Habari zinasema meli ya Sea Bus imekwama katika  bahari ya Hindi wakati ikitokea  Pemba.  Imekwama katika eneo hilo kwa zaidi ya masaa manne sasa.Habari kutoka eneo la tukio zinadai kuwa kukwama kwa meli hiyo kumesababishwa na injini ya meli hiyo kuzimika ghafla katika eneo hilo ambalo ni eneo lenye mkondo mkali na kina kirefu zaidi wa bahari.Baadhi ya abiria waliozungumza wamedai kuwa hadi sasa hali ya taharuki imeendelea kujitokeza katika meli hiyo huku mawimbi makali yakendelea kuipiga meli hiyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hivi MV Mapinduzi ipo wapi? Maana naona sasa tunaleteana ujinga kila siku.

    ReplyDelete
  2. Ankal, tafadhali fuatilia mtafaruku huu kwa ukaribu sana na utupe updates kila baada ya muda mfupi. Otherwise ninawaombea kwa Mungu muweze kulitatua tatizo hili na mmalizie safari yenu kwa usalama kabisa.

    Lakini pia, masaa manne ni mengi sana, hao abiria walipaswa wawe wamekwishaondolewa kwenye hiyo meli muda mwingi uliopita. Wahusika wanasubiri nini kuwaokoa abiria, au hadi boti ibinuke?????????!!!!!! Aaaghhhh, kwa kweli!!!!

    ReplyDelete
  3. Here we go again.

    ReplyDelete
  4. Ee Mungu mwingi wa rehema tunakuangukia utuepushe na majanga mengine katika kipindi hichi kigumu.

    Leo hii boti imezama ilikuwa inatokea Tanga kwenda Pemba, na sasa ndiyo boti hiyo imekwama kwenye mkondo mkali wa Nungwi.

    ReplyDelete
  5. kunani huko pemba naona wamekasirika sana hakiendi kitu bila kuwa na misukosuko??!!!!

    ReplyDelete
  6. Hiyo inaweza kuwa janja ya wenye Meli ili wenzao walipata ajali juzi wasionekane walikuwa wamezidisha abiria na mizigo. Hao wanantaka iaminike kwamba eneo hilo ndio chimbuko la matatizo. Hata hivyo kufa kwa injini hakuwezi kuakafanya meli izame kama haikuwa na mzigo ulioizidia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...