Simba imeingia mkataba na mchezaji Gervais Anold Kago kutoka klabu ya Olympic Real de Bangui ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kwa ajili ya kuichezea timu hiyo kwenye Ligi Kuu ya Vodacom na michuano ya kimataifa.
Lakini wakati Kago akiwa bado hajapata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) tumemruhusu achezee timu yake ya Simba kwenye mechi dhidi ya Yanga itakayofanyika kesho (Agosti 17 mwaka huu) kutokana na sababu zifuatazo;
Mechi hiyo ni ya Ngao ya Jamii (Community Shield) na lengo lake ni kusaidia jamii. Pili, ni kuzindua msimu mpya wa Ligi na tatu, Simba imeonesha nia ya kumhamisha kutoka CAR.
Kwa vile Kago ni mchezaji wa kulipwa ni lazima apate ITC kupitia mfumo wa mtandao wa Transfer Matching System (TMS) ili aweze kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom na michuano ya kimataifa. Hiyo inatokana na ukweli kuwa Simba imeingia mkataba na Kago kama mchezaji wa kulipwa ambaye uhamisho wake ni lazima ufanywe kwa TMS na si ITC ya karatasi ambayo inatumika kwa wachezaji wa ridhaa.
Kwa mujibu wa Ibara ya 2(2) ya Kanuni za Uhamisho wa Wachezaji za Shirkisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), mchezaji wa kulipwa ni yule ambaye ana mkataba wa maandishi na klabu na analipwa kutokana na shughuli ya kucheza mpira.
Pia si kweli kuwa CAR hawamo kwenye TMS. Nchi hiyo inatumia mfumo huo wa mtandao na Meneja wao wa TMS ni Elie-Delphin Feidangamo.
Kwa mujibu wa annexe 3(5) ya Kanuni hizo za FIFA kuhusu uhamisho wa wachezaji, utumiaji wa mfumo wa TMS kwa uhamisho wa wachezaji wa kiume wa kimataifa ni lazima.

Alex Mgongolwa
Mwenyekiti
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Suala hili nilitegemea Rais wa TFF alifafanue mwenyewe kama kiongozi wa juu, kwa kuwa mazingira yalivyo sio rahisi kwa wapenzi wa Simba kuamini wanayosema viongozi wengine kwa kuwa wanajulikana ni wana Yanga na wameshiriki ktk masuala mbali mbali ya Yanga kwa hiyo yanga wakikosea wataambiwa mapema sio kuviziana. Ingawa Tenga naye ni mwana Yanga lakini ni kiongozi wa mwisho ktk soka letu.

    ReplyDelete
  2. suala la kago ni la kisheria zaidi kuliko siasa za usimba na uyanga.asiyeridhika na uamuzi wa kamati ya mgongolwa akate rufaa ngazi ya juu zaidi badala ya kuichonganisha tff na wanasimba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...