Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu waumini waliohudhuria swala ya Iddi katika msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiswali swala ya Iddi katika msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni mapipa jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapa mkono wa Iddi baadhi ya waumini waliohudhuria swala ya Iddi katika msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam leo asubuhi(picha na Freddy Maro)



:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Ibrahim Lipumba, baada ya kumalizika kwa Swala ya Eid El-Fitr leo viwanja vya |Bustani ya Mnazi Moja jijini Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo

Imamu Mkuu wa Msikiti wa Manyema jijini Dar es Salaam, Sheikh  Masoud Mohamed Jongo,  akiswalisha jamaa katika  swala ya Eid El-Fitr iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Alhad Salum, wajumuika pamoja na waumini wa dini ya kiislamu kuswali swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Bro Michu mbona hutoi picha za kina mama waliosali Idd, tuma binti aingie kwa kinamama awapige picha mbona mnaleta ubaguzi vipi bro? Idd inasaliwa na kina baba tuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...