In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player
THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT - BEYOND THE ORDINARY - NATURALLY' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.










  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com












Archive for April 2011

Wizi uliotukuka Mlimani City...

Ankal,
Naandika email hii kwa masikitiko makubwa kwa wizi unaoendelea mlimani city. This past Friday I was with 3 friends at samaki x2, after few drinks we dicided to call it a day at around 11 pm, wote tulikuta tumeibiwa site mirror za kushoto, except me was driving a BMW X5 ambapo nilikuta site mirror imevinjika into 4 pieces maana its not easy kuipachua.

I have been reading from your blog kuhusu wizi wa mlimani city but I think improvement will come from boycotts. Please any one reading this email let's stop from going to bars at Mlimani city and this will make owners raise a flag against management and changes will come positively.

Honestly mimi sitaenda tena pale for life.

Mdau wa Globu ya Jamii
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom


DR. SHEIN AENDELEA NA ZIARA YAKE NCHINI UTURUKI

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, Pamoja na Ujumbe wake wakiangalia MIchungwa Iliyoteshwa kwa utaalamu maalum,ikiwa tayari inatoa machungwa kwa muda wa miezi miwili,katika kituo cha utafiti wa kilimo cha Batem,Mjini Antaliya nchini uturuki kwa katika ziara ya Mualiko wa Serikali ya Nchi hiyo.,(kushoto) ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Batem Dr Suat Yilmaz.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,akipata maelezo na MKurugenzi Dr Suat Yilmaz,wa Taasisi ya Batem,wakati alipotembelea kituo cha utafiti wa mazao ya kilimo ,katika mji wa Antaliya nchini Uturuki leo,alioangalia badhi ya tafiti mbali mbali za mazao katika kituo hicho.
Picha na Ramadhan Othman Uturuki.


Faraja Kihongole na Projestus Rwegarulila wameremeta leo

Mwandishi mwandamizi wa kituo cha Televisheni cha Channel 10, Da' Faraja Kihongole akiwa na akiwa amepozi na mume wake, Projestus Rwegarulila baada ya kumeremeta leo Alasiri katika Kanisa la St. Peter Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Da' Faraja Kihongole akiwa amepozi na mai hazbendi ake,
Projestus Rwegarulila pamoja na wapambe wao.
Nondozz zikionyeshwa mara baada ya kumwaga wino.
Shemeji Projestus Rwegarulila akimwaga
wino huku mai waifu wake pamoja na padri wakiangalia.
Da' Faraja Kihongole akimwaga wino.
Wakiingia kanisani.


msaada tutani

Kaka Michuzi pole kwa kazi ya kuendeleza blogu ya jamii.

Mimi ninashida na anuani ya ubalozi wa Tanzania, Bangkok, Thailand. Nilijaribu kutafuta katika mtandao (Google) na nikapata anuani hii (Tanzania Honorary Consulate , Thailand, S.L.D. Condominium, 3rdFL., 501 Saladaeng 1, Rama IV Road,Bangkok10500,Thailand,
Phone: +66-2-2358282 ,+66-2-2358283 ,
Fax:+66-2-2361977).

Nilipofuatilia ubalozi katika anuani hiyo hapo nilipewa maelezo kwamba walishahama miaka 10 iliyopita! Sikukata tamaa na niliamua kuwapigia simu. Simu ikapokelewa na nikajibiwa kwamba hiyo line kwasasa inatumiwa na ubalozi wa New Zealand.

Kaka Michuzi, nimeamua nije hapa kwenye kwenye blogu ya jamii kwani inatembelewa na watu mbalimbali labda kuna mmoja wa wapenzi wa blogu hii anawezakua anafahamu anuani ya ubalozi wa heshima wa Tanzania kule Bangkok, Thailand.

Ombi langu ni kwamba, wadau wa libeneke (blogu ya jamii) tafadhari kama kuna mtu anafahamu anuani au hata namba ya simu nitapenda kufahamishwa! Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Kwa yeyote mwenye anuani hiyo au namba ya simu ya mtu anaeshughurikia masuala ya kibalozi, Bangkok, tafadhari usisite kunifahamisha kwa kutumia barua pepe
52910601@st.kmutt.ac.th

Asanteni sana wadau wa blogu ya jamii.

