Leo majira ya adhuhuri nikifuatilia cheti cha kuzaliwa cha mtoto wangu pale ofisi za RITA upanga nilikutana na kadhia ambayo kwa mimi nafikiri ni ukiukwaji wa makusudi au kuto kuelewa sheria za kazi.

Nikiwa nimevalia kaptula ndefu ikiwa kati ya magoti na pingili za miguu, nikasimamishwa na walinzi katika lango kuu la kuingia ofisi za RITA, nikatii amri na kusikiliza.

Askari wa zamu akanieleza yakuwa kwa vazi nililovaa siruhusiwi kuingia pale mjengoni. Wakasema hizo ni taratibu na sheria zilizowekwa na Utawala. Wakasema tangazo lipo kwenye nguzo mojawapo nje ya geti.

Nikabahatika kusoma tangazo hilo na kupiga picha kwa kutumia simu yangu ya kiganjani kama linavyosomeka hapo chini.


Kwa hili naomba msaada wa utata wa hili tangazo na sheria gani imetumika kwenye vigezo vyao.
-          Ni kweli NIKAB ni vazi lisilofaa na halina heshma?
Mdau DAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 68 mpaka sasa

  1. Mimi sijui wewe ulivaaje, lakini kama hiyo ofisi ya Serikali, mbona kiswahili chake ni cha kihuni? Wameshindwa kutafuta mtu wa kuandika kiswahili fasaha? Nini maana ya Kaptula, Singlet, Parma, Kininja?

    ReplyDelete
  2. Sawa kabisaaa! Tena hili liingizwe kwenye katiba mpya mapemaaa! Ila yaruhusiwe tu Bar, mpirani shambani na watu wakiwa majumbani kwao.

    ReplyDelete
  3. sie watanzania tunaopiga mabox huku mamtoni tunashangaa sana baadhi ya vitu pale bongo. hii inaweza attract a very nice lawsuit, hmm ukiwa na USA lawyer hapo unaweza kula bingo tu, yani ofisi ya serikali unazuiliwa ingia wakati kodi yako ndo inarun the whole operation na hata hiyo tangazo print ni kodi zako!!! teh teh, something always wrong with africa.
    ras

    ReplyDelete
  4. Huyu aliyeandika tangazo hilo atakuwa shahada ya Udaktari.

    ReplyDelete
  5. Mdao acha 'UHIYO' sasa kisichoeleweka ni nini katika tangazo hili la OFISI YA SIRIKALI? That is their DRESS CODE - period. Uchimeze uteme bachi. Sasa next time uvae cheni sikioni bungeni kama Ana hajakutoa mkuku - waulize watani zetu...

    ReplyDelete
  6. wendawazimu hao sheria hiyo,imepitishwa bungeni?akija mzungu ataingia na wala hato ulizwa chochote waache ujinga mambo hayo yameshapitwa na wakati waende sijui wapi wakafanye hayo dunia hii ya leo?mdau bwegenaz

    ReplyDelete
  7. ndugu michuzi kuna watu wanapenda kudharau kila kitu hata kama kina maana nzuri tu,embu tazama huyu bwana anaeleza alivaa kaptula ndefu(maana yake nini?ktk tangazo,No. 3 inakata kaptula,hata kama kaptula haizuii printer ku-print hicho cheti chako,nenda tu binamu kavae suruali uchukue cheti bila kupoteza mda....Binamu balaa hapa

    ReplyDelete
  8. KAKA KAMA UMESOMA QURAN VIZURI BASI HIVI VITIMBI VYOOTE VISIKUSHITUZE.. siku ya siku ndo tutajua ukweli

    ReplyDelete
  9. Nini tatizo katika hilo tangazo mdau mwenzangu? Kila ofisi ina uhuru wa kuamua nani anaruhusiwa kuingia, ukizingatia ni ofisi ya serikali vazi hilo la NIKAB halikubaliki kiusalama na sio kwa maana nyingine zaidi. Inatakiwa kila mtu aonekane wazi au atambulikane.
    Sorry kama umeielewa vibaya, haiwezekani kumridhisha kila mtu, cha muhimu ni kuhakikisha wachache hawasumbui amani ya wengi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nilivyomuelewa Mimi huyu jamaa anakubaliana na tangazo Hilo kutokana na alinyovaa yaani amakubali kweli kaptula hairuhusiwi pale Ila Kama mjuavyo anataka kuingiza mdahalo wa nikab ili aone waislam watareact vipi kuhusu nikab! Kwa hiyo hapa anachonganisha tu, hv inakuingia akilini kweli unaongea na mtu anayetaka huduma halafu kajifunika uso? Jamani watanzania wenzangu fungukeni vichwa ( NIkab ni nini hasa Iogopwe eti watu waijadili hivi?)

