Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Maalim Seif Sharif Hamad
 
Na Zahira Bilali na Khadija Khamis-Maelezo Zanzibar.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema jambo linalowagusa zaidi Wazanzibari katika kuelekea kupata Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano ni kuwa na mfumo wa Muungano ambao hauwabani Wazanzibari katika nyanja zote ikiwemo kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Amesema, kwa Wazanzibari ambao tayari wanayo Katiba yao iliyo sawa na ile ya Jamhuri ya Muungano, suala kubwa wanalopaswa kulizingatia ni kuwepo katiba mpya itakayotoa haki sawa kati ya pande mbili za Muungano huo, bila ya kuwepo dhana ya mkubwa au mdogo.

Maalim Seif ameyasema hayo leo huko hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar, wakati alipokuwa akifungua mkutano wa pili wa Hali ya Siasa Zanzibar, ulioandaliwa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Wazanzibari watakuwa na fursa ya kipekee kuamua aina gani ya Muungano wenye maslahi kwao, uwe kama ulivyo sasa, uwe Muungano wa serikali tatu au Muungano wa mkataba kwa mambo watakayo kubaliana pande mbili, badala ya ule wa kufungana kikatiba”, alisema Maalim Seif.

Makamau wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alisema jambo la muhimu katika kufanikisha lengo hilo, ni wananchi kote Zanzibar wanapaswa wajipange vizuri, ili wakati wa kutoa maoni utakaofika waweze kutoa maoni juu ya katiba mpya yenye maslahi kwao.

Alieleza kwamba, yeye pamoja na viongozi wengine kama vile Rais Dk. Ali Mohammed Shein na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd na viongozi wengine wamekuwa wakiwahimiza wananchi wa Zanzibar kufuatilia kwa makini mchakato wa kupata katiba hiyo mpya, itakayokuwa na maslahi kwa wananchi wa Zanzibar na wenzao wa Tanzania Bara.

Maalim Seif alisema malengo hayo yatakapoweza kufikiwa migogoro, malalamiko na manung’uniko mengi ambayo yamekuwa yakijitokeza tokea Muungano huo ulipoasisiwa mwaka 1964, yataweza kupungua na kuondoka kabisa.

Akizungumzia Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Maalim Seif alisema mfumo huo wa serikali umeleta faida kubwa kwa Zanzibar, tokea ulioanzishwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita, ikiwemo kuondoa kabisa tabia ya mivutano inayotokana na itikadi za kisiasa.

Alisema huko nyuma kabla ya kufikiwa maridhiano wananchi wa Zanzibar walikabiliwa na mifarakano ya hali ya juu, hali iliyosababisha kwa kiasi kikubwa maendeleo yao kusua sua.

Alieleza kuwa kupatikana kwa maridhiano ya kweli na baadaye kuundwa serikali ya aina hiyo, kumelata umoja miongoni mwa wananchi na hivi sasa Wazanzibari wote wanachangia na kushiriki katika harakati za maendeleo ya nchi yao.

Alisema miongoni mwa wananchi hao ni wale ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiishi nje ya Zanzibar, ambao hivi sasa wamekuwa na hamu kubwa ya kuona Zanzibar inapia hatua kubwa ya maendeleo.

“Wazanzibari wanaoishi nje wamekuwa wakieleza kufurahishwa kwao na maelewano yetu, baadhi yao hivi sasa wanajumuika kusaidia wenzao kwa kuleta misaada na vifaa kama vya elimu na afya na wengine wanafuatilia hatua za kufungua miradi ya uwekezaji”, alisema Maalim Seif.

Alifahamisha kuwa faida kubwa nyengine zinazopatikana hivi sasa ni kuonesha mshikamano wa wanajamii wote, kama hali iliyojitokeza mwezi Septemba mwaka jana, baada ya kutokea maafa ya kuzama kwa meli ya MV. Spice Islander, jambo ambalo huko nyuma wakati kukiwa hakuna maelewano, mshikamano kama huo usingeweza kupatikana.

Alisema mbali na wananchi wenyewe wa Zanzibar, pia wawekezaji vitegauchumi kutoka nje ya nchi wameridhishwa na hali ya amani na utulivu, amabyo ni muhimu katika shughuli za kufungua miradi ya kiuchumi.

Akizungumzia changamoto zinazojitokeza kwenye serikali ya Umoja wa Kitaifa, Maalim Seif alisema kati ya hizo ni kuwepo baadhi ya viongozi na watu ambao hawafurahishwi na Maridhiano ya Wazanzibari.

“Watu hao ni wachache, baadhi yao wamekuwa wakijaribu kutia fitna, ili kuvuruga maelewano, kwa bahati mbaya yapo magazeti machache yanayotolewa Tanzania Bara ambayo yamepania kuleta chokochoko, ili kuvuruga kuaminiana kuliko jengeka”, alionya Maalim Seif.

Hata hivyo, Makamu wa Kwanza wa Rais, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, alisema azma ya watu hao wachache haitafanikiwa na badala yake mshikamano na umoja miongoni mwa Wazanzibari utaendelea kuimarika.