Mdau wa blogu ya jamii.


JK awaapisha makatibu wakuu wa wizara leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Charles Amos , kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Anna Maembe. kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete, akimwapisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT, Eng. Mussa Ibrahim kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Hab Mkwizu, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma, wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

BOFYA HAPA

kuona picha zaidi.


VODACOM MISS TZ YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR

Hivi ndivyo nembo ya Vodacom Miss Tanzania 2011 itakavyokuwa,ilizinduliwa rasmi hapo jana katika Hotel ya kimataifa ya Kilimanjaro Kempnsiky jijini Dares Salaam.
Mkurugenzi wa Lino Internation Agency waandaji wa Miss Tanzania,Hashimu Lundenga akiongea na kuwatambulisha baadhi ya warembo waliowahi kushiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania miaka ya nyuma katika uzinduzi rasmi wa Vodacom Miss Tanzania 2011.
Mkuu wa udhamini wa Vodacom Tanzania,George Rwehumbiza akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya itakayotumika katika shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 na shindano hilo kuzinduliwa rasmi hapo jana katika Hotel ya kimataifa ya Kilimanjaro Kempnsiky wengine ni baadhi ya warembo waliowahi kushiriki katika kinyang’anyiro cha Vodacom miss Tanzania miaka iliyopita.

kwa picha zaidi
BOFYA HAPA
Link


msaada tutani

Uncle Michuzi mimi namtafuta rafiki yangu niliyesoma naye kwenye shule ya secondary SINZA WAZAZI (ITEBA) miaka ya 2003 - 2004.

Huyu jamaa tulikua tunamwita KC KABETA (Bahati mbaya sikumbuki jina lake kamili) huyu jamaa alikua maarufu saana pale sinza wazazi (iteba). Yeye kipindi hicho alikua anatokea Mburahati.

Uncle Michuzi mimi ni Mjasiria mali niliyepo huku Ughaibuni kwa sasa nataka nifungue kijimtego (Kitega uchumi) hapo Dar es salaam japo kiweze kunisaidia kujikwamua matatizo madogo madogo hapo nyumbani.

Kutokana na tabia za kijitega uchumi hiki kitafaa saaana na naamini kitaenda vyema kikiwa mikononi mwa huyu rafiki yangu KC KABETA, jamaa kwa jinsi alivyo nimependezewa niweke hiki kijitega uchumi mikononi mwake ingawa ni mda mrefu hatujawasiliana na sijui anaendelea vipi na yuko wapi naamini rafiki yangu KC KABETA atanisaidia saana kwani ana sifa zinazoendana na hiki kijitega uchumi.

KC KABETA popote ulipo usomapo ujumbe huu tafadhari tuwasiliane kaka, Ni muhimu saana.

Yeyote anaye mfahamu KC KABETA tafadhari naomba anisaidie ni vipi nitampata.

KC KABETA naomba tuwasiliane kwa email yangu hii
nimimi20@yahoo.com

Asante saana Uncle Michuzi,
Mjasiliamali wa Ughaibuni.


mji wa bukoba unavyoonekana leo

Sehemu ya Mji wa Bukoba unavyoonekana kutokea juu.
Uwanja wa Ndege wa Bukoba.
Kibao kinachokukaribisha katika Mji wa Bukoba.
Jengo la benki ya CRDB tawi la Bukoba linavyomeremeta katika mji huo.
Soko kuu la Mji wa Bukoba linavyoonekana leo.Mitaa ya katikati ya mji wa Bukoba.

kwa picha nyingi zinazoonyesha mandhari ya mji huu wa Bukoba na matukio mengine mengi,tembelea libeneke la Mtaa kwa Mtaa linaloendeshwa na Ankal Othman Michuzi kwa kubofya


