UCHAGUZI WA VIONGOZI CECAFA
Mkutano Mkuu wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) utafanyika kesho (Novemba 24 mwaka huu) kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam.

Moja ya ajenda katika mkutano huo utakaonza saa 4.00 asubuhi ni uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya CECAFA. Nafasi zinazogombewa ni tano; (Mwenyekiti na wajumbe wane wa Kamati ya Utendaji).

Wagombea uenyekiti ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ambaye anatetea nafasi hiyo. Mpinzani wa Tenga ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Djibouti, Fadoul Hussein.

Nafasi nne za Kamati ya Utendaji zinagombewa na watu wanane. Wagombea hao ni Abdiqani Saeed Arab (Somalia), Tariq Atta Salih (Sudan), Justus Mugisha (Uganda), Tesfaye Gebreyesus (Eritrea), Hafidh Ali Tahir (Zanzibar), Sahilu Wolde (Ethiopia), Raoul Gisanura (Rwanda) na Abubakar Nkejimana (Burundi).

Baada ya Mkutano Mkuu, saa 7.00 mchana kutakuwa na mkutano na waandishi wa habari ambao utafanyika hapo hapo hoteli ya JB Belmont.

MICHUANO YA CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP 2011
Timu zinazoshiriki CECAFA Tusker Challenge Cup zinaendelea kuwasili Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano hayo yatakayoanza Novemba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa.

Somali na Djibouti tayari zimeshawasili. Timu hizo zilitua nchini jana mchana kwa nyakati tofauti. Ratiba ya ujio wa timu nyingine ni kama ifuatavyo;

Team Arrival: Accommodation:
Burundi Nov 23rd 1545hrs RwandAir - Lunch Time Hotel (Ubungo)
Djibouti Nov 22nd 1320hrs Ethiopian Airlines - Wanyama Hotel (Sinza)
Ethiopia Nov 24th Ethiopian Airlines - Johannesburg Hotel (Sinza)
Kenya Nov 27th Kenya Airways - Rungwe Hotel (Kariakoo)
Malawi Nov 27th Air Malawi - Rombo Green View Hotel (Sinza)
Rwanda Nov 23rd 1545hrs RwandAir - Rungwe Hotel (Kariakoo)
Somalia Nov 22nd Kenya Airways - Wanyama Hotel (Sinza)
Sudan Nov 23rd 1320hrs Ethiopian Airlines - Marriot Hotel (Mabibo External)
Tanzania - Rainbow Hotel (Morogoro Rd)
Uganda Nov 23rd 1600hrs Air Uganda - Royal Valentino Hotel (Kariakoo)
Zanzibar Nov 23rd by boat- afternoon - Rombo Green View Hotel (Sinza)

Viwanja vya mazoezi kwa ajili ya timu zinazoshiriki michuano hiyo ni; Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (viwanja viwili), Shule ya Sekondari Loyola na Uwanja wa Karume.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Vipi mambo ya Supersport9 yatakuwepo kwa cc ambao hatuko Daresalaam?

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...