In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player
THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT - BEYOND THE ORDINARY - NATURALLY' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.










  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com












Archive for October 2011

NAPE AMALIZA MGOGORO CCM HOUSTON.

Katibu wa NEC ya CCM,Nape Nnauye akiongea jambo kwenye mkutano wa Viongozi na wanachama Tawi  la CCM Houston,Texas,Nchini Marekani.
Juu na chini ni Wadau na wanachama wa CCM Tawi la Houston,Texas wakimsikiliza Katibu wa NEC ya CCM,Nape Nnauye alipokua akizungumuza nao kwenye mkutano huo.
Viongozi wa CCM tawi la Houston,Texas,Nchini Marekani wakipata picha ya pamoja baada ya mkutano huo.
 Wakubaliana kufungua tawi  kila Jimbo
: Ageuka kivutio mkutanoni.
: Wasema kwa mwendo huu CCM jabali.
: Wampa jina Simba wa Vita Mtoto.
: Asema atakufa kwa mapenzi ya Mungu si ya binadamu.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi bwana Nape Nnauye amemaliza mgogoro wa CCM Houston uliodumu kwa muda mrefu sasa kwa kuwataka wanaCCM waaishio Marekani kufungua matawi kila jimbo wanapoweza ili kukisogeza Chama karibu na watu.
"Uamuzi wa kukisogeza Chama kwa wanachama zaidi ni maagizo ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM. Hamuwezi kuwa na tawi moja Marekani nzima na mkadhani litafanya kazi vizuri kwa ufanisi, kila jimbo idadi ya wanachama ikitosheleza fungueni mashina kisha tawi" alieleza Nape.

Akihitimisha ziara yake kwa jimbo la Texas jijini Houston juzi, Nape alikutana na Jumuiya ya Watanzania waashio Houston na kutangaza uamuzi huo ambao ulipokelewa kwa furaha na Wana CCM na Watanzania waishio hapo.

" hakika CCM imepata katibu mwenezi, mgogoro huu ulidumu kwa muda na kukiathiri sana chama hapa Marekani lakini kuja kwa huyu bwana kumekata kabisa mzizi wa fitina, sasa CCM itaimarika zaidi Marekani" Alisema bwana Kittoga Mtanzania aishie Houston.

Nape akiwaeleza watanzania waliokusanyika  kumsikiliza, akisema kulikuwa na matatizo kidogo ya tafsiri ya katiba ya CCM na maamuzi ya Chama jambo ambalo sasa amelimaliza na anamatumaini kuwa CCM Marekani itakuwa imara na chachu nzuri ya mabadiliko ndani ya Chama na nchini Tanzania kwa ujumla.
"kimsingi tofauti zilizokuwepo zimekwisha, hazikuwa kubwa ila ilikuwa ni tofauti za tafisiri tu katika utekelezaji wa katiba na majukumu ya kila siku ya Chama hapa Houston. Tumeyamaliza na sasa kazi ni moja, tawi hili liwe chachu ya mabadiliko ndani ya chama na nchi na liwe chanzo cha Umoja na mshikamano kwa Watanzania waishio Jimbo la Texas." alisema Nape.

Alipofika jijini Houston, Nape ambaye ameambatana na Katibu Msaidizi mkuu Itikadi na Uenezi Ndg. Sixtus Mapunda alifanya kikao na viongozi wa CCM Houston na kujadili mgogoro uliotokea na jinsi ya kuutatua. Kikao hicho kifanyika mpaka usiku wa manane wa tarehe 28/10/2011.

Kesho yake jioni Ndg. Nape na ujumbe wake walikutana na jumuiya ya Watanzania waishio Houston ambapo alitumia muda mwingi kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa Watanzania hao na kuelezea mambo mbalimbali yanayoendelea nyumbani Tanzania.

Katika hali isiyotarajiwa vijana wawili wa Kitanzania waliojitambulisha kama wanachama wa Chadema walifika eneo la mkutano na mabango yaliyokuwa na kauli mbalimbali za kuikejeli CCM, lakini Nape alikwenda na kupokea mabango hayo na kuwashukuru vijana hao kwa kutumia uhuru wao wa kujieleza kueleza wanachokiwaza juu ya CCM.
" siasa sio ugomvi, hawa rafiki zangu wametumia uhuru wao wa kujieleza na kuandika mabango haya, japo ni kijiko kimoja cha sukari baharini, si sawa na kutokuwepo kabisa, mmefanya mkutano uwe mzuri, sasa kaeni msikilize sera badala ya kuimba ngojera za kwenye mabango" aliwaambia Nape.