WAFANYAKAZI IDARA YA HABARI (MAELEZO) WAMUAGA RASMI MKURUGENZI CLEMENT MSHANA

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Clement Mshana (kushoto) akikabidhiwa zawadi iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Afisa Habari Mwandamizi Bi. Anna Itenda (kulia)wakati wa hafla fupi ya kumuaga rasmi jijini Dar es salaam jana, Bw. Clement Mshana ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) .
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Clement Mshana akiongea na wafanyakazi wa Idara ya Habari jijini Dar es salaam jana wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na wafanyakazi hao.
Wafanyakazi wa Idara ya Habari(MAELEZO) wakiwa katika picha ya pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Clement Mshana(katikati) mara baada ya hafla fupi ya kumuaga rasmi jijini Dar es salaam jana.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.


Rais wa UNDER THE SAME SUN atembelea shule ya msingi Mugeza Mseto Wilayani Bukoba





TWANGA KUWASUGULUSHA KISIGINO VIMWANA WA TWANGA PEPETA MANGO GARDEN.

Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” Jumamosi tarehe 30-04-2011 inataraji kutumia onyesho lake katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni, kuwasugulisha kisigino washiriki wa shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011.

Sugua Kisigino ni mtindo unaotumiwa na Twanga Pepeta na ni moja ya staili zitakazotumika kwenye shindano hilo, hivyo washiriki watatumia fursa hiyo ili kufahamu jinsi ya kucheza staili hiyo.

Washiriki watatumia onyesho hilo ili kusalimu mashabiki wa Mango Garden ukumbi ambao una historia ndefu na Twanga Pepeta.

Onyesho rasmi la utambulisho wa Vimwana wa Twanga Pepeta 2011 unatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 06-05-2011 ndani ya Club ya Sun Cirro iliyoko Sinza na Fainali itakuwa Ijumaa tarehe 03-06-2011.

Burudani ya Utambulisho wa Shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 itatolewa na Wakali wa Dansi Tanzania, African Stars Band “Twanga Pepeta” na Msanii Abbas Kinzasa maarufu kama 20 percent au asilimia ishirini, pamoja na shoo kali ya Nyonga teketeke ya Vimwana wa Twanga Pepeta.

MAIMARTHA JESSE
MRATIBU WA SHINDANO.


mwali wa zanzibar soccer bonanza afichuliwa rasmi



MWALI ATAYEGOMBEWA NA KAMPUNI ZINAZOJIUSISHA NA HUDUMA ZA KITALII HUKO VISIWANI ZANZIBAR AMEFICHULIWA LEO RASMI TAYARI KWA MTANANGE HUO SIKU YA MEI MOSI JUMAPILI KATIKA BONANZA LA MPIRA WA MIGUU, LITAKALO FANYIKA KWENYE UWANJA WA MAO TSE TUNG.


LENGO NI KUKUTANA NA KUFURAHI PAMOJA

NJE YA MAJUKUMU YETU YA KAZI.

WASHIRIKI NI ZANZIBAR SERENA INN, THE RESIDENCE, ZANTEL, THE MONIVARO GROUP, FISHERMAN TOURS NA ZAMANI KEMPINSKI. BONANZA LIANZA SAA MBILI ASUBUHI MPAKA SAA TISA MCHANA.

TUNATARAJIA BONANZA LILATAKOLO KUWA NA HAMASA KUBWA NA KUACHA GUMZO ZANZIBAR, LIKISINDIKIZWA NA MUZIKI MKUBWA

KAMA WEWE MPENDA SOKA NJOO USHUHUDIE VIPAJI VILIVYOJIFICHA KWENYE HII SEKTA USIACHE KUMWAMBIA MWENZAKO KWANI HATAKUPENDA TENA AKIKOSA KUWEPO.

Charles Kisaka
Assistant Front Office Manager
Zanzibar Serena Inn
Zanzibar


NEWS ALERT: MDAU MWEMA AMNUNULIA WHEELCHAIR KIJANA MLEMAVU YOHANA BENJAMIN

Wheelchair mdau aliyojitolea kumnunulia kijana mlemavu Yohana Benjamin aliyeomba msaada tutani katika Globu ya Jamii majuzi (BOFYA HAPA). Mdau mwema huyu kaomba jina na bei ya wheelchair tuweke kapuni.

