MAREHEMU RICHARD AUGUSTINO MWARABU


MPENDWA BABA YETU RICHARD AUGUSTINO MWARABU, ILIKUWA SIKU, MWEZI NA HATIMAYE LEO TAREHE 09/03/2012 UMETIMIZA MIAKA 16 TOKA UTUTOKE KATIKA DUNIA HII.TUNAFARIJIKA KWASABABU TUNA AMANI UKO PAMOJA NASI KIROHO SIKU ZOTE.

BABA HAKUNA SIKU IPITAYO KWETU BILA KUKUMBUKA KWA UPENDO NA UKARIMU WAKO,USHAURI MWEMA, MISIMAMO BORA NA BUSARA ZAKO KATIKA KUTULEA NA KUTUUNGANISHA SISI WANAO NA FAMILIA PAMOJA,BUSARA ZAKO ZIMEKUWA DIRA NA NURU KATIKA MAISHA YETU.TUNAENDELEA KUKUOMBEA NA TUNAENDELEZA YALIYO MEMA KWA WAJUKUU ZAKO UPUMZIKE KWA AMANI.

DAIMA UNAKUMBUKWA NA MKEO MWIVEI, WATOTO WAKO: CHARLES, MARTIN,PATRICK,MVUNILWA,PETRO,EZEKIEL, ESTHER NA MAMNTAMBO,.WAJUKUU ZAKO PIA WANA KUKUMBKA, KAKA YAKO KOMESHA NA DADA ZAKO TONI, MAKALATA, VERIANA NA SARA NA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI ZAKO.DAIMA TUTAKUKUMBUKA MILELE.


BABA TULIKUPENDA SANA, LAKINI MUNGU BABA WA MBINGUNI ALIKUPENDA ZAIDI.BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE, AMEN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Namkumbuka vizuri Mzee wetu Mwarabu alikuwa akifanya kazi benki, tumeishi nae Dodoma na kucheza pamoja na watoto wake akina Petro,Mvunilwa na Ezekiel. Kaka yao Patrick alikuwa akisoma Kazima tukimuona wakati wa likizo dodoma.

    Baadae wakahamia Tanga na sisi tukahamia Tanga, what a coincidence! tukiishi Chumbageni wao Sahare.

    Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.

    Petro upo wapi? niandikie mdau saidiyakubu@gmail.com

    Mdau
    Saidi Yakubu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...