Kauli iliyopokelewa kwa makofi na vifijo na kelele za ccm, ccm,ccm. Kisha Nape akapiga nao picha wakiwa na mabango yao nakuwa hakikishia kuwa ujumbewao umefika.

Baada ya masaa mawili na nusu ya maswali na majibu, Nape aligeuka kuwa kivutio kikubwa pale alipoonyesha uwezo mkubwa wa kuelezea mambo yanavyoendelea nyumbani, mafanikio na changamoto zake, kiasi cha kupelekea mashabiki wa Chadema ukumbini kulipuka kwa furaha wakimwita Nape Simba wa Vita mtoto.
" hakika bwana mdogo kiboko! Kwanza umeonyesha uvumilivu mkubwa wa kisiasa kwa kipokea mabango yetu. Lakini jinsi ulivyojibu maswali hata yaliyokuwa yanakera sana, wewe ni simba wa vita mtoto baada ya Mzee Kawawa. Sasa CCM mmeamka! Ntachukua kadi ya CCM!" alisema kada mmoja wa Chadema.

Baada ya kikao hicho karibu Watanzania wote waliokuwepo ukumbini ambao hawakuwa wanachama wa CCM walikwenda kuomba kupewa kadi za CCM kwa madai kuwa kwa mwendo huo CCM sasa imepata mwelekeo mpya wenye matumaini.

" tulishapoteza matumaini sana na Chama hichi hasa sisi vijana, lakini kwa mwendo huu sasa matumaini yapo. Alikuja Zito hapa alipata watu kama kumi na moja hivi, kaja huyu Nape watu hapa ni zaidi ya sitini na wote wameondoka wameridhika hili si jambo la kawaida Houston" alisema Liliani Mtanzania aishie Dallas.

Akijibu swala la Bwana Fue juu ya hoja kuwa kuna wanasiasa wanatafutwa kuuawa kwasababu ya misimamo yao juu vita dhidi ya ufisadi naye Nape akitajwa, Nape alisema.
"siamini kabisa kama naweza kufa kwa mapenzi ya binadamu. Mkisikia nimekufa mjue ni mapenzi ya Mungu kwani Mungu ninaye mwamini yuko juu ya yote, hata wanaowaza mabaya juu yangu"

" hata hivyo kuwaza mabaya juu ya vita hii ya matumizi mazuri ya rasilimali za nchi, hawamuwazii mabaya Nape ila watanzania wote na wapenda nchi yetu wote, hivyo kwa hakika hawatashinda, kwani sauti ya wengi ni sauti ya Mungu." alisisitiza Nape

Kwenye muafaka,  Nape kawaelekeza wana CCM wa Texas kuacha mifarakano na kuwataka kufanya mchakato wa kufungua mashina manne ya CCM Texas na kisha ameahidi kuja mwenyewe kwenye ufunguzi wa Tawi la CCM Texas na majimbo mengine kama watakavyojipanga.

Aidha alimalizia kwa kuwataka Wana CCM kutumia matawi yao ya Chama kuwaunganisha Watanzania badala a kugeuka vijiwe vya majungu na kubaguana kwa vigezo vyovyote vile, huku akiwataka kuweka Utanzania wao kwanza kuliko itikadi na tofauti zao malimbali.

Nape anaendelea na ziara yake nchini Marekani yenye lengo la kukagua uhai wa chama, ambapo atatembelea Columbus-Ohio, New York na atamalizia Washington Dc, kabla ya kurejea nchini Tanzania wiki ya kwanza ya mwezi Novemba.