Ndugu Michuzi kwanza nikushukru kwa kazi nzuri unayoifanya kwa faida ya jamii. Hongera sana. Pichani nimemkubidhi bwana Robert Revocatus – 0763 299960 Wheel Chair kwa ajili ya kijana Yohana Benjamin kama ulivyo onyesha umma kwenye Blog ya Jamii na TBC1 kwenye taarifa ya habari yao ya hapo jana.



Nimehakikishiwa kuwa kesho Robert atapelekwa Pugu Secondary ili akaendelee na masomo yake. Misaada zaidi itatakiwa ukizingatia hali yake na hali harisi ya shule zetu za umma. Kwa nyongeza tu nimekuja kujua kuwa Robert na Yohana ni watu wa Manyovu Kasulu waliohamia Kasangezi. Zaidi mnaweza kuwasiliana naye.
Asante sana kwa kazi nzuri.


TEGETA OYEEE!.


UFAFANUZI WA KAULI YA KATIBU WA BUNGE KUHUSU UELEWA WA KANUNI KWA WABUNGE WAPYA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tarehe 27 Aprili, 2011, Katibu wa Bunge, Dr. Thomas D. Kashililah alizunguza na vyombo vya habari kuhusu masuala makuu matatu:-

1. Utaratibu wa kutunga sheria Bungeni kwa mambo ya jumla
2. Mamlaka ya Spika katika Kazi za Bunge
3. Mwenendo wa Bunge la Kumi hasa Mkutano wa Tatu

Katika maelezo yake Katibu wa Bunge alitoa ufafanuzi wa kina juu ya namna mchakato wa Muswada wa Marekebisho ya Katiba na matumizi ya hati ya dharura (Certificate of Urgency).

Aidha, Katibu wa Bunge pia alifafanua mamlaka ya Spika katika Kazi za Bunge kwa kueleza kuwa katika kazi zake Spika anaongozwa na Kanuni za Bunge ambazo zinampa fursa ya kutoa adhabu kwa Wabunge ambao wanavunja Kanuni au kuonesha vitendo visivyostahili Bungeni na kusababisha uvunjifu wa amani na utulivu Bungeni.

Katika hilo na kuzungumza yaliyojiri katika Mkutano wa Tatu, Katibu wa Bunge alieleza kuwa Spika pia kwa kutambua kuwa wengi wa Waheshimiwa Wabunge ni wapya (asilimia 69 ya Wabunge wa sasa) ambao hawana uzoefu wa mambo ya Bunge, hutumia busara katika maamuzi yake kwa kuwa kutokana na ugeni wao, Wabunge hao bado hawajawa na uelewa mpana wa Kanuni na hivyo lililo muhimu sio kutoa adhabu bali kutoa elimu na kuwaelekeza wanapotenda/kutoa kauli sizo.

Aidha, ni kwa kuzingatia hilo, Ofisi ya Bunge iliandaa semina mbili elekezi zilizofanyika Jijini Dar es Salaam na pia kugharamia semina za vyama vikuu Bungeni – Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyofanyika Dar es Salaam na semina ya Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyofanyika Bagamoyo, mkoani Pwani.
Ofisi ya Bunge imesikitishwa na taarifa potofu zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Katibu wa Bunge amewaita Waheshimiwa Wabunge “mbumbumbu” neno ambalo halikutumika katika mazungumzo.

Ofisi ya Bunge inatambua na kuheshimu kwa kiasi kikubwa elimu na taaluma za Waheshimiwa Wabunge na hili halikuwa sehemu ya mazungumzo na waandishi wa habari.

Ofisi ya Bunge inaheshimu na kuzingatia uhuru wa vyombo vya habari katika kufanya kazi yao lakini inasisitiza kuwa uhuru huo usitafsiriwe kama ni fursa ya kuchonganisha pande mbalimbali katika jamii. Kupachika neno “mbumbumbu” kama kielelezo cha Wabunge kupewa muda wa kuzielewa Kanuni ni upotoshaji mkubwa wa maudhui ya aliyozungumza Katibu wa Bunge ambao hauna lengo jema.

