In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player
THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT - BEYOND THE ORDINARY - NATURALLY' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupokea Ripoti Maalum siku chache zijazo toka Tume iliyoundwa kuchunguza chanzo cha kuzama kwa Meli ya M.V Spice Islanders

‘TAARIFA YA MAAFA ILIFIKA HADI MILIMANI’ HII NI KAULI YA MKUU WA MKOA WA MANYARA MHE, ELASTON MBWILO WAKATI ALIPOKUTANA NA BALOZI SEIF ALI IDDI KWA LENGO LA KUKABIDHI MCHANGO WA WANANCHI WA MKOA WA MANYARA KUFUATIA AJARI YA MELI YA MV SPICE KATIKA BAHARI YA NUNGWI.

Na Othman Khamis Ame - OMPRZ.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatarajia kupokea Ripoti Maalum siku chache zijazo kutoka kwa Tume iliyoundwa kuchunguza chanzo cha kuzama kwa Meli ya M.V Spice Islanders katika Mkondo wa Nungwi Mkoa Kaskazini Unguja usiku wa kuamkia Tarehe 10 Septemba mwaka 2011.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo hapo Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Elaston Mbwilo aliyefika kukabidhi mchango uliotolewa na Wananchi wa Mkoa huo kusaidia Kamati ya Maafa Zanzibar kufuatia msiba wa ajali ya M.V Spise Islanders na kusababisha Vifo vya Watu 206.

Alisema Ripoti hiyo ndio itakayokuwa sahihi ya tukio zima lililopelekea jamii kupata mtafaruku uliosababishwa na kauli Tofauti za baadhi ya Watu zilizosababisha kuwachanganya Wananchi.

Balozi Seif lisema Licha ya kazi kubwa inayowakabili wajumbe wa Tume hiyo kufanya Uchunguzi lakini kazi inakwenda vyema na Serikali imewahakikishia Wananchi kwamba Ripoti hiyo itafanyiwa kazi na uadilifu utatumika katika kuona haki inatendeka kwa kila muhusika wa tukio hilo.

Amewatoa hofu Wananchi kwamba Fedha zinazoendelea kutolewa na Wahisani mbali mbali kuchangia mfuko wa Maafa hazijaguswa kabisa kwa matumizi mengine yaliyo nje ya utaratibu.

‘‘ Hatujagusa hata Senti moja katika Fedha zilizotolewa na Wahisani na Watu mbali mbali kuchangia Mfuko wa Maafa. Hata Gharama za Tume iliyoundwa kuchunguza chanzo cha Ajali ya Meli ya M.V Spice zimetolewa kutoka Mfuko wa Serikali ’’. Alifafanua Balozi Seif Ali Iddi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alifahamisha kwamba Hivi sasa Ofisi yake iko katika matayarisho ya kuandaa Ripoti kuhusu makusanyo ya fedha za Michango ziliyotolewa na wahisani ili ipelekwe Serikalini kupata maamuzi ya namna zitakavyotumika fedha hizo.

Lakini Alisisitiza kwamba lengo litakuwa lile lile la kuwagusa moja kwa moja wahusika wa Tukio hilo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Aliwapongeza Wananchi wa Mkoa wa Manyara kwa moyo wao wa kuguswa na tukio hili lililowapata wananchi wa Zanzibar.

Mapema Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Elaston Mbwilo alisema wao kama Watanzania wengine walikuwa na haki ya kuguswa na msiba huo ambao ni wa Kihistoria kuwahi kutokea Zanzibar.

Mh. Mbwilo Aliwataka wananchi kuendelea kuwa na subra wakati wanapopatwa na Majanga mbali mbali ambayo baadaye pelekea kuleta maafa.

Idadi ya watu
Idadi ya watu
eXTReMe Tracker