In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player
THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT - BEYOND THE ORDINARY - NATURALLY' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.










  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com












Archive for February 2011

KUMBUKUMBU

Mr. Matthew Douglas Ramadhani

Today marks 50 years since you suddenly depart this world. Words can’t express the pain you left behind; it was such a great loss to us as family and nation.

You are truly missed by your beloved wife Bridget, bro Bishop John your children Marina, Augustino, Hendry, Maud, Mary and Bridget and grandchildren’s who never got the opportunity to know you……but can’t stop wishing you were here.

You were such a great father to this family. There will be a service at the All Saints Cathedral at Vinghawe, Mpwapwa, where the Bishop’s throne and Canons stalls will be consecrated in your memory.


Siku 100 baada ya kuteuliwa kuwa Mbunge wa Arusha Mjini

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Jonathan Lema na Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha Mjini Elifuraha Paul Mtowe wakihutubia jumuiya iliyofika katika hafla hiyo, Mheshimiwa Lema aliwahakikishia watoto hao watasoma na kupata matibabu bure na Mwenyekiti wa ArDF aliwahakikishiwa licha ya kupatiwa Ada na Matibabu pia watapatiwa Chakula kufuatia kampuni ya Arusha Mambo kuazima shamba lake lenye Ukubwa wa ekari 30 lilimwe na chakula kitakachopatikana kigawanywe katika shule za Kata na Vituo vya watoto yatima, hata hivyo aliomba jamii, mashirika na wadau mbalimbali kuendelea kuchangia Taasisi yao ili imudu kuwasomesha watoto hawa na kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Jonathan Lema na Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha Mjini Elifuraha Paul Mtowe wakimpatia mmoja wa wazazi Cheti cha kuthibitisha kupatiwa msaada wa Ada na Matibabu kwa watoto wake kwa kipindi cha miaka minne.
Kati ya watoto wenye kuishi katika mazingira ya kati waliojitokeza kuwahamasisha watoto wenzao wenye kuishi katika mazingira magumu kuwa watashinda na siku moja wataishi katika Nchi yenye neema wakiwa na Mbunge wa Arusha Mjini na mmoja wa mzazi aliyejitokeza kusaidia watoto wenye uhitaji baada ya kununua tshirt za ArDF kama mchango wao kwa watoto wenzao.
Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakiwasajili na kugawa Tshirt na Bendera za Taifa kwa Watoto waliofika katika hafya hiyo kabla hawajaimba wimbo wa Tanzania Nakupenda na baadae wimbo wa Taifa.
Baadhi ya Wazazi na Walezi waliojitokeza wakiwa katika picha ya Pamoja na Mbunge Pamoja na Mwenyekiti wa ArDF baada ya watoto wao kupatiwa Ada, Kadi za Matibabu, Daftari na Kalama Ili kuendelea na kutimiza ndoto zao.
Baadhi ya Watoto kati ya watoto 400 watakaopatiwa msaada wa Ada na Kadi za Afya na Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha Mjini kwa kupitia Ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo, watoto hao waliojitokeza kwenye Ofisi ya Mbunge wa JImbo la Arusha Mjini kupokea Msaada huo wa Ada wenye thamani ya Shilingi Milioni 60 na kadi za bima ya Afya zilizopata udhamini kutoka Shirika lisilo la Kiserekali la Green Hope linalopata msaada kutoka Serekali ya Canada.
Baadhi ya watoto na Madiwani waliojitokeza katika picha ya Pamoja na Mbunge Pamoja na Mwenyekiti wa ArDF baada ya kupatiwa Ada, Kadi za Matibabu, Daftari na Kalama Ili kumudu mahitaji ya masomo yao.