Ofisi ya Bunge inatoa wito kwa waandishi kuzingatia maadili na miiko ya kazi zao wanapotekeleza kazi zao hasa habari za Bunge na Wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi.


Imetolewa Ijumaa tarehe 29 Aprili, 2011 na:-

Idara ya Habari, Elimu kwa Umma
na Ushirikiano wa Kimataifa
Ofisi ya Bunge
S. L. P. 9133
DAR ES SALAAM.


TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA UWEKEZAJI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) Dk. Adelhelm Meru (Kushoto) akizungumza na waandishi Dar es Salaam jana kuhusu mkutano wa pili wa shirikisho la Maeneo huru ya Uwekezaji Afrika utakaofanyika Dar es Salaam mwezi Mei 11-13 mwaka huu

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa uwekezaji wa kimataifa utakao fanyika jijini dare s salaam kuanzia Mei 11 hadi 13 mwaka huu.

Akizungumza na na waandishi wa habari jijini jana Mkurugenzi Mkuu wa kanda ya uwekezaji Tanzania (EPZA) Dk Adelhem Meru, alisema pamoja na Tanzania kuwa mgeni katika kanda huru za uwekezaji duniani, ime onyesha mafanikio na kupewa heshima ya kuwa mwenyeji mkutano huo.

Tuna tarajia kupata washiriki na wa taalamu kutoka mataifa mbalimbali ambao wamefanikiwa na kupiga hatua kiuchumi kupitia fursa huru za uwekezaji na wegeni wengine watatoka Benki ya dunia alisema Dk Meru

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo wa EPZA watoa mada katika mkutano huo Alberto Castronovo ambaye ni mwakilishi wa ukanda huru wa uwekezaji duniani kutoka Italia, Mkurugenzi mkuu wa REPOA Profesa Samweli Wangwe, Thomas Farile kutoka Benki ya dunia wataalam kutoka china Africa na Malaysia.

Lengo la mkutano huu ni kubadilishana uzoefu na utaalamu tunataka kujua wenzetu wamefanikiwaje katika fursa huru ya uwekezaji hadi kufikia kiwango cha juu katika uchumi, tunatakiwa kujifunza kutoka kwa wataalamu hao, kutanua nafasi ya uwekezaji na jinsi ya kuimarisha uongozi tunatumaini tutapata majibu ya pamoja yatakayo saidia kukuza na kuendeleza uwekezaji Barani Afrika.

Alisema pia Mkutano huo utafunguliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda


mdau timoth albert apata kipaimala

Mchungaji wa Kanisa la Mtakatifu Johnson la Mwananyamala jijini Dar es Salaam,Elias Maguu akimpa sakaramenti ya Kimaimala kwa kumuwekea mkono kichwani Timoth Albert wakati wa ibada ya Kipaimala iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Baba mzazi wa Timoth Albert ,Albert Mkomba akimvisha taji la mwanae baada ya kupata sakaramenti ya Kipaimala katika Kanisa la Mtakatifu Johnson Mwananyamala jijini Dar es Salaam,(kushoto) mama yake Elice Mkomba.tafrija ilifanyika katika ukumbi wa Gadern Mwananyamala.
Timoth Albert akinyweshwa Shampeni na mpambe wake Charles Kamaleki wakati wa sherehe ya Kipaimala iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Johnson jijini Dar es Salaam.


BUSTA RHYMES TO HEADLINE BIG BROTHER AMPLIFIED OPENING SHOW!

Busta Rhymes

The news is official and it’s big!

Iconic hip hop superstar Busta Rhymes will headline the two-hour launch show for M-Net’s BIG BROTHER AMPLIFIED when it kicks off on DStv on Sunday May 1 at 20:00. The legendary performer is jetting into Johannesburg this weekend to perform on the Big Brother stage on a night when the continent will meet the new Big Brother housemates!

