Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Bi. Ashura Kassala, mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam aliyelazwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma kufuatia kupata majeraha makubwa kutokana na ajali ya basi La Champion lililopata ajali juzi mkoani Dodoma.Rais Kikwete alikwenda kuwapa pole majeruhi hao baada ya kulihutubia baraza la Iddi lililofanyika katika msikiti wa Gaddafi mkoani Dodoma.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Bwana Winston Chinduge mkazi wa Gairo,mkoani Morogoro ambaye ni mmoja wa majeruhi wa Basi la Champion lililopata ajali juzi mkoani Dodoma.Majeruhi hao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia baraza la Iddi lililofanyika katika msikiti wa Gadaffi mjini Dodoma leo jioni
Sheikh Mkuu na mufti wa Tanzania Issa bin Shabaan Simba akipeana mikono na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Baraza la Iddi lililofanyika katika msikiti wa Gaddafi Mkoani Dodoma. Picha zote na mdau Freddy Maro wa Ikulu















































Tatizo la siku ya eid ni lini liko hapa!
Mchangiaji wa kwanza sijakufahamu na hiyo sentence yako!!!