Ankali Habari za Swaumu na kuliendeleza libenenge la blogu ya Jamii,
Imenichukua muda kupata moyo wa kuleta shida yangu hapa, nikizingatia wenzangu walionitangulia kuleta shida zao hapa walivyonyanyambuliwa badala ya kusaidiwa. Ila nimepata moyo kuona kwamba ndani ya hiyo minyanyambuo na mishuo kuna wasamaria wema wanatoaga ushauri mzuri tu, nami naamua kuwalenga hao na kuwaacha wasukutua vinywa kama unavyowaitaga wasukutue watakavyo. Lakini najua kuna mmoja ama wawili aatanisaidia.
Ni kwamba mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 29, ni muislamu, nimeolewa na hivi karibuni tumejaaliwa kupata mtoto wa kiume. Tatizo langu liko pale pale kwenye chakula cha usiku ambalo, kwa kuwa niko ndoani sidhani kama ni makosa kukila. Ama sivyo ankali, maana ushairi nimeona kwa mwenzangu majuzi, nami nimejiridhisha kuwa ni hivyo. Tatizo langu ni kwamba mtoto wetu ndio kwanza ana miezi mitatu, na mwenzangu na mie anaanza kuwa na hamu ya kula chakula cha usiku. Mie namkataza kwa kuwa nimesikia tukila chakula cha usiku katika umri huo kuna hatari ya kumbemenda mtoto.
Hivyo kwa heshima na taadhima naomba wasamalia mlio wema mnijuvye. maana hata kule kliniki tumekatazwa kula chakula cha usiku hadi mtoto akue. lakini nimeulizia kwingine naambiwa hayo ni mambo ia kiswahili na ya kizamani, na kwamba nile tu mlo wa usiku bila shida na hakuna kitachotokea. Sasa mie mwenzenu ndio nshachanganyikiwa hivyo, hata sijui nishike lipi na nimsikilize nani. Na kama ni mwiko kula chakula cha usiku wakati mtoto bado mchanga, je ni umri gani wa muafaka kwani nahofu mwenzangu asije kula kona bure, tukaleteana malazi nyumbani. Jamani naomba msaaada nifahamishwe nifanyeje??


Ndimi CKK 
(ankal email weka kapuni, jamaa akijua atanila mbichi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 43 mpaka sasa

  1. Kama umejufungua kwa njia ya Caesarean ama kisu, basi ni muhimu kuwasiliana na Daktari wako baada ya wiki sita ili atadhmini kama mwili wako uko katika hali ya kula hicho chakula kama unavyosema. Lakini inabidi utumie vidonge vya majira, kwani mama anayenyonyesha kama wewe ni rahisi sana kushika Mimba nyingine kwa haraka zaidi.

    Kwa kawaida swala la mapenzi baadaya ya kujifungua laweza kuwa baada ya mwezi mmoja na nusu hivi, ama miwili, inategemea umeponaje. Na usifanyie ndalilo, maana bado hujapona kisawasawa. Na mwambie mmeo hujapona kisawasawa, asijifanye kuwa na hamu kubwa kuliko.

    ReplyDelete
  2. Dada kubemenda mtoto ndo nini?hahaha! swala la unyumba baada ya kuzaa intakiwa ufuate ushauri wa daktari. mambo ya kiswahili hayo achana nayo. kweli we dada unaona kuna uhusiano gani kati ya uroda na kuadhrika kwa mtoto? sababu muhimu ya kuzuia kula uroda baada ya kuzaa ni infection control! kwani unapozaa maungo ya uzazi yanapita kitu tunna ita " tissue trauma" kwa hiyo maungo yanahitaji muda wa kupona kwanza kabla ujaanza kuyaadhibu na " muhogo" (nyama). kurudi kwenye swala la infection ni kwamba baba watoto anapomwaga yale mambo yake huko ndani kwako kuna hasirimia kubwa sana kama haujapona vizuri unaweza kudevelop infection mbaya sana! kwa ushauri wa wataalam ni kwamba usile uroda for 6 to 8 weeks baada ya kujifungua, kwa hiyo kama kijana ana miezi mitatu.. basi mashaallah chakula ya usiku ni hewalla tu.
    Mpiga Box kutoka USA.ahsante:)

    ReplyDelete
  3. Haina matatizo wewe kula tu cha kuogopa ni mimba ukipata mimba na ukiendelea kumnyonyesha mtoto ndio unaweza ukamuathiri mtoto lakini kama hautapata mimba na huyo ni baba yake kweli hakuna cha kubemenda wala nini.

