Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa akimnadi mgombea wa CCM jimbo la Igunga Dk. Dalaly Peter Kafumu kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM kwenye viwanja vya kumbukumbu ya sokoine mjini Igunga mkoani Tabora.
 Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa akihutubia mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Igunga, leo katika viwanja vya Kumbukumbu ya Sokoine mjini Ingunga.
 Katibu Muu wa CCM, Wilson Mukama akihutubia katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM kwenye viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga leo.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, mbunge wa Bunda, Steven Wasira akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM mkoani Tabora leo.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)  Pius Msekwa akizungumza katika mkutano huo
 Vijana waliohamasika wakirejesha kadi za CHADEMA kwa Mkapa baada ya kuhamasika kwenye mkutano huo.
 Orijino Komedi wakishambulia kujwaa wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM kwenye viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga mkoani Tabora leo.
 Msanii Ummy Wenslaus 'Dokii' akifanya vimbwanga vyake jukwaani wakati wa mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za CCM.
 Vijana wakiwa na ujumbe kukataa fujo Igunga.
Maelfu ya wananchi wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya Kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM leo.Picha na Bashir Nkoromo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. hii imetulia kumbe ccm bado kiboko sisi tupo kilimanjaro na arusha inavyoelekea hata shinyanga na mwanza ccm watatushinda

    ReplyDelete
  2. wako wapi hao wabishi.Sisi ni Wanyamwezi hatuhitaji fujo.Bahati yenu leo kun msiba wa Zanzibar

    ReplyDelete
  3. kazi nzuri tumeona tuko pamoja, na pamoja tutashinda. Ila Mtukumbuke na umeme na usafili.

    ReplyDelete
  4. TANZANIA NI SAWA NA SHILINGI YENYE UBAVU MIWILI-KICHWA NA MKIA-AMA KICHWA KUNA KAMPENI NA MISS TANZANIA ILA MKIA KUNA MSIBA NA HUZUNI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...