Pichani ni Baadhi ya wanafunzi wa kike wakiwa nje ya club kusibiri wateja, Huko Jalan P-Ramlee jijini Kuala Lumpur Malaysia.

Na Pius Micky.

Imeripotiwa kuwa baadhi ya wasichana wa kiafrika wengi wao wanaokwenda nchini Malaysia kwa njia ya masomo ya juu wamejiingiza kwenye biashara ya ukahaba.

Kwa mujibu wa gazeti kubwa la nchini Malaysia The Star, wanafunzi hao wamekuwa wakionekana hadharani nje ya kumbi za starehe/burudani hasa nyakati za usiku huku wakionekana wakizungumza na wateja wao kwa kupatana bei.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo,wakinadada hao ambao wanachaji kiasi cha RM 200 kwa show time   (chap chap) sawa na Tsh 80,000/- na RM 600 ambayo ni sawa na laki tatu kasoro ushee kwa kulala hadi asubuhi.

Nchi ya Malaysia imekuwa kimbilio kwa wanawake wengi wanaojiuza toka nchi nyingi hasa za jirani na Malaysia kwa vile jiji la Kuala Lumpur limekuwa likipokea watalii wengi hasa wanaokimbia majira ya baridi huko nchi za Ulaya.

Kwa miaka ya karibuni kumekuwa na wanafunzi wengi sana toka nchi za Afrika wakienda kusoma nchini Malaysia kutokana na elimu yao kuwa ya kiwango cha juu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo wanafunzi hao ambao wana umri kati ya miaka 20 hadi 30 inasemekana wanatoka nchi za Ghana, Tanzania, Togo, Cameroon, Botswana na Nigeria.

Kwa mujibu wa ripoti za kichunguzi toka jarida la Star Metro linasema wana dadapoa hao wana uwezo mkubwa wa kumkamata mteja kutokana na vigezo wanavyovitumia ambavyo vina mshawishi mteja kwa haraka.

Wanafunzi hawa wote huwa wanakuwa na copy za Passport zao pamoja na barua zinazoawatambulisha kuwa ni wanafunzi toka vyuoni mwao.

“Niko hapa kwa miezi miwili tu na utafurahia huduma yangu” alisema mmoja wa mabinti hao mwenye umri wa miaka 22 ambaye alijitambulisha kuwa yeye ni Binti wa Kitanzania.

Kumekuwa na wimbi kubwa la wanafunzi wa Kiafrika kwenda kusoma Malaysia, na kiukweli kuna tatizo kubwa sana ambalo wanakutana nalo wanafunzi hao wakiwa huko Malaysia,kwani hairuhusu kwa wanafunzi yeyote wa kigeni kufanya kazi na hata ukipata kazi ya kufanya huwa hazilipi kama ilivyo kwa nchi zingine.

Mdau Pius Micky ambaye alitoka kwenye nchi hiyo ya Malaysia aliiambia Globu ya Jamii kuwa hali hiyo ipo na kwa wanafunzi hao na anaongea kutokana na Experience aliyonayo na mji ule. 

Maisha nchini Malaysia ni magumu hasa kama huna kipato na unategemea kupata pesa toka kwa wazazi kwani ukikosea hesabu inabidi ukae mpaka pesa zitumwe tena toka nyumbani,hali ambayo inawapelekea wanafunzi wengine kuingia katika biashara hiyo.

Jijini Kuala Lumpur maisha yako juu kulinganisha na miji mingine nje ya jiji hilo, wengi wa wanafunzi ni kweli wamekuwa wakifanya biashara hizi na wengine wamejiingiza kwenye biashara hatari ya madawa ya kulevya ambayo haina adhabu mbadala nchini Malaysia/ Singapore zaidi ya kunyongwa ndani ya masaa 24.

Tunawaasa wazazi wa watoto hao wawe karibu na watoto wao na wajue gharama halisi za kusomesha watoto nchini humo ambazo ma agent wengi wa shule hawawaambii ukweli wazazi kuhusu gharama hizi, matokeo yake wakifika kule ndio wanatumbukia humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Maisha ni magumu usiwalaumu kama hiyo biashara itawasaidia kusoma basi wafumbe macho. Hapa Ukerewe wakerewe wenyewe wanafanya hiyo kazi, hivyo si kitu cha ajabu!!