    Miezi mitatu inatosha kabisa jamaa kuanza kujisevia maana kama gari limeshatoka gereji lipo safi kabisa.

    ReplyDelete
  4. Inaonekana wewe ulikuwa huendagi kliniki kwani hayo yote yanafundishwa huko,mpe mumeo haki yake,kosa ni pale utakapogawa kwa mtu asiye mumeo kwani ukitoka nje ya ndoa ndo unaweza kumbemenda mtoto

    ReplyDelete
  5. Shoga pole, sijui mwenzetu uko karne ya ngapi weweee, na sijui umesoma na sijui pia hujui kutumia internet kutafuta kile usichokijua! sijui hata nikueleze nini kwa kweli, shosti umebowa!!! na je wale wanawake wa zamani waliokuwa wakipata mimba ilhali ndani ya arobaini ya kichanga kingine wana wao walibemendekaa???

    ReplyDelete
  6. hakuna hiyo tena umemtesa mwenzio. unabemenda kama mmoja wenu katoka nje otherwise pateni msosi wa jioni taratibuuuuuuuuuuuu mkimezea na kinywaji muruaaaa serengeti serengeti aha aha aha.

    ReplyDelete
  7. Sometimes watu mnakuwa huru sana kuongea mambo yenu ya ndani mbele ya jamii nzima hadi inakera kwa kweli. Suala unalouliza ni muhimu ila sidhani kama linapaswa kuwa la halaiki. Ni vema tutenganishe mambo ya kushea na mambo ya siri so as not to misuse and abuse freedom of speech, maana nayo ina criteria zake.

    ReplyDelete
  8. mwanamke anaweza kula chakula baada ya wiki 6, kama hatakua na matatizo ya kipeke, kwabahati nzuri kuna mtalamu kutoka kenya ameelezea kwa undani kuhusu kupata chakula hicho wakati mwanamke akiwa na mimba na baada ya kujifungua, nenda kwenye internet google K24TV's Channel-YouTube/connect episode 17, nadhani itakusaidia na utaokoa ndoa yako, asante

    ReplyDelete
  9. Kama wewe muislam je hujui dini inasemaje kuhusu hilo suala lako? Halafu inaonyesha wewe uwelewa wako ni mdogo, mwezi kama huu unaleta masuala ya kula chakula hujui kuwa utasababisha watu wavunje swaumu zao. Kwa taratibu za kiislamu mzazi akimaliza siku 40 tu basi amtayarishie mwenza chakula. Wenzio wanakula kila leo na watoto hawapati, shukuru ulichonacho.

    ReplyDelete
  10. Mimi sio mtu wa medical field ila ninavyoelewa miezi mitatu inatosha kabisa kuanza kula msosi bila shida. Na hayo mambo ya kubemenda ni stori tu za kiswahili, not scientific.

    Ila to be sure, kamuone mtalaamu wa uzazi bora nina uhakika unaweza kupiga msosi bila shida baada ya miezi mitatu.

    ReplyDelete
  11. unaweza kufanya ila ukimaliza tu muoge janaba kabla kumshika mtoto.Sio mshakula msosi then huogi unakaa kwanza mtamdhuru mtoto. Enjoy ur meal.

    ReplyDelete
  12. CKK,

    Kwanza, usasa hupo na ukale hupo pia. Wa kale walikuwa wakifundana na kupewa taratibu za kufanya katika hali yako kama hiyo, na wakale pia wnataratibu nyingi za kufanya pia.

    Nani amesema kuwa kula chakula cha usiku ni kosa ukiwa na mtoto wa mwezi mitatu. Unaruhusiwa isipokuwa kunataratibu za kufanya ili kulinda mtoto wako asipate matatizo. Zipo za wazee wa kale na hata za zamani. Rudi kwa somo ukajifunze ndoa sio chakula cha usiku tu. Inaonekana mengi yatakuwa yamekupita. Au wewe ndio wale wanapata kitchen party katika kumbi kubwa na watu kibao!!!. Kwa maoni yangu unahitaji misingi ya ndoa na sio hilo la chakula cha usiku tu.

    ReplyDelete
  13. Wasikudanganye, chakula cha usiku kinalika vizuri tu chakuzingatia ni usafi na uangalifu kwa sababu unakuwa hujui siku zako zitaanza lini. Mkijisahau mnaweza kuta mtoto mwingine anatokea huyo akiwa bado mchanga!

