Chama cha wafanyakazi wa railway (TRAWU) kimetangaza kufanya mgomo wafanyakazi wa Reli nchini TRL na TAZARA baada ya serikali kushindwa kutatua matatizo yao.

TRAWU ilitangaza mgogoro na menejment leo asubuhi mbele ya wanahabari na wafanyakazi wa reli ambao ndio wanachama baada ya kukubaliana kuchukua hatua hiyo.

Wafanyakazi hao wanapinga ununuzi wa injini chakavu za kuvuta treni kama kweli nia ya serikali ni kufufua usafiri huo kwa maslahi ya watanzania.

Mbali na hilo, TRAWU kesho imeahidi kuchukua fomu Tume ya usuluhishi na uamuzi (CMA) chini ya hati ya dharula na kama haitafua dafu basi watatangaza mgomo usio na kikomo.

Emanuel Jomalema ambaye ni Kaimu mwenyekiti wa TRAWU, aliyataja matamko yao kwa TRL ni:

1. Mkataba wa hali bora za kazi: Majadiliano ya hali bora za kazi yalifanyika 3/11/2011 mkataba ulipaswa kutiwa saini ndani ya wiki moja baada ya kumalizika lakini hadi leo mkataba haujatiwa saini.

2. Dhamana katika mabenki: Wafanyakazi wanakosa kuaminiwa katika mabenki ili kukopesheka kwa kuwa hawana dhamana toka kwa mwajiri wao toka 1997 hali hiyo inatokana na serikali kushindwa kuthibitisha umiliki wa TRL kwa 100% kimaandishi.

3. Nyongeza za mishahara: kwa mara ya mwisho nyongeza hizo ziliongezwa mwaka 2008 hadi leo hakuna kilichoongezeka kwa kupanda daraja au ongezeko la kawaida tofauti na wafanyakazi wenzao wa RAHCO ambao wanalipwa vizuri bila kuzalisha.

4. Railway ACT ya 2002 itazamwe upya ili kuondoa urasimu huo uliopo kati ya RAHCO na TRA unaozorotesha utendaji wa kazi.

Sheria mpya ya manunuzi: Tunatahadharisha serikali pamoja na kupita kwa sheria mpya ya manunuzi kutonunua injini za RITE kwa vile zilikwisha thibitika hazifai na ni chakavu, tumeamini kwamba nia njema ya serikali kufufua kampuni ya Reli TRL sheria mpya haitahusu ununuzi wa injini na mabehewa ya kampuni ya RITE bali itaangalia njia nyingine mbadala zilizopo.

KUHUSU TAZARA

1 Muundo wa mishahara na utumishi imechukua zaidi ya miaka 10 katika majadiliano bila mafanikio hivyo kamati kuu inatangaza kuingia katika mgogoro na menejimenti.

2 Kucheleweshwa kwa mishahara kwa wafanyakazi kumekuwa sugu. Maana hakuna tarehe maalum ya kulipwa mishahara pamoja na menejimenti ya TZR kuahidi kulipa mishahara hiyo mbele ya Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu kila tarehe 25 ya mwezi.

3 Mikataba mibovu isiyo na tija inayoingiwa na mamlaka, inayosababisha kuyumba kwa shirika na kukosekana kwa maslahi ya wafanyakazi.

4 Interterritorial Allowance: Malipo haya hutolewa kwa wafanyakazi wanaotoka nje ya nchi ya 55% ya mshahara. Utaratibu huo umesababisha kuingiza wafanyakazi wengi kuliko wa ndani hivyo kusababisha maelewano kazini kuwa mabaya na kubana nafasi za ajira kwa watanzania tunataka haki sawa kwa kazi sawa.

5 Sheria inayounda TZR (ACT) itazamwe na kuundwa upya kwa vile sheria hiyo iko kisiasa zaidi kuliko kibiashara.

Chama kimesema kimeshauri wakati wote Serikali kuchukua hatua stahiki kutokana na malalamiko ya wafanyakazi pamoja na kuwasihi wafanyakazi kuwa wavumilivu lakini sasa kamati kuu imeamua swala hili lirudishwe kwa wafanyakazi waamue, nao wakaamua mgogoro na menejimenti.

Wanachama ambao ni wafanyakazi wa TRL na TZR wakichangia hoja hiyo walidai kuwa wameamua kuingia katika mgogoro na serikali kwasababu kama imeamua kuwekeza katika kampuni hiyo ni vema kujali maslahi yao pamoja na kununua injini zinazofaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...