Martin Luther King Jr Drum Major award to the Committee of Six

The U.S Ambassador to Tanzania Alfonso E. Lenhardt delivering his remarks before conferring the 2011 Dr. Martin Luther King Drum Major for Justice Award to the Committee of Six of the Zanzibar House of Representatives in recognition of its role in helping establish the Government of National Unity in Zanzibar and making 2010 the year of Zanzibar's reconciliation. The award ceremony was held on February 28, 2011 at the U.S. Embassy in Dar es Salaam.
The U.S Ambassador to Tanzania Alfonso E. Lenhardt (right) receiving a copy of the amended constitution of Zanzibar from the Hon. Ali Mzee Ali of the Committee of Six of the House of Representatives. The amended constitution which laid a legal framework for the formulation of the Government of National Unit in Zanzibar resulted from a referendum by the people of Zanzibar. Ambassador Lenhardt conferred upon the Committee of Six the 2011 Dr. Martin Luther King Award in recognition of the vital role in played in the Zanzibar reconciliation.
The U.S Ambassador to Tanzania Alfonso E. Lenhardt delivering his remarks before conferring the 2011 Dr. Martin Luther King Drum Major for Justice Award to the Committee of Six of the Zanzibar House of Representatives in recognition of its role in helping establish the Government of National Unity in Zanzibar and making 2010 the year of Zanzibar's reconciliation. The award ceremony was held on February 28, 2011 at the U.S. Embassy in Dar es Salaam.
The U.S Ambassador to Tanzania Alfonso E. Lenhardt (center) with some of members of the Committee of Six of the Zanzibar House of Representatives; Hon. Ali Abdallah Ali, Hon. Zakiya Omar Juma (left) Hon. Ali Mzee Ali (second from right ) and Ibrahim Mzee Ibrahim the House Clerk who served as a Committee's Secretary. Ambassador Lenhardt conferred upon the Committee of six the 2011 Dr Martin Luther King Drum Major for Justice Award in recognition of its role in helping establish the Government of National Unity in Zanzibar and making 2010 the year of Zanzibar's reconciliation. The award ceremony was held on February 28, 2011 at the U.S. Embassy in Dar es Salaam.


serengeti breweries yatoa msaada kwa waathirika wa mabomu gongo la mboto

Waziri Mkuu,Mh Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Teddy Mapunda mara baada ya kupokea misaada hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Teddy Mapunda akipeana mkono na Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda mara baada ya kumkakabidhi msaada wa vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni 15 mapema leo Ukonga jijini Dar,msaada huo ikiwemo Mabati 300,Cementi 300,mashuka 200 pamoja na vyandarua 200 vyote vikiwa ni kwa ajili ya kusaidia waliothirika na milipuko ya Mabomu iliyotokea hivi karibuni,Gongo la Mboto,jijini Dar.
Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Teddy Mapunda akikabidhi msaada wa vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni 15 kwa Waziri Mkuu,Mh Mizengo Pinda (pichani kulia) mapema leo Ukonga jijini Dar,msaada huo ikiwemo Mabati 300,Cementi 300,mashuka 200 pamoja na vyandarua 200 vyote vikiwa ni kwa ajili ya kusaidia waliothirika na milipuko ya Mabomu iliyotokea hivi karibuni,Gongo la Mboto,jijini Dar.


WAZIRI MKUU ATEMBELEA WAATHIRIKA WA MABOMU GONGO LA MBOTO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akizungumza na wakazi wa Gongolamboto (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kuwaona waathirika wa milipuko ya mabomu iliyotokea katika kambi ya JWTZ Gongolamboto leo jijini Dar es salaam ambapo ametoa wito kwa mamlaka zinazohusika na ugawaji wa misaada kuhakikisha kuwa misaada hiyo inawafikia walengwa.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia moja ya nyumba iliyoteketea kwa moto kutokana na milipuko ya mabomu eneo la Majohe leo jijini Dar es salaam.
Wajasilia mali wa kikundi cha SEUMA kutoka Segerea jijini Dar es salaam wakimkabidhi Waziri mkuu Mizengo Pinda msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa milipuko ya mabomu ya Gongolamboto leo jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa nne kulia) Pinda akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw.Gabriel Fuime(wa sita kushoto) kuhusu upokeaji na uhifadhi wa misaada mbalimbali inayotolewa kuwasaidia waathirika wa mabomu Gongolamboto inavyohifadhiwa na kugawiwa kwa walengwa husika leo eneo la Shule ya Sekondari Pugu jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi akikabidhi kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda msaada wa tani 17 za vyakula mbalimbali na hundi ya shilingi milioni 15 kwa ajili ya kutoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao kutokana na milipuko ya mabomu iliyotokea eneo la Gongolamboto.Wasanii wa Muziki na Filamu wakipita mbele ya Waziri mkuu Mizengo Pinda na kuwasilisha michango mbalimbali ya fedha na vitu vyenye thamani ya shilingi milioni 76 waliyoipata kutokana na tamasha walilolifanya kuchangia waathirika wa Mabomu katika eneo la Gongolamboto jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia)akizungumza na baadhi ya familia za waathirika wa milipuko ya mabomu eneo la Majohe leo jijini Dar es salaam na kuwahakikishia kuwa serikali itafanya kila linalowezekana kuwasaidia.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa pole baadhi ya wananchi wa Majohe ambao nyumba zao ziliharibiwa na mabomu yaliyolipuka katika kambi ya JWTZ ya Gongolamboto hivi karibuni wakati alipoeatembelea leo.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.