    ReplyDelete
  14. Du, miezi mitatu bado hamjaanza kupata chakula cha usiku? Hakuna swala la kubemenda mtoto, cha muhimu ni kuhakikisha mnatumia njia ya uzazi wa mpango kuakikisha haubebi mimba kipindi hiki wakati mtoto wenu bado mdogo. Tembelea vituo vya uzazi wa mpango wakuelekeze vizuri na uchague mojawapo. Kama imani yako haikuruhusu unaweza kuchagua njia ya asili ya kuangalia ute na kalenda though ni very risk maana mnaweza kuta umeconcive bila kutarajia. Kumbukeni usafi ili mtoto asiwe contaminated.

    ReplyDelete
  15. mama mtoto, kwanza hongera ya kupata mtoto na pili, ushauri wangu kwako ni ule chakula mara tatu kwa siku (asubuhi, mchana na jioni). hiyo habari ya kutokula cha kula cha usiku sijui ni docta gani mwenye akili timamu anatoa ushauri kama huo kwa mtu aliyejifungua labda kama docta wako ni mganga wa kienyeji kwamaana hao ndo husemaga vitu vya ajabu ajabu. Kula chakula na weka afya yako vyema ili uweze kumlisha mtoto maziwa bora ya mama.Pia ningekushauri uwe unatembelea
    http://tzmomsabroad.blogspot.com/ kwa maana hii site huongelea mambo ya kina mama na wanawake kwa ujumla.

    ReplyDelete
  16. uKweli kama ulivyosema hayo nimambo yakiswahili.Jaribu kufikiria hivi kunauhusiano gani kati ya hili la mtoto na chakula cha usiku?hakuna usuhusiano wowote na huyo nesi anayesema hivyo sijui nishule ipi kasomea,labda kwa kukusaidia wewe na wengine nikuwa huwa tunapenda tendo la ndoa litendeke mama kujifungua akae apate nguvu na afya yake irudi vizuri hii inategemeana na jinsi alivyo mama kiafya.Acheni mila za zamani kuwa mama harusiwi kula mayai au kwa ndugu zangu wa kagera mama haruhusiwi kula senene nimambo yakizamani yasiyo na uhusiano kisayansi

    ReplyDelete
  17. Hamna shida miezi mitatu poa kabisa labda kama bado una matatizo ya uzazi. Kamuone doctor akuchunguze!

    ReplyDelete
  18. Mimi si daktari, lakini nafahamu kwamba hakuna madhara yoyote kwa mtoto mchanga kwa kula chakula cha usiku ili mradi tu mama viungo vyake viko tayari kwa ajili ya ile shughuli. Jambo la kuangalia tu ni kwamba ni vizuri utumie vitu vya uzazi wa mpango ili usije ukapata ujauzito bila kujua. Hii ni kwa sababu kwa akina mama wengine hali yao ya damu ya mwezi uchukua mda kabla haijajitokeza kwa ratiba ya kawaida. Hivyo hustukia wamekuwa wajawazito tena bila kujua. Mridhishe mmeo, la sivyo atatoka nje au atakutafutia mke mwenza. Ubarikiwe.

    ReplyDelete
  19. Dada yangu hizo ni fikira za kizamani,me nilianza kula hiyo daku kabla hata siku arobaini hazijafika na mpk kesho mwendo mdundo.so usimbanie mwenzako hakuna kitakachoharibika,sharing is caring,kula vitu kwa raha zenu

    ReplyDelete
  20. dada hakuna madhara yoyote ni maneno ya kiswahili hakuna ushahidi wa kisayansa kula chakula cha usiku kwa raha zako jitahidi tu usafi

    ReplyDelete
  21. waweza kula chakula cha usiku baada ya wiki sita tu baada ya kujifungua. hayo maneno mengine ni uzushi tu.

    experienced woman.

