Mmoja wa Viongozi wa Tume ya Taifa ya Unesco, ( wapili kushoto aliyesimama) akitoa maelezo juu ya matumizi ya vifaa vya kufundishia somo la sayansi kwa wanafunzi wa shule mbili za Msingi katika Manispaa ya Morogoro, zilizoingizwa kwenye mpango wa kuhamasisha wanafunzi hao kuvutiwa na masomo ya sayansi,( wapili kushoto walioketi) ni Katibu Mtendaji wa UNESCO , Profesa Elizabeth Kiondo.
Wanafunzi wa shule mbili za Msingi katika Manispaa ya Morogoro, Solomoni Mahlangu na Kigurunyembe ,ambazo zimeingizwa kwenye mpango wa mradi wa kuhamasisha wanafunzi hao kuvutiwa na masomo ya sayansi,wakiwa katika picha ya pamoja na nje ya ukumbi baada ya kuzinduliwa kwa mpango wa mradi wa kuhamasisha wanafunzi katika shule za Msingi kuvutiwa na masomo ya Sayansi , Mradi huo unasimamiwa na UNESCO na kuendeshwa katika Mikoa sita ya Tanzania, ambayo ni Zanzibar, Arusha, Kilimanjaaro, Pwani, Dar es Salaam na Morogoro
Baadhi ya wanafunzi wa shule mbili za Msingi katika Manispaa ya Morogoro, ambazo ni Solomoni Mahlangu na Kigurunyembe , zilizoingizwa kwenye mpango wa kuhamasisha wanafunzi hao kuvutiwa na masomo ya sayansi,wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi baada ya kuzinduliwa kwa mpango wa kuhamasisha wanafunzi katika shule za Msingi kuvutiwa na masomo ya Sayansi , Mradi huo unasimamiwa na UNESCO na kuendeshwa katika Mikoa sita ya Tanzania. Picha na John Nditi
Haya ndio mawazo mazuri ya kujitoa kwenye shida na umaskini ktk nyanja za teknologia,ila tuwaendeleze hawa vijana kwenye nafasi za kitaifa ili angalau waje kutusaidia baadaye.
ReplyDeleteWapewe kipaumbele na serikali kuu kwa gharama zozote.Tuige mifano ya nchi zilizoendelea,kwa mfano NASA wanawaandaa watoto from low level mpaka wanamaliza elimu ya juu.
Tuache kuwashirikisha wasomi na siasa, tunapoteza wataalamu wengi(vichwa).
Sasa nimeelewa kwa nini watu wanajazana mijini. Lini tutapeleka huduma vijijini?. Na hayo mashangingi ya DFP ni ya kutelezea taun tuu?. Tukumbuke wenzetu swekeni(!) tafadhali.
ReplyDelete