Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohd Shein akiwahutubia viongozi na wananchi mbalimbali hawapo pichani katika ukumbi wa salama Holl Bwawani zanzibar baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani.
Naibu mufti wa Zanzibar Sheikh Swaleh Omar Kaabi akimkaribisha Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuhutubia katika Baraza la Idi ambalo lilifanyika katika ukumbi wa Salama Holl Bwawani mjini Zanzibar.
Umati katika Swala ya Iddi uwanja wa Maisara
Baadhi ya kinamama waliohudhuria katika swala ya Idi Elfitri huko katika kiwanja cha Maisara mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar Alhaji Dr,Ali Mohd Shein pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali na wananchi,wakiwa katika swala ya iddi ambayo imeswaliwa kitaifa katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Alhaji Dr,Ali Mohd Shein pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali na wananchi,wakiwa katika swala ya iddi ambayo imeswaliwa kitaifa katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.
Rais wa zanziba Dr Ali Mohd Shein akisalimiana na Rais Mstaafu Mh. Amani Abeid Karume katika kiwanja cha Maisara mjini zanzibar kwa ajili ya kuswali swala ya Idi Elfitri.
Makamo wa kwanza wa Rais Seif Sharif Hamadi akisalimiana na Waziri wa katiba na Sheria wa Zanzibar Abubakari Khamis Bakari baada ya kuingia katika kiwanja cha maisara mjini zanzibar kwa ajili ya kuswali swala ya Idi Elfitri.
Rais mtaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume akisalimiana na Waziri wa katiba na sheria wa Zanzibar Abubakari khamis Bakari baada ya kuingia katika kiwanja cha maisara mjini zanzibar kwa ajili ya kuswali swala ya Idi Elfitri.
PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI MAELEZO ZANZIBAR
Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi M, Al Hajj Dk Ali Mohamed Shein amesema Serikali imeandaa mipango kuhakikisha inaongeza fursa zaidi za ajira rasmi na zisizo rasmi Visiwani Zanzibar.
Akihutubia Baraza la Eid-El-Fitri Mjini hapa jana, Dk Shein alisema katika mwaka wa Fedha 2011/2012 Serikali inatarajia kuajiri watu 2,476 kulingana na mahitaji na uwezo uliopo.
“Tunaelewa kuwa mahitaji ya fursa hizo ni makubwa zaidi…katika kukabiliana na uhaba wa fursa za ajira, Serikali inashajiisha wananchi kujiunga katika vikundi vya Ushirika ili waweze kunufaika” Alisema Rais Dk Shein.
Dk Shein alisema kuwa mkazo umewekwa katika kuvisaidia vikundi vya uzalishaji mali vinavyoanzishwa na vijana na wanawake ili waweze kujiajiri wenyewe wajiongezee kipato na kupambana na umaskini.
Akizungumzia mwezi mtukufu wa Ramadhan, Rais Dk Shein aliwakumbusha waumini wa Dini ya Kiislamu na wananchi wote nchini kuitumia elimu waliyoipata katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani kuimarisha mwenendo mwema na kujenga maisha bora ya duniani na akhera.
Dk Shein alisema suala la kudumisha amani, umoja na kuheshimiana miongoni mwa waislamu na wale wa dini nyengine kumewezesha kuendesha ibada hiyo katika hali ya amani na utulivu.
Alisema kwamba kuendeleza mwenendo mwema na kujiepusha na vishawishi vinavyoweza kuleta matatizo na kusisitiza suala la kujenga uadilifu hasa katika sehemu za kazi kwa wafanyakazi kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Sherehe hizo zilitanguliwa na swala ya Iddi iliyofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja na kuhudhuriwa na Makamu wa kwanza wa Rais, Seif Shariff Hamad, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd na viongozi wengine wa Serikali, Dini na Vyama vya siasa.