Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kusimamia Michezo ya Kubahatisha nchini, Abbas Tarimba (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kampuni ya Winlot Tanzania ilivyofanikiwa kupewa leseni ya kuendesha michezo ya kubahatisha itakayoanza rasmi kuchezesha michezo hiyo hapa nchini Desemba Mosi Mwaka huu.kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Arvind Dhariyal .

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Bodi ya michezo ya bahati nasibu ya Taifa imeipatia kampuni ya Winlot Tanzania Limited.Kibali cha kuendesha bahati nasibu ya Taifa ya serikali kwa niaba ya serikali katika mchakato wa makampuni saba ya kimataifa yaliyo omba kibali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salam Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni hiyo alisema,Kampuni yake inatarajia kuzindua bahati nasibu ya taifa,ambayo wateja watatakiwa kuchagua namba na kama namba zilizochaguliwa zitafanana na namba za ushindi wateja watajipatia zawadi za pesa taslim.

Alisema hii ni fursa kwa watanzania kushiriki katika bahati nasibu tofauti ambazo zitakazowafanya kujishindia hadi kufikia zaidi ya milioni mia moja. Bahati nasibu hizi ni kama vile tiketi kuuzwa tuu baada ya mteja kuchagua namba anazopenda na baada ya kuchezechwa kwa namba alizochagua mteja zikifanana na namba za ushindi basi mteja ataweza kujishindia mpaka zaidi ya millioni mia moja.

Kampuni hiyo itachezesha michezo ya kubahatisha yenye mfumo wa draw na ile ya zawadi za papo kwa hapo, michezo hii itakuwa katika aina ya 5/90, 5/39 na 6/49. Pamoja na mifumo mingi, Winlot Tanzania itatumia pia mfumo unaojulikana kama Weaver.

 Weaver ni mfumo mahiri, wenye ubunifu mkubwa, unaotumia teknolojia mpya inaosadia pia kurahisisha michezo ya bahati nasibu kiujumla. Ni mfumo wenye umakini katika kila hatua ya michezo ya bahati nasibu.

Bwana Amani Honestus alitaja njia mbalimbali zitazo kuwa zikitumika kuchezesha bahati nasibu kuwa ni pamoja na:-

1. Tiketi tatu zitajishindia kuingia katika draw za kila siku na kila wiki.

2. Mchezo aina yaTwiga 6/49; Huu utachezeshwa kila jumamosi saa kumi na mbili na dakika arobaini na tano ( 12:45pm). Zawadi ni hadi kufikia zaidi ya shilingi milioni mia moja. Mchezo huu utaonyeshwa katika televisheni.Namba za ushindi zikitangazwa, mshindia atatakiwa kwenda kuchukua zawadi zake katika ofisi za Winlot Tanzania.

3. Mchezo aina ya Duma 5/39; Mchezo huu utachezeshwa mara moja kila siku, zawadi ni hadi kufikia shilingi milioni kumi. Namba za ushindi zikitangazwa mshindi atatakiwa kwenda kuchukua zawadi zake kwa mawakala wa bahati nasibu.

4. Mchezo aina ya Simba 5/90; Mchezo huu pia utachezeshwa mara tisa kila siku, zawadi za hadi kufikia shilingi milioni mbili na nusu zitanyakuliwa.

5. Mara baada ya kutangazwa namba za ushindi,zawadi zinatakiwa kuchukuliwa katika kipindi cha siku saba. Baada ya hapo tiketi itapoteza uhalali wake.

6. Kama ilivyo katika sheria za nchi yetu, kila mshindi wa bahati nasibu atatakiwa kulipia kodi za serikali kutoka katika zawadi aliyoshinda.

7. Ili kuchukua zawadi, mshindi anatakiwa kuja na Tiketi yenye namba za ushindi.

8. Uchezeshwaji wa Draw utafanywa kila siku za Jumatatu hadi Jumamosi, saa kumi na mbili na dakika arobaini na tano (12:45pm) jioni na utashuhudiwa na mwakilishi kutoka bahati nasibu yaTaifa.

9. Tiketi zitauzwa kwa bei ndogo ya shilingi mia tano tu, hii nikutoa nafasi kwa kila mtu kuwa na uwezo wakushiriki na kujaribu bahati yake.

10. Kadri unavyonunua tiketi nyingi zaidi ndivyo unavyojiongezea nafasi yako ya kuibuka mshindi.

11. Mteja atatakiwa kutunza Tiketi yake mpaka mchezo utakapochezeshwa na matokeo kutangazwa.

Winlot Tanzania inasimamia miundombinu ya bahati nasibu na inabuni aina tofauti za michezo ya kubahatisha, inatoa mbinu za masoko kusaidia bidhaa za michezo ya kubahatisha, inatoa usaidizi muda wote kwa wanunuaji wa tiketi za bahati nasibu na washindi wake, na inasimamia mfumo huu wa biashara kwa ufanisi mkubwa sana.

Winlot Tanzania isingependa kubania mafanikio yake inayopata katika kusimamia michezo ya bahati nasibunabiasharanyinginezo, imejitolea kufurahia sehemu ya mafanikio haya na watu wenye uhitaji katika jamii yetu. 

Ukiachilia mbali kuwatambulisha watu wanaostahili sifa katika mafanikio yao ikiwa ni wanafunzi au raia watu wengine, Winlot Tanzania inasaidia taasisi zinazojihusisha na kazi za kujitolea katika sekta za afya, elimu nk.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Haya tena!!!!!!!!!!!! Upatu haoooooooo

    ReplyDelete
  2. Abasi unataka kuchezesha kamari!!

    ReplyDelete
  3. kwanini zile bahati nasibu zilizo kuwa zikiendeshwa na mengi zilizimwa.

    ReplyDelete
  4. Ankal...huyu mheshimiwa Tarimba mbona yuko kimya sana siku hizi kulikoni????hata kwenye Uyanga wake nako kimyaaaaa!! duuh

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...