    ReplyDelete
  22. Ndugu yangu, hapa hakuna kuosha vinywa umeuliza swali la MAANA, hivyo kupewa ushauri ni haki yako. Jambo kama hili liliwahi kuulizwa kwenye hadhira hii hapo nyuma na nakumbuka ulitolewa ushauri wa kidaktari, kwa kifupi ni kuwa UNARUHUSIWA kabisa kula chakula cha usiku na mwenzio tena bila wasiwasi isipokuwa tu tahadhari unatakiwa kuiweka ili kulinda afya ya mtoto, kama vile kuzuia kupata mimba kabla ya wakati ili mtoto apate muda wa kutosha wa kunyonya maziwa ya mama ambapo inashauriwa walau miaka 3 . Pia ni vizuri kuzingatia usafi wa hali ya juu baada ya chakula unapotarajia kumnyonyesha mtoto. Lakini lililokubwa ni kutazama kama via vyako vya uzazi vinaruhusu kula chakula kwa wakati huu, kwani kujifungua kuna mambo mengi. Lipo tatizo la wahudumu wa afya kubaki msitu wa MILA vichwani mwao pamoja na kuwa wameelimishwa vya kutosha. Ukienda kliniki ya Wazazi waone wahudumu wa MCH ikiwa na maana Mother Child Health hawa ndio waliobobea katika masuala ya afya ya Mama na Mtoto. Anza haraka kumpa Baba haki yake iwapo tu umezingatia vigezo nilivyosema hapo juu.
    Furahia ndoa yako kwa kupata mtoto na pia kufurahia tunda la tendo la ndoa ndani ya ndoa.

    ReplyDelete
  23. unaweza kukutana kimwili na BABA WA MTOTO baada ya mtoto kutimiza siku arobaini toka kuzaliwa na mtoto hawezi dhurika. mimi ni mama niko kwenye ndoa mwaka wa 6 na nina watoto

    ReplyDelete
  24. DADA CKK SOMA HIYO


    Iwe umejifungua kawaida au kwa mkasi mwili unahitaji muda kupona. Unashauriwa na wataalamu wengi kusubiri kwa kati ya wiki nne mpaka sita kuanza tena kula tundi huu muda unaruhusu cervix kujifunga, kusimama kwa bleeding na kupona kwa vidonda vyovyote vilivyotokea kwenye tunda wakati wa kujifungua.
    Ila muda muafaka unategemea sana na mama mwenyewe, wengine wanaweza kutoa tunda ndani ya wiki chache wakati wengine wanahitaji miezi michache au zaidi kutokana na feeling za mwili baada ya tendo zima la kujifungua.

    Kuhusu la kumbemenda mtoto kwa kula tunda hayo ni mambo ya kizamani saana suala kubwa ni huo muda wa kitaalamu na feeling za mwili kama umepona kuweza kuhimili sex life again. Kwa wa kwako huyo mwenye miezi mitatu we jirushe tu na mzee ila chonde chonde muangalie msije mkamlalia mtoto wakati wa makasheshe...!!


    MDAU
    EDD

    ReplyDelete
  25. mbona umechelea sana? Kamuone gyana akushauri uzazi wa mpango ulio bora kama sindano/vidonge/lupu etc Alafu kula chakula kwa kwenda mbele. Ukizidi kusubiri atafuturu akitoka kibaruani...

    ReplyDelete
  26. Sikiliza CKK
    kumbemenda mtoto ni wewe ukitoka nje kwenda kula hicho chakula cha usiku lakini chakula hiho ukila na mwenzio uliyefunga nae ndoa hakina matata kula tu na mtoto atakuwa vizuri.

    Unajua CKK kisichotakiwa kwenye malezi ya watoto ni kitu kinaitwa JANABA hii janaba ikimgusa mtoto tu anakuwa tayali amebemendwa. Ndio maana ni vizuri kuoga kila unapotoka matembezi yoyote hata kama huko ulikoenda hukula chakula cha usiku lakini uliongea maonezi ambayo uyalikutoa Manii hadi ukafikia hatua ya kujihisi unakula hicho chakula cha usiku. Au wakati mwingine ukasalimiana na mtu aliyetoka kula hicho chakula na kukuachia hiyo Janaba. hivyo basi ni vizuri ukanawa mikono na sabuni ili kujiridhisha kuwa uko safi. huo ni mtazamo wangu. Kula tu chakula chako Mungu amekupa usikiogope wala kukipangia masharti yatakayo leta mwenzio baadae..........Kizito!!!