Premier Betting watoa msaada kwa wahanga wa gongo la mboto


Kampuni ya bahati nasibu ya Premier Betting kupitia mchezo wake wa Premier Bingo imekabidhi msaada kwa waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto msaada huo ni wa thamani ya shilingi milioni moja.

Akikabidhi msaada huo kwa mratibu wa misaada wa kituo cha Clouds FM Muhidin Mrope Meneja Masoko wa kampuni hiyo Afsa Hamad alisema kuwa kampuni ya Premier Betting imeguswa na matatizo yanayowagusa waathirika wa Gongo la Mboto.

Msaada huo ni mipira 22, kilo mia mia za mchele, sukari, maharage na gunia mbili za sabuni ya unga.


Evans Bukuku's Comedy Club


MAMA CHIKU SHOMARI ASTAAFU RASMI

Afisa Utamaduni Mkuu wa Wizara ya Habari ,Vijana ,Utamaduni na Michezo Mama Chiku Shomari akimshukuru Mungu ofisini kwake baada ya kustaafu rasmi leo jijini Dar es Salaam.
Mzee Shomari akimzawadia mkewe mama Chiku Shomari kwa kumaliza na kustaafu salama kazi kwenye mlango wa Ofisi ya Utamaduni wakati anaondoka rasmi leo jijini Dar es Salaam.Picha na Anna Itenda -Maelezo


waziri wa mazingira akutana na balozi iran nchini leo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Terezya Huvisa akizungumza na Balozi wa Iran Nchini Tanzania, Bw. Movahhedi Ghomi wakati alipofika Ofisini kwake Kujadili Mkutano wa Mkataba wa Kuhifadhi ardhi Oevu utakaofanyika Nchini Iran.Tanzania ni Miongoni mwa Nchi zinazotekeleza Mkataba wa Ramsa.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Dk. Terezya Huvisa akisalimiana na Balozi wa Iran Nchini Tanzania, Bw. Movahhedi Ghomi wakati alipofika Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli kujadili Maandalizi ya Mkutano wa Mkataba wa Kuhifadhi ardhi Oevu utakaofanyika Nchini Iran.(Picha na Ali Meja)



We are an import/export company based in the United Kingdom with global dealings. We offer specific services to suit each individual client.

Whether you require a single service or an annual requirement, Locus Impex will treat you with care, consideration and most of all the best solution for your requirements. We pride ourselves in our service and welcome any job regardless of size.

*AIRFREIGHT SERVICES TO AFRICA FROM £2.00 PER KILO – no handling fee until March 2nd2011!

WE SHIP ALL TYPES OF CARGO TO AFRICA AT UNBEATABLE RATES, i.e. CONTAINERS, TRUCKS, CARS, MACHINES ETC.WE ALSO SELL USED VEHICLES & MACHINERY FROM UK.

CARS (SALOON) TO DAR OR MOMBASA

4X4 TO DAR OR MOMBASA

40' CONTAINER TO DAR

40' CONTAINER TO MOMBASA

40' CONTAINER TO ZANZIBAR

40' CONTAINER TO TANGA

20' CONTAINER TO DAR

At Locus Impex , we aim to : -

* Put the Customer First *
* Give Cost-Effective Pricing *
* Provide High Quality Service

Marketing Director
Locus Impex Ltd- Reading Branch
TEL(Office) +44 118 954 5890/ Mob (Office)+44 7900043224
Emergency Tel: +44 7977807295

www.locusimpex.com


KUMBUKUMBU

Marehemu FUNDIKIRA MSABILA KASSEMBO

Waweza kuwa ni muda mchache au mrefu lakini ni mwaka sasa umetimia tangu ulipotutoka Fundikira (28 Feb 2010)Tunakukumbuka sana sisi watoto,mke,wazazi,kaka,dada pamoja ndugu na jamaa sisi tulikupenda lakini Mwenye enzi alikupenda zaidi ! Tuamuomba sana Mwenye Enzi mtukufu akupumzishe kwa amani.

Amina !