      Delete
  10. Kwa hiyo unataka ufafanuzi wa hiyo nikab au huo mkaputura wako usio na heshima mbele za watu?

    Abiola Jr.
    Mafia kiduka cha juice

    ReplyDelete
  11. ndio ni kweli. Huwezi kumjua nani yupo kwenye vazi hilo. Hizo ni sheria na tuzingatie jamanii tusilete siasa kwenye kila kitu.

    ReplyDelete
  12. Inawezekana ni vazi la heshima ndio lakini linaweza kuwa hatarishi kwa upande wa usalama kwani mhalifu anaweza kulitumia vibaya kwa kuficha maovu hivyo wanapendelea mavazi ambayo yatakuwa hayana utata.

    ReplyDelete
  13. sasa wewe mdau tatizo lako nini?jibu unalo mwenyewe tayari ushawekewa maelezo kamili nenda kavae suruali yako urudi hapo utakwendaje ktk maosifi ya watu wa vikaputula?wewe una makosa bwana lazima tubadilike tusipende kulaumu sana tu,hizo sheria hapo zimewekwa tayari matatizo yashawakuta hapo ofisini ndio wanataka mavazi ya heshima,vichupi vyako kavalie mbagala huko ktk live dar

    ReplyDelete
  14. Ndugu yangu mimi nimefurahi sana kwa kuchukua ushahidi huu wa tangazo lenyewe, kuliko kama ungelalamika tu, hii ni safi kabisa ulivyo fanya ili sasa watu tunapo kuelewesha tunakuwa na msingi(grounds).
    Kwanza napenda nikuambie kuwa kuna sheria za aina mbili;
    1) sheria inayotungwa na bunge{state law) hii ni sheria ya nchi.
    2) Sheria ndogondogo( by-laws), sheria hizi hutungwa na watu wa kawaida wa eneo fulani kulingana na athari wanazo ziona kutokana na mambo hayo waliyo yatungia hiyo sheria, na ndo hii uliyo pambana nayo wewe siku hiyo.
    Sasa ni kwamba sheria ni sheria iwe imetungwa na bunge au na mtu au kundi la watu kulingana na mazingira yao zote ni za kutii na wala usithubutu kuivunja kwa makusudi au kwa ubishi itakufunga, wametumia vigezo vibaya au vizuri haijarishi ilimradi hiyo sheria ipo ifuate.
    Hawa jamaa hawana kosa wewe waache tu hivyo hivyo, huwezi kujua kiliwapata ni nini mpaka wakatunga sheria hiyo, nadhani umenielewa, asante.Naitwa komba mwasheria.

    ReplyDelete
  15. mimi binafsi nalikubali tangazo hilo kumbuka kuwa mila na desturi zetu zipo palepale hakuna haja ya kuzipindisha mambo ya wazungu tuwaachie wenyewe utamaduni tuliojiwekeea wafrika hautakiwi kupindisha kaptula ni kaptula tu wala huwezi kuibadilisha iwe suruali ifike gotini bado itaitwa kaptula naupongeza sana uongozi RITA shikilieni uzi huohuo mungu awabariki sana

    ReplyDelete
  16. Acha ujinga,,,unaendaje kwenye ofisi za serekali na kaptula!? Huelewi kila ofisi zina taratibu, kanuni na sheria zake? Au wewe unadhani sheria hadi ziandikwe kwenye katiba!? Hongereni RITA,,,watu lazima wajue kuheshimu kazi za wengine! Hata huku kwa wageni si kila mahali wanapokwenda wanavaa kaptula, tene wana nidhamu ya kutosha wanapoingia ofisi za watu!

    ReplyDelete
  17. Kwa joto la DSM unakataza watu waliovaa kaptula kuingia oficn..baba yangu anamiaka zaidi ya 70 na anavaa kaptula analalamika joto litaua...

    ReplyDelete
  18. ama kweli dunia imekwisha vimini vinaruhusiwa lakini nikab nooo

    ReplyDelete
  19. Rita wako sahihi kuzuia nikab kwani unaweza jikuta unahudumia mtu asiye mwenyewe,lazima tuvae mavazi yanayomtambulisha mtu kwa sura yake,mbona kwenye vitambulisho hatuoni hizo nikab zikiwa zimevaliwa?