Busta Rhymes has been setting the standard as a rapper and hip-hop icon, having collaborated with stars such as Diddy, Pharrell, Janet Jackson, Chris Brown & Lil Wayne, including featuring on Tiësto and Diplo track "C'mon (Catch 'Em By Surprise). He has also made several appearances on the big screen including roles on Shaft, Finding Forrester and Halloween Resurrection. His 2006 album, The Big Bang, debuted at No. 1 on the Billboard Top 200 album chart. Seen by many as a living legend, the artist most recently formed his own record label, The Conglomerate, which he partnered with his artist , J Doe and Reek the Villain on the soon to be released movie soundtrack of the Fast & Furious 5 “This is How We Roll” (remix). Busta Rhymes continues to cement his position in the industry as one of the most undeniable performers of all time!

M-Net’s BIG BROTHER AMPLIFIED starts on DStv channel 198 on Sunday May 1. The series is available 24/7 to DStv Premium, Compact Plus and Compact subscribers. The series is headline sponsored by Coca-Cola and produced for M-Net by Endemol South Africa. BIG BROTHER AMPLIFIED will also be available on DStv Mobile in Ghana, Kenya, Namibia and Nigeria.

PLUS in other exciting news…last night (Thursday April 28), the official BIG BROTHER AMPLIFIED website (www.mnetafrica.com/bigbrother) broke with series tradition and gave eager fans a sneak peek of 14 BIG


BROTHER AMPLIFIED housemates

going into the house on Sunday. They are:

TV broadcaster Bhoke from Tanzania (26)

Nightclub manager Confidence from Ghana (37)

Singer and student Hanni from Ethiopia (22)

Rapper and Radio host Herminio from Mozambique (32)

Recording Artist and Marketing/Sales manager Jossy from Namibia (28)

Radio and Club DJ Lomwe from Malawi (27)

Actor and acting coach Luclay from South Africa (28)

Actress Millicent from Kenya (28)

Radio DJ Mumba from Zambia (24)

Artist and Musician Sharon O from Uganda (25)

Model Vimbai from Zimbabwe (24)

Radio Presenter Vina from Nigeria (26)

TV Presenter and Model Weza from Angola (26)

Entrepreneur, artist and marketer Zeus from Botswana (24)


So remember to tune in on Sunday May 1 at 20:00 ,

DStv channel 198!


balozi kallaghe akiwasili harusini

video
Balozi wetu Uingereza Mh. Peter Kallaghe akiwasili Westminster Abbey kuhudhuria harusi ya mwana mfalme William na Kate muda mchache uliopita. Nyuma yake ni Waziri Mkuu mstaafu wa Uingereza Bw. John Major.


mnuso seattle jumamosi hii


WATANZANIA: SEATTLE, WA NA PORTLAND, OR

Kwa niaba ya Mwenyekiti TANZASEATTLE nawakumbusha kuwa sherehe zetu za Muungano ni Jumamosi
hii tar. 30/4/2011 katika ukumbi wa Eritrean Association Hall (1528 Valentine
Place South, Seattle, WA, 98144).
Sherehe zitaanza saa kumi jioni.

Kiingilio ni dola 15 (utapata chakula, utaburudika kwa fashion show, utapata
burudani ya ngoma, utacheza muziki mpaka majogoo). Vinywaji vitauzwa ukumbini (maji na soda ni dola moja moja, bia dola 3). Tutapokea cash au check tu.

Niwakumbushe tu kuwa Fashion show itaongozwa na dada ASIA IDOROUS- KHAMSIN
kutoka Texas, Ngoma na Mr. Kedmon Mapana (Jiandae kucheza ngoma, usisahau khanga za kujifunga) , Muziki na DJ Dully).

Tafadhali usikose, alika jamaa na marafiki
(wageni wote watalipa kiingilio kama
kawaida)

================= NJOO TUSELEBUKE ==============


kumbukumbu

MAREHEMU MWALIMU MUNGUATOSHA KALEBI TEMU

(1923-2010)

Leo tarehe 29/04/2011 umetimia mwaka mmoja tangu Mungu alipomuita baba yetu katika makao ya milele. Japo hayupo pamoja nasi kimwili, lakini bado yuko nasi mioyoni mwetu. Tunakumbuka upendo, ukarimu na ucheshi wake, pamoja na mafundisho, maonyo na maelekezo aliyokuwa akitupa. Tunamshukuru Mungu kwa uvumilivu na ujasiri aliotupa tangu baba alipotutoka.