Familia ya Msabila Kassembo


wanafunzi wa IFM wakiwa katika mgomo wao asubihi ya leo

Wanafunzi wa Chuo cha IFM,jijini Dar wakiwa wamekusanyika asubuhi hii kwenye moja ya sehemu ya wazi ya chuo hicho kwa madhumuni ya kuanzisha mgomo wa kupinga wanafunzi wenzao kuzuiwa kufanya mitihani kwa sababu tu hawakumaliza kulipa ada ya semester ya kwanza.
Wanafunzi wa chuo cha IFM,wakiwa wamekusanyika leo asubuhi ndani ya uwanja wa chuo hicho,wakiwa na mgomo kwa kile walichodai kupinga wanafunzi wenzao kuzuiwa kufanya mitihani kwa sababu tu hawakumaliza kulipa ada ya semester ya kwanza

Aidha imeelezwa kwamba kutokana na kugoma kwa wanafunzi hao ni kupinga uonevu na mfumo mbovu unaofanywa na chuo hiko kwao wakati serikali ilishaweka wazi kuwa hakuna na marufuku kwa wanafunzi wa vyuo vya umma kuzuiwa kufanya mitihani


airtel kicks off Africa-India job transfer program


* Empowering and harnessing local manpower vital to its business strategy
* Staff from African operations to work across various units of airtel India’s operations
* Indo-Africa experience to provide insights for cross continental synergies

Nairobi February 28, 2011 … airtel Africa today announced the kick off of a unique staff transfer program that will see the first batch of employees from Africa work within the operations of its parent company in India, starting 23rd February, 2011.

The initial phase of the program saw the integration of specialized staff from Bharti airtel into some markets. In this phase of the program, the initial group from Africa to India will be employees from airtel’s operations in Congo, Tanzania, Kenya, the democratic Republic of Congo (DRC), Niger and Zambia.

They will spend up to one year working within various units, which include Bharti airtel’s network infrastructure development, solutions for medium sized enterprises, sales & distribution, financial systems, marketing and other functions.

Speaking on the initiative, Manoj Kohli, CEO (International) & Joint Managing Director of Bharti airtel, said: “Our strongest pillar is people. We invest considerable resources in developing capabilities whilst giving our human capital opportunities to grow. The transfer of knowledge is a conscious strategy informed by the fact that globalization has changed the required skill sets of the team.”

According to Mr. Kohli, the transfer program is a mutually beneficial program between all airtel operations in Africa and the Indian sub-continent. “The need for consumers to leapfrog existing technologies and embrace new innovations is a reality as evidenced by some of the latest innovations rolled out by airtel in Africa. We need to ensure that our solutions connect in a cultural and socio-economic context” he added. “This initiative is just a first step of getting our teams connected across the Globe.”

During the launch of its operations in Africa, the telecom operator reiterated its intention to harness local manpower which stands at over 6,500 employees across the African continent.

In addition to investing in the skill sets, airtel has partnered with some of the leading technology providers to develop specialized skills and nurture job opportunities across the continent.

The company has kicked off partnerships with global technology leaders such as IBM, Nokia Siemens, Huawei, Ericsson and Business outsourcing partners such as Spanco & Tech Mahindra.


gari la faya katika uwanja wa ndege wa nduli

Hili ni gari pekee linalotumika na kikosi cha zimamoto katika uwanja wa ndege wa Nduli,Mkoani Iringa.Wadau mnaliongeleaje hili?? (Picha na Mdau Francis Godwin)



hepi besdei ya kuzaliwa mtabutwa


Habari za kazi kaka Michuzi.
Tafadhali naomba unipeperushie pongezi zangu kwa binti yangu mpendwa.Mtabutwa Makanya kwa kutimiza miaka minne siku ya leo 28/2. Mwenyezi Mungu amjalie maisha mema na merefu yenye wingi wa rehema,upendo, hekima na busara.
Asante. Aunt Rachel M.


chadema wamtembelea mama maria nyerere butiama

Mbunge wa jimbo la Kawe Mh. Halima Mdee akiweka shada la maua katika kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, wakati viongozi na baadhi ya wabunge wa chama hicho, walipomtembelea Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Butiama Jumapili hii.
Mama Maria Nyerere akiteta jambo na katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, wakati viongozi wa Chama hicho na baadhi ya wabunge, walipomtembelea nyumbani kwake Butiama.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akitoa salamu za chama hicho kwa Familia ya Mwalimu Nyerere, wakati vongozi mbali mbali na wabunge wa chama hicho, walipomtembela Mama Maria Nyerere (katikati) nyumbani kwake Butiama. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilibrod Slaa.Picha zote na mdau Joseph Senga.


