Meneja Masoko wa TBL,Fimbo Buttallah akitoa ufafanuzi juu ya Tamasha la mitindo la Redd’s Uni-Fashion Bash litakalowakutanisha wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu katika mikoa ya Dar,Dodoma,Moshi na Mwanza.kushoto ni Meneja wa kinywaji cha Redd’s Original,Vicky Kimaro.
Meneja wa kinywaji cha Redd’s Original,Vicky Kimaro (katikati) akionyesha fomu ya kujiunga kwa washiriki  wa Tamasha hilo.kulia ni Meneja Masoko wa TBL,Fimbo Buttallah na kulia ni Meneja Uhusiano wa TBL,Edith Mushi.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original leo imezindua tamasha la aina yake la mitindo kwa vyuo vya elimu ya juu. Tamasha hili litakalojulikana kama “Redd’s Uni-Fashion Bash” kwa mwaka huu litaanza mwezi huu wa Octoba hadi Novemba na kushirikisha vyuo vyote vya elimu ya juu vilivyo katika mikoa minne ambayo ni Dar Es Salaam, Kilimanjaro, Dodoma na Mwanza.

Akizungumza katika uzinduzi huo, meneja wa Kinywaji cha Redd’s Bi Victoria Kimaro alisema; “Tamasha hili la mitindo lina lengo la kuinua vipaji vya wanafunzi wa vyuo katika tasnia ya mitindo kupitia maonesho yatakayofanywa katika vyuo, ambapo wanafunzi wenye vipaji vya ubunifu watapata fursa ya kuonesha ubunifu wao wa mitindo. Hii ni fursa kubwa kwao kujitangaza na kudhihirisha uwezo wao.”

Bi Kimaro, pia alielezea utaratibu wote wa kuwapata wabunifu watakaoonesha kazi zao jukwaani wakati wa matamasha haya ya aina yake kwa kusema; “Uzinduzi huu utafuatiwa na usajili wa wanafunzi wabunifu na wanamitindo kupitia fomu maalum zitakazosambazwa vyuoni, kisha majaji watachambua fomu zote zilizowasilishwa na kupata wabunifu 10 katika kila mkoa watakaokidhi vigezo, ambao watapata fursa ya kuonesha mavazi yao siku ya tamasha, pia kutakuwa na nafasi 10 kwa wanamitindo watakaovaa mavazi hayo jukwaani. 

Majaji wataangalia vigezo na kupata washindi ambao watapata zawadi toka kwa kinywaji cha Redd’s Original.”

Akizungumzia zawadi kwa washindi, meneja Masoko wa TBL Fimbo Butallah alisema; Zaidi ya kuwapatia jukwaa wabunifu na wanamitindo hawa ili waweze kuonesha vipaji vyao, Redd’s pia itawapatia zawadi za pesa washindi watano katika kila mkoa watakaoshika nafasi za juu kama ifuatavyo;

WABUNIFU
MSHINDI WA KWANZA 700,000
MSHINDI WA PILI 500,000
MSHINDI WA TATU 300,000
MSHINDI WA NNE NA WA TANO 100,000 KILA MMOJA

WANAMITINDO
MSHINDI WA KWANZA 500,000
MSHINDI WA PILI 400,000
MSHINDI WA TATU 300,000
MSHINDI WA NNE NA WA TANO 100,000 KILA MMOJA

Tuna imani kubwa kuwa zawadi hizi zitaongeza chachu kwa wabunifu kujidhatiti katika kuendeleza ubunifu katika tasnia hii ya mitindo. Lakini pia matamasha haya yatahusisha burudani mbalimbali za kuvutia na hivyo kuwa sehemu muhimu ya kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo na kada mbalimbali katika kufurahia na kubadilishana mawazo juu ya masuala ya ubunifu na mitindo.

Kinywaji cha Redd’s Original kimekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza tasnia ya urembo, ubunifu na mitindo hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...