na kuituma katika ofisi za kampuni hiyo.

Alisema kuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo pamoja na familia zao, hawataruhusiwa kushiriki na vigezo na masharti vitazingatiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...