Unaendela kukumbukwa na mke wako Santa, watoto wako na wenzi wao, dada zako, mdogo wako, shemeji zako, wajukuu, vitukuu, marafiki na wanaukoo wote.

“BWANA ALITOA NA BWANA AMETWA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE”


Moshi wazindua mradi wa hifadhi mazingira

Meya wa manispaa ya Moshi,Mstahiki Jafary Michael akizungumza na wananchi katika kata ya Kiusa ambako alizundua mpango wa hifadhi mazingira .
Sajini Meja wa kambi ya polisi iliyopo kata ya Kiusa Afande George akipanda mti katika eneo la line polisi mara baaada ya uzinduzi wa mpango wa kuhifadhi mazingira katika kata ya Kiusa.
Mstahiki Meya wa Moshi Jafary Michael akiotesha mti wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuhifadhi
mazingira uliozinduliwa katika kata ya Kiusa.
Mstahiki Meya Jafary Michael akipanda mti
Diwani wa kata ya Kiusa Bw. Steven Ngasa akimnawisha mikono Meya Jafary Michael mara baada ya kuzindua mpango wa hifadhi mazingira katika kata ya kiusa.

Picha na habari na Dixon Busagaga
wa Globu ya Jamii, Moshi.

MEYA wa manispaa ya Moshi,Mstahiki ,Jafary Michael(Chadema) amezindua mpango rasmi wa hifadhi na utunzaji wa mazingira katika maeneo ya wazi,vyanzo vya maji na makazi ya wananchi ambapo kwa kipindi cha mwaka huu wanatarajia kuotesha na kuitunza zaidi ya miti 2000 katika kata ya Kiusa.

Akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni hiyo,Meya Michael alipongeza kata ya Kata ya kiusa kwa kutambua suala la mazingira ambalo ni sehemu ya mipango ya manispaa katika kutunza mazingira jambo ambalo limeiujengea heshma mji huo.

Alitoa rai kwa kata nyingine kuiga mfano huo ili kuleta mapinduzi ya mji wa Moshi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma na kwamba manispaa itawaunga mkono wananchi katika utekelezaji wa suala hilo.

Aidha Meya Michael alisema manispaa pia inafanya mipango ya kutunga sheria ndogo ndogo ambazo zitavithamini,kuvitambua na kuvilinda vikundi vya kijamii ambavyo vimeundwa kwa lengo la kutunza mazingira.

Awali diwani wa kata hiyo,Stephen Ngasa alisema mpango wa utunzaji mazingira utahusisha zaidi ya nyumba 16,000 katika kata hiyo ambapo kila nyumba inatakiwa kuotesha miti mawili mbele ya nyumba.
Alisema katika uzinduzi huo zaidi ya miti 700 iliyotolewa na kikundi cha mazingira kata ya Kiusa(KIMAKAKI)itaoteshwa katika eneo lililopo mkabala na kambi ya jeshi la Polisi mjini humo huku pia familia za
askari zitashirikisha ili kuotesha katika makazi yao.

Mapema mwenyekiti wa Kikundi cha Kimakaki,Redemta Shirima alisema kikundi hicho kilichoanzishwa mwaka 2006 tayari kimeotesha na kuitunza zaidi ya miti 3000 katika shule za Msingi Kilimanjaro,Muungano,Kiusa na Jamuhuri kando ya barabara tofauti.

Bi Shirima pia aliomba manispaa hiyo kuwasaidia misaada mbalimbali ikiwamo utaalamu wa kudhibiti magonjwa ya mimea,vyanzo vya kudumu ya mapato ili waweze kupata uwezo wa kueneza elimu ya utunzaji wa mazingira katika taasisi nyingi zaidi..


ratiba ya msiba wa leicester na tanzania

Align Center
Hayati Sheikh Ali Samin Jaha

Assalaam Alaikum,

Inna lillahi wa inna ilaihi raajiuun. Jumuiya ya Watanzania Leicester, Uingereza inasikitika kutangaza kifo cha ndugu yao, Sheikh Ali Salmin Jaha, kilichotokea tarehe 27 Aprili 2011. Maiti itaswaliwa saa kumi na moja na nusu jioni (5.30 pm) Leicester Central Mosque, Conduit Street, LE2 OJN. Karibu na train station.

