Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Meck Said Meck Sadick wakati alipowasiri nchini leo akitokea nchini Botswana alikohudhuria Sherehe za Miaka 50 ya kuzaliwa kwa Chama Tawala cha nchi hiyo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais-Mahusiano na Uratibu,Mh. Stephen Wassira wakati alipowasiri nchini leo akitokea nchini Botswana alikohudhuria Sherehe za Miaka 50 ya kuzaliwa kwa Chama Tawala cha nchi hiyo.Wengine Pichani ni Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe (wa pili kushoto),Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaa,Suleiman Kova (kushoto).

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick wakati alipowasiri nchini leo akitokea nchini Botswana alikohudhuria Sherehe za Miaka 50 ya kuzaliwa kwa Chama Tawala cha nchi hiyo.Wengine Pichani ni Viongozi Mbali mbali wa Serikali waliofika kumpokea Rais Kikwete leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais wa Botswana,Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama wakati alipokuwa akiondoka nchini Botswana mapema leo asubuhi,kurejea jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa Botswana wakati akindoka nchini humo kurejea jijini Dar es Salaam leo.Kushoto kwake ni Mwenyeji wake,Rais wa Botswana,Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. hivi jamani hawa wanaoendaga kumpokea rais kila anaporudi safari mbona sioni nchi za wenzetu zilizoendelea.
    Au kuna kuwa na maana yake...NIJULISHENI TAFADHALI

    ReplyDelete
  2. Ni protokali kwanza, labda zaidi ni heshima. Na sio Tz tu, nchi zote Afrika, mkuu wa nchi na amiri mkuu wa jeshi anapokewa na viongozi wa eneo husika. Anaweza kuwa anapata taarifa kutoka kwao kuhusu yaliyojiri katika jimbo hilo tangu asafiri. Lakini naamini ukiuliza wahusika wataweza kukupa majibu sahihi kwa nini wanao utaratibu huo na Tz pia. Labda jaribu kulielekeza swali kwa wahusika, kwa sababu sisi tutakupa maoni yetu tu na siyo jibu kamili au kweli kama utakalopata kwa wahusika.

    ReplyDelete
  3. Yaeh ni protokali ni hara ukiangalia vyeo wanaotakiwa kuwepo ndo hao yaani akiwakilishwa basi yy anakuwa hayupo lkn ni viongozi wa juu maana yy ndiye muajiri wa wote hao,membe kawakilisha foreign,wasira ikulu,meck mkoa dsm,mwema usalama taifa polisi,mwamunyange usalama taifa jeshi,kova usalama mkoa polisi,then woote hao wanawezakuja na wasaidizi lkn haji ngeleja wa dr haji mponda hapo unless iwe safari ilihusu mambo ya wuzara zao na mostly na wai wangesafiri. Na huwa anapata brf ya lolote ambalo lilitokea nchini wakati akiw a safari,mfano hapo sasa mauaji y a songea lazima apate brf yake.

    ReplyDelete
  4. Just because it's so called "protocol" it does not make it necessary or right for that matter. If anything it's a useless protocol, why not meet the President at the white house and brief him there if there is a need for briefing. The trip was useless to begin with anyway let alone the welcoming.

    ReplyDelete
  5. Karibu nyubani JK, yale makhirikhiri uliyochezewa yalikuwa balaa hadi tukadhani 'utajimwaga' na wewe.Huku nyumbani kwema isipokuwa Songea.Nipo Dakar,Senegal hapa kura zimepigwa asubuhi tareh 26 na matokeo ya Rais yanatoka leo leo hakuna kusubiri sijui tume ikusanye matokeo kutoka sijui wapi.Sijui kujumlisha nini,wagombea nafasi ya urais walikuwa 14!!!

    David V

    ReplyDelete
  6. Vipi utaratibu wa miavuli? Ni kwa ajili ya kujikinga na mvua au jua? Maana tangu awasili, naona wanapotembea wanawekewa miavuli juu yao (marais tu). Wengine wanaowazunguka hakuna mwenye mwavuli. Ushauri: Kama ni kujikinga na jua sawa, lakini kama ni kwa ajili ya mvua wawe makini sana. Maana hii miavuli ni design ya kizamani. Ina ncha kali juu, ambayo ni kivutio kizuri sana cha radi. Mdau-Mtaalam wa 'Lightning flashes, and lightning protection'.

    ReplyDelete
  7. viongozi wengi wa afrika ni kukumbukana zaidi kuliko kuwajibika.vile vile viongozi wetu wengi wamepatikana kwa kujuana kuliko kiutendaji.Kwa hiyo kuwa karibu na mkubwa wako ni bima ya kazi yako.Angalia mfano mzuri ni wenzetu uingereza daktari alimfukuza waziri mkuu kutoka wodini kwa vile tu, waziri mkuu hakuosha mikono kabla ya kuingia wodini.KAZI NA URAFIKI AU UNDUGU NI ADUI WA UWAJIBIKAJI.

    ReplyDelete
  8. Hi serikali ina ndege ngapi za Raisi?
    Hii mimi sijawahi kuiona! Pia kuna Jetstream na Forker..

    ReplyDelete
  9. Kwa mara ya kwanza nimeona leo Ankal ameruhusu maoni yanayohoji mambo ya rais wa tz...alhamdulilah labda mwenyezi mungu ameanza kubadili roho ya ankal imeanza kuwa ya kidemokrasia kidogo

    ReplyDelete
  10. Mtanuna , JK ndo huyo karudi , nyie bwabwajeni mwenzenu apaa.!!! MTANUNAJEEE! teh teh teh JK usiwasikilize hawa wasio na fadhila ! kaza buti

    ReplyDelete
  11. Wacheni atanue wakati wake. Tuko nyuma yako Mtoto wa Mrisho. Usiache kusali rakaateni zinawatosha wanafiki. Amka saa nane usiku tawadha weka msala wako sali rakaa zako mbili na muombe M-Mungu akuondolee uadui huu. Halafu acha kudura ya mola inavyofanya kazi.

    ReplyDelete
  12. Mdau hapo juu ameuliza serikali ina ndege ngapi za Rais. Kifupi Serikali ina ndege nne, ambazo zinaendeshwa na kutunzwa na Wakala wa ndege za Serikali( TGFA). Ndege hizo ni hizi zifuatazo; Gulf Stream 550 (5H-One), ambayo ina uwezo wa kusafiri masafa marefu na kwa spidi bila kulazimika kusimama sana kwa ajili ya refuelling, Fokker 28 (5H-CCM) ambayo ndo hiyo aliyoitumia kwenda Botswana (ndege hii inatumika toka miaka ya 70), Fokker 50 (5H-TGF)ambayo mara nyingi hutumika kwa safari za hapa nchini kutokana na uwezo wake wa kutua hata katika viwanja visivyo na lami(Imeanza kutumika miaka ya 90) na nyingine ndogo aina ya piper navajo, ambayo nadhani hutumika kibiashara zaidi(Chatter). Ndege hizi zote, ukiacha Gulfstream, ni ndege za zamani, ila bado zinatumika. Natumai nimejaribu kujibu hoja yako, na kama kuna maelezo nimepindisha, mwenye maelezo sahihi zaidi anaweza kusahihisha.

    Mdau

    ReplyDelete
  13. Wewe nani kakwambia huko Ulaya au Amerika rais apokelewi na wenyeji wa mahali pale? Ni lazima apokelewe na msafara kama kawaida. Yule ni mkuu wa nchi - heshima yake ni kubwa kuliko unavyoacha wewe kufikiria. Tuambie nchi gani rais apokelewi huko barani Ulaya na Amerika?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...