Alisema kwamba watu hao wenye mawazo tenganishi watashindwa, kwasababu wananchi wengi wa Zanzibar wanaona hali ya umoja na maelewano miongoni mwao ina faida kubwa zaidi kuliko kutengana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mengi yamesemwa kuhusiana na hiyo Serikali inayoitwa ya Umoja wa kitaifa. Ukweli ni kwamba kujakwa serikali hiyo kumeongeza ugumu wa maisha maradufu kwa walalahoi walio wengi ila kwa viongozi wanaoendesha serikali hiyo wao kwao ni neema na mbaya zaidi ni kile kitendo cha kwamba sasa hakuna ukemeaji wa ugumu huo wa maisha miongoni mwa wanasiasa, hasa wa upinzani kwaa maana ya CUF. Binafsi kinachonifurahisha ni kile kitendo cha kwamba kipenzi changu Maalim Seif nae yumo ndani ya madarakani hivyo hiyo njia nzuri ya kuelekea ikulu uchaguzi ujao kwa vile sasa anafahamu kila mbinu ya watawala!! Kwangu mimi suala la maisha magumu wala halinisumbui mradi tu Maalim na watendaji wetu wengine wamo ndani ya serikali. Kilichoharibika kidogo ndani ya wiki hii ni kumuingiza Mohamed Raza ndani ya Baraza la Wawakilishi, hata hivyo tutamzima.

    ReplyDelete
  2. Usitegemee Serikali ikukwamue kimaisha, Suluhisho la kukabiliana na maisha ni wewe mwenyewe Mwananchi kuacha Umwinyi na kujituma!

    AINA YA MUUNGANO UTAKAO WAFAA WAZANZIBAR,,,Ndugu zetu Visiwani msitegemee kupewa kipaumbele na upendeleo ktk Muungano wenye Maslahi ya Upande mmoja yani kwenu(Kwa Tiketi ya Muungano kama mlivyotumia umeme bure kwa miongo kadhaa na kuanza kulipa bili za umeme miaka ya 2005 huko nyuma ilifikia ninyi kufikiri umeme ni nguvu za asili kama jua au mvua!),,,(inajulikana kuwa ninyi ni walalamishi sana, hata Viongozi wenu wanalijua hili),,,NI LAZIMA TUNUFAIKE WOTE PANDE MBILI BARA NA VISIWANI.

    ReplyDelete
  3. Wewe Mpemba wa kwanza hapo juu CUF inabidi uelewe kuwa Dunia nzima mnapiga Kura wengi lakini anachaguliwa kwa Uongozi mtu mmoja!

    UGUMU WA MAISHA:
    Cha msingi ili kukabiliana na ugumu wa maisha ili hali umesha furahi ya kuwa Kiongozi wako kipenzi Maalim Seif yupo Serikalini, huku ukiwa upo katika Muunngano ingefaa utambue faida ya Muungano huo kwa kuhamia sehemu zingine za Bara zenye neema badala ya kulalamikia ugumu wa maisha huku ukiwa umejikita huko Visiwani kwenu kwenye njaa!.

    FUNGUKA HARAKA JIKWAMUE:
    Mpemba, fanya uamuzi wa haraka, ninyi si ndio mna beza hamtaki Muungano?,,,sasa ulitakiwa utumie neema na nafasi ya dhahabu ya kuwa ktk Muungano kwa vile nchi yetu Tanzania unayoiita wewe (Tanganyika) ni kubwa kwa:

    1.Kuhamia Shinyanga ili kulima pamba na kuchunga ng'ombe,

    2.Unaweza ukahamia Kaliuwa-Tabora ukafuga nyuki na kupakua asali, kama hujui Watanznia Vijijini ni wakarimu sana utakaribishwa utavalishwa Mgolole ,ni kama Msuli wa kiunoni au zile shuka zenu mnazovaa tu(usiogope makalio kuwa wazi maana Wapemba ninyi waoga sana, utavaa na Kaptula au Pensi la Jinsi ndani),utapanda juu ya mti utapakua asali!

    3.Unaweza ukahamia Mbarali au Rujewa Mbeya ukalima mpunga.

    4.Unaweza ukahamia Dodoma Bahi au Kintinku Singida ukavunja kokoto.

    5.Unaweza hamia Dakawa au Mvomero Morogoro ukalima nyanya (Tungule).

    6.Unaweza hamia bonde la Malagarasi-Kigoma ukalima Mabwawa ya chumvi.

    7.Unaweza ukahamia Sumbawanga msitu mkubwa kule Mpanda ukachana mbao.

    Zote hizi 7 ni njia tofauti ukiwa katika Muungano wa Tanzania (hii ndio faida ya Muungano)kuweza kumudu maisha magumu (licha ya kejeli zako na dharau za kuubeza Muungano), hata huyo Maalim Seif Kiongozi wako mpendwa ukimuona atakubali na Ushauri huu!....Mpemba Upo hapo?

    ReplyDelete
  4. MAPINDUZI DAIMA:
    MUUNGANO DAIMA:

    KATIKA NDOA ZA ASILI KUNA KUOANA HAKUNA KUACHANA, WANANDOA WAKIFARAKANA AU KUPISHANA, SHAURI LAO HUFIKISHWA KATIKA BARAZA LA WAZEE AU MAHAKAMA YA JADI WAKASHIKISHWA MIKONO WAKARUDI KUENDELEA NA MAISHA!

    Kwa taarifa yenu Wandugu Visiwani, Muungano ni ndoa ya JADI HAINA TALAKA!

    ReplyDelete
  5. Wandugu Wapemba,

    Msilalamike maisha magumu huku mmeng'ang'ana Visiwani kwenu, mje huku Bara mpewe na mashamba ya kilimo muanze maisha mapya!

    Msiwe na shaka ninyi mnajulikana ni Vijogoo wazuri mkabidhiwe Wake hata wanne mkija huku kwa kila mmoja wenu!

    ReplyDelete
  6. Wapemba msitegemee kuyapatia maisha huku mtu ukiwa juu ya mkeka unacheza bao.

    MAONGEZI YA KWENYE BAO.
    Duka langu hili hapa,,, nasafiri vile nalala pale,,,SO WHAT???

    INGIENI KATIKA KILIMO NA KAZI ZA NGUVU ZA SULUBU ILI MPATE KULA VYA HALALI KWA JASHO LENU,,,EBO!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...