    Ningeshauri pia hilo vazi la nikab lipigwe marufuku tu kuvaliwa sehemu yoyote ile hapa nchini kwani hata mkeo akilivaa mtapishana njiani bila kumfahamu na siku hizi wanawake wanaitumia kuingia gesti bila kutambulika.

    ReplyDelete
  20. Mimi nadhani hili la Nikab ifisi ya selikali imekosea kukataza. Ila kwa wewe kuvaa kaptula, au mafulana yasoyo na mikono yanayoacha makwapa nje na kutembea mjini si maadili yetu. Unaiga tu mambo ya nchi za nje na kujionyesha kuwa wewe mjuaji. Hii ikiruhusiwa kuna wakati vijana wataingia mjini na mataulo viunoni!!!

    Hebu piga picha umepanda na jamaa kwenye daladala lemjaa ameshikilia bomba juu mikwapa nje na joto lote hili, unatafuna BIG G yako kuchangamsha mdomo sasa utameza mate au utatema?

    ReplyDelete
  21. Sa si ufuate utaratibu kama unavyotaka ukiwa roma ishi kama roma

    ReplyDelete
  22. Utawala umevunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania "Mipaka kwa haki na uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu" Sheria ya mwaka 1984 Na.15 ib.6 na Sheria ya 1994 Na.34 ib.6
    Kwahiyo mdau unaweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu.

    ReplyDelete
  23. Wateja hawakupaswa kuwekewa vikwazo hivyo, Nadhani hiyo ilifaa itumike kwa watumishi wa ofic hiyo. kwamba hawaruhusiwi kuvaa hivyo na sio wateja. Kuhusu hiyo namba moja 1. nadhani huo ni unyanyasaji wa hali ya juu,kwani hilo vazi la nikab ni kinyume na hayo mengine yote hapo ni vazi la heshima kwa mwanamke linalositiri maumbile ya mwanamke na kumletea heshima kwa jamii,kama ni kwa ajili ya security anaruhusiwa kuonyesha sura yake na taratibu zikaendelea. Mwanamke aliyevaa kitop na aliyevaa niqab unaweza kuwaweka kundi moja?nadhani hapo wamekosea.

    ReplyDelete
  24. Huyu mdau aliyeleta hii naona haelewi anachoandika,mtu kafunika uso wote hata huwezi kumtambua kama inavyosemekana NINJA anataka aruhusiwe kwenye ofisi ili iwe nini?hapo ni ofisini unatakiwa uvae kiheshima NINJA si vazi la kistaarabu!

    ReplyDelete
  25. Hii ndo Tanzania yetu kuna mabunge mengi yanayo tunga sheria. Usishangae unaingia ofisi za Serekali unakuta Dada Kajibana kalegeza blauzi yake Matiti nje na viongozi wetu wamevaa 9Kaund Suti) vifua wazi mpaka nywele za kifuaani zinaonekana lakini hayo ni mavazi ya heshima. Sasa waislam ndo mujue hawa wadada, Wake, Wamama zenu mnaowavalisha nikabu Serekali yenu inaona kwamba ni Mavazi yasiyoofaa na ya aibu ??????

    ReplyDelete
  26. Mbona mdau kataja NIKAB tu? Sheria mtu anayojiwekea lazima ifuatwe. Mbona tukienda visiting kwa watoto wetu tunalazimishwa kuvaa staili fulani wakati staili hizo sisi wengine hatuzitumii? Tunafanya hivyo kwa kuwa ndivyo walivyojiwekea, hivyo na mdau lazima akubali sheria walizoweka RITA. Hata yeye ana sheria zake nyumbani kwake ambazo familia yake wanazifuata hata kama hawazipendi.

    ReplyDelete
  27. Mm pia siwaelewi RITA kabisaaa ..wanaingilia uhuru wa mavazi as wao kazi yao ni kukagua mavazi???Fanyeni kazi zenu zinazowalipa mshahara na si kuleta kazii zilizo nje ya mipaka yenu.Ni sheria gani mliyoitumia??ya mwaka gani?inaitwaje??upuuz tuuu hebu badilikeni na mtupatie vyeti vyeti ndani ya muda na si longolongo zisiozhusu

    ReplyDelete
  28. Mtoa hoja yaelekea anapenda sana ligi ? Kwanini asionane na utawala au kuomba contact za Utawala akapewa ufafanuzi hadi aitangazie dunia. Kwa uelewa mdogo nilio nao Tangazo hilo inawezekana Utawala hauhusiki kwa sababu Matangazo yote ya RITA ninayoona yakitolewa kwenye Magazeti au Media huwa yana Muhuli wa RITA na yanatolewa kwenye Karatasi yenye nembo ya RITA (Headed Paper) ! Na RITA hawawezi kubandika Tangazo kwenye Nguzo ya Stimu au Mti. Mdau hapo umekosea usituchonganishe kwa kutumia Item # 1.

