Na Boniface Wambura, 
Marrakech,
Tanzania (Taifa Stars) imefungwa mabao 3-1 na Morocco katika mechi ya mchujo kuwania tiketi ya AFCON 2012 iliyochezwa leo hapa Grand Stadium na kushuhudia na maelfu ya watazamaji kwenye uwanja huo wenye viti 43,000. Hadi mapumziko matokeo yalikuwa sare ya bao 1-1.
Wenyeji Morocco ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 19 mfungaji akiwa Marouane Chamakh kwa mpira wa kichwa ambao ulidunda kabla ya kumpita kipa Juma Kaseja wa Taifa Stars. Abdi Kassim aliisawazishia Stars dakika ya 40 kwa shuti la nguvu- umbali wa meta 35 lililomshinda kipa Nadir Lamyaghri kufuatia pasi ya Idrisa Rajab.
Mabao mengine ya Morocco ambayo imepata tiketi ya kucheza fainali za AFCON zitakazochezwa mwakani katika nchi za Equatorial Guinea na Gabon yalifungwa dakika ya 68 na Adel Taarabt. Mbark alifuta matumaini ya Stars kupata sare katika mechi hiyo kwa bao lake la tatu alilifunga dakika ya 90 kwa shuti la chini akiwa ndani ya eneo la hatari.
Mwamuzi Bakary Gassema kutoka Gambia aliwaonya kwa kadi za njano Idrisa Rajab, Juma Nyoso, Dan Mrwanda na Mohamed Rajab wa Stars wakati kwa upande wa Morocoo aliyeoneshwa kadi ya njano alikuwa nahodha wa timu hiyo Houcine Kharja.
Akizungumza baada ya pambano hilo, Kocha wa Taifa Stars, Jan Poulsen aliwataka wachezaji wake wasikate tamaa kutokana na matokeo hayo kwa vile walicheza na timu bora kuliko wao. Alisema hivi sasa wanatakiwa kuelekeza akili kwenye mechi mbili zilizo mbele yao dhidi ya Chad. Mechi hizo za mchujo kwa ajili ya kuingia hatua ya makundi ya mchujo Kanda ya Afrika kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil mwaka 2014 zitachezwa Novemba 11 mwaka huu jijini Ndjamena na Novemba 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni/Nassoro Cholo, Idrisa Rajab, Juma Nyoso, Aggrey Morris, Shabani Nditi, Dan Mrwanda, Henry Joseph, Mbwana Samata/John Bocco, Abdi Kassim na Mohamed Rajab/Mrisho Ngasa.
Morocco; Nadir Lamyaghri, Michael Basser, Abdelhamid El Kaoutari, Badri El Kaddouri, Mehdi Benatia, Younes Belhanda, Houcine Kharja, Mbark Boussoufa, Adel Taarabt/Youssef El Arabi, Marouane Chamakh/Said Fettah na Oussama Assaidi/Karim Al Ahmadi.
Taifa Stars inatarajiwa kurejea Dar es Salaam saa 2.30 asubuhi Oktoba 11 mwaka huu kwa ndege ya Qatar Airways

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Ashakum si matusi,sijawahi kuona timu ya taifa mbovu ya TZ kama timu hii,na kocha anasema msivunjike moyo,waandhi wa habari wanasema Taifa Stars wamejitahidi,wamejitahidi na nini.Hakuna hata pasi moja ilyokamilika mchezo mzima zaidi ya kufanya faul zisizokuwa na maana na kusababisha free kick za hatari golini,kweli Tz tume-drop ki-football lakini hii too much.

    ReplyDelete
  2. Hakuna kipa hapo mtakula kichapo sana, mpaka mlijue hilo.

    ReplyDelete
  3. Nimeangalia mpira na vijana wamejitahidi hasa Kaseja ameokoa mipira mingi ambayo ingekuwa magori. Tunahitaji kutafuta mkoba (5) iliyotulia wa kucommand defence nzima, vinginevyo namba nne na tano wote wanacheza kama nne!!!!