    ReplyDelete
  27. Habari!
    Dada usiwe na wasiwasi, hiyo ilikuwa imani za kizamani, kwa mume wako haina shida kabisa, mpe agonge hata kila siku; kumbemenda mtoto itatokea kama unaibia nje na ukirudi unambeba mtoto bila kuoga wala kunawa.
    Baajun Korea Kusini

    ReplyDelete
  28. Dada yangu pole kwa njiapanda hiyo. Naomba tu usikilize maoni ya wataalamu wanasema nini. Mimi waliniambia hakuna madhara yoyote kwa mtoto. Nina watoto watano na mara zote tumekuwa tukipata chakula cha usiku kama kawa bila madhara wala mikwaruzo yoyote kwa afya ya watoto wetu. Baada ya kusema hivyo naomba muwe na kiasi. Mtoto anapokuwa amelala basi mnapata unyumba na kujiweka katika hali ya usafi ili akiamka tu kama anataka kunyonya basi inakuwa mswano tu!

    ReplyDelete
  29. Hakuna tatizo kama ni mzima afya na nifasi imekoma,cha muhimu ni kujizuia na mimba kwa njia uiwezayo kama vidonge, sindano,vipande na condom ila pata ushauri wa daktari kabla ya kutumia njia nyingine za kuzuia zaidi ya condom kwa kuwa unanyonyesha,vinginevyo kula raha

    ReplyDelete
  30. Ebu mpe chakula wewe.Unataka akale kwa mama lishe halafu akuletee magonjwa ya Tumbo hey?

    David V

    ReplyDelete
  31. Wewe kula chakula usiku tu,ila utumie dawa ya penzi,kuogopa kujitokeza mengine,ila hakikisha unapotaka kumnyonyesha mtoto unakuwa msafi kwa maana usafi,
    Iwa mwema,wakatabahu
    king'ang'anizi

    ReplyDelete
  32. CKK, tafadhali anza kula chakula cha usiku usiku wa leo. Hakuna kubemenda. Mimi ni mwanaume, nimeoa na tumejaaliwa watoto wawili. Mmoja ana umri wa miezi mitano. Wa kwanza ana miaka mitatu. Tumekuwa twala chakula kitukufu baada tu ya mke wangu kujisikia yuko sawa kimaumbile baada ya kujifungua. Km wewe ulijifungua kwa njia ya kawaida na huna tatizo lolote la kiafya basi kula. Watoto wote wana afya njema na warembo hao ajabu.

    Mnapaswa kuzingatia usafi tu. Msimshike/kumgusa/kumnyonyesha mtoto baada ya chakula. Hakikisheni mnaoga mara tu baada ya chakula. Hakuna kubemenda. Na kwa tahadhari yako. Wanawake siku hizi wako wengi afu wengi wao wakijua una mke ndo unafuatw zaidi. Ukiendelea kumnyima chakula basi ujuwe umeliwa. Usije ukarudi hapa kueleza kuwa mme wako ameivisha simu yake nailoni ili aweze kuoga nayo.

    ReplyDelete
  33. dada kwa huo muda aliwonao mtoto unaweza tu ukala chakula cha usiku ila kubwa kinachotakiwa ni kuwa msafi tu baada ya kula hicho chakula...mie nakupa mfano wangu nina mtoto wa miaka sita sasa alinilianza kula chakula akiwa na umri huu wa miezi mitatu,kuhusu la kubemenda mtoto inatokea kama mama utakuwa umepata mimba na ukaendelea kumnyoshesha mtoto hapo mtoto uwa ana hadhili na maziwa hayo anayokuwa ananyonya...na kama kati yenu atakuwa natoka nje ya ndoa lazima mtoto pia hatapata madhala na ndiyo maaana unashauri ukiwa mzazi unanyoshe unatakiwa kabla ya kuonyesha unakatiwa kusafisa kwanza maziwa au hata kuoga kwanza na hata baba akitoka kwenye mizunguko yake ya kila siku ni vizuri kuoga kwanza kabla ya kumkamata mtoto..hayo ni kwa ufahamu wangu tu nakutakia malezi mema..

    ReplyDelete
  34. kula mama kwa raha zako, ni vyema kutumia condom ili usipate mimba tena, maana siku zimevurugika

    ReplyDelete
  35. hakuna kitu kama hicho utamharibu mtoto ikiwa utafanya na baba mwingine sio babake na hivyo hivyo ukishamaliza lazima utawaze!

    ReplyDelete
  36. nadhani c mbaya wala hakuna tatizo

    ReplyDelete
  37. Kwa uelewa wangu wa kawaida na si wa kitaalam kama hofu ya kumbemenda mtoto ni ya kiimani basi mwaweza kuvumilia hadi mtoto akuwe, ila kama ni ya kisayansi basi mtumie kinga (kondomu) na muendelee kupeana haki ya ndoa kistaarabu.

