Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad wakiwa ni wenye huzuni sana wakati walifika eneo la tukio la ajali ya meli ya Spice Islander, iliyozama katika bahari ya Nungwi mkoa wa kaskazini Unguja.
Baadhi ya wanajeshi wa vikosi mbali mbali vya ulinzi wakibeba majeruhi walionusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv Spice Islander,katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja usiku wa kuamkia leo.
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha jeshi la polisi (FFU) pamoja na wnaharakati wengine wa uokozi wakibeba majeruhi aliyenusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv SpiceIslander,katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja usiku wa kuamkia leo.
Baadhi ya wanajeshi wa vikosi mbali mbali vya ulinzi wakibeba majeruhi Marium Mohamed Muradi (29) kutoka Tanga,aliyenusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv SpiceIslander,katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja usiku wa kuamkia leo.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR, MHE. BALOZI SEIF ALI IDDI AKIONGOZWA NA NAIBU KADHI MKUU WA ZANZIBAR SHEKHE KHAMIS HAJI KHAMIS WAKITOKA NDANI YA HEMA MAALUM LILILOJENGWA KATIKA VIWANJA VYA MAISARA KWA AJILI YA KUPOKELEA MAITI ZA AJARI YA MV.SPICE ISLANDERS ILIYOKUWA IKITOKEA UNGUJA KWENDA PEMBA USIKU WA KUAMKIA LEO.
BALOZI SEIF ALI IDDI AKITOA MAELEKEZO JUU YA UTARATIWA WA KUFUATWA KWA WATU WATAKAOKUJA KUANGALIA MAITI ZAO NDANI YA HEMA, HADI MUDA HUU TAYARI MAITI MBILI ZIMESHA HIFADHIWA NDANI YA HEMA ILO TAYARI KWA KUTAMBULIWA KATIKA MAANDALIZI HAYO IDARA YA MAAFA WAKISHIRIKIANA NA OFISI YA MUFTI WA ZANZIBAR WATAZIHUDUMIA MAITI ZOTE KWA KUZIKOSHA,KUZIVIKA SANDA NA KUZIKA
WATU WALIOJAZANA KUANZIA UWANJA WA MAISARA HADI HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA WAKISUBIRI KUWATAMBUA MAITI ZAO,KARIBU MATAYARISHO YOTE YANAYO STAIKI KUFANYIWA MAITI YAMEKAMILIKA KINACHOSUBILIWA NI UPOKEAJI WA MAITI, TAYARI WATU WASIOPUNGUA 300 WAMEOKOLEWA WAKIWA WAZIMA WENGI WAO NI WATOTO NA KINAMAMA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Poleni wafiwa na pia sote watanzania kwa ujumla. Hali inatisha

    ReplyDelete
  2. Thanks ankala kwa kutupa updates.

    ReplyDelete
  3. Poleni sana mlofiwa na ndugu zenu. Mola awape nguvu katika kipindi hiki cha maombolezo.

    ReplyDelete
  4. Inna lillahi wa inna ilayhi rrajiun.

    Ni kweli siku ya mtu ikifika ni lazima aondoke duniani lakini huu ni uzembe wa hali ya juu uliofanyika.

    Tafadhali wahusika wachukuliwe hatua inayofaa.

    ReplyDelete
  5. pole kwa msiba.Mwenyewe Mungu awalaze marehemu wote mahali penma na awape nguvu wafiwa wote na waliojereheliwa kwa kipendi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  6. INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUUN
    Mola aziweke roho za marehemu pahali pema peponi milele.
    Yaa allah wapesubra wafiwa wote na wananchi kwa jumla "Amin".