    ReplyDelete
  29. Usibishe wewe mdau ambae unaona kila kitu unaonewa na serikali haifanya mazuri yoyote. Angalia sheria za utumishi wa umma na kanuni zake pamoja na sheria ya maadili ya umma zinawekwa kwa umma wakati wakihudumiwa. Haya hata kama tuseme hizo sheria hazipo lakini kama taasisi lazima iwe na utaratibu wa kufanya mambo na hii iko kila sehemu, mfano huezi kufanya kazi benki kama wewe ni wa jinsi ya kiume afu usivae tai, au ukiwa TRA lazima uvae suruali nyeusi na shati jeupe uliza maagent wote watakueleza lakini hakuna sehemu imeandikwa kama sheria kufanya watu wafanyakazi wavae hivyo ila ni utaratibu umewekwa. Jamani ndugu yangu, isije kuwa ni kwa sababu ni ofisi ua umma ndio watu wasifuate taratibu, watu wengine wangetaka kwenda uchi pale na wapewe huduma na ukiwauliza watakwambia wako huru, hii sio sawa. kwa hayo machache napenda kukuelimisha kuwa hata nyumbani kwako kuna utaratibu sio kila kitu kinafanyika shaghalabagala. Na mwisho kabisa usipende kutumia neno "YALE YALEEEE......." kama huna uhakika na jambo usilolijua. Maana ya kutumia neno hilo ni kwa mfano sehemu imeandikwa usikojoe hapa afu unamkuta mtu anafanya jambo hilo hilo. Mdau!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  30. wewe mshamba nini, unalalamika nini hoja yako mbovu hakuna wa kukutetea, hujui unaingia ofisini na sio klabu ya pombe au disco. Hizo ni taratibu utaendaje uliwa umevaa kihuni au hata kanisani au msikitini unaingia hivyo? pia mimi ukija ofisini kwangu umevaa kihuni sikuhudumii ng'o. NINAWAPA BIG UP RITA UZI HUO HUO.

    ReplyDelete
  31. wala usishangae ni kweli ofisi nyingi za serikali zinautaratibu huo.unatakiwa kwenda umevaa suruali tena ofisi nyingine ukivaa jinsi wanakurudisha. kwa wadada pia ukivaa vijinguo vifupi vitop vinavyoachia mwili wazi nao pia hurudishwa. Ni katika hali ya kuhakikisha maadili hasa upande wa mavazi yananazingatiwa.

    ReplyDelete
  32. MZEE WA BUNJUFebruary 16, 2012

    nani kakwambia "Nikab" sio vazi la heshima???

    ReplyDelete
  33. tumedhubutu tumeweza na tunasonga mbele,what the hell is that?

    ReplyDelete
  34. Chief Kimweri Jr.

    Ndugu yangu umeshindwa kulielewa tangazo na pia una chembe chembe za uchochezi na uchonganishi.

    1. tangazo limejieleza wazi kuwa vazi lisilofaa kwa pale ofisini kwao ni kofia kubwa, nikab na pensi kama ulilovaa wewe. mimi kama muislam ninatambua nikab kama vazi la heshima na ninaliheshimu sana ila kwa utaratibu wao halifai ofisini kwao na si kwamba si la heshima!

    2. Mavazi yasiyo ya heshima ni kama vitop, nguo za kubana na kuonyesha maungo ya mvaaji, suruali za mlegezo n.k.

    3. Tangazo lipo vyema ila unatafsiri ili ionekane umeonewa na unatafuta uhalali wa hilo.

    4. Kwani ni lazima uvae kaptula ndefu? Suruali si zipo?

    5. Alamsiq!

    ReplyDelete
  35. NIKAB ni vazi la heshima. Bora wangepiga marufuku vimini, visuruali vya kubana na blauzi maziwa nje... Kwa NIKAB wamepotoka. Ofisi yetu ni ya serikali, tena ya uhakika lakini NIKAB ruhusa hata kwa wafanyakazi wetu.

