In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player
THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT - BEYOND THE ORDINARY - NATURALLY' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.










  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com












Archive for December 2011

Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda awatembelea waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar hivi karibuni

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa pole baadhi ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es salaam kwenye shule ya sekondari ya Benjamin Mkapa wakati alipowatembelea leo Desemba 31, 2011.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea Dar es salaam ambao wameweka kambi katika shule ya sekondari ya Benjamin Mkapa leo Desemba 31, 2011.
Vijana wakipika ugali kwa ajili ya waathirika wa mafuriko ya Dar es salaam walioweka kambi kwenye shule ya sekondari ya Benjamin jijini Dar es salaam wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipowatembelea leo Desemba 31, 2011.


TAARIFA KUJIUZURU KWA BW. ABSALOM KIBANDA KAMA MJUMBE WA KAMATI YA TAIFA YA MCHAKATO WA KUPATA VAZI LA TAIFA

Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo imepokea kwa masikitiko taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media Bw. Absalom Kibanda ya kujitoa kwenye Kamati ya Taifa ya kukamilisha mchakato wa kupata vazi la Taifa, Wizara haina pingamizi na uamuzi wake huo.

Wizara imesikitishwa na sehemu ya tamko lake kudai kuwa namnukuu,

“Nimelazimika kufikia uamuzi huu, baada ya kujiridhisha pasipo shaka kwamba mchakato mzima uliohusisha sakata langu kama Mhariri Mtendaji kuhojiwa na kufunguliwa mashitaka na Polisi na hatimaye kufikishwa kwangu Mahakamani usingeweza kufikiwa pasipo kuishirikisha Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inayoongozwa na Waziri Nchimbi”, mwisho wa nukuu.

Kwa taarifa hii Wizara inapenda kuutarifu umma kuwa Habari hiyo ni uzushi usio na mashiko wenye nia ya kuharibu uhusiano mzuri uliopo kati ya Wizara na wadau wa Habari nchini.

Kwa mujibu wa majukumu ya Wizara, si sehemu ya kazi za wizara hii kushauri, kuchunguza au kuandaa tuhuma za makosa ya jinai. Ni vema iwe wazi kuwa Wizara hii, viongozi , watendaji, na watumishi wake hawajashiriki, hawajashirikishwa na hawajajishirikisha na hawajashauri wala kushauriwa juu ya tuhuma na mashitaka dhidi ya Bw. Kibanda.

Wizara inavisihi vyombo vya Habari kuendelea kuzingatia weledi, mila na desturi zetu katika kutekeleza majukumu yake.

Imetolewa na,
Msemaji wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.


daladala ..... daladala..... daladala........!!!

Hivi ni hatua gani za lazima zinazopaswa kuchukuliwa ili kuwafanya hawa madereva wa daladala kufuata sheria za barabarani bila kushurutishwa??maana hebu ona hapa anachokifanya,kasimama barabarani anapakia abiria huku magari mengine yamepanga msururu nyuma kusubiri amalize.halafu hana hata wasiwasi kwamba kuna magari yanasubiri nyuma yake.


RAIS KIKWETE AMUAPISHA BALOZI SEFUE KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI IKULU LEO

Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo (kushoto) akimkabidhi nyaraka za serikali maalum kwa kuapishiwa na Biblia, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, ili kuanza kuapishwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha rasmi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, kuwa Katibu Mkuu Kiongozi badala ya Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, aliyemaliza muda wake. Hafla hiyo ya kumuapisha Balozi Sefue, imefanyika leo Ikulu Dar es Salaam. Wa pili (kushoto) kwa Rais ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phllemon Luhanjo, akisimamia zoezi hilo.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Nyaraka za Serikali, Katibu Mkuu Kiongozi mpya Balozi Ombeni Yohana Sefue, mara baada ya kumuapisha rasmi, leo Ikulu Dar es Salaam.
Balozi Ombeni Yohana Sefue, akiwa ukumbini wakati akisubiri kuapishwa rasmi kushika madaraka ya Katibu Mkuu Kiongozi badala ya Phillemon Luhanjo, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Ikulu Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue (kushoto) akifurahia jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, wakati wa hafla hiyo ya kuapishwa katibu Mkuu kiongozi Ikulu Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiingia katika ukumbi wakati wa hafla fupi ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, aliyeapishwa na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, wakipiga picha ya pamoja baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa katibu huyo leo Ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue na Balozi Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, wakizungumza jambo baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa katibu huyo leo Ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, wakipiga picha ya pamoja na Makatibu wakuu, baada ya hafla hiyo ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi iliyofanyika leo Ikulu Dar es Salaam. 
Picha na Muhidin Sufiani-OMR.


VODACOM BABATI HALF MARATHON YAFANA MANYARA

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Elaston Mbwilo mwenye truck suit nyeupe akipuliza kipenga kuashilia kuanza kwa Mbio za Vodacom Babati half Marathon kwenye office za Manyara Internet café. Kulia kwake ni Meneja masoko wa Vodacom Kanda ya kaskazini ndugu Jerome Munisi.
Mshindi wa kwanza wa Mbio za Vodacom Babati half marathon kwa upande wa wanaume ndugu Sambu Andrea kutokea club ya Arusha sport Arusha akiingia kwenye viwanja vya Kwaraa mjini Babati. Alitumia muda wa 1:04:51:97.
Mshindi wa kwanza wa Mbio za Vodacom Babati half marathon kwa upande wa Wanawake Bi.Catherine Langa kutokea Arusha akiingia kwenye viwanja vya Kwaraa mjini Babati. Alitumia muda wa 1:20:15:88.
Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Manyara Mh. Elaston Mbwilo akitoa hotuba kwa wananchi pamoja na washiriki wa mashindano ya Vodacom babati half marathon kwenye viwanja vya Kwaraa mjini Babati. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa mashindano hayo ndugu Mohamed Bajwa, Mbunge wa Babati vijijini Mh. Jituson Patel (CCM), Mbunge wa viti maalum Chadema Mh. Paulina Gekuu na Meneja Masoko kanda ya kaskazini ndugu Jerome Munisi.
Washindi wa mbio zote wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na wadhamini Vodacom na waheshimiwa wabunge wa mkoa wa Manyara.

Katika kusherehekea sherehe za kuuaga mwaka 2011 mjini Babati Manyara, kulifanyika mashindano ya Vodacom Babati half marathon (KM 21). Mbio hizo zilidhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom. Mgeni rasmi katika mashindano hayo alikuwa ni mkuu wa mkoa Mh.Elaston Mbwilo akiambatana na uongozi mzima wa mkoa wa Manyara yaani mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Babati, Mkuu wa polisi Mkoa, Mbunge wa Viti maalum Chadema Mh. Paulina Gekuu na Mbunge wa CCM Babati vijijini Mh. Jituson Patel.


KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM ZANZIBAR YAKUTANA LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Taifa Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,katika viwanja vya Ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipohudhuria kikao cha kamati Malum ya Halmashauri Kuu ya CCM.
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,pia Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amaani Abeid Karume,akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Yussuf Mohamed ,alipowasili katika viwanja vya CCM Kisiwandui kuendesha kikao cha kamati maalum ya Halmashauri kuu ya CCM Zanzibar,kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo leo.
Rais Mstaafu wa Tanzania,pia Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi Mzee Ali Hassan Mwinyi,akisalimiana na viongozi wa CCM Ofisi ya chama hicho Kisiwandui Mjini Zanzibar,ambapo jana kilifanyika kikao cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi,aliposalimiana na Viongozi wa CCM Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, alipohudhuria kikao cha kamati Maalum ya Halamashauri kuu ya chama hicho,kilichofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa jengo la Ofisi hiyo Mjini Zanzibar.
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,pia Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amaani Abeid Karume (katikati) ,akiendesha kikao cha kamati maalum ya Halmashauri kuu ya CCM Zanzibar,kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo,(kushoto) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,Dk Ali Mohamed Shein,na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,(kulia).
Baadhi ya wajumbe wa CCM wa Kikao cha kamati maalum ya Halamashauri kuu ya CCM Zanzibar,wakisikiliza mada zilizotolewa katika kikao hicho kilichofanyika jana katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi kuu ya Chama hicho Kisiwandui Mjini Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman IKULU


TTCL YAGAWA MISADA MBALIMBALI JIJINI DAR

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Bw. Said Amir Said (katikati) na Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw. Amin Mbaga (kulia) wakimkabidhi sehemu ya msaada walioutoa kwa Mratibu wa Maafa Manispaa ya Ilala Bw. Mwasabite Elioth kwa ajili ya watu waliokubwa na mafuriko.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Bw. Said Amir Said (kushoto) na Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw. Amin Mbaga (kulia) wakikabidhi sehemu ya msaada walioutoa kwa Mkurugenzi wa Kijiji cha SOS kinacholea watoto yatima, Dkt. Alex Lengeju Dar es salaam jana kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya.
Baadhi ya Maofisa kutoka Kampuni ya Simu Tanzania TTCL wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima baada ya kuwapa vyakula mbalimbali kwa msimu huu wa sikukuuu.


RAIS KIKWETE AKIWA NA KATIBU MKUU KIONGOZI MSTAAFU NA MPYA IKULU JIJINI DAR

Rais Jakaya Kikwete akiongea na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Mh Philemon Luhanjo (kulia) na Katibu Mkuu kiongozi mteule Balozi Ombeni Sefue ofisini kwake Ikulu Dar es salaam Ijumaa usiku mara baada ya kufanya uteuzi huo.


PONGEZI ZA WANANEW YORK KWA MHE. BALOZI OMBENI SEFUE

UONGOZI WA NEW YORK TANZANIAN COMMUNITY PAMOJA NA WANAJUMUIYA WOTE TUNATOA PONGEZI ZETU ZA DHATI KWA MUHESHIMIWA MLEZI WETU BALOZI OMBENI SEFUE KWA KUTEULIWA KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI.

TUMEPOKEA KWA FURAHA TAARIFA ZA UTEUZI WAKO NA TUNAAMINI UTEUZI WAKO UMETOKANA NA UPEO NA HISTORIA YAKO KATIKA KUONGOZA.TUNAAMINI KUWA BUSARA NA HEKIMA ZAKO NI HAZINA KWA TAIFA LETU CHANGA.

VILE VILE TUNAMPONGEZA MUHESHIMIWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,DK. JAKAYA KIKWETE KWA MAAMUZI YAKE YA BUSARA..

TUNAMUOMBA MOLA AKUZIDISHIENI HEKIMA MARADUFU NA AKUPENI AFYA ILI MUWEZE KUTUONGOZA VEMA..

HAJJI KHAMIS
CHAIRMAN
NEW YORK TANZANIAN COMMUNITY


somo juu ya kukabiliana na mafuriko


Mdahalo kujenga uwezo wa kutoa maoni ya Katiba wafanyika wilayani korogwe,Tanga

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bw. Erasto Sima, akifungua mdahalo ulioandaliwa na Mtandao wa Asasi za Kiraia wilayani Korogwe na kufanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kanisa Katoliki katika mji wa Mombo, wilaya Korogwe, lengo la mdahalo huo lilikuwa ni kuwajengea uwezo wananchi wa wilaya hiyo ili waweze kutoa maoni yao wakati wa tume ya kukusanya maoni hayo itakapopita katika maeneo mbalimbali nchini.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Bw. Stephen Ngonyani 'Almaarufu Profesa Majimarefu', akitoa utangulizi kwa wajumbe waliohudhuria mdahalo kwenye ukumbi wa kanisa katoliki lililopo katika mji mdogo wa Mombo ambapo mbunge huyo alisema wananchi wana umuhimu mkubwa wa kutoa maoni ya katiba hiyo kwa kamati hiyo kwa faida ya maendeleo ya nchi yetu na vizazi vijavyo.
Mtoa mada Bw. Jonathan Ernest Mgongola ambaye ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Handeni mkoani Tanga, akichambua vifungu mbalimbali vya katiba pamoja na kuwaeleza wajumbe wa mdahalo huo umuhimu na faida ya kushiriki kutoa maoni wakati kamati itakayoundwa na Rais kupita na kukusanya maoni yao juu ya marekebisho hayo ya katiba.
Wazee ambao nao walishiriki mdahalo huo uliofanyika kwenye ukumbi wa kanisa Katoliki katika mji mdogo wa Mombo wilayani Korogwe, wakisikiliza kwa makini jinsi watoa mada wakifafanua vipengele mbalimbali vya katiba ya sasa ili waweze kuwa na uelewa mpana wa katiba kabla ya kutoa maoni hayo kwa kamati itakayoundwa na Rais.Picha na Mashaka Mhando wa Globu ya jamii, Tanga


Uzinduzi wa ugavi wa Kompyuta kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria wafanyika leo

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Philipo Mulugo (katikati) akibonyeza Kompyuta za Lap Top wakati wa Uzinduzi wa ugavi wa Kompyuta kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria zilizotolewa na Kampuni ya Royal Mark kwa bei ya Tsh laki nne na nusu (450000) tu.wa pili kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho,Prof Tolly Mbwette na kushoto ni rais wa serikali ya wanachuo,Mlagula John.


Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar akutana na Balozi Mdogo wa Oman nchini

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AKIZUNGUMZA NA BALOZI MDOGO WA OMAN ALIYEPO ZANZIBAR BWANA MANSOOR AL- BUSAID.BALOZI MANSOOR AL- BUSAID AMBAYE NI MPYA ALIFIKA OFISINI KWA BALOZI KUJITAMBULISHA KUWEPO KWAKE RASMI.

Na Othman Khamis Ame,OMPRZ

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiano zaidi kwa Balozi Mdogo Mpya wa Oman aliyepo hapa Zanzibar ili kuona uhusiano wa Kihistoria uliopo kati ya pande hizo mbili unazidi kuimarika.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake vuga wakati wa mazungumzo yake na Balozi Mdogo mpya wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Mansoor Al- Busaid aliyefika kujitambulisha rasmi.

Balozi Seif alisema Zanzibar na Oman zina Historia ndefu inayofanana kutokana na baadhi ya wananachi wake kupelekea kuingiliana kidamu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuhakikishia Balozi Mansoor kwamba jitihada za makusudi zitafanywa ili kuona kazi zake zinatekelezeka kwa mujibu wa taratibu zinavyoruhusu.

“ Kwa kweli kazi ya Kidiplomasia ni ngumu na kufanikiwa kwake inahitajika nguvu za pamoja zinazohusisha moja kwa moja uongozi wa ngazi za juu wa Nchi husika ”. Alisisitiza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Balozi Seif alimshauri Balozi Mdogo wa Oman kuangalia uwezekano wa Nchi hiyo kusaidia Utaalamu na vifaa katika Sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji maji.

Alisema Oman imeweza kupiga hatua kubwa katika Uzalishaji wa Kilimo kupitia Mfumo huo. Hivyo unaweza pia kusaidia harakati za Kilimo hapa Zanzibar ambapo Wananchi walio wengi wanategemea Sekta hiyo.

Mapema Balozi Mdogo wa Oman hapa Zanzibar Bwana Mansoor Al- Busaid alisema anaendelea kupata faraja kuona uhusiano wa pande hizo mbili unaimarika kila siku.

Balozi Mansoor alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba katika Utumishi wake hapa Zanzibar atasimamia kuona maombi aliyopewa na yale aliyoyakuta yanafanyiwa kazi.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliendelea kupokea mchango wa pole kufuatia ajali ya M.V. Spice Islanders kutoka kwa Watanzania wanaoishi Nchini Zambia.

Mchango huo umewasilishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Tanzania Mh. Mahadhi Juma Maalim.

Akitoa shukrani zake Balozi Seif amesema Watanzania hao wameonyesha kuthamini na kuguswa na tukio hilo licha ya kwamba wako mbali na nyumbani kwao.

Watanzania hao wametoa mchango wa zaidi ya Shilingi milioni moja za Kitanzania {1,118.600/- }.


WASANII WA AIRTEL BONGO 50 NA AIRTEL WATOA POLE NA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO DAR LEO

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania,Jackson Mmbando akizungumza na Waandishi wa habari wakati kampuni Airtel ambayo ilikuwa imejumuka pamoja na wasanii wa Muziki nchini kwenda kutoa msaada kwa waathirika wa mafuriko waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni,jijini Dar es Salaam.
Mtayarishaji wa Muziki (Producer) wa Bongo Flava mkongwe P Funk Majani akikabidhi sehemu ya msaada pamoja na umoja wa wasanii wa Airtel Bongo 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Jordan Rugimbana maalum kwa waathirika wa mafuriko waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni, Wasanii hao pamoja na Airtel wametoa msaada huo leo vikiwemo vifaa vya nyumbani zikiwemo nguo na vyakula vyote vinathamani ya Shilingi milioni 10/-
Ofisa Rasilimalii Watu wa Airtel aliyeongozana na wafanyakazi wengine wa Airtel na wasanii muziki wa Bongo Flava,Doris Kibasa akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel pamoja na umoja wa wasanii wa Bongo 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Jordan Rugimbana maalum kwa waathirika wa mafuriko waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni, Wasanii hao pamoja na Airtel wametoa msaada huo leo vikiwemo vifaa vya nyumbani zikiwemo nguo na vyakula vyote vinathamani ya Shilingi milioni 10/-
Kiongozi wa Bendi ya Exta Bongo,Ally Choki akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel pamoja na umoja wa wasanii wa Bongo 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana maalum kwa waathirika wa mafuriko waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni, Wasanii hao pamoja na Airtel wametoa msaada huo leo vikiwemo vifaa vya nyumbani zikiwemo nguo na vyakula vyote vinathamani ya Shilingi milioni 10/-
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Flava’ wa Kundi la Wanaume Halisi wakiongozwa na mkali Juma Nature na wakikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel pamoja na umoja wa wasanii wa Bongo 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana maalum kwa waathirika wa mafuriko jijini Dar es salaam waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni, Wasanii hao pamoja na Airtel wametoa msaada huo leo vikiwemo vifaa vya nyumbani zikiwemo nguo na vyakula vyote vinathamani ya Shilingi milioni 10/-.


dukuduku la mdau kuhusu chuo cha mipango Dodoma

Habari kaka michuzi

Naomba unitolee dukuduku langu katika blog yako. Mimi ni mhitimu katika chuo cha mipango Dodoma (Institute of Rural Development Planning). 

Tatizo ni kwamba toka tumemaliza masomo yetu mwezi wa sita (2011) mpaka sasa tunazungushwa sana kupata Transcript zetu. Yaani tulitegemea zingekua tayari mara tu baada ya graduation ambayo ilifanyika tarehe 25 November mwaka 2011, lakini kila siku wanatupiga danadana. 

Walisema zingekuwa tayari kuanzia tarehe 15 mwezi December 2011 lakini ghafla wakabadilisha tena na kusema kuwa wataanza kuzitoa kuanzia tarehe 10 mwezi Januari 2012. 

Kwakweli kitendo cha kushindwa kupewa vyetu vyetu kinatusababishia kushindwa kupata ajira na ukizingatia waajiri hawahitaji provision results. Hili ni tatizo kubwa na linatukosesha kazi. 

Ninaomba uongozi wa chuo ushughulikie swala hili kwa umakini. Hiki chuo kimekuwa kikiendeshwa kiholela mno na hakiendi na wakati. Tunaomba wajifunze kutoka vyuo vingine ambavyo mwanafunzi anapomaliza tu anapewa na vyeti vyake wakati huo huo.

Hiki chuo kinatuharibia. Tunahitaji vyeti vyetu tutafute kazi.

Asante.


RAIS KIKWETE ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MTANGAZAJI WA TBC MAREHEMU HALIMA MCHUKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI LEO

Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa TBC,Bw Clement Mshana wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mtangazaji wa TBC Taifa,Halim Mchuka leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kabla ya kwenda kuzikwa makaburi ya Msasani baada ya Sala ya Ijumaa.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na kuwapa pole baadhi ya ndugu wa Marehemu Halima Mchuka,leo wakati alipofika kutoa heshima za mwisho.
Rais Jakaya Kikwete akiungana na viongozi wa msikiti wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na wakazi wa jiji la Dar es salaam kuuombea dua mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) marehemu Halima Mchuka aliyefariki tarehe 29 Desemba mwaka huu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) marehemu Halima Mchuka aliyefariki tarehe 29 Desemba mwaka huu jijini Dar es salaam. Mwili wa marehemu umezikwa leo katika makaburi ya Msasani jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo wakitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) marehemu Halima Mchuka wakiongozwa na Naibu waziri wa wizara hiyo Dkt. Fennela Mukangara (wa kwanza kulia) katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya ndugu na watoto wa marehemu wakiuombea dua mwili wa marehemu Halima Mchuka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wanataaluma wa tasnia ya habari nchini na wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakiwa na majonzi mara baada ya kuuaga mwili wa marehemu Halima Mchuka aliyekuwa mtangazaji wa shirika hilo kwa takribani miaka 19 leo jijini Dar es salaam.
Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa TBC Halima Mchuka ukiingizwa ndani ya msikiti wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya Ibada maalum kabla ya kupelekwa katika makaburi ya Msasani kwa ajili ya Mazishi.
Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa TBC Halima Mchuka ukiwekwa katika makao ya kudumu katika makaburi ya Msasani leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akishiriki mazishi ya aliyekuwa mtangazaji wa TBC marehemu Halima Mchuka leo jijini Dar es salaam katika makaburi ya Msasani.
Picha ya Marehemu ikiwa Juu ya Jeneza.
Mkurugenzi wa Zamani wa TBC,Bw. Tido Mhando akiwa kajumuika na waombolezaji wengine kwenye msiba wa Halima Mchuka.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO na IKULU.


Idadi ya watu
Idadi ya watu
eXTReMe Tracker