    Hata hivyo hatuwa muhimu za kinidhamu kwa wazembe na wapenda pesa kuliko roho za wanaadamu wenzao kuchukuliwa pamoja na kuwajibika uongozi mzima wa bandari ya Zanzibar wenye dhamana ya navigation control na zaidi port master na wenzake wote.

    vilevile chombo muhimu cha ukaguzi wa vyombo vya usafiri baharini yaoneka hakikuwajibika ama hakipo kabisa kwani wao ndio nyenzo muhimu ya kuhakikisha ubora wa vyombo hivyo unafikiwa na kusimamiwa "SMZ zinduka hakuna kulala" lazima mujiandae kikamilifu kuepusha ajali kama hizi zenye kulete msiba Mkubwa na upotevu wa mali.
    Kweli ajali haiepukiki lakini kinga bora kuliko...
    Inawezaka tuwajibike

    Mdau niliyeguswa sana

    ReplyDelete
  7. poleni sana. Nawaonea huruma kweli.

    ReplyDelete
  8. tumepowa nimefurahi kuona lambilambi kutoka kwa nduguzetu watanzania bara asanteni mungu akupeni imani

    ReplyDelete
  9. theresia gama anasema:
    poleni sana wapendwa,mungu awajalie nguvu na matumaini katika hili tatizo tupo pamoja.

    ReplyDelete
  10. meshack mtweveSeptember 13, 2011

    inasikitisha sana ila ndo maisha safari yetu sote ni hiyo mola atujaaliye kutenda mema siku za maisha yetu amen

    ReplyDelete
  11. SUBHANNALLAHH..YANI HII MELI INASEMEKANA IMETENGEZWA UGIRIKI MWAKA 1967,NA IMETUMIKA NJE YA NCHI NA IMENUNULIWA NA KUJA NCHINI MWAKA 2005.MIAKA 44 HIVI SASA UMRI WAKE..DAAH YAANI SERIAKLAI INAPIGA MARFUKU MAGARI CHAKAVU KUINGIA NCHINI NAKUCANCEL BAADHI YA MAJUMBA YALIOKUWA YANAHATARISHA MAISHA YA WATU NA KUITA MAGARI CHAKAVU KUMBEHUKU KUNA VYOMBO VYA USAFIRI WA BAHARINI NA ANGA OLD MDEL ZAIDI NA HATARI ZAIDI..HIZO MELI ZA MV MAPINDUZI NA MV MAENDLEO ZILIZCANCELIWA NA SERIKALI BASI ZIMETENGENEZWA KATIKA MIAKA YA KATI 70..NA ZIMEPITWA NA WAKATI NA KUCANCELIWA..LEO VIPI BOTI ILIOKUWA YA ZAMANI KAMA HIVI NA CHAKAVU INARUHUSIWA BADO KUTOA HUDUMA NA KUCHUKUWA ABIRIA? WANANCHI NA SERIKALI LAZIMA TUKIO HILI LITUFUMBUWE MACHO NA KUCHUKUA SOMO,ILIOPITA NDIO YAMESHTAOKEA LKN HILI NI FUNZO LAZIMA SERIKALI IAMKE,IANGALIE TENA MELI NA BOTI NA HATA NDEGE NA VYOMBO VYA USAFIRI VYOTE VILIVYOPO NCHINI AMBAVYO BADO VINANENDLEA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI AU MIZIGO..VILIOYOKUWA VYA ZAMANI NA VIPO KATIKA HALI MBAYA VISISMAMISHWE NA VINAVYOTAKA MATENGEZO YA LAZIMA VITENGENEZWE..NA ISIRUHUSU KUANZIA SASA KWA MASHIRIKA BINAFSI KUINGIZA NCHINI VYOMBO VYA USAFIRI VILIVYOPITWA NA WAKATI KAMA INAVYOPIGA MARUFUKU KUINGIZA MAGARI YA ZAMANI NA MACHAKAVU,BASI HATARI VYYA VYOMBO VYA BAHARINI NA ANGANI NI ZAIDI,,HAPA NI LAIZMA TUTOKE NA MAFUNZO MENGI SANA KATIKA AJALI HII ILI KOSA LISITOKEE TENA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...