    ReplyDelete
  2. Wazazi ndio wenye makosa, kwanini watoto wasijiuze? Wanawapeleka watoto wao nje alafu wanawabania matumizi. Garama za nje ya nchi si mchezo, hakuna kukopana. Wazazi fikirieni kabla hamjawapeleka watoto nje ya nchi kimasomo. Zaidi mtajutia

    ReplyDelete
  3. mdau wa kwanza hapo juu acha hizo wewe yani unasema si kitu cha adabu dada zetu wajiuze?je angekuwa binti yako dada yako au mama yako ungesemaje? acha hizo, ni kweli maisha magumu lakini jamani kuna mengineyo ya kufanga japo kuwa hawaruhusiwi kufanya kazi wanafunzi wa nje.

    ReplyDelete
  4. Unajua kuna watu hawana habari za kurepoti,sasa hawa dada zetu wanajitafutia ridhiki au mshiko,isitoshe hawavunji duka wala nyumba ya mtu! kosa la jinai lipo wapi? akidada endeleeni na shughuli yenu msikose kutumia condom ni muhimu

    ReplyDelete
  5. Hiyo biashara imeshakuwa jambo la kawaida kwa wanawake wengi (including wallioolewa) siku hizi hasa wanaokwenda kusoma nje ya nchi.

    Pamoja na maisha magumu lakini pia wamezidisha tamaa ya pesa za harakaharaka.

    ReplyDelete
  6. Kujiendekeza tu hakuna cha maisha magumu wala nini mbona hata wa hapa home wanajiuza kama kawa

    ReplyDelete
  7. E BWANA MBELE KWA MBELE kwetu kuna mafisadi na wao wanataka kuja jenga bongo sio kina fulani tu ,mbona machangu wengi bongo mbona hawasemwi na wao ni hivyo wako kwenye vita ya maisha, UMALAYA ULIKUWEPO TANGU ENZI ZA MTUME MUHAMMAD NA UTAENDELEA KUWEPO1

    endelezeni dada zetu wala msiogope mpaka kijulikane

    ReplyDelete
  8. Labda elimu yetu haina ubora wakuridhisha maana huwa najiuliza kwanini siku hizi wabongo wengi wanakwenda kusoma nje ya nchi?Hii iwe ni challenge kwa serikali,Elimu yetu ikiboreshwa wananchi watarudisha imani na elimu ya bongo.Maana vyuo vikuu vya bongo tunasomea kugoma tu kutokana na ubabaishaji wa elimu yenyewe.Ona sasa dada zetu wanadhalilika ughaibuni!!

    ReplyDelete
  9. Naona watanzania wameamua kufungua KONA BAR hadi Ughaibuni...daah...condom muhimu kwa kweli.

    ReplyDelete
  10. Nikiwa sekondari nchi ya Malaysia kwenye jiografia ilikuwa ikiitwa "MALAYA" kwa kiswahili. Basi mnaosoma "MALAYA" muwe waangalifu sana!!

    ReplyDelete
  11. Mdau wa 04:21PM 20011 Uko sawa tu kwa unayosema. kwani wenye waume zao ambao waliwapa ruhusa kwa upendo kwenda soma Nnje nao wanajiingiza katika fani hii chafu isiyostahili kupewa support hata punje. Ukweli inasikitisha sana kwa tabia hii yenye kujengwa na tamaa na vishawishi vya kila aina hapa ughaibuni.

    Kuhusu kazi Malaysia wanafunzi wanaruhusiwa kufanya kazi ila kwa utaratibu maalumu uliowekwa na serikali, Ila ubaguzi ndio unaotwala sana hasa kwa watu kutoka Sub-sahara Africa (Nigro).

    Wazee fuatilieni wana wenu haya yaliohabarishwa na The star News ni ya ukweki kwa hakikika kabisa. Pia sasa kuna wimbi kubwa la waganda ambao hawakuripotiwa hapa.

