Mbunge wa Ilala Mh. Azzan Zungu na Mbunge wa Mafia Mh. Shah akiperuzi kitabu cha hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji iliyowasilishwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mh. Steven Wassira kwa niaba ya Waziri wa Maji profesa Mark Mwandosya ambaye yuko nchini India kwa matibabu. Kwa mujibu wa Spika Anne Makinda hali ya Profesa Mwandosya inaendelea vyema, Bajeti ya wizara ya Maji inajadiliwa kwa siku mbili na wabunge wengi waliochangia wameitaka serikali ifanya kila iwezalo kutatua tatizo sugu la maji nchini
 Mbunge wa Bariadi Mashariki Mh. John Cheyo, Mbunge wa Kigoma Kusini Mh. David  Kafulila na Mbunge wa Vunjo Mh. Augustine Lyatonga Mrema wakiwa bungeni leo
 Viongozi wa Wizara ya Maji, EWURA na wadau wa maji wakifuatilia kinachoendelea bungeni leo
 Sehemu ya Wabunge ambao  ni mawaziri
 Baadhi ya wabunge kikaoni
 Baadhi ya waheshimiwa wabunge bungeni
 Toka shoto ni Mbunge wa Lushoto Dr Abdallah Kigoda, Mbunge wa Tabora Mjini Mh Aden Rage na Mbunge wa Singida kusini Mh. Mohamed Misanga. Mh. Rage pia ni Mwenyekiti wa Simba wakati Mh Misanga ni mwenyekiti Mstaafu wa Yanga
 Mbunge wa Mafia Mh Abdulkarim Hassan Shah akiongea na mdogo wake na kaka bungeni leo
 Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda (kulia) akiongea na Mbunge wa Musoma mjini Mh Vicent Nyerere 
 Mbunge wa Korogwe vijijni Mh Stephen Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu (shoto) na Waziri wa Fedha na mbunge wa Mh Mustafa Mkullo wakiangalia magazeti ya leo yanayouzwa bungeni
Mbunge wa Bumbuli, Mh January Makamba (shoto), Mbunge wa Sumve Mh Richard Ndassa (kulia) wakiongea na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Profesa Tolly Mbwete wakati wa mapumziko 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. hivi John Cheyo ni mbunge wa Magu au Bariadi?

    ReplyDelete
  2. Dr. Kigoda tangu lini mbunge wa Lushoto?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...