Mwili wa marehemu utasafirishwa siku ya jumamosi tarehe 30 Aprili 2011 kuelekea Dar es salaam inshaAllah na pia mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya jumaapili tarehe 1 may 2011

Kwa yeyote mwenye mchango wake wa hali na mali awasiliane nasi kwa namba zifuatazo:

Namba za simu : Suwedi Abdallah +447796080601

Salim Awadh +447949421087

Rashid Saadallah +447896916032


mama bishanga ameremeta

Msanii mkongwe wa tasnia ya filamu Bi Christina Innocent a.k.a Mama Bishanga akiwa na mai hazbendi wake Bw. Marolen wakati wa kumeremeta hivi karibuni katika kanisa la St. Peters jijini Dar. Bw Harusi anatokea Limpopo, Sauzi. Hivi sasa wako Columbus, Ohio, Marekani ambako ndiko wanaishi
Ni wakati wa kukata keki kwenye mnuso hoteli ya Peacock jijini Dar
Bi Harusi akiingia Peacock hotel kwenye ukumbi kwa mila za Wamakua wanawake hulala chini na bibi harusi kupita juu yao mpaka kwenye kiti atapokaa


washiriki wa Big Brother amplified inayoanza jumapili

Another exciting new development this season is that Sunday's Launch Show will be going multi-media!
There will be live streaming of the two-hour opening on the official website at no cost, marking the first time in the history of the African series that this has happened!
And for audiences who log on early, there’s a special 15 minute pre-show exclusive to online audiences that begins at 18:45 CAT on Sunday 1 May.

Watch Online from Anywhere
So whether you’re watching online or whether you are watching on DStv, make sure you don’t miss the start ofBig Brother Amplified.
Big Brother Amplified starts on DStv Channel 198 on Sunday, 1 May at 19:00 CAT.
The series is available 24/7 to DStv Premium, Compact Plus and Compact subscribers.
The series' headline sponsor is Coca-Cola and it is produced for M-Net by Endemol SA.
Big Brother Amplified will also be available on DStv Mobile in Ghana, Kenya, Namibia and Nigeria.


Bhoke
Age 26
Hometown Dar es Salaam, TANZANIA
Occupation TV Broadcaster
Confidence
Age 37
Hometown Accra, GHANA
Occupation CEO of MultiMedia Company / Aphrodisiac Nightclub
Hanni
Age 22
Hometown Addis Ababa, ETHIOPIA.
Occupation Singer and Student
Herminio
Age 32
Hometown Maputo, MOZAMBIQUE
Occupation Rapper and Radio Host
Jossy
Age 28
Hometown Windhoek, NAMIBIA.
Occupation Recording Artist / Marketing,Sales and Ad Manager
Lomwe
Age 27
Hometown Blantyre, MALAWI
Occupation Radio and Club DJ
Luclay
Age 28
Hometown Cape Town, SOUTH AFRICA
Occupation Actor / Acting Coach
Millicent
Age 28
Hometown Nairobi, KENYA.
Occupation Actress
Mumba
Age 24
Hometown Lusaka, ZAMBIA
Occupation Radio DJ
Sharon
Age 25
Hometown Kampala, UGANDA
Occupation Artist / Musician
Vimbai
Age 24
Hometown Harare, ZIMBABWE
Occupation Model
Vina
Age 26
Hometown Lagos, NIGERIA
Occupation Radio Presenter
Weza
Age 26
Hometown Luanda ANGOLA
Occupation TV Presenter, Model
Zeus
Age 24
Hometown Gaborone, BOTSWANA
Occupation Entrepreneur, Artist, Marketer


Idadi ya watu
Idadi ya watu
eXTReMe Tracker