    ReplyDelete
  12. Makubwa haya madogo yana wenyewe! Yaani Michuzi umenifanya nifikirie kukaa na wanangu Uni, maana jinsi walivyo wadogo hata miaka 20 wengine hawajafikisha mbona hatari!! Isitoshe hao watoto wa kike wana viboyfriend vyao vya kiume ambavyo ni watoto wetu pia, wazazi tumekwisha mbonaa?

    Yaani ukipeleka watoto kusoma Uganda tabu wanawekwa kinyumba, ukiwapeleka nje, ndio hivyo wanataka kushindana na wadada wanaoonekana kwenye mablogu wamevaa CL na bags za hermes na designer clothes matokeo yake wanaishia kujiuza. Wakibaki Dar mapedeshee wanawafuata, jamani sasa tutaponea wapi sisi wazazi?

    Na nyie mnaolaumu wazazi hamjui tu siku hizi watoto wa kike wanataka mambo makubwa, wanataka kwenda na fasheni, wavae kama kina so and so au wadada wa mujini, mablogu yanaonyesha nguo na viatu vya bei mbaya ambavyo hata anayefanya kazi Bongo kwa mshahara size ya kati hawezi kuafford. Lakini watoto wetu walioko vyuoni wanataka wapige pamba wakiwa bado wanasoma, ndio matokeo yake hayo.

    Sikilizeni mabinti zangu, maisha yapo mtayakuta tu acheni tamaa, ilimradi kama Mzazi wako ameweza kukulipia kodi ya nyumba ya mwaka, basi wewe gangamala hivyo na chakula cha kujipikia mwenyewe upate elimu yako. Achana na luxury hazikusaidii kitu kipindi hiki. Mimi aunty yenu niko shule sasa hivi, ninavaa mitumba ya Ulaya na tena niko Ulaya kuanzia nguo, viatu mpaka handbags, ninachonunua dukani ni nguo za ndani tu. Ninanunua chakula kwenye maduka yaliyo cheap kama Aldi, Lidl na Asda, na ninanunua brands za supermakets ambazo ni cheap. Asda ninanunua Smartprice ambazo ni lowest product. Ninajua nikitoka hapa nitakapomaliza shule yangu nitakuwa na uwezo wa kuvaa designer clothes, shoes na handbags kwa mshahara wangu. Someni kwanza mabinti zetu jamani wanawake walioko vijijini wanatutegemea sisi tuwakomboe kutoka kwenye umasikini uliokithiri.

    Mama Iman

    ReplyDelete
  13. kuala lumpuh ni jiji la ngono , na wateja wanalipa pesa nzuri tu. msema kweli mpenzi wa mungu hata mimi mteja wao mzuri tu. watoto wanafanya day waka , asubuhi darasani , usiku malindoni mwisho wa mwaka wana ondoka na saving zao poa tu na degree yao. sasa kibaya kipo wapi hapo.wa malay awatoi ajira sasa acheni watu wajiajiri na walivyo umbwa navyo.

    mdau malaysia

    ReplyDelete
  14. ndugu zangu mna uhakika hizo picha ni za kina dada wetu wa kibongo?? wanaweza kua ni wakenya, burundi au waganda..

    ReplyDelete
  15. Mambo ya kuuza mwili si kwa watoto walioko nje ya nchi tu hata wanasoma vyuo vya ndani nao ndo sana tu..mbona watu wanasoma CBE,IFM and UDSM nao tunawaona sana kona bar,Maisha club,Jolly club,Masai na Buguruni..Hii ni ishakuwa Tabia kwa wasichana wengi wa Kitanzania.Nawaomba dada zangu wa kitanzania popote mlipo muache na mridhike na maisha yenu..
    Tamaa mbaya hata 20% alishaimba.

    ReplyDelete
  16. Maisha magumu kwa wasichana tu? Wavulana wanaishi?Maisha magumu kwa wasichana tu? Wavulana wanaishi?