MAMBO YA GADO


SIMBA YAILAMBISHA MTIBWA VIJIKO VINNE VYA SUKARI

Mbwana Samata akishangilia bao la kwanza alililoifungia timu yake pamoja na wachezaji wenzake. Kulia ni Nico Nyagawa na aliyembeba ni Amri Kihemba.
Mshambuliaji wa Simba, Mbwana Aamata akiipangua ngome ya Mtibwa Sugar.
Mshambuliaji wa Simba, Shija Mkina akimiliki mpira mbele ya golikipa wa Mtibwa Sugar huku akiwa na kipa Omary Ally wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jioni hii. Simba ilishinda 4-1 Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii.


MSAADA TUTANI TAFADHALI

Bro Michuzi Assalaam alaykum,

Tafadhali naomba unisaidie kunikutanisha na wadau mbalimbali wa hapa mtandaoni ili wanisaidie kupata baadhi ya vifaa ninavyohitaji.

Vifaa hivyo ninavyohitaji viwe used ama vipya na viwe hapa Nchini au vya kuagiza toka nje ni Mixer ya kukandia unga yenye uwezo wa kukanda unga kuanzia Kilo 25 na kuendelea na Bread Oven yenye uwezo wa kuhifadhi mikate zaidi ya 60 kwa wakati.

Tafadhali kwa yeyote atakayekuwa na ufahamu wa vitu hivyo si mbaya kunijulisha kupitia namba yangu na mail nilivyoorodhesha hapa chini.

HASSAN MBILILI
MOB:+255 715 251148
mail: hmbilili@yahoo.com

Wakatabahu.


news alert: IFM kugoma kesho?

habari yako anko michu

nakutaarifu wewe kama mwana habari kuwa kesho asubuhi kuanzia saa 1 wanafunzi wa ifm chuo kizima kutakuwa na mgomo kupinga wanafunzi wenzao kuzuiwa kufanya mitihani kwasababu tu hawakumaliza kulipa ada ya semester ya kwanza

wanafunzi wanapinga uonevu na mfumo mbovu unaofanywa na chuo hiko kwao wakati serikali ilishaweka wazi kuwa hakuna na marufuku kwa wanafunzi wa vyuo vya umma kuzuiwa kufanya mitihani

haya ankal nisiwe mbeya sana fika pale asubuhi angalau kupata vijipicha na taswira kidogo

mwanaharakati wa Globu ya jamii


Kili Marathon 2011 yafana sana

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi akihutubia baada ya kumalizika kwa Kili Marathon 2011 uwanja wa Ushirika mjini Moshi leo
Wadau toka sehemu mbalimbali walijitokeza
kushiriki kwenye Vodacom 5km Fun Run

Mkuu wa Wilaya ya Hai akiwa na washiriki
na waandaazi wa mbio hizo

Doris akimvika kilemba mshindi wa mwaka huu wa
Kili Marathon kwa wanawake Anna Kamau toka kenya
Dkt. Nchimbi akimpongeza mshindi wa
kwanza wa wanawake Anna Kamau

Dkt. Nchimbi akipozi na washindi 10 bora
wa mbio za wanawake, akiwa na maofisa wa TBL

Dkt. Nchimbi na washindi wanaume wa
mbio hizo pamoja na maafisa wa TBL

Bosi wa Trans Africa Logistics Bw. Dewar Twist alikuja na mbwa wake Banny mwenye umri wa miaka 4, na kumaliza mbio hizo na wote wakapewa medali
Wakimbiaji toka mataifa mbalimbali walishiriki
MBIO za Tisa za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon zilirindima jana mjini hapa huku ikishuhudiwa Watanzania watatu pekee Banuelia Brighton, Mary Naali na Stephen Huche wakiingia tatu bora mbele ya Wakenya ambao walitawala vilivyo mbio hizo.

Banuelia ambaye ndiye anashikilia rekodi ya Taifa ya Marathoni kamili kwa Wanawake, aliibuka nafasi ya pili katika mbio hizo za Kilomita 42, akitumia saa 3: 02.52 akitanguliwa na mshindi wa kwanza Anna Kamau aliyetumia saa 3:00.16 kutoka Kenya huku nafasi ya tatu ikienda kwa mwenzake Ophra Oruke 3:03.20.

Machungu yaliwazidi Watanzania mbele ya mgeni rasmi, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, pale kwa upande wa wanaume ambako nafasi ya kwanza ilienda kwa Mkenya Kipkemboi Kipsang aliyetumia saa 2: 17.08 akifuatiwa na Julius Kilimo 2:17.10 huku nafasi ikinyakuliwa mwanariadha anayechipukia hapa nchini Steven Huche saa 2:19.24.

