Naibu Waziri wa Maji, Gerson (kushoto) akimkabidhi tuzo  ya utendaji mzuri wa kazi aliyekuwa Waziri wa Maji wa kwanza ambaye pia ni mwanzilishi wa wizara hiyo, Dk. Pius Ngwa’ndu (kulia) leo wakati wa ufungaji wa Sherehe za maadhimisho ya  miaka 50 ya Uhuru ya  wizara hiyo.
Naibu Waziri wa Maji, Gerson (kushoto) akibadilishana  mawazo na  aliyekuwa Waziri wa Maji wa  kwanza , ambaye pia ni mwanzilishi wa wizara hiyo, Dk. Pius Ngwa’ndu (kulia) na kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo,  Mhandisi Christopher Sayi leo  wakati wa ufungaji wa Sherehe za maadhimisho ya  miaka 50 ya Uhuru ya  wizara hiyo.
Mwanafunzi wa Chuo cha Maendeleo na Usimamizi wa Maji kilichopo Ubungo jijini Dares Salaam, Adam Massam akiwaonesha baadhi ya wananchi teknolojia ya kuvuna maji ya mvua, ambayo hunaweza kutumia kumwagilia mazao na matumizi mengine leo  wakati wa ufungaji wa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru ya Wizara ya Maji.
Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kupunguza Madini ya Floraidi kilichopo Ngurudoto Arusha, Godfrey Mkongo (kulia) akitoa maelezo jinsi kupunguza floraidi katika maji kwa kutumia teknolojia rahisi ya mifupa ya ngo’mbe kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo na Usimamizi wa Maji wakiwemo wananchi leo wakati wa ufungaji wa Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru ya wizara hiyo.
picha ya pamoja.
baadhi ya wanachi na watumishi wa Wizara ya Maji wakifuatilia kwa makini maadhimidho ya miaka 50 ya wizara hiyo leo wakati ufungaji wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Maendeleo na Usimamizi wa Maji kilichopo Ubungo jijini Dares Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Chuo cha maendeleo na usimamizi wa maji ndiyo kilekile Chuo cha maji cha Lwegarulila.
    Mmm,what a kumbukumbu!Huyu bwana alikuwa muasisi wa wazo la kuanzisha hiki chuo na mchango wake wizara ya maji uliuwa beyond compare.
    I wander what was the thought process here. Unajua hili jina la chuo litakuwa lefu sana, lets chop Lwegarulila off.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...