THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT - BEYOND THE ORDINARY - NATURALLY' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com

SAMSUNG YAPATA WASHINDI WA OFA MAALUM YA KIPINDI CHA VALENTINE

Meneja Mauzo na Usambazaji wa kitengo cha Samsung Mobile kwa Tanzania,Sylvester Manyara (kushoto mwenye miwani) akimtangaza Nasma Ghani wa Ubungo Dar Es Salaam kuwa mshindi wa shindano la Samsung Valentines Day ambapo ataenda nchini Afrika kusini na ampendae kwa siku mbili,Hii ni baada ya kuwa mshindi wa kwanza kwa Mwaka huu,Kushoto ni mwakilishi wa Bahati nasibu ya Taifa Bwana Mrisho.

Kampuni ya SAMSUNG Tanzania leo imefunga rasmi kampeni yake kubwa ya kipindi cha Valentine ambapo wateja walionunua bidhaa aina ya Samsung Galaxy walipata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kwenye uchezeshwaji wa Droo hiyo, Meneja Mauzo na Usambazaji wa kitengo cha Samsung Mobile kwa Tanzania Bwana Sylvester Manyara alisema mwaka huu Samsung iliona kuna umuhimu mkubwa wa kuwazadia wateja wake katika kipindi hiki cha kuadhimisha siku ya wapendao kwa kuwapa zawadi ambazo zinaendana na msimu huu.

Alisema maduka yaliyohusika na kampeni hii ni yale tu ya mawakala wa Samsung Mobile waliothibitishwa. Wateja walioonunua moja kati ya bidhaa za Samung Galaxy ambazo ni Galaxy Tab 10.1, Galaxy Tab 7.0 Plus, Galaxy Y Pro, na Galaxy Mini, kuanzia Ijumaa Tarehe 10/02/2012 hadi Jumapili tarehe 25/02/2012 walipata nafasi ya kuingia katika bahati nasibu iliyochezeshwa leo na kuwezesha kupatikana kwa washindi zawadi zetu tatu kubwa za leo.

Alisema washindi wote walioshinda zawadi hizi tatu za leo wote watapata fursa yakuzitumia na wenza wao. Mshindi wa kwanza atalipiwa gharama za usafiri na malazi kwenda Cape Town kwa mapumziko ya siku mbili, yeye na mwenza wake. Mshindi wa pili atapata nafasi na mwenza wake kutembelea mji mkongwe wa Zanzibar kwa siku mbili, gharama za usafiri na malazi zitalipiwa. Mshindi wa tatu na mwenza wake watapata zawadi ya kula chakula cha jioni katika hoteli yoyote ya hadhi ya nyota tano hapa Dar Es Salaam.
Ili kuleta haki na usawa, Droo ya kuwapata washindi hawa inashuhudiwa na kiongozi kutoka bodi ya kusimamia michezo ya kubahatisha Tanzania na infanyika leo jumapili tarehe 26/02/2012 katika duka la Samsung la hapa Mlimani City,Washindi wote wa waliopatikana leo watatakiwa kupanga tarehe ya safari yao iwe siku yoyote katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia siku ya leo.

Bwana Manyara alisema lengo kuu la kampeni hii ni kuwazawadia wateja wake ambao wanatumia bidhaa za Samsung Mobile siku hadi siku. Mbali na wateja kufurahia bidhaa hizi bora kabisa, Samsung inawajali na inaonyesha upendo wake kwao katika kipindi hiki cha maadhimisho ya siku ya wapendanao duniani, yaani Valentine Day!.na leo tumetiza ahadi yetu tuliyoitoa kwa wateja wetu na tutaendelea kufanya hivi kila tunapoona kuna umuhimu na kwa kuzingatia mahitajio ya wateja wetu kwa kuwapatia kile kilichokuwa bora zaidi

Idadi ya watu
Idadi ya watu
eXTReMe Tracker