Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Ally Amour wakati alipofika kumjulia hali mtoto Said Gerald (6) aliyenusurika katika ajali ya Meli eneo la Nungwi usiku wa kuamkia leo, akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar. Aliyempakata ni mama yake mzazi, Mariam Hemed. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakiwa katika viwanja vya Hospitali ya Mnazi Mmoja, wakati alipofika kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Nungwi. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakimjulia hali mmoja kati ya majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Nungwi, Mussa Hemed, mkazi wa Wete Pemba, aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakimjulia hali mmoja kati ya majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Nungwi, Mussa Hemed, mkazi wa Wete Pemba, aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar. Baada ya hapo Makamu wa Rais alitembelea katika Viwanja vya Maisala na kutembelea shughuli za kiusaidia na kutambua maiti waliopatikana. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. http://www.tanzaniansingreece.org/apps/blog/ ukurasa maalum kuchangia kuhusu ajali ya meli

    ReplyDelete
  2. Ajali zikisha tokea ndiyo wanaenda kutoa pole wakati hizi ajali zinaweza zuilika. Michuzi, ukii toa hii usiitoe shauri yako lakini umeiona.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...