    ReplyDelete
  17. Si malaysia tu nimekaa nchi nyingi za ulaya Greece ITaly,SWeden, FRance Holland uk na kote huko hakufai mwenye ndugu yake wa kike sishauri amruhusu ni aibu wak za watu wengine waume zao wapo hapo hapo. Hapo Greece maradhi nje nje ila wao hujiuza kiaina si mabaa ni makubaliano tu.uk ukienda vyuoni usiiku kwa 5 pound mtu anakungangania na hayo si makosayao wazaziwaloaruhusu

    ReplyDelete
  18. Wakinadada kujiuza kupo duniani kote. Sio kitu cha kushangaza. Hapa Australia wachina, wahindi, Wamalaysia, Waindonesia, Wathailand na Wakorea ndio wafanya bishara wakubwa wa Ngono. Wanataka wakirudi nyumbani wajenge magorofa na kununua magari ya kifahari. Ni bishara haramu lakini hata tupige kelele vipi hatutaweza kuwazuia. Dawa ni kuwaacha tu walete hizo pesa nyumbani na sisi tufaidike.
    Cha kushangaza Malaysia ni nchi ya Kiislamu ambapo wao ndio hujiita mabingwa maadili lakni hata dada zao wenyewe ni wafanya bisahara wakubwa wa ngono.

    ReplyDelete
  19. Yote haya hujengwa na tamaa za watoto na kuporomoshwa kwa maadii. wazee wasilaumiwe, ila ni muhimu kwao kuzingatia kwanza popote pale waapelekao wtt wao.

    Haya yanaukweli na tunayaona kila siku

    ReplyDelete
  20. Nyie mnaopongeza hamna watoto nini acheni ujinga hii kitu haitakiwi izoeeke na ni bora imeletwa tumejua

    ReplyDelete
  21. Mbona hamjawasema wanaume kujiuza na wapo kibao na tena wanachukuliwa na majimama wakubwa.
    Je na wale wanaume wanaokuja kusoma na kuwa na wake mbona hamwasemi. Mnawaoneaga sana wanawake kwani wanafanya wenyewe kwa wenyewe au na wanaume? Acheni hizo dhambi ni dhambi tu. Kina dada mrudieni Mungu anaweza kusamehe hata kama dhambi ni kubwa kuliko.

    ReplyDelete
  22. Mdau uliyesema wakina kaka wapo wanaojiuza kwa majimama na kwa wanaume wenzao, upo sahihi kabisa lakini tunaangalia wingi wa wanaofanya hiyo biashara. Ungewapiga picha hao wanaume ili nao tuwaseme. Tunachowalaumu wananwake i kwamba inapotokea njia ya mkato kama hiyo wengi wataacha kujishughulisha na mambo ya maana na kukimbilia kwenye njia za mikato. Kujiuza ni njia ya mkato ambayo haitumii akili. Hata hao wanaume unaosema wanajiuza, ndio maana tunawaita " sio riziki". Manake wanafanya mambo yasiyo ya kawaida na hivyo hawastahili kuwa katika kundi la binadamu wa kawaida. Pia haimaanishi kwamba kama kuna wanaume wawili watatu wanaojiuza basi na ninyi ndio mhalalishe kujiuza.

    ReplyDelete
  23. Kuna mwanamke wa kiafrika asiyejiuza? Nani kati yenu amewahi kufanya mapemzi na mwanamke bila kudaiwa chochote? Je huko sio kujiuza? Au kwa vile hakuenda kwenye maeneo wanamojiuzaia na bei anayokuchaji ni ndogo? Kujiuza ni kujiuza tu hata uuze kwa bei ndogo. Mnawalaumu tu hao bure. Mimi nawasifu kwani wameweza kutafuta mahali watakapopata kipato kikubwa kuliko kujiuza kwa vijisenti hapa bongo.

    Kina dada wa malaysia na kwingineko endeleeni kufanya maisha manavyotaka malete pesa nyumbani. Mzazi gani atakataa mwane akimnunulia gari hata kama limepatikana kwa umalaya? Ni mzazi gani atakataa kujengewa nyumba na mwanawe hata kama ilijengwa kwa umalaya? Acheni kina dada watafute pesa. Isitoshe hiyo kitu haichakai. Mimi naomba atakayekosa mchumba kwa vile alikuwa anajiuza anitafute nitamwoa ili mradi tu akirudi bongo aache kujiuza.

    Kuhusu wanaume wanaojiuza sishauri wafanye hivyo. Hao ni wavivu wa kufikiri na sio wanaume wa kweli ndio maana mwanaume wa kweli yupo tayari hata awe kibaka au jambazi kuliko kujiuza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...