Jumamosi sisi wana wa kituo cha kulea yatima cha  Guardian Angel tulitembelewa na dada Anna Peter wa East Africa Redio  wa kipindi cha Power Jams. Alikuja kufanya mahojiano na watoto pamoja na Uongozi wa Kituo chetu. Tunashukuru sana dada Anna kwa kuja kututia moyo kwa kuzungumza na sisi. Mungu akubariki sana!
Watoto hawa  bado hawana vitanda vya kutosha, magodoro na chakula kama kuna yeyote atakayependa kusaidia. 
Mawasiliano yetu ni 0757 855858 au 0655 855858

 Anna na watoto hao
Hapa Mkurugenzi wa kituo Miriam Msangi (kulia)  Anna wakipozi na baadhi ya watoto yatima wanaolelewa hapo  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Jamani jamani hebu saidieni kwa hili! hawa watoto tunawapenda sisi ndugu zao: akina baba wadogo, mama wadogo , mabibi, mashangazi , wajomba , mababu n.k. Lakini watoto hawa serikali badala ya kuwasaidia tu kwa mali , hebu waangalie kuwasaidia katika maadili.

    Kusema kweli watoto hawa wakishafiwa na wazazi, hawaleleki, wanakuwa hawana maadili tena. Na ukithubutu kumchukua kukaa naye, hataki umguse kwa lolote lile... kumuonya, kumtuma kashughuli kokote. Ukimtuma tu au kumuonya tu tayari anakwambia unamnyanyasa kwa kuwa hana wazazi. Mara moja anakimbilia kituo cha kulea yatima. Tunaomba ili watoto hawa wapate malezi mema tunaomba na NGO zinazowasaidia kwa mali basi na maadili iwe hivyo hivyo. Hii misaada ya serikali au NGOS si endelevu, hata kama ni endelevu, basi na ndugu tuwezeshwe kwa kupungziwa mzigo huu wa maadili ya watoto hawa.

    Nawasilisha

    ReplyDelete
  2. Mtoa maoni wa kwanza namuunga mkono.

    Mie natoa wito kwa walezo NGOS wasiwapokee watoto hivi hivi tu halimradi kakimbilia kwao. Sawa mpokee lakini wafanye uchunguzi..watoto wa siku hizi si wa zamani... wenye wazazi hawaleleki sembuse wasonao! Mie kwa upande wangu naona kweli maadili kwa watoto yatima yazingatiwe....hawa ni wabaya zaidi wasipoangaliwa ipasavyo. Wengine wanaona fahari kufiwa ili waweze kujiwatala vema..

    ReplyDelete
  3. Ni kweli wachangia maoni mliotangulia mpo sahihi ila ni sisi wenyewe wanandugu tulio mstari wa mbele katika kuwafanya watoto hawa wakae katika mazingira magumu, kwani wengi huwa hawawajali na hata malezi yao huwa sio ya kuwafuatilia kwa sana, na wengi ambao wapo tayari kuhudumia watoto hawa baada ya kufiwa pia hali zao kimaisha huwa ni duni hata mazingira yao huwa hivyo. Kutokana na hili hata uangalizi wa watoto hao huwa sio timilifu. mfano kituo chetu Guardian Angel tulikuwa na watoto wengi sana, ila tumewapunguza kwa kutafuta ndugu zao na kuwawezesha wale wasio na uwezo kwa mitaji ya biashara ndogondogo ambazo zinawafanya waweze kuwasupport watoto hao na sasa wanaendelea vizuri kiasi cha kwamba hawahitaji kuwa kituoni. Tunawatembelea na kutoa semina mbalimbali kuhusu malezi ya watoto na ujasiriamali. Watoto wenye viburi hao hawajapata walezi wenye msimamo na kujua jinsi gani ya kumlea mtoto ambaye amepata matatizo hayo. Kumbuka japo ni watoto lakini wana haki ya kusikilizwa, kuonyeshwa upendo na hata kama amefanya kosa gani tafuta jinsi ya kuzungumza nae vizuri atakuelewa tuuu na hakuna mtu asiyeweza kubadilika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...