    ReplyDelete
  38. OK DADA CKK KWANZA NAKUPA HONGERA KWA KUWA MUWAZI NA HIVI NDIVYO TUISHIVYO KIJAMII KUHUSU OMBI LAKO WATALAMU WANASEMA BAADA YA MAMA KUJIFUNGUA HUTAKIWA AKAE SIKU 40 PASIPO KUFANYA TENDO LA NGONO KWANI KIPINDI HICHO NI KIPINDA CHA MJIFUNGUA VIUNGO VYAKE BAADA YA KUJIFUNGUA HUWA VINA JIRUDISHA KTK HALI YA KAWAIDA BAADA YA HAPO WAWEZA ONANA NA MUMEO KAMA KAWAIDA ILA KWA TAADHARI YA KUTOSHIKA UJAUZITO TENA KWA SASA NI KUTUMIA KONDOMU TU NO WAY JAPO KUNA NJIA ZA ASILI PIA WAKATI WAONANA NA MUMEO CHA MSINGI MZEE ASIPENDE KUCHEZEA CHAKULA YA MTOTO YANI MAZIWA YAKO HAPO NDIPO KWENYE TATIZO LA KUHUSIANA KUSEMWAKO KUBEMENDA MTOTO KWANI HAYO MATITI YAMEBEBA CHUKULA YA MTOTO WAKATI WA TENDO YAKICHEZEWA HUWA YANACHACHUKA HIVYO ANYONYAPO MTOTO HUWA TATIZO KWAKE PIA LINGINE BAADA TENDO NA MUMEO KABLA YA KUMNYONYESHA MTOTO YAKUPASA UWE UNAZIOSHA CHUCHU ZA MAZIWA YAKO NDIPO UNAMNYONYESHA MWANAO NI HAYO DADA TAKE CARE KWA MUMEO ONLY BY uncle richie wa ughaibuni

    ReplyDelete
  39. kula chakula mama utambemenda kama utakwenda kwa mwanaume mwingine na si mumeo.

    ReplyDelete
  40. Bwana wee, yaani mi nilifikiri waafrika ni wajuaji zaidi ya wazungu ktk suala la chakula cha (sio usiku tu jamani anytime) kumbe la.
    Jamani dada yangu sikiliza na wengine wengi mtakaosoma hapa; Mwanamke kama hauwezi kutoa huko chini k'sababu ya kuzaa au anything, kuna in between maziwa au katikati ya mapaja au hata mikono yako inaweza kumridhisha mwanaume afike Cli..x. Haya mambo wenzetu wa huku juu mbona wanayafahamu nashangaa hamna hata mtu mmoja hapa aliecomment. Pia kama hatojali na imani zenu zinaruhusu mpe blow job, meaning mdomo wako unaweza mfikisha. Hauwezi ukakaa unasubiri mpaka huko chini kupone au ujisikie kiafya kuna jinsi nyingi wandugu za kusaidiana/ kuridhishana km hauwezi kumpa kupitia chini sorry my language lakini hili somo linahitaji uwazi wandugu.

    ReplyDelete
  41. kama anahamu mpe ila kwa Condom, haina effect mwanakwetu.

    ReplyDelete
  42. Ajabu kwa TZ mada kama hizi watu ndio wapewe nini tena.Hata hivyo jambo hili lilipaswa kujadiliwa nanyi wawili ama baada ya kupata ushauri pahali husika na sio hadharani, Tunza siri yako na jamii ukustiri.
    Pole sana.

    ReplyDelete
  43. Heeeh heeeh heeeeeeeh, jamani hivi mama Teri siku hizi yuko wapi? Angemsaidia dada yetu. Pole dada, hukupitia kitchen party?
    Du mume wako mvumilivu, mi wakwangu nilimuonjesha baada ya wiki tatu then tukawa tunaonjeshana hadi ilipofika 40 days ndo tukajiburudisha maana sikutaka aonje nje harafu akomalie huko anisahau nilikuwa namsaidia hata before 3weeks. Halafu wanawake wa Africa wakishazaa tunawapenda sana watoto kuliko waume zetu. Kumbukeni kuna muda wa mtoto na wa baba yake. Si unajiachia akirudi unanukia maziwa na kucheua kwa mtoto hata kuoga hujaoga. Pendeza puliza pafium ile light ambayo haitamfanya mtoto kupata mafua. Then pata raha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...