Dr Shein azindua tawi la benki ya wananchi wa zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi wa Chake chake Pemba wakati wa uzinduzi wa tawi la benki ya wananchi wa Zanzibar PBZ, Pemba,ambapo huduma ya ATM pia itapatikana kwa saa 24.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Kaimu Waziri wa Fedha Dk Mwinyihaji Makame,akitoa nasaha kwa wananchi na kuwataka kuweka fedha zao katika benki ya watu wa Zanzibar tawi la Chake chake leo,wakati wa uzinduzi rasmi uliofanywa na Rais wa Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein,akitoa pesa kwa kutumia huduma ya ATM mara baada ya kulizindua  Tawi jipyala PBZ huko Chake chake,Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein,akionesha pesa alizotoa kupitia matandao wa ATM kwa benki ya watu wa Zanzibar PBZ,baada ya kuzindua rasmi tawi jipya la chake chake Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein,akijaza fomu ya kujiunga na benki hiyo mara baada ya kulizindua  Tawi jipya la PBZ huko Chake chake,Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk Ali Mohamed Shein,akitia saini fomu za kuweza kupatiwa ATM card ya kutolea pesa katika Benki ya watu wa Zanzibar katika sehemu lilipo tawi la Benki hiyo,wakati wa uzinduzi wa tawila PBZ Chake chake Pemba jana,(kushoto) Mkurugenzi mtendaji Juma Amour.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk Ali Mohamed Shein,akiteta jambo na Mkurugenzi wa Benki ya watu wa Zanzibar PBZ Juma Amour,wakati wa sherehe za uzindu wa   Tawi jipyala PBZ huko Chake chake,Mkoa wa Kusini Pemba.
Baadhi ya waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa Tawi la Benki ya watu wa Zanzibar PBZ,wilaya ya Chake chake Pemba,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi katika sherehe za uzinduzi wa tawi hilo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na wasoma utenzi wakati wa uzinduzi rasmi w2a tawi la PBZ leo huko Chake chake Pemba.Picha na Ramadhan Othman Pemba.


Kumbukumbu ya Mama Bernadette Wawuda Msafiri: October 24, 1943 – November 1, 2010

Hatukujua asubuhi ile Mungu angekuita.
Katika maisha tulikupenda na katika kifo hivyo hivyo. 

Tulivunjika moyo kukupoteza, hukwenda peke yako bali sehemu yetu ilikwenda pamoja nawe siku ile Mungu alipokuita nyumbani.

Umetuachia kumbukumbu nzuri, upendo wako ni muongozo wetu. Japo hatukuoni wakati wote uko pamoja nasi. Kiungo katika familia yetu kimevunjika, maisha yetu hayako sawa tena. 
Lakini kadri Mungu atakavyotuita mmoja mmoja viungo vitaungana tena.

Unakumbukwa na Mume wako, watoto, 
wajukuu, ndugu, jamaa na marafiki.

Kutakuwa na Misa ya Kumbukumbu siku ya Jumatano 
tarehe 2 Novemba 2011 saa 11 jioni 
katika makaburi ya KONDO ( Tegeta ), Dar es salaam


Nyote Mnakaribishwa


Mawasiliano simu namba 
+255 754 434632/+255 656 238471
(Francesca Msafiri)

BWANA ALITOA,  NA BWANA AMETWAA
JINA LAKE NA LIHIMIDIWE
AMINA


kampuni ya mawasiliano ya UHURU ONE yaingia sokoni kwa kishindo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa kampunia ya  Uhuru One, Bw. Mihayo Wilmore, kuhusu matumizi rahisi ya kompyuta ndogo na mpango wa kuzisambaza na kuwawezesha wanafunzi wa Tanzania kutumia kompyuta hizo, wakati wakati akikagua banda la maonyesho la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) uliofanyika Geneva, Switzerland Oktoba 24, 2011. Kulia ni  Bw. Tahir Haroub Othman, mmoja wa wakurugenzi wa Uhuru One, kampuni inayokuja juu sana nchini Tanzania katika sekta ya mwasiliano kwa njia ya mtandao.


wasanii Carolla kinasha na paul ndunguru wakiwakilisha katika tamasha la umoja Music festival jijini Maputo, Msumbiji

 Sanamu ya kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Msumbiji Hayati Samora Machel jijini Maputo baada ya uzinduzi wake Oktoba 19, 2011 ambapo wasanii Carolla kinasha na Paul Ndunguru walishuhudia na kushiriki katika tamasha la Umoja Music Festival lililoenda sambamba na uzinduzi huo
 Msanii Paul Ndunguru (kulia) akiwa na gwiji la muziki toka Zimbabwe Oliver Mutukudzi kwenye tamasha hilo
Paul Ndunguru (wa tatu shoto) na Carolla Kinasha wakijumuika na wanamuziki Ray Phili (shoto) na Oliver Mutukudzi jukwaani (wa tano toka shoto) pamoja na wasanii wengine kwenye tamasha hilo.

Wasanii maarufu wa muziki halisia,  Paul Ndunguru na Da' Karola Kinasha hivi karibuni wamemetoka Maputo, Msumbiji, kwenye tamasha kubwa la muziki la Umoja Music Festival linalofanyika kila mwaka likijumuisha nchi ya Kenya Uganda,Afrika kusini na wenyeji Msumbiji.

Wasanii hawa wanajisikia kupata heshima kubwa kuimba na magwiji kama Oliver Mutukuzi wa Zimbabwe na Ray Phiri wa Afrika kusini ambaye ni mpiga gita na mwimbaji,  ambaye ndiye  aliyetunga na kutengeneza nyimbo sita kwenye album ya 'Grace land'  iliyompa umaarufu,  heshima na utajiri nguli wa muziki Paul Simon, wakati huo akiwa katika harakati za  kushinikiza Nelson Mandela aachiwe huru. 

Ray Phiri anasema "najivunia kwa jinsi (Mandela)  alivyotoka jela, niliuza haki miliki ya nyimbo kwa mzungu huyo. Hivyo hivyo nilimtumia mzungu kupata nichotaka kwa nchi yangu, Mandela anatambua hilo" mwisho wa kunukuu.

Lingine kubwa waliloshuhudia Paul na Carolla ni uzinduzi wa sanamu ya kumbukumbu ya Rais wa kwanza wa Msumbiji, Hayati Samora Machel, iliyo zinduliwa tarehe Oktoba 19, 2011. Katika sanamu hiyo Hayati Samora anaonekana akiwa amenyoosha kidole kimoja kukumbuka maneno yake aliyosema."Kama ninapata kilo moja ya mchele, basi kila Mmozambiki apate kilo moja ya mchele"

Paula na Carolla wanasema inaleta raha kuona jinsi wananchi wa Msumbiji wanavyomuenzi shujaa wao na wanajiuliza sisi watanzania tunamuenzi vipi BABA WA TAIFA? Hawapendi i kuzungumzia kwama sanamu hii,   kama ile ya Dr Martin Luther king jr kule  Washington kuwa imetengenezwa na Mchina, licha ya kwamba Wamakonde wa 'Nchumbiji' kuchonga masanamu ndio kazi yao......


In everlasting memory

The late Mwl. Zephaniah
E. R. N. Memba 


Our beloved father,
It seems like yesterday but it’s already six years since you departed from us to join our father in Heaven.  

You are still vivid and real in our hearts and minds.  Although physically you are not with us, spiritually you are in our hearts daily.  Indeed you were a special gift to us from GOD. We thank the Almighty GOD for the time you spent with us. We miss you great but we always take courage and hope in the verse you left with us from Romans 8: 31 
“If GOD Be For US, Who Can Be against Us?”

You are deeply missed and remembered by your wife, Mama Ukende P Memba, Your children, Joyce, Albert, Rhoda, Imani, Flora and Peter, in-laws, Maria Makalla Memba, William Stephen Kotta, Johnson Nyingi, and grandchildren, Joshua, Milan David, Nkambujah Romeo, Rodney Ngadumka, Ukende Ronia, Rowan Tyalambula, Ukende Rondelle, Rochelle and Ukende Ashley. 


UNFPA lasherehekea kilele cha dunia kufikisha watu bilioni 7,yatoa msaada wa vifaa mbalimbali hospitali ya Temeke jijini dar leo.

Muwakilishi wa shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania,Dr . Julitta Onabanjo akiwa amembeba mtoto aliyezaliwa usiku wa kuamkia leo,kwenye hospitali ya Wilaya ya Temeke, jijini Dar Es Salaam,ambapo Dunia ilikuwa inatimiza idadi ya watu Billioni 7. Kulia ni Mama wa Mtoto huyo Bi Kulwa Juma. Picha Zaidi BOFYA HAPA


Dont miss Filamu Lounge this coming wednesday


shirika la nyumba la taifa laweka historia kwa kuanzisha mfumo wa mikopo ya nyumba likishirikiana na mabenki saba

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka (katikati, nguo nyekundu), Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu (wa nne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa benki saba zilizosaini makubaliano ya ushirikiano na NHC ambapo wananchi sasa watakuwa na fursa ya kujenga nyumba kwa njia ya mikopo (mortgage) badala ya huu mtindo uliopo wa kujenga hadi ghorofa ishirini kwa kutumia keshi. Kwa habari kamili na mapicha ya kumwaga BOFYA HAPA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KATIKA baadhi ya vyombo vya habari jana na leo, kumeripotiwa taarifa za kuwapo kwa ugomvi baina ya wachezaji wawili wa Simba, Emmanuel Arnold Okwi na Haruna Moshi Shaaban (Boban). Ugomvi huo umeripotiwa kutokea mara baada ya pambano la watani wa jadi lililofanyika jana katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Vyombo hivyo viliripoti kuwa chanzo cha ugomvi huo ni madai ya hujuma na kutoaminiana ndani ya timu. Kwa masikitiko makubwa, Simba Sports Club (SSC) inapenda kukanusha kwa nguvu zote kuwapo kwa ugomvi wa aina yoyote baina ya wachezaji au viongozi wa klabu mara baada ya pambano la Jumamosi.

Mara baada ya mechi, hali iliyotamalaki ilikuwa ni ya fadhaa na huzuni kwa wote wanaohusika na Simba, wakiwamo wachezaji na washabiki. Habari hizo za ugomvi wa wachezaji ni uzushi unaoenezwa na watu wasioitakia mema SSC.

Kuna mambo mawili yanayoweza kubainisha kuwa habari hizo hazikuwa za ukweli. Kwanza, kwamba vipo vyombo vilivyodai kuwa Okwi alipigwa hadi kuvimba uso. Ukweli ni kuwa Okwi yuko salama, buheri wa afya na hajavimba popote mwilini mwake, achilia mbali usoni.

Pili, kuna magazeti yaliyoandika kuwa Okwi alipigwa vichwa vinne na Boban kabla hawajaamuliwa. Mengine yakaripoti kichwa kimoja. Kuna redio imeripoti kuwa vilikuwa vichwa vitatu. Tukio moja, taarifa tofauti lukuki. Kikubwa ni kuwa, hakuna mwandishi wa habari hata mmoja aliyeshuhudia tukio hilo na kulithibitisha pasi na shaka zaidi ya kusimuliwa na wale waeneza uongo.

SSC inashukuru kwa ushirikiano mzuri inaopata kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya nchini na nje. Tunawaomba wana Simba wawe watulivu katika kipindi hiki na tujipange kwa ajili ya mechi yetu ijayo ya VPL dhidi ya Moro United. Kama tutashinda, tutaongoza ligi hadi mwakani.

Timu inarejea kambini leo tayari kujiandaa na pambano hilo la mwisho la raundi ya kwanza ya VPL.

Ezekiel Kamwaga
Msemaji
SSC


cheka unenepe na lugha gongana: English as a second language

*These are actual occurences: English teacher at a  secondary School: "The girl goes to school, goesn't  she?

*A teacher in a school:  Both of you three...come here!"


*An irritated teacher to a student: "Tomorrow I want you to come 
with your father, your mother and both your parents!"

*On seeing twins enter his office, the deputy principal at a certain 
school said:" You look together; are you twice?"

*A guy heard a teacher scolding  two boys who were arguing: "Don't speak twice together, man, Speak once upon a time!

*An English teacher inquiring as to who took his pen: "Who took my pen 
yesterday? 
- John replies: "Not me teacher I tookn't, Sharifa took it." 
- Sharifa to John: "Took me, Took you?'' 
- John replies: "Took you!"



* Teacher to students in class: "Its bad manners if you go into a house in-direct without knocking before..."


nyumba inauza Kihonda-Bima, Morogoro

  Nyumba inauzwa mjini Morogoro. Ina  3 bedrooms, 1 self container, Sebule, Jiko, Na Toilet. Pia ina eneo la kutosha, na ipo barabarani. Ipo maeneo ya Kihonda-Bima. Bei sh 28 millioni, ila maelewano yapo. Kwa mawasiliano jinsi ya kuiona piga/sms +255 762 560088.


KLINIKI YA SOKA YA AIRTEL RISING STAR YAANZA UWANJA WA TAIFA

 Kocha wa soka ya vijana kutoka Manchester United, Paul Bright akionyesha kwa vitendo namna ya kusakata kabumbu wakati wa mafunzo ya kliniki ya soka ya kimataifa ya vijana ya 'Airtel Rising Stars' yaliyoanza jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam. Katikati ni Graham Naftali na Samir Omary (kulia).
 Mshiriki wa kliniki ya soka ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, Naomi Njeri akimtoka mshiriki mwenzake Emily Auma wakati wa mafunzo ya kliniki hiyo yaliyoanza jana kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi mkuu wa kliniki ya soka ya kimataifa ya vijana ya 'Airtel rising Stars', Billy Miller kutoka klabu ya manchester United ya Uingereza, akijadili jambo na kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Vijana ya Tanzania, Kim Poulsen, wakati wa mafunzo hayo yaliyoanza jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


LADISLAUS J. MWAMANGA ateuliwa kuwa MKURUGENZI MTENDAJI TASAF

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bwana LADISLAUS J. MWAMANGA kuwa MKURUGENZI  MTENDAJI WA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF).
            Kabla ya hapo Bwana Mwamanga alikuwa 
Meneja wa Mifumo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF.

            Uteuzi huu unaanzia tarehe 1 Novemba, 2011.

Peter A. Ilomo
Kny:  KATIBU MKUU, IKULU


hawa choka ala nondozzzz ya kumaliza kidato cha 4 shule ya kandoto

 Mama Faiza Choka akimpongeza bintiye  Hawa Choka  baada ya kula nondozzz ya kuhitimu  kidato cha 4 siku ya Jumamosi katika  Shule ya Sekondari ya Sayansi Wasichana ya Kandoto, Same.
Picha ya pamoja Bamdogo Maez, Mama Mzazi Faiza Choka na bintiye  Hawa Choka baada ya kula Nondozz Kidato cha 4 Kandotio Girls.


MATUKIO KIJIJINI NYANDIRA ,TARAFA YA MGETA, WILAYA YA MVOMERO, MOROGORO LEO

 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kulia) akiongozana na DAS wa Wilaya ya Mvomero ( kushoto) pamoja na Viongozi wengine baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa Kata ya Nyandira, Tarafa  ya Mgeta, Oktoba 29, mwaka huu.
 Wakazi wa Kata ya Nyandira, Tarafa ya Mgeta, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, wakiwa na matumaini ya kupata nishati ya umeme baada ya nguzo kuwekewa baadhi ya maeneo ya Kata hiyo kama zinavyoonekana.
Gari la Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, likitelemka kwenye milima ya safu ya Uluguru Kaskazini na Ulunguru Kusini, katika Tarafa ya Mgeta, Wilaya ya Mvomero, Mkoani Morogoro, Oktoba 29, mwaka huu, wakati Mkuu wa Mkoa huo, Joel Bendera alipowatembelea wananchi wa Tarafa hiyo, ambapo aliifananisha milima hiyo na ile ya Lushoto kwa mandhari maridhawa. 
Picha na John Nditi


Afisa Mambo ya Nje, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Bi Ramla Hamisi, Afisa Mambo ya Nje, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akipeana mkono na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Ban Ki Moon. Bi Ramla alikutana na Ban Ki Moon Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, hivi karibuni wakati yeye na Maafisa wengine kutoka nchi 25 walipokuwa katika mafunzo ya miezi miwili kuhusu "Upokonyaji wa Silaha"
Afisa Mambo ya Nje, Bi Ramla Hamisi wa sita kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wenzake kutoka nchi 25 pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Ban Ki Moon, mara baada ya kumaliza mafunzo yao ya miezi miwili kuhusu Upokonyaji wa Silaha. Kama sehemu ya Mafunzo yao, maafisa hao walitembelea Japan, Geneva, China, Uholanzi, Austria na Marekani. Maafisa hao walitoka Tanzania, Kenya, Togo, Afrika ya Kusini, Ujeruman, Marekani, Beralus, Chile, Estoni, Spain, Russia, Iraq, Japan, China, Serbia, Uzbekistan, Honduras , Chile, Dominica, Mexico, Cape Verde Egypy, Malaysia, Switzerland na Kazakhstan.


uchimbaji wa kisima na utengenezaji wa mabomba ya hospitali ya Amana kupitia Shear Charity Ball waanza

Mafundi wa Drilling and Dam Construction Agency (DDCA) wakianza hatua za mwanzo za uchimbaji wa kisima na utengenezaji wa mabomba ya hospitali ya Amana ambao ni walengwa wa mfuko wa Shear Charity Ball iliyofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Movenpick Dar es Salaam na kudhaminiwa na makampuni ya Serengeti breweries, Bilicanas Group, TCRA, GS4, NSSF, Azania Bank, National Housing Corporation, 540, Clouds FM, Clouds TV, Precision, Benchmark Production, Peacock Hotel, S.S Concrete, Tinamaria , imaging smart, Hugo Domingo, DTP, Pepsi, Advertisin dar, AIESEC, Coastal Travels, Cocotan, i-view media, Maxcom, THT.


Official Launch of TANZICT and Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) in Dar es Salaam

Hon. Prof. Makame Mbarawa (MP), Minister of Communication, Science & Technology officially launches the TANZICT and Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) during the ribbon cutting ceremony held at Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) in Dar es Salaam. Looking on is Ms. Anne Sipiläinen (left), Under-Secretary of State, Development Cooperation and Policy from Ministry of Foreign Affairs in Finland.
Minister of Communication, Science & Technology, Hon. Prof. Makame Mbarawa (MP), giving his remarks during the opening ceremony of the TANZICT and Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) held at Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) in Dar es Salaam.
Mr. Arnold P. Minde (right), Director of Safari Yetu Company, explains services provided by his company. Listening on are Ms. Valarie D'Costa, infoDev Programme Manager (1st-left), Ms. Sinikka Antila, Ambassador of Finland in Tanzania (2nd-left) and Ms. Anne Sipiläinen (3d-left), Under-Secretary of State, Development Cooperation and Policy from Ministry of Foreign Affairs in Finland. Other on photo is Hon. Prof. Makame Mbarawa (MP), Minister of Communication, Science & Technology (4th-left).
Finnish envoys looking at presentation of Mr. Vincent Kimaro (not on photo), Technical Director of DayOne Softcom Technologies (T) Ltd. On photo are Ms. Sinikka Antila, Ambassador of Finland in Tanzania (1st-right), Ms. Anne Sipiläinen (2nd-left), Under-Secretary of State, Development Cooperation and Policy from Ministry of Foreign Affairs in Finland. Others on photo are Hon. Prof. Makame Mbarawa (MP), Minister of Communication, Science & Technology (2nd-right), and Mr. George Mulamula, Chief Executive Officer of Dar Teknohama Business Incubator (DTBi). (Photo by Tagie Daisy Mwakawago of Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation).


Kuelekea kuundwa Katiba Mpya, mchakato wapamba moto

 Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Sheria na Utawala Mhe. Pindi Chana akiongoza kikao cha kamati hiyo wakati ilipokutana Dar es Salaam leo kujadili Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala Mhe. Tundu Lisu akichangia leo wakati kamati hiyo ilipokutana Dar es Salaam kujadili Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.
 Mhe. Ole Konnay, Mjumbe wa Kamati ya Sheria, Katiba na Utawala akitoa ushauri wake wakati wa majadala.
 Mjumbe wa Kamati ya Sheria, Katiba Utawala Mhe. Andrew Chenge akitoa angalizo na ushauri wa kitaalamu wakati wa mjadala wa Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011
 Wajumbe wa Kamati

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala ikiwa imekaa leo katika Ofisi ndogo ya Bunge Dar es Salaam.Picha na Prosper Minja - Bunge.


ULINZI WAIMARISHWA RUVUMA KWA TAHADHALI YA AL_SHABAB

Maofisa wa jeshi la Polisi mkoani Ruvuma,wakimuhoji raia wa Tanzania mwenye asili ya Somalia,Harbi Ismail Katoto (kulia) nje ya kituo kidogo cha Polisi standi kuu ya mabasi mjini songea baada ya kumtilia mashaka na uraia wake kutokana na tishio la mashambulizi la kikundi cha al - shabab cha somalia kuanza kuyalipua baadhi ya maeneo katika nchi jirani ya kenya na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha yao hivi karibuni


Vodacom yawekeza milioni 90 kwa shule 20 za msingi mkoa wa Dar es Salaam

 Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimkabidhi msaada wa madawati Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwongozo  Elly Shuma  kwa niaba ya walimu wenzake wa shule tano zilizonufaika na msaada huo wa madawati  225 yenye thamani ya  zaidi ya shilingi Milioni shirini na ishirini na tano elf(20,25,000)kwa shule tano za wilaya ya Kinondoni na Ilala,Jumla ya  madawati Elf moja  yenye thamani ya Milion 90 yametolewa msaada kwa shule 20 za Mkoa wa Dares Salaam  mwaka huu.
Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimsisitiza jambo Mwanafunzi wa  Shule ya Msingi Mwongozo  darasa la kwanza Sara Uhuru  mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati  225 yenye thamani ya  zaidi ya shilingi Milioni ishirini na ishirini na tano elf(20,25,000)kwa shule tano za wilaya ya Kinondoni na Ilala,Jumla ya  madawati Elf moja  yenye thamani ya Milion 90 yametolewa msaada kwa shule 20 za Mkoa wa Dares Salaam  mwaka huu.
 Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwongozo iliyopo Wilaya ya Kinondoni Jijini Dares Salaam mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati  225 yenye thamani ya  zaidi ya shilingi Milioni 20,25,000,kwa shule tano za wilaya ya Kinondoni na Ilala,Jumla ya  madawati Elf moja  yenye thamani ya Milion 90 yametolewa msaada kwa shule 20 za Mkoa wa Dares Salaam  mwaka huu.

Vodacom Foundation leo imetoa madawati 225 kwa shule 5 za Wilaya Ilala na Kinondoni ikiwa ni zoezi lililoanza mwezi wa nne la kutoa msaada wa madawati 1000 katika Mkoa wa Dar es salaam.


Tatizo la uhaba wa madawati katika shule mbalimbali za msingi hapa nchini ambalo limekuwa kwa namna moja ama nyingine likichangia kukosekana kwa mazingira dhabiti mashuleni linazidi kupata msukumo wa kutatuliwa kutoka kwa taasisi na mashirika binafsi nchini.



Moja ya mashirika hayo ni mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambao leo umekabidhi madawati mia mbili na ishirini na tano yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni ishirini na ishirini na tano elf,ikiwa ni utekelezaji wa muendelezo wa utoaji wa madawati katika shule za msingi za  mkoa wa Dar es salaam.



 Akizungumzia mradi huo Afisa Mkuu wa masoko na uhusiano wa kampuni hiyo Bi. Mwamvita Makamba  amesema mradi huo ni sehemu ya kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wa kitanzania kama nyenzo muhimu ya kuwajengea mazingira bora ya kuja kujisaidia katika maisha yao na kulisadia pia taifa katika fani  mbalimbali.

Vodacom Foundation imekuwa ikiweka mkazo kusaidia sekta ya elimu kama eneo muhimu la kuchangia nguvu na juhudi za serikali katika ustawi wa jamii nchini, hii ni awamu ya pili kwa mwaka huu na ni imani ya Vodacom kwamba madawati hayo yatapunguza uhaba katika shule ambazo zitaguswa.



 "Tunatambua ukubwa wa tatizo na kwamba lipo takribani nchi nzima na tunaguswa nalo kama kampuni yenye kujali maisha ya watanzania na ndio maana kila mwaka tumekuwa tukiendesha kampeni maalum ya kuchangia madawati ni imani yetu kwamba ipo siku changamoto hii itabakia kuwa historia"

Aliongeza Mwamvita Amesema ukosefu wa madawati nchini ni changamoto ambayo dhahiri ahitaji kufumbiwa macho wala kuzibiwa masikio inahitaji nguvu za pamoja za kila wadau ili kuwawezesha wanafunzi ambao ndio nguvu kazi ijayo ya taifa kuwa na mazingira bora, salama na kuwawezesha kufanya vema katika masomo yao.



"Inaumiza sana unapoona watoto wameketi sakafuni au kubanana katika dawati moja darasani, hii lazima itapunguza uwezo wao wa uelewa na ufuatiliaji masomo darasani ndio maana tukaamua kama kampuni inayoungwa mkono na watanzania kuonesha upendo wetu kwa kuwa na kampeni kabambe ya kusaidia madawati mashuleni"Amesema Afisa Mkuu wa  Masoko na uhusiano wa Vodacom.



Awamu hii imenufaisha shule za msingi tano ambazo ni Maarifa shule ya Msingi (Ilala) Kombo shule ya Msingi (Ilala) Vingunguti Shule ya Msingi (Ilala) Mwongozo Shule ya Msingi (Kinondoni) Kimara B Shule ya Msingi (Kinondoni)  Mwisho.


Idadi ya watu
Idadi ya watu
eXTReMe Tracker