    ReplyDelete
  36. sasa kwani hao RITA hawana njia yeyote ya kuhudumia wateja wake mpaka waingie ndani ya ofisi,mimi naona wangeamua kuweka madirisha kwa nnje ili kuhudumia watu wakiwa nnje ya madilisha bila ya kuingia ndani na huyo dada mwenye nikab anaweza kumuomba amwonyeshe sura yake na baadae aendelee kumuhudumia,sasa alievaa kaptula?na beachkoma,na alievaa msuli?au kikoyi na dada alievaa sketi hawa vp?maana hivyo vyote ni sio suruali au gauni inatakiwa ifike mpaka ibuluze,?naomba msaada bwegenaz.

    ReplyDelete
  37. kwani hata huyo aliyevaa nikab akififa rita wakti anataka cheti si wamwambie kwa muda atoe wamuone sura yake kama yeye ni mhusika ? au wanataka waanzishe migogoro tu.. hawana lao jambo kazi zao zimewashindwa na subiri watakipata wanachokitafuta ... pambafff

    ReplyDelete
  38. Ama kweli kiswahili kigumu! Huwezi hata kutofautisha kaptula na suruali? Tena unabahati wangekunyangánya na hiyo unayoiita kaptula ndefu!

    ReplyDelete
  39. Mashariti Ofisi ya Serikali kibao, hadi kuingia!

    Huyo Afisa aliyeandika au kuweka mpango huu kama sio ndio kwanza amepewa Cheo sasa anatafuta sifa, itakuwa anatafuta kupewa Cheo au ndio kwanzaa mgeni hapo.

    Lakini Rushwa,,,ahhh mkono mbele kupokea, kwa nini wasiongeze shariti la Wageni kutowapa rushwa Wafanyakazi hapo RITA?

    ReplyDelete
  40. Mimi nasikitika sana kwamba vazi la heshima la Mwanamke wa Kiislam "Nikab" hao watu wameliita vazi lisilo la heshima na lisilofaa. Nalifanyia kazi na kulifikisha kwa Waislamu tuweze kuchukua hatua zaidi.
    Kila kinachofanyika Ulaya kwetu ni dhahabu na hawa wangekuwa na maamuzi wangekubaliana na David Cameroon kuhusu ushoga kwani hapa wanatekeleza sera ya Ufaransa. Inna lillahi wa inna ilahi rajiuna.

    Wameshazoea kuvaa vizuri nje lakini mioyo yao michafu na haistahili kuwa sehemu ya binadamu.
    Hiyo ofisi ingekuwa inajali maadili wasingsumbua watu kuomba rushwa.

    ReplyDelete
  41. binafsi sijaona tatizo la hilo tangazo. Hizo ni sheria za ofisi yao,ili uweze kuingia inabidi ufuate masharti yao,kaptula si vazi la kiofisi,nikab hali kadhalika, so km mvaaji wa nikab (ninja), unaweza kuvaa ukifika getini kwao unatoa jiyo ninja then unaonekana sura yako unaingia,tatizo liko wapi kwani?

    ReplyDelete
  42. je wanaruhusiwa ndani ya ofisi, wamasai, wamakonde, waweka tattoo,... tunajicontradict tu, kila mtu atabeba msalaba wake...

    alimradi havunji sheria za nchi, full stop....

    halafu tabia ya kuassociate Nikab, kama ni vazi la kidini la waislam kwenye notice board, it is totally wrong,

    I guess the same can be said about priest na vazi lake, Roman catholics sister, na muweka msalaba, pia ni security issue anaweza kutumia kama silaha, if the issue ni security, acheni XENOPHOBIA hizo

    ReplyDelete
  43. je kitop kinachoonyesha maziwa...

    ReplyDelete
  44. Nakumbuka zamani pale Sanawari na Mianzini Arusha kulikuwa na Suruali ya kijiji kwa sababu sisi wamasai/waarusha tulikuwa haturuhusiwi kukanyaga Arusha town na lubega...
    Sasa jamaa mmoja alipoazima suruali alijisahau wakati anajisaidia kuwa anapaswa kuivua kwanza..duh Suruali ya kijiji ikapatwa na msukosuko kama hivyooo
    Janani tuvaeje ili iwe heshima?
    Sasa hiyo ofisi inapaswa kuweka mavazi ya kuazima hapo nje kwa walinzi ili mtu anapokuja bila vazi linalostahili apewe avae, na akimaliza shughuli zake arejeshe vazi la kuazima.

    ReplyDelete
  45. Hivi mzungu akiingia hapo na singlet na kaptula watamfanya nini? Kwa wenzetu hayo ni mavazi ya kawaida kabisa kwenda nayo sehemu kama hizi.