Katika Nusu Marathoni wanawake Valentine Kipketer aliibuka kidedea akitumia saa 1:15.08 akifuatiwa na Loren Kitita 1:15.48 wote kutoka Kenya huku Mtanzania Mary Naali akikamata nafasi ya tatu kwa saa 1:15.55.

Kwa wanaume Michael Kemau aliibuka mshindi wa kwanza akitumia saa 1:03.58 akifuatiwa na Leonard Muchare huku nafasi ya tatu ikienda kwa Geofrey Ndungu saa 1:04.04 wote kutoka Kenya.

Washindi katika mbio hizo walizawadiwa zawadi zao na Waziri Nchimbi ambaye mbali ya kuwashukuru waandaaji kwa kumualika pia alitoa shukrani za pekee kwa wadhamini wakuu wa mbio hizi bia ya Kilimanjaro Premium Lager na wadhamini shirikishi kwa mchango wao katika kukuza mchezo wa riadha.

Alisema, jitihada zao za kuwekeza rasilimali na fedha katika mbio hizo zimeleta faida kubwa kwa kuwapa fursa wanariadha wa Tanzania kujipima na wanariadha wa kimataifa na hatimaye kukuza viwango.

“Mwaka kesho mbio hizi zitafikisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake na vilevile kutakuwa na mashindano ya Olimpiki jijini London Uingereza. Nawaomba msituangushe, jitahidi mtuletee medali za dhahabu kwa upande wa marathoni. Mwaka 2006, Samson Ramadhani alipotwaa medali ya dhahabu kwenye mashindano ya Madola yaliyofanyika Melbourne Australia, sote tulijisikia rah asana na tulifarijika sana. Nawaomba wajitokeze akina Samson wengine watuletee medali za dhahabu,” alisema.

Alisisitiza kuwa, kufanya vema kwa wanamichezo wa hapa nchini Kimataifa kunawapa raha Watanzania, jambo ambalo ni muhimu kwani linawafanya Watanzania kufurahi na kusahau matatizo yao ya kawaida, mbali ya kulitangaza vema jina la nchi kimataifa.

Pia Waziri Nchimbi alielezea kuguswa na maoni ya wadau wakiwamo wa nje ya nchi juu ya utamaduni uliozoeleka kwa viongozi wengi kuthamini soka pekee, hivyo kusisitiza kuwa, yeye si wa aina hiyo ni mdau wa michezo yote na kutoa wito kwa kampuni, taasisi na wadau mbalimbali kujikita katika kuwekeza katika riadha mchezo ambao umeliletea sifa taifa kimataifa kuliko michezo yote.

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa TBL, Emmy Oriyo alisema, kwa kuwa mwaka kesho mbio hizo zinatimiza mwaka wa 10 tangu kuanzishwa kwake, Kilimanjaro Premium Lager inatoa ahadi kwamba itawekeza zaidi katika mbio hizo ili kuhakikisha maadhimisho ya kumi yanakuja na ongezeko la zawadi na udhamini mkubwa zaidi katika maeneo mengine yote.

“Tunatambua kwamba kukimbia marathoni ni jambo gumu sana na changamoto kubwa, lakini tunafarijika kuona vijana wakiwa kwenye ari na msukumo wa aina yake kuhakikisha wanailetea heshima nchi yetu. Nawapongeza sana wanariadha wote walioweza kushiriki mbio hizi na wale wote walioshiriki kujifurahisha kwa kutuunga mkono, maana uwepo wenu ndio umefanya tukio hili kuwa kubwa kama ambavyo nyote mnajionea,” Alisema Oriyo.

Kwa upande wa burudani bendi ya The African Stars Entertainment ‘Twanga Pepeta’ TMK Wanaume Family na Joseph Payne ‘Mzungu wa BSS’ walipagawisha vilivyo.

Mbio hizo za Kilimanjaro Marathoni zimedhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambao ndio wadhamini wakuu, huku wadhamini shirikishi ni Vodacom Tanzania (5 km Fun Run), DT Dobie, TPC Sugar, Kilimanjaro Water, Tanzanite One, Simba Cement, Keys Hotel, Tanzanite One, Precisionair, KK Security na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), huku waratibu wakiwa ni Wild Frontiers ya Afrika Kusini na Executive Solution ya Dar es Salaam.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA






Idadi ya watu
Idadi ya watu
eXTReMe Tracker