Familia ya Bw Alhaj Abdul Risasi wa Kawe jijini Dar es Salaam inatangaza kupotelewa na mtoto wao Hussein Risasi (15) anayesoma shule ya Msingi Olympio iliyopo Upanga Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Alhaj Risasi ni kwamba Hussein alitoweka nyumbani kwao Kawe jijini Dar es Salaam Ocktoba 25 mwaka huu mara baada ya kurejea akitokea shuleni.
Kabla ya tukio hilo Hussein alianza utoro wa kwenda shule kwa madai kwamba amekuwa haelewi anachofundishwa na walimu wake na kwamba wanafunzi wenzake wamekuwa wakimcheka kitendo ambacho hakukipenda.
Akifafanua  zaidi Alhaj Risasi amesema kuwa, kutokana na tabia hiyo ya utoro aliyoianza Hussein ambaye ni pacha na Hassan Risasi anayesoma Nairobi, alimwita na kumkanya kutokana na vitendo hivyo.
Hussein amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya athma tangu utoto wake jambo linaloathiri pia afya yake mara kwa mara.
Kwa yeyote atakayemuona anaombwa kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi nchini au kupitia namba za simu 0715  611 277, 0713  314  442  au 0787 377 822.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jamani poleni sana. Mapacha huwa hawatenganishwi kutokana na kuwa wana vitu vingi ambavyo wanashirikiana na unapowatenga uwezo wa mmoja unashuka na kufanya awe mpweke. Mimi ni pacha nimeoa na mwenzangu ameoa ila baadhi ya mambo mengi tunapanga wenyewe na kushauriana wenyewe kabla hata wake zetu hawajajua na mara nyingi hata kama ni jambo dogo tu hatuwezi kufanya mmoja kwa ufasaha.
    Mi naomba muulizeni pacha yake kwanza kwa makini pasipo kumtishia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...