    ReplyDelete
  46. Mbona club billicanas walisema the same thing lakini hamkutoa huku? coz ni ofisi ya serikali ndo mnalitolea macho? Embu tuwe waelewa maana hata majumbani mwenu kila mtu anataratibu zake nami nikifika huko napaswa kuzifuata lakini nikiwa kwangu mtu asiniingilie kabisa. Tuwe wastaarabu na waelewa wandugu..

    ReplyDelete
  47. NYIE WOTE MLIOTOA MAONI NI WEHU! WALA SIONI CHA MAANA MLICHOCHANGIA UPUUZI MTUPU,WATANZANIA TUNAONGOZA KWA MAMBO YAKI...S....N.....G....E MWAKA 1994 NILISHUHUDIA MKAPA ALIKUWA ANAFUNGUA MRADI WA BARABARA HUKO MWANZA YULE PROJECT MANAGER WA ULE MRADI ALIKUWA AMEVAA KAKAPUTLA KAFUPI MPAKA KIJIJI KINAONEKANA HAFU ALIKUWA KWENYE SAFU YA WAGENI ALIPOKUWEPO PRESIDENT NA JAMAA ALIPEWA WASAA WA KUZUNGUMZA AKACHANA UMOMBO SWAAFI NA AKAELEZEA JINSI WALIVYOKUWA WAMEJIPANGA KUBEBA BOX BARABARA IKAJENGWA BILA TATIZO WATANZANIA KWA KUONGEA TU AAAH! KAZI HAMNA MNATIA KINYAA KAMA MAVI PUMBAVU TOA HIYO KITU HAPO,KWANZA MMEKUNYWA CHAI? NA CHAUKULA CHA MCHANA? STUPID!

    ReplyDelete
  48. Nilimuona Dwight Howard katika picha na JK pale Ikulu akiwa amevunja sheria hiyo ya serikali. Hii ni kwaajili ya watanzania pekeyake au inawahusu pia mastaa wa kimarekani?

    ReplyDelete
  49. Hahahaaaa...Magufuli, Museveni na Silva Kiir wa Sudan Kusini..... wakiingia na maparma yao watazuiwa getini!! Heshima iko moyoni mwa mtu, wala si ndani ya kofia, sketi ama suruali yake.

    ReplyDelete
  50. Alaaniwe na Mwenyezi Mungu aliyeandika kuwa "Nikab ni vazi lisilo na heshima".

    Kama kilikaa kikao kwa ajili ya hilo, ewe Mwenyezi Mungu wa Haqqi laani kila aliyeshiriki pamoja na kuidhinisha kulidhalilisha vazi letu la Kiislamu - AMIN YAA RABBI

    ReplyDelete
  51. TANGAZO LIMETULIA. FUATA TARATIBU ZA MAHALI HUSIKA. KAMA HUTAKI TEMBEA MAANA HAWAJAKUITA. UNAPOKWENDA MAHALI FULANI HAKIKISHA UNAHESHIMU TARATIBU NA SHERIA ZA MAHALI HAPO MANA SIYO NYUMBANI KWAKO

    ReplyDelete
  52. utavaaje NIJA ktk ofisi kama ile nita ku- tambuaje kama wewe ndio mwenye nyaraka?

    ReplyDelete
  53. Ni sawa kabisa hilo tangazo. Jamani hata majumbani watu wanaweka sheria zao. Na sio RITA tu hata ofisi zingine wanasheria zao za mavazi. Nikab ni vazi la heshima lakini ni hatari sana kwa usalama! Majambazi wengi hulitumia ndiyo maana baadhi ya ofisi wanalipiga marufuku na lingefaa kupigwa marufuku nchi nzima! Lakini kibembe chake tutakiona!

    ReplyDelete
  54. SAFI SANA RITA. OFISI ZA WIZARA YA ULINZI HAWARUHUSU HATA SURUALI ZA JINSI NA FLANA. LAZIMA TUJIFUNZE KUWA SMATI.

    ReplyDelete
  55. Nani alikwambia Nikab ni vazi la heshima? lingekuwa la heshima alkaida wasingelitumia kufanya unyama.
    Usichanganye mambo, nchi hii haina dini, sheria zinazowekwa haziangalii dini. Dini unayo wewe, kijana fuata kilichoandikwa.

    ReplyDelete
  56. Acheni kupoteza muuda wa watu!Huyu mtoa mada kitu gani hakikueleweka katika tangazo hilo?

    Umekatazwa kaptula,wewe unasema umevaa kaptula ndefu ndo unatueleza nini.

    Msomi,na mtu anayejua lugha awaye yeyote yule,akiambiwa 'usivae kaptula' maana yake iwe fupi au ndefu usivae.

    ReplyDelete
  57. NDUGU ULIVAA KAPTULA, PERIOD! sasa hapo unataka tukutetee vipi mtu unaingia ofisini na kaptula, ofisini kwako ungeingia umevaa kaptula? tena am sure ilikuwa ile ya mlegesheo, kaptula gani itafikaje kwenye ankle?

    ReplyDelete
  58. nadhani labda unahitaji maombi, sidhani kama kuna makosa katika tangazo hilo, siku hizi kina mama wanaiba laptop na kuficha katika nikab zao nimeshuhudia hilo, nakuuliza ulishawahi kuvaa kaptula ofisini kwako au unapokwenda kufanya interview ? acheni mambo haya ofisi ya RITA nawapongeza ongezeni na sheria hata walionyoa denge MARUFUKU !!!

    ReplyDelete
  59. Mdau wa 3 kuchangia unasema huko USA hukatazwi kuingia ofisi ya serikali.Je ukienda uchi utaruhusiwa kwa vile eti unalipa kodi?
    Mimi ninachokiona hapa ni kuchanganya mambo,huo ni utaratibu wa ofisi husika na lazima zitakuwepo sababu zilizopelekea kuweka tangazo hilo kutokana aidha na kadhia au usumbufu unaosababishwa na mavazi yaliyotajwa.Mimi binafsi ninaona ni sahihi.
    Kuna watu wamefungwa na udini hivyo tangazo hilo tayari wamelichukulia kama kuna dini yao imenyanyaswa na kuanza kutumia lugha za hasira.
    Jamani tumpende Mungu dini haitupeleki popote kama hatumpendi Mungu.Kuwa na hasira tu hiyo kwa Mungu ni dhambi.Ukiweka kinyongo dhambi pia. Watanzania tuamke tuache kutumikia dini na badala yake tumtumikie Mungu.

    ReplyDelete
  60. Mdau wa maguFebruary 16, 2012

    Waziri MAGUFULI imekula kwake na pama lake analovaa saa zote,Tusubiri na tuone. hahahahaha. RITA nawasifu hawana mizengwe kwenye kutoa vyeti, kwa hili ninawasifu sana, Kifupi wamejipanga...

    ReplyDelete
  61. kigezo ni heshima au rasmi, tungeomba mwongozo zaidi, maana kama ukisema heshima! je nauliza nikab-ninja ni la kihuni!? kama ukisema rasmi! atakuja mzungu wa kike na kibukta then anakuwaambi hii rasmi kwa majira ya joto huku kwenu, je naye atazuiliwa? jaman tuache kunyanyasa jamii flani maana hata hiyo sheria atuijui, tuache mamlaka husika zikiwemo bunge n.k, zitoe uhalali kwanza, sio sheria vichochoro zitawale. mfano kama ndio mie nipo na mama yangu au mke wangu kavaa hiyo ninja, sijui ffu wangekuja au lah!
    mpaka wangenieleza nani kawaongopea hizo sheria vichochoro.
    mdau jp.

    ReplyDelete
  62. MTANIWIA RADHI NTATUMIA HERUFI KUBWA SABABU NATAKA MAONI YANGU YAONEKANE WAZI ZAIDI HASA KWA WALE AMBAO WANAONEKANA KUCHANGIA TU ILIMRADI WAMERIDHISHA NAFSI ZAO.
    1. KWA NINI KATIKA HIYO LIST HAKUNA VIMINI? SLEEVELESS BLOUSE KWA WANAWAKE?
    2. MUANDIKA TANGAZO AMEKOSEA KUUFIKISHA UJUMBE KWA SABABU AMECHANGANYA VITU VYOTE KWA PAMOJA NA KULETA TASWIRA MBAYA....ANGELIWEKA LIST YA MAVAZI YASIYOFAA NA LIST YA YASIYO NA HESHIMA.
    3. WACHANGIAJI WALOSEMA KWAMBA NIQAB HAIRUHUSIWI KWA SABABU ZA KIUSALAMA NADHANI WANA MTAZAMO FINYU. KWANI MTU AKITAKA KUBEBA MABOMU LAZIMA AVAE NIQAB? NA KWA HILI WANGELIWEKA WAZI KWAMBA WENYE NIQAB WATATAKIWA KUONYESHA SURA ZAO KWENYE KUTAMBULIWA HATA HII KWA RITA MI NAONA NI NONSENSE. IKIWA UMESHAWAHI KUFANYA HIZI TARATIBU ZA VYETI UTAJUA KWAMBA PALE HATA KITAMBULISHO HUULIZWI...WAULIZWA MAELEZO MENGINE TU...SO I DONT SEE ANY POINT YA KUSEMA HAIRUHUSIWI NIQAB...HAILETI MAANA UNLESS WAHUSIKA WALIKUWA WANATAKA KUKIDHI MAHITAJI YAO BINAFSI.

    ReplyDelete
  63. HUU NI UPEO MDOGO WA VIONGOZI WA RITA! WALINZI NA WAFANYAKAZI WOTE WA OFISI ILE! NASIKITIKA SANA DUNIA YA SASA MNAWEKA MIPAKA YA MAVAZI YA MTU! HAPO ZAMANI WATU WOTE WALIKUWA WANAVAA MAGOME YA MITI NA MAJANI KUFICHA SEHEMU ZA SIRI! KWANI UKIVAA SURUALI AU SUTI NDIO UTAONEKANA UNA HESHIMA? AU WAKINA MAMA WAKIVAA NGUO NDEFU NDIO WANA HESHIMA? HUU NI MTAZAMO FINYU WA WATU WENGI SANA WASIO NA UFAHAMU! JOTO LOTE HILO LA DAR, MTU UNATAKIWA KUVAA CHOCHOTE UNACHOONA KINAKUFAA, UTUMWA UMEWAJAA WATU WENGI SANA BILA KUJITAMBUA! FANYENI MAMBO YA MUHIMU KUISAIDIA JAMII INAYOWAZUNGUKA KULIKO KULETA CHUKI NA WATU WENGI AMBAO HATA JINSI YA KUPATA MLO MMOJA WA SIKU HAWAJUI! UMEBAHATIKA KUKAA KATIKA HIYO OFISI TOA HUDUMA KAMA INAVYOTAKIWA, MAVAZI YA MTU HAYAUSIANI NA CHETI ANACHOTAKA MTU! TATIZO RUSHWA IMETAWALA KATIKA OFISI ZOTE ZA SERIKALI! BINADAMU WOTE NI SAWA HAKUNA ANAEMPITA MWENZAKE, HUO USOMI WENU WA KUKARIRI MAKARATASI MLIYOWEKEWA NA WAINGEREZA, NDIO UNWAFANYA MNAKUWA NYUMA MPAKA LEO! KULE KIJIJINI KWENU ULIPOTOKA MPAKA LEO WATU WANAVAA NGUO MATAKO YAKIWA WAZI! MAVAZI YOTE NI SAWA ALIEKWAMBIA VAZI FULANI NI LA HESHIMA AMEKUTEKA AKILI YAKO, KILA MTU ANA UHURU WA KUFANYA ANACHOTAKA AKIWA HAI, MWISHO WA SIKU YAKE IKIFIKA ATAACHA KILA KITU ATAKWENDA KAMA ALIVYOZALIWA. MICHUZI BANIA NA HII TENA:

    ReplyDelete
  64. huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

    ReplyDelete
  65. Kwa jinsi ninavyomfahamu Mungu aliyeumba mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana si Mungu wa Niqab.Kuna mchangiaji katoa hadi laana kwamba wanaosema niqab si vazi la heshima walaaniwe. Hii laana haitoki kwa Mungu aliye hai yaani aishie juu mbinguni labda miungu maana biblia inasema miungu ipo na watu wanaiabudu wengine kwa kujua au kutokujua kuwa ni Mungu aliyeumba mbingu na nchi. Tuamke watanzania huu udini utatupeleka jehanamu.Niqab ni vazi kama mavazi mengine na sio kwamba si vazi la heshima ila kama ofisi imezuia kwanini kupiga kelele na kuanza kuingiza udini?Kama dini yako inakufanya ugombane au kupigana na watu wengine kwa ajili ya kulinda masilahi ya dini hiyo hapo Mungu hayupo wala hausiki labda miungu.

    ReplyDelete
  66. we na mkaputura wako ulikuwa unaenda nao wapi, inaelekea hujui uvae nini mahali gani. tena wapige marufuku na visuruali vya kubana maofisini, hasa kwa wageni.

    ReplyDelete
  67. MBONA UGONJWA WA DADA ZETU VIMINI HAVIKUANDIKWA HAPO?HIVI KIMINI NA NIKAB LIPI VAZI LA KIHUNI?VYOTE VILIVYOANDIKWA HAPO HATA VIKIACHWA VIENDELEE HAVINA ATHARI KUBWA KAMA MWANAMKE KUTEMBEA MAPAJA NJE!TANGAZO LINA MAPUNGUFU!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...