Na Mwandishi Wetu
UNAMFAHAMU muigizaji mkongwe anayekwenda kwa jina la ‘Mzee Kipara?” Kama jibu ni ndiyo basi soma habari hii.

Mzee Kipara ambaye jina lake halisi ni Saidi Fundi (pichani) hivi sasa anasumbuliwa na miguu kukosa nguvu, tatizo ambalo endapo atapelekwa hospitali pengine linaweza kupata nafuu kama si kupona kabisa.

Kampuni ya Global Publishers inayochapisha Magazeti ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda na Championi imempa simu ya mkononi msanii huyo mkongwe, ambayo itamsaidia katika mawasiliano na wasamaria wema ambao tunawaomba mumchangie kwa njia yoyote hasa ya M-Pesa.

Simu hiyo ilikabidhiwa kwa mzee huyo wiki iliyopita na mmoja wa wahariri wa magazeti yetu, Mohammed Kuyunga, Kigogo Mbuyuni jijini Dar anakoishi.

Kuyunga alisema kuwa kampuni imeguswa na hali aliyonayo Mzee Kipara hivyo kupitia simu hiyo inaamini watu wengi walioguswa na maradhi yake wataweza kumsaidia kwa hali na mali.

“Hii simu tumempa pamoja na laini yenye namba 0753 92 34 54 ambayo imeunganiswa na huduma ya M-Pesa ili kuwa rahisi kwa watu kuweza kumtumia fedha,” alisema Kuyunga.
N.B. Kutoa ni moyo na siyo utajiri, hivyo hima popote ulipo nchini, msaidie mzee huyu kwa kumtumia kiasi chochote utakachojaaliwa kwa njia ya M-PESA AU TIGO PESA, itamfikia mwenyewe moja kwa moja na unaweza kuongea nae kwanza. Elfu 2 utakayomtumia ina msaada mkubwa kwake na Mungu atakulipa - WEB MASTER.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. hongera GL,but ndio watamwibia hao ndugu zake mpaka basi uaminifu siku hizi zero,kwa sababu ye mwenyewe hawezi fuatilia,ni vizuri lakini utafutwe utaratibu mwingine wa uhakika zaidi ya huu.

    ReplyDelete
  2. I'm impressed with Global publishers kwa harakati hizi hii ndio maana ya ungwana sasa ndugu zanguni tufanye michakato ya kumsaidia huyu gwiji wa sanaa ya maigizo

    ReplyDelete
  3. Hivi najiuliza hawa Bongo movie kila siku nasikia wanacheza mpira wanaenda dodoma.. kwanini wasiandae hata mechi ya hisani kumsaidia huyu mzee?

    ReplyDelete
  4. impressed !!!watu wengine jamani !! sijui tuuite upambe,je ? unajua maana ya Global ?? jina kuuuubwa msaada ka simu kakichina !!! saa nyingine ni bora kutotoa kuliko kutoa, mzee anahitaji dawa the sooner possible,otherwise hako ka mfupa ka kichina,it will be too late.

    ReplyDelete
  5. kama kutoa si moyo wala utajiri,im sure global publisher can manage to take care this talented mzee...its amazing kuona jinsi mdau Erick Shigongo anavyo spend in politics and politicians millions of millions afu ati hili la mzee katoa simu kaunganisha na M-pesa..if the mzee was MP contituency,usingeamini...sie wenzie na mzee tunamwombea kwa mola...

    ReplyDelete
  6. Big up sana Global publishers mungu akubariki sana kwa kazi nzuri kama hizo,but wasani wenzake hawana moyo kama huo, coz wangeunga kwa mchango wa elfu 2 kila moja ,ingemsaidia sana huyu mzee kipara,ndo waanzilishi wa sanaa nnchini kipindi cha MAMABO HAYO,

    KANUMBA UKO WAPI/ EBU PIGA KAMAPENI YA HUYU MZEE WAKO NA UNGANA NA GLOBAL

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...