    ReplyDelete
  4. Kama kawaida yetu,kichwa cha mwenda wazimu!!

    ReplyDelete
  5. Maximo vs Poulsen nani zaidi?

    ReplyDelete
  6. nasikia Mh. Pinda kaenda kumfuata Maximo Brasil.

    ReplyDelete
  7. kichwa cha mwenda wazimu!!

    ReplyDelete
  8. Tujitoe kimataifa hata kwa hata kwa miaka mitano hv, tupumzike na vipigo hv !

    ReplyDelete
  9. Kwa Kawaida Timu Bora pekee ndizo zafuzu katika michuano yoyote ile, Hivyo basi Ili Tanzania iweze kufuzu siku moja ni lazima nayo iwe Bora na siyo kujitahidi kama kawaida yetu,kwakuwa ilicheza,sasa katika michuano kuna Timu kama Senegal,Ivery Coast,Cameroon,Ghana,Nigeria,Burkina Faso,n.k tungewaweza?.
    Sasa hatakama tukifuzu hilo kombe la Dunia kwa miujiza si tutatia haibu, maana Tutapata kundi gani sijui; Ukizingatia makundi yanagawanywa kwa mabara na Ubora wa timu,just imagine tu tuna fuzu siku moja na kuwa kundi moja na Ujerumani,Japan, Mexico situtaondoka na kapu? , Mpira siyo ndoto za abunuasi ndugu zangu tusilewe sifa tukubali kukosolewa.Unakuta Mchezaji anamiaka 23 lakini anacheza ligi kuu miaka kumi tayari, Taifa zima linajua kama niuonga lakini Hakuna kitu kinachofanyika, sasa kila siku tunajidanganya wenyewe na bado hatufanikiwi.

    ReplyDelete
  10. halafu mnashangaa tunaposhabikia man uu, sasa kama timu inakupa raha badala ya majonzi kwa nini usiipende??? walah naipenda manchester mnoo acheni tu hata siui kama bongokuna timu mie na man u tuu!

    ReplyDelete
  11. Kwa kweli Taifa Stars wamejitahidi. Msisahau kuwa timu ya Morocco ina wachezaji sita wa kulipwa wanaocheza katika ligi za Ulaya. Ufumbuzi ni kuwa na 'academies' katika kila mkoa ili kuwaendeleza watoto wenye kipaji.

    ReplyDelete
  12. Mnafungwa hata na wazenji ambao kila siku pesa za FIFA zikija mnaztumia peke yenu na wao hawana msaada wowote.

    ReplyDelete
  13. Kama nilivyo sema biriani na nyama choma haviendani na football kabsaaaaaaa,sasa sijui kwanini mnailaumu serekali na huyo kocha wawatu? Haiwezekani hao wachezaji wale wali na nyama choma halafu eti wakacheze kabumbu yani ni mission impossible . Wakulaumiwa ni hao hao wachezaji sio serekali . Kwani serekali ni nini? si ni mimi na wewe na yule na wale na sisi wote na nyinyi wote sasa lawama za nini kwa serekali? Mdau toka bujumbura

    ReplyDelete
  14. hii inaitwa timu ya Tanganyika na mtaendelea kufungwa mpaka mumtafute aliyekurogeni Shabash

    ReplyDelete
  15. chamsingi hapa bana wala tusihangaike na timu hii jamani wachezaji wetu wazee sana ,na hawajui mpira kabisa kujirekebisha walishakuwa hawawezi tena.age goo sana ,cha msingi kwanza tupumzike kama miaka 3 tufanye mambo mengine bana sio kila siku wanasababisha gharama zisizo za msingi!! .unaniambia moroko timu kubwa kwa hiyo unaniambia sie tunatakiwa kuwa na timu zipi sasa ili tuweze kucheza nazo tuwaambie FIFA basi watutafutie timu hizo!!.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...