Ubao wa Matokeo ulivyokuwa ukionyesha.
Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars, Said Maulid (kushoto) akichuana na beki wa Djibout, Ilyas Hassan Dyama katika mchezo wa kombe la Chalenji uliofanyika leo kwenye Uwanja  wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kilimanjaro Stars ilishinda 3-0.
 Kikosi cha Djibouti
 Kilimanjaro Stars
Hekaheka langoni pa Djibouti.
 Wachezaji wa timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars,Godfrey Taita (kushoto),Yusuf Rashid (kati) na Said Maulid wakishangilia bao la tatu lililofungwa na Yusuf Rashid katika mchezo uliopigwa jioni ya leo dhidi ya Djibouti kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.Kilimanjaro Stars ilishinda bao 3-0.
 Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars Thomas Ulimwengu akichuana vikali na Beki wa Timu ya Djibouti Mohamed Kadar wakati wa mchezo wao uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.Kilimanjaro Stars ilishinda bao 3-0.
 Kiungo wa Kilimanjaro Stars,Nurdin Bakari awania mpira na Beki wa Djibouti.
Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hatuwezi kujisifia kuifunga Djibouti. Djibouti ni timu ndogo sana!

    ReplyDelete
  2. Ari hii ilitakiwa siku ile na Rwanda...sio na hawa Wasomali wa Kifaransa!

    ReplyDelete
  3. boban mbona hachezeshwi

    ReplyDelete
  4. Matobwe wezenu hao

    ReplyDelete
  5. hao ndio mnaowaweza djibouti,ethiopia eritrea ndio mwisho wenu
    wafungeni wanaume wanaohitajika kufungwa ili kusogea nafasi za mbele sio kufunga hao watoto wa timu za mitaani kule djibouti.

    ReplyDelete
  6. Mbona wabongo hamuendi uwanjani? Uwanja uko tupu eti! Ingekuwa kuna fiesta mngeshaenda na kujaza huo uwanja. Badilikeni eti ndugu zangu.

    ReplyDelete
  7. Yaani Mbwa kumkamata panya unawenza kumsifia mbwa wako anajua kushika????!!!

    Kama akiweza kumkamata chui, kweli unao uwezo wa kutamba.

    Yaani Djibuti tumeifunga, magazeti, TV, nk maneno kibao. Ati ooh Taifa Stars yafufua matumaini!! Na ninyi watoa habari mnazidi kuharibu fani. Ndiyo maana hatusongi mbele. Mnatoa sifa kubwa pasipo sababu.

    Ningaekuwa mimi mwandishi wa michezo, ningandika Taifa Stars sasa yajikongoja. Huu ndiyo ukweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...