Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohd Shein akiwahutubia viongozi na wananchi mbalimbali hawapo pichani katika ukumbi wa salama Holl Bwawani zanzibar baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani.
 Naibu mufti wa Zanzibar Sheikh Swaleh Omar Kaabi akimkaribisha Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuhutubia katika Baraza la Idi ambalo lilifanyika  katika ukumbi wa Salama Holl Bwawani mjini Zanzibar.
 Umati katika Swala ya Iddi uwanja wa Maisara
 Baadhi ya kinamama waliohudhuria katika swala ya Idi Elfitri huko katika kiwanja cha Maisara mjini Zanzibar
 Rais wa Zanzibar Alhaji Dr,Ali Mohd Shein pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali  na wananchi,wakiwa katika swala ya iddi ambayo imeswaliwa kitaifa katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar Alhaji Dr,Ali Mohd Shein pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali  na wananchi,wakiwa katika swala ya iddi ambayo imeswaliwa kitaifa katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.
 Rais wa zanziba Dr Ali Mohd Shein akisalimiana na Rais Mstaafu Mh. Amani Abeid Karume  katika kiwanja cha Maisara mjini zanzibar kwa ajili ya kuswali swala ya Idi Elfitri.
 Makamo wa kwanza wa Rais Seif Sharif Hamadi akisalimiana na Waziri wa katiba  na Sheria wa Zanzibar Abubakari Khamis Bakari baada ya kuingia katika kiwanja cha maisara mjini zanzibar kwa ajili ya kuswali swala ya Idi Elfitri.
Rais mtaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume akisalimiana na Waziri wa katiba na sheria wa Zanzibar Abubakari khamis Bakari baada ya kuingia katika kiwanja cha maisara mjini zanzibar kwa ajili ya kuswali swala ya Idi Elfitri.
PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI MAELEZO ZANZIBAR

Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi M, Al Hajj Dk Ali Mohamed Shein amesema Serikali imeandaa mipango kuhakikisha inaongeza fursa zaidi za ajira rasmi na zisizo rasmi Visiwani Zanzibar.

Akihutubia Baraza la Eid-El-Fitri Mjini hapa jana, Dk Shein alisema katika mwaka wa Fedha 2011/2012 Serikali inatarajia kuajiri watu 2,476 kulingana na mahitaji na uwezo uliopo.

“Tunaelewa kuwa mahitaji ya fursa hizo ni makubwa zaidi…katika kukabiliana na uhaba wa fursa za ajira, Serikali inashajiisha wananchi kujiunga katika vikundi vya Ushirika ili waweze kunufaika” Alisema Rais Dk Shein.

Dk Shein alisema kuwa mkazo umewekwa katika kuvisaidia vikundi vya uzalishaji mali vinavyoanzishwa na vijana na wanawake ili waweze kujiajiri wenyewe wajiongezee kipato na kupambana na umaskini.

Akizungumzia mwezi mtukufu wa Ramadhan, Rais Dk Shein aliwakumbusha waumini wa Dini ya Kiislamu na wananchi wote nchini kuitumia elimu waliyoipata katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani kuimarisha mwenendo mwema na kujenga maisha bora ya duniani na akhera.

Dk Shein alisema suala la kudumisha amani, umoja na kuheshimiana miongoni mwa waislamu na wale wa dini nyengine kumewezesha kuendesha ibada hiyo katika hali ya amani na utulivu.

Alisema kwamba kuendeleza mwenendo mwema na kujiepusha na vishawishi vinavyoweza kuleta matatizo na kusisitiza suala la kujenga uadilifu hasa katika sehemu za kazi kwa wafanyakazi kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Sherehe hizo zilitanguliwa na swala ya Iddi iliyofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja na kuhudhuriwa na Makamu wa kwanza wa Rais, Seif Shariff Hamad, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd na viongozi wengine wa Serikali, Dini na Vyama vya siasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. WHEN I WE GOING TO SEE ALL MUSLIM AROUND THE WORLD CELEBRATING THIS DAY TOGETHER? THE WORLD IS CHANGED NOW COMPARING TO THE ERA OF 15-16 CENTURIES WHERE MEANS OF COMMUNICATION WAS NOT AVAILABLE!
    NOW THE WORLD HAVE ALL SORTS OF COMMUNICATION. FROM PHONES TO INTERNET, FROM TELEVISION TO TELEGRAPHS YOU NAME IT...BUT WE ARE STILL WITNESSING THIS DAY MUSLIM WORLD WHO SPENT THE WHOLE MONTH FASTING RAMADHAN TO WORSHIP ONE OF THE PILLARS, DIVIDED WHEN IT COMES TO CELEBRATE THIS PARTICULAR DAY?
    I WAS WATCHING ON TV MUSLIM OF MAKKAH MUKARAM WHERE EVERY MUSLIM WHO ARE ABLE TO GO THERE, THEY PRAYED EID ON TUESDAY!!! WHY DON'T THE MUSLIM COMMUNICATE WITH MUFTI OF MAKKAH-THE HEART OF ISLAM- THE HOLY PLACE OF ISLAM AND DECIDED THAT THE EID EL FITR IS TUESDAY!!!
    EID IS FIRST DAY OF NEW MONTH IN ISLAM CALLED- SHAWAL. SO TODAY OTHER MUSLIM ARE IN SECOND DAY OF THE MONTH. OTHERS LIKE HERE IN ZANZIBAR, IS FIRST DAY. WHEN DO THE MUSLIM WORLD ARE GOING TO CELEBRATE EID EL HAJJ WHILE THEY START SHAWAL MONTH ON DIFFERENT DAY?
    IS THERE ANY MUSLIM CAN HELP ME ON THIS? IF YOU GUYS ARE DEVIDED IN THIS DAY WHILE WE NON MUSLIM DON'T DIVIDE ON OUR HOLIDAYS LIKE X-MAS EASTER AND SO ON, HOW CAN YOU CONVINCE NON MUSLIM TO FOLLOW YOU AS THE ONLY AND TRUE RELIGION BROUGHT BY MUHAMMAD (SAW)?
    IT'S VERY CONTRADICTING, FRUSTRATING AND EVEN NOT KNOW WHO IS REAL DEAL HERE CAUSE I DON'T KNOW WHO IS REAL REAL MUSLIM IN THIS WORLD. IS IT MAKKAH AND MADINAH, OR PAKISTAN, IRAN, IRAQ AND AFRICA. OR MUSLIM OF EUROPE AND AMERICA WHO SOME OF THEM THEY FOLLOW MAKKAH. JUST SOME AND NOT ALL! IT'S SCANDALOUS!!!!
    ANY ANSWERS PLEASE! THANKS

    ReplyDelete
  2. IT SHOWS HOW SARCASTIC YOU ARE ...THAT'S THE ANSWER
    MDAU SAFARINI TRIPOLI

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza kabla hujatoa mcharuko fanya homework ya issue unayozungumza, hamuwezi kusali siku moja kwa kuwa dunia inazunguka, wachina wako mbele siku nzima na Tanzania, hata krismas tunasali siku tofauti wao wanaanza sisi tunafatia ndivyo hivyo mwezi huandama siku tofauti inategemea uko nchi gani, take a chill pill mdau dunia inazunguka jua au umesahau somo la sayansi? Idd Mubarak

    ReplyDelete
  4. Mdau wa kwanza ni kuwa dini ya kiislam ina taratibu zake. Moja katika hizo taratibu ni kuwa mwanzo na mwisho wa mwezi unatokana na kuonekana kwa mwezi angani kwa kutumia macho ya watu. Kwa kizungu tunaita "LUNAR MONTH". Waislam pia wanafata Quran na Hadith za mtume (SAW). Hakuna aya ya Quran wala Hadith ya Mtume (SAW) inayosema kuwa watu wote dunia nzima wafanye mawasiliano ili kujua nani kauona mwezi halafu wamfuate. Waislam wenye hekima wamekubaliana kuwa nchi zilizokuwa karibu wanaweza kufunga pamoja kama mojapo ya hiyo nchi imeona mwezi. Ndio maana watu wa Africa Mashariki wanavyofanya hivyo. Hii ni hekima tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...