Baadhi ya Wanahabari  wakiwa hawana la kufanya nje ya jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, baada ya mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya msanii maarufu wa filamu, Steven Kanumba, Elizaberth Michael ‘Lulu’ kufikishwa na kuondolewa chap-chap kwa kificho mahakamani hapo kutokana na kuhofia usalama wake. Hata hivyo Globu ya Jamii imeweza kupata picha ya Lulu akiwa mahakamani
Muigizaji wa Filamu nchini anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba,Bi Elizabeth Michael a.k.a Lulu (pichani) amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake kuhusiana/kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.

Akisomewa mashitaka na wakili wa serikali, Beatrice Kaganda Lulu alidaiwa kufanya mauaji hayo April 7 2012 huko Vatican Sinza jijini Dar es Salaam.

Lulu alipingana na mwendesha mashitaka Kaganda pale alipotajiwa kuwa yeye hana umri wa miaka 18 na  akadai kuwa umri wake ni miaka 17 na kuwa ni kweli mkaazi wa Tabata, Dar es Salaam.

Lulu ambaye alionekana mtu aliyekuwa na mawazo mengi na hofu kubwa, macho yake kama mtu aliyekata tamaa akisubiri huruma, Hakutakiwa kujibu lolote kwasababu mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo ya mauaji hivyo kesi iliahirishwa hadi April23 2012.

Lulu kama lilivyo jina lake, ndivyo alivyoingizwa mahakamani na kuondolewa, akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari kanzu waliomuingiza kwa haraka na kumtoa kwa haraka wakikimbia naye kwa kupitia mlango wa nyuma kuingia kwenye gari iliyokuwa na tint nyeusi iliyoondoka kwa speed.

Waandishi wa habari wa vyombo tofauti tofauti walibaki na mshangao wasielewe tafsiri ya kitendo kile cha kumficha mtuhumiwa huyo kuliko wengine ambao huletwa na kuondolewa bila ulinzi huo.

Habari  zinaeleza kuwa mtuhumiwa amepelekwa gereza la segerea na 
kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena A pril 23 mwaka huu.

Muigizaji huyo aliletwa mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi chini ya  ulinzi mkali  wa polisi. Na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya suzuki grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 60 mpaka sasa

  1. Oooh......God pole sana mdogo wangu,inackikitisha sana, umeingia hatiani bila ya kutarajia,omba na sali sana mungu akutangulie katika kila kitu!!!!

    ReplyDelete
  2. OMG!! can't wait to hear this news, So sad the lady looks like is completely confused and don't know what to do just leave what court will address to her, Pole lulu yu so young!!!

    ReplyDelete
  3. Habari Watanzania,
    Mimi ni moja katika watu walioguswa sana na msiba huu japo siyo mpenzi sana wa filamu ziwe za kwetu au za nje.
    Ninachoomba kwa wenzangu Watanzania ni kwamba tuwe watulivu na tusimjaji huyu mtoto na tuachie mahakama kazi yake. Hakuna anayejua haswa nini kilitokea kati ya wawili hao na wenyewe tu ndo walioshuhudia japo hatuwezi kupata utetezi wa upande wa pili. Lakini kutokana na uelewa wangu ukweli utajulikana kwa kufuata sheria. Tuweke ushabiki nyuma na tuache watu wafanye kazi yao. Tumhurumie huyu mtoto japo lililotokea limetuuma sana na tuombe kwa Mwenyezimungu haki ipatikane kwa upande ule unaostahili. Hili linaweza kutokea kwa mtu yeyote kwani tukumbuke sisi ambao tumeshakuwa katika mahusiano au hata ndoa kabisa mara nyingine huwa tunapenda kucheza na wapenzi wetu na hata kusukumana kwa mchezo tu na tujue lililotokea laweza kutokea hata kwenye michezo.
    Lakini kwa hili tunajua kwamba lilitokea katika hali ya ugomvi kati ya wawili hao, lakini je, tuna uhakika kuwa nani alianza na kwamba yaliyotokea yalitokea katika kujihami(self defence) au ni shambulio la dhamira? Hatujui, hivyo nawaomba Watanzania wenzangu turidhike na kuamini mahakama zetu kwamba ukweli utapatikana. Najaribu kuvaa kiatu cha huyu mtoto, cha baba yake, cha mama yake na naogopa sana nikijiweka katika hali hiyo. Naamini wako katika wakati mgumu sana na pia huyu binti yuko katika wakati mgumu sana.
    Ninachoomba kwa waangalizi wanaohusika kumuangalia huyu binti kuwe na utaratibu wa kumpatia daktari wa saikolojia ili aweze kumfanya awe na matumaini. Bado ni mchanga sana kubeba huu mzigo na ni mdhaifu sana kuwa katika hali hii.
    -Mdau wa Mwanza.

    ReplyDelete
  4. Poor little girl, I really feel sorry for her, where is Women Legal Rights team to assist her. Let the courts determine if she is guilty but atm she needs all the help she can get. Did she really hit him or he fell down? There are many things to be considered. Nashangaa polisi was Bongo walivyo efficient, it has taken them less than a week kudetermine kumbwa she has a case to answer, phewwwwwwwwwwwwwwwwwww, mtu kafa hapa!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. KAWAIDA MAJIBU KUTOKA KWA MEDICAL EXAMINER YANACHUKUA MUDA INA MAANA MARA HII MAJIBU YAMESHAPATIKANA???HUYU BINTI WANGEMUACHIA HURU MPAKA HAPO ITAKAPOGUNDULIKA KAMA YEYE NDIE ALIYEUA YAWEZAKUWA STEIVE ALILKUFA KWA SHINIKIZO LA MOYO VILE VILE

    ReplyDelete
  6. Lulu angaliwe kwani bado ni bint mdogo anayehitaji bado uangalizi wa karibu wa jamii .Hatuwezi kumuhukumu hatukuepo katika tukio tumuombee na jamii ijifunze kitu kutokana na yaliyotokea .

    MDAU.

    ReplyDelete
  7. Jamani sio kuhusu Mwanamke au Mwanamme najuwa wengi wataanza oh haki ya Mwananmke hizi haki za Mwanamke zinakuja wakizidiwa tu hhata kwenye ukweli ila stil haka ni Katoto jamani 17 mpeni zamana awe nje ila kwenye mikono ya ulinzi apuwe ale aoge angalau kwenye nyumba ya hata Polisi wa kike.. Tukaonee huruma huku kesi inaenda. Masudi

    ReplyDelete
  8. pole sana lulu mungu atakusaidia mdogo wangu kwasababu naamini kabisa hukukusudia ni bahati mbaya

    ReplyDelete
  9. Wapenzi wa marehemu Kanumba ni wanafiki wakubwa kujitokeza kumlilia lakini hakuna anayezungumzia kufuatilia hii kesi ili marehemu apate haki yake.
    Kulia kote huko kwa nini kama haki haitatendeka?

    ReplyDelete
  10. pole zake!

    ReplyDelete
  11. Pole sana mama na muombe Mungu tu yatakwisha.

    Ni siku zake zilifika na wewe 'ukawa daraja'hivyo jipe moyo mkuu mama.

    Bali kwa wasioelewa watakulaumu sana.

    ReplyDelete
  12. muschi b.c.April 11, 2012

    Elizabeth
    usijali kama ulihusika ama hukusika Mungu ndiye anajua. Hata kama mahakama itaamua kukufunga maisha au kukunyongwa haitasaidia. Mtegemee Mungu ndiye mweza wa yote. Nakuombea afya njema uweze kukabiliana na hali hii ngumu iliyo mbele yako!

    ReplyDelete
  13. Dont worry Lulu!,Everything will be fine.
    God still loves You,no matter what the world will judge you!.But Only God gives pure love and forgiveness!,just allow yourself to receive forgiveness.
    Be blessed.
    R.I.P Kanumba

    ReplyDelete
  14. LULU DADA KUWA MUWAZI TU ELEZEA ILIVYOKUA,HATA KAMA