Mdau Mwantumu Dau akfurahi baada ya kula nondozzz ya Masters ya Msc Risk Management toka Chuo Kikuu cha  University of East London.Mahafali yalifanyika kwenye ukumbi wa London O2



Mwantumu akfuraha na Papaa Haruna Mbeyu 'Meya wa London'
Mwantumu na mdau baada ya kula nondozzz zake

Furaha na familia baada ya Nondozzz

Wadau wakjumuka na Mwantumu baada ya kula nondozzzzzz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. pliz plz naomba contact na hiii familia ya mwantumu,,naitwa shesha ni mwanachuo hapa nchini algeria,,,my contact +213553748785

    ReplyDelete
  2. congraturation wasomi kama niyie mnahitajika huku msibaki huko kujilipua, dada mwenye pink mrembo ila huo mkoba kama kabeba mabomu ya kujilipua apewe nae uraia,ila nimempenda mzuri.


    JESUS CRIST.

    ReplyDelete
  3. Mdau hapo juu unapekua sana,hujui mikoba ya dada zetu siku hizi lazima iwe mikubwa ili na juice siwemo humo.warembo wazuri ila make-up zimezidi.

    MDAU

    AMON HONGOLI
    NORWAY

    ReplyDelete
  4. Wasomi muache hulka ya Kujilipua au pia kukaa sana Ughaibuni kwa muda mrefu bila mpango wa maana!

    Jengeni kujiamini na kuona pia nyumbani hata kama hamkai huku angalau mnaweza fanya mambo huku Bongo wakati mpo huko Majuu kama:

    Mnaweza shiriki katika,
    -Ufugaji wa Nyuki na Upakuaji asali Tabora.
    -Kushiriki mipango ya kuondoa umaskini kwa ku invest DOLLA na POUND zenu huku baada ya kubeba mabox huko. (Najua mtangáka labda Ohhh pesa yangu itapotea, kwani hamna waelewa masula ya Uendeshaji wa Fedha mingoni mwenu?,,,(FINANCE MANAGEMENT au kama hiyo yako dada Mwantumu RISK MANAGEMENT)

    -Miradi ya kukata mkaa Kaliua-Tabora sambamba na Uhifandhi wa Mazingira,

    Na mipango mingine mingi kibaoo!

    ReplyDelete
  5. HARUNA....MEYA WA LONDON HEHEHEHE..HAJITUPI HUYU NI MTU WA WATU JAMANI.

    ReplyDelete
  6. Congratulation mummy your family is behind in each step of your life.... your son abubakar issa

    ReplyDelete
  7. DAU MKURUGENZI WA NSSF, TUNAKUPONGEZA SANA KWA JINSI UNAVYOSAIDIA NA KUWA KARIBU NA NDUGU ZAKO. ANGALIA MARAFIKI ZAKO WALIOFANIKIWA KAMA WEWE WENGINE WANAKATAA HATA NDUGU ZAO. MUNGU AKUBARIKI KAKA NA AKUZIDISHIE.

    ReplyDelete
  8. Nakuona Mariam Mungula,Advocate Abdulfattah mwalimu wangu wa Sheria IFM.

    Hongereni sana.Hawa watu ni Watanzania Halisi na wazalendo wakubwa kwa Nchi yao.mambo ya kujilipua yametokea wapi?

    Dada Mwantum Dau ni mtendaji Mwandamizi Wizara ya Fedha.kweli jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza.

    naona ni wivu kama mdau wa hapo juu kusema kuwa waende kuvuna Mkaa Kaliua-Tabora kweli wasomi kama hawa wakauze mkaa? ni chuki na dharau.

    ReplyDelete
  9. Kamanda Mbeyu ni JK wetu hapa Uingereza.kama watanzania wote tungekuwa kama Haruna Mbeyu basi tungepiga hatua kubwa ya maendeleo.
    Safi sana Dada Mwantum tutakumiss kwenye Community yetu.
    Bwana ashukuriwe.

    ReplyDelete
  10. Mdau Anonymous wa Sun Jan 08, 11:05:00 PM 2012

    KUKATA MKAA KALIUA-TABORA

    Kazi nia kazi bora mkono uende kinywani! na ili mradi iwe ya halali!

    Nani alikwambia kuwa kwa sababu umesoma iwe huwezi kufanya kazi kama Kukata Mkaa?

    Nani alikwambia kwa kuwa unaishi Ughaibuni kama Uingereza huwezi shiriki ktk shughuli za kawaida kama kilimo, ufugaji za zinginezo huku nyumbani?

    Ninyi ndio wajinga wachache wenye kudharau kazi zingine na kufikiri kusoma ndio pekee njia ya kufikia malengo ya maisha!, na pia hadhi na heshima ya utu wa mtu inatokana na elimu aliyonayo!

    Wivu gani?, Dharau gani?

    TUNATAKA JAMII YA WATANZANIA,INAYOTHAMINI MCHANGO WA KAZI, INAYOWEZA KUJITUMA KATIKA KAZI ZA AINA ZOTE BILA KUBAGUA AU KUDHARAU ,VILE HIZI ZOTE NDIO SEKTA ZA UCHUMI WETU NA MAENDELEO YETU NCHINI TANZANIA!

    ReplyDelete
  11. MAANA YA KUSOMA KWA JAMII ZILIZO PIGA HATUA:

    Kwa jamii zilizopiga hatua ya maendeleo kama Israel na Japan, kusoma sio ukuta unaokuondoa katika shuhguli za mikono kama:
    -Bustani za maua na mboga,
    -Kazi ndogo ndogo za usindikaji wa vyakula,
    -Kazi za mazingira na za kujitolea
    -Mchango wa kushiriki kutoa fikra kwa fadia na kazi za jamii na mengineyo mengi kutokana na elimu aliyo nayo.

    TOFAUTI YA MSOMI WA JAMII HIZO ISRAEL NA JAPAN NA MSOMI WA TANZANIA NI KUWA HUYU MSOMI MKONONGO HATA BUSTANI YA MAUA KWAKE NI VIGUMU KUTUNZA KWA VILE AMESOMA!

    NDIO MAANA MDAU ANASHANGAA SUALA LA MSOMI KUKATA MKAA KALIUA-TABORA AKIDAI NI KUONEWA WIVU AU KUDHARAULIWA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...