Rais Jakaya kikwete akiwa na Rais wa SMZ Dr Ali Mohamed Shein  wakiaangalia miili ya watoto  mjini Zanzibar leo hii. 


NI KIKAO ALICHO KITAYARISHA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR MHE BALOZI SEIF ALI IDDI KWA VIONGOZI WA SERIKALI WALIOKUWEPO KISIWANI PEMBA CHENYE LENGO LA KUWEKA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA UPOKEAJI WA WAHANGA WA AJALI YA MELI YA MV SPICE ISLANDERS, KATIKA HICHO WAMEKUBALIANA KUWEKA VITUO VYA DHARULA KATIKA MAENEO YA MKOANI,CHAKE NA WETE ILI KUPOKEA WATU WALIOPATWA NA MAAFA HAYO KWA KUWAPATIA HUDUMA.
 Baadhi ya abiria 525 waliookolewa kutoka katika Meli iliozama huko katika mkondo wa Nungwi Zanzibar wakiwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja mjini Zanzibar
 Watoto waliookolewa kutoka ktika Meli iliozama ya Spici huko katika mkondo wa Nungwi zanzibar wakiwa katika Hospitali ya mnazi mmoja kabla ya kuruhusiwa kurudi nyumbani.
 Umati wa watu wakiwa katika Hospitali ya mnazi mmoja kupata taarifa za watu wao kuhusiana na kuzama kwa meli ya Spice Islanders huko katika mkondo wa Nungwi
 Vikosi vya Ulinzi na Usalama ni miongoni mwa Taasisi zilizokuwa mstari wa mbele katika harakati za uokoaji na usafirishaji wa maiti zilizopatikana kutoka katika meli iliozama ya spici iliokuwa ikielekea Pemba, kama wanavyoonekana katika picha.
  Mmoja kati ya waokozi akiwa katika hali ya majonzi baada ya kuchukuwammoja kati ya maiti zilizoletwa bandarini zanzibar na chombo cha bawe kutoka katika meli iliozama huko katika mkondo wa Nungwi.

 Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akibadilishana mawazo na Naibu kadhi wa Zanzibar kutokana na msiba mkubwa uliotokea zanzibar jana.
 Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akizungumza na Madaktari huko katika viwanja vya maisara mjini Zanzibar kuhusiana na Msiba mkubwa ulolikumba taifa letu la kuzama kwa meli ya Spici huko katika mkondo wa Nungwi kaskazini unguja.

Madaktari,Wauguzi na watu mbalimbali wakipokea maiti ya kwanza iliofikishwa huko katika viwanja vya  Maisara kutoka katika meli ya spici iliozama hapo jana huko katika mkondo wa Nungwi. PICHA ZOTE NA HAMAD HIJA-MAELEZO ZANZIBAR



Na Hamad Hija Maelezo zanzibar

MAMIA ya wananchi wakiwemo viongozi wakuu walimiminika katika viwanja vya Maisara na Hospital ya Mnazi mmoja pamoja na bandari kuu ya zanzibar ili kwenda kuona na watambuwa watoto wao wazee wao  ambao walikuwepo katika meli iliyopata ajali huko Nungwi ikielekea kisiwani Pemba hapo jana

Waliomiminika katika sehemu hizo kutoka sehemu mbali mbali za Unguja kunafuatia habari zilizoanza kutangazwa jana katika vyombo mbali mbali vya habari kwamba chombo cha Spice kimezama na ni kwamba kilikuwa kimechukuwa abiria kikielekea Pemba

Kwa mujibu wa habari zilizokuwa zikisimuliwa na baadhi ya wananchi waliofika hapo maisara wamesema kuwa suala kubwa lililochangia kutokea ajali hiyo ni kuwa vyombo vimechoka sana na wengine wamesema kuwa kujaa sana kwa chombo hicho hapo jana pia ni sababu ambazo zilichangia tukio hilo

Katika Viwaja vya Maisara umati wa watu ulikuwa umejaa kupita kiasi halikadhalika hata Hospital ya Mnazi mmoja umati ulikuwa umejaa vikle vile lengo kubwa la kuwepo hapo ni kuona na kuwatambua vijana wao ambao wameruhiwa na ambao wanapata matibabu

Halikadhalika umati mkubwa ulikuwa umejazana sana katika bandari mkuu ya Zanzibar ambapo maiti na majeruhi wa ajali hiyo walikuwa wakifikia hapo kutoka sehemu ya tokeo

Kufuatia ajali hii hiiitakuwa mara ya pili katika pindi cha nyuma meli yam v Fathi ilizama ambapo watu kadhaa wafariki dunia na baadhi ya mizigo ilpotea kutokana na ajali hiyo iliyotokea hapo nyuma

Kufuatia tokeo hilo wananchi wa zanzibar leo walikuwa wamejikusanya vikundi kila sehemu kuzungumzia tukio hili ambalo limetoke hapo jana likiwa limeacha majonzi makubwa kutokana na msiba huo uliotokea hapa zanzibar






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Inna LiLLAH Wa InnaILLAihi Rrajiun,Habari ya ajali ya meli imenistusha na kunihuzunisha, my heartfelt condolences goes to all the families who have lost their loved ones.ni vizuri kuona viongozi walivyofika kushughulikia zoezi la uokoaji lakini, serikali inabidi ichukue hatua kali kwa wale wote waliohusika kwenye janga hili. Kwa kuanza na waziri anayeshughulikia usagirishaji wa vyombo vya baharini, wamiliki wa vyombo,captain kama yuko hai. Waziri alitakiwa kuweka mikakati madhubuti ili kuepusha janga kama hili kama vile kuwa na maofisa wa usalama bandarini watakayeangalia kila chombo kabla hakijaondoka kuona abiria hawaja jaa kupita idadi inayoruhusiwa kihalali. Mmiliki nae alitakiwa kuajiri watu ambao ni madhubuti kuangalia namba ya abiria inazingatiwa na captain alitakiwa kutoondoa meli bandarini mpaka idadi ya watu imepunguzwa. Tumechoshwa na vifo vya watu ambavyo vinaweza kuzuilika japo watu wa imani watasema ni
    Mipango ya mungu lakini inabidi kuangalia na kuweka mikakati itakayoepusha ajali kama hii na kama ajali itatokea itakua ni juu ya nje ya uwezo wa binadamu.

    Msiba mkubwa na namuomba mola muumba awape wafiwa wote nguvu katika wakati huu mgumu na awasamehe marehemu makosa yao. Ameen!!

    Mohammed

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...