Bibi harusi Joyce Kiria akiwa amepozi huku akismile kwa furaha jioni ya leo mara baada ya kufunga ndoa,na hafla fupi imefanyika kwenye hoteli ya Atrium,Sinza jijini Dar.
Pichani shoto ni Bwana harusi Henry John Kileo na Mkewe Joyce Kiria wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungishwa ndoa jioni ya leo.
 Pichani kulia ni Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini (CHADEMA) Mh Godbless Lema na Mkewe ambao walikuwa ndiyo wapambe wa maharusi jioni ya leo.
 Maharusi wakikabidhiwa vyeti vyao ndoa jioni ya leo.
 Maharusi wakionyesha vyeti vyao vya ndoa mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani),jioni ya leo.
Pichani mkono wa kusho ni Mbunge wa jimbo la Ubungo (CHADEMA),Mh John Mnyika,Bibi harusi pamoja na mdau wakiwa wamepozi kwa picha jioni ya leo.
 Mwenyekiti wa kambi ya Upinzani kupitia chama cha CHADEMA,na Mbunge wa jimbo la Hai,Mh Freeman Mbowe akisalimia na bibi harusi jioni ya leo mara baada ya kufunga ndoa na mumewe Henry John Kileo.
  Maharusi wakiwa wamepozi na wadau jioni ya leo.
 Bwana harusi Henry Joseph akila kiapo cha ndoa,mbele ya wageni waalkwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo iliofanyika kwenye hoteli ya Atrium,Sinza jijini Dar,kulia kwake ni Bi harusi Joyce Kiria akisikiliza kiapo hicho kwa makini.
Bibi Harusi Joyce Kiria akila kiapo cha ndoa jioni ya leo.
Pichani juu na chini ni  Maharusi wakivalishana pete ya ndoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. hii nimeipenda sana , arusi imekaa ki chadema chadema , especial hizo suti zao kali sna , naomba kuuliza huyu bwana harusi ni nani , namuona kwenye maandamano ya chadema sana akiwa mbele. jamaa anaonekana upo cool sana, mke katulia kwa kweli inavutia hii.

    mdau china

    ReplyDelete
  2. Ako michuzi naomba kukuambia siri moja, watu wengi walikuwa wanapenda sana ku visit hii blog yako kwa sababu ya freedom ya comments za watu , ambazo nyingi zinaweza hata kututoa stress after along day at work. hila sikuizi una bana sana. tunakuomba uturudishie utamu wetu anko

    mdau uk

    ReplyDelete
  3. Duuh bwana harusi kweli ni mwana CHADEMA. Naona yuko ndani ya gwandaz!

    I wish you guys all the best! Bado Zitto. Hivi Mnyika umeshaoa?

    ReplyDelete
  4. Harusi imependeza sana. Simple na Clear hakuna cha makeke wala nini. Safi sana. Ila Mnyika na wewe Magwandaz hadi kwenye Harusi?

    ReplyDelete
  5. nakubaliana na mdau wa pili hapo juu michuzi mmeanza kuboa sasa hivi cos kila coment ambayo inacritisaizi nyie hamuiweki yaani mnataka sisi tujifanye tunapenda kila kitu kinachowekwa hata kama ni cha kizushi sisi sio wanafik bana michuzi hilo lazima ulijue tunaweka mawazo yetu kutokana na reality ya kitu kwa hio kama mtu kaleta coment anaponda may be we ziweke as long as hazina matusi makubwa ambayo hayakubaliki kwa jamiii mimi mwenyewe niliisha weka coment ya kucritisaizi na hakukuwa na matusi ila haikuwekwa sasa hio inakua sio fair man hata kama unadelegate hii kazi vijana wako plse waambie waache kutunyima utamu wa waosha vinywa

    ReplyDelete
  6. michuzi anaboa sana tuuuuu, nshamwambia hasikii anavimba kichwa na vodacom tuuuu.
    anyway...hiiii style nimeipenda pamoja iko kiitikadi ila nina uhakika kwenye kukata ndovu watu wote walikuwa pamoja. biashara ya michango na matarumbeta noma sana these dayz jamaa. mnyika kupiga gwanda ...labda ni kuonesha yuko serious 100% na chadema. huyo zitto tutampandisha kwa shehe very soon kumrasimisha maana habari zake tunazo.
    michuzi you may wish to trash my comments mazee maana ndo zako

    ReplyDelete
  7. Duh kwani walitoka kwenye mando mando (maandamano kwa kiswahili cha kidosi) Magwanda hadi harusini lakini nisitie neno kwa hata Fulanazz inatingaga kwenye harusi vile vile

    ReplyDelete
  8. wao my sister Joyce Kiria umependeza balaa.na hongera sana kwa hatua iyo jamani hongera pia kuwa mama natumai mwanao ata-enjoy sana kwani ana mama shujaa(super women) + baba ake if upo chadema atakuwa upo safii.hongereni sana.

    ReplyDelete
  9. HARUSI MBONA IPO KICHAMA SANA JAMANI NAONA HAIPENDEZI SANA KUWA HIVI MANA SIE WA CCJ TULISHINDWA KWENDA JAPO TULIALIKWA. ITS THE WEDDING DAY AND PEOPLE WOULD DRESS ANY HOW BUT NOT IN POLITICAL DRESSING CODE PLEASE. BY THE WAY IT WAS SIMPLE ILA SIJAELEWA HAPA NI KISERIKALI AU KIDINI ZAIDI. BRIDE ANG GROOM BE BLESSED ALLWAYS.

    ReplyDelete
  10. Sio Mnyika tu wote wamepiga magwanda ya CHADEMA tu. kweli hii Harusi ni ya siasa lakini wamefungia/wamefungishwa kwa Mkuu wa Wilaya - WA CCM.

    ReplyDelete
  11. yees Hii imefunfungishwa na Mwanaserikali wa Serikali ya Chama Tawala...so hakuna uchama hapo.
    Ila hili vazi la chadema naona ni zaidi ya itikadi. Mbona liko chicha tuu likipigwa rangi tofauti na ile ya khaki...
    Mimi nimeikubali hii. Hawa ni makamanda naomba nipate data za namna ya kulipata hilo vazi

    ReplyDelete
  12. Ni kweli michuzi nowadays unatubania hata wale walikuwa wakiandika kuchekesha watu huwapi nafasi mi mwenyewe nimeweka comm. few days ago hujaweka ni vema kukubali kuwa kuna upinzani kila kona and not everyone will accept what you want.Now kaka zangu wa kichaga mmependeza but imekuwa kichadema chadema too much is good to look different but is much better kuwepo na mambo ya chama kama chama na after there mue na nguo zenu za kawaida. Naipenda sana chadema but inanifanyaga nijiulize nitavaa lini nguo zangu maana wakati wote na uniform. Kubalini kuwa tunawapenda na kura zetu mtazipata hasa huku kilimanjaro. Bibi harusi umelook mwwwaaaah. Wachaga wanasura nzuri hasa wale point five.

    ReplyDelete
  13. Mbona bi harusi hajavaa gwanda ubaguzi huu jamani

    ReplyDelete
  14. Actually wthr iko kichama au sio, i dont care ila hawa watu wameonyesha mfano sana, simple wedding and attractve. Kiria mama, Hongera. Hakika chadema ni wabana matumizi, kumbe hadi katika mambo yanayowahusu, big up aisee. Ingekuwa Chama hapoo, Dooooooh, hadi misafara, sipati picha ingekuwaje. Big up wanandoa. Be Blessed.

    ReplyDelete
  15. wachaga bhana,unatia mimba kwanza ndo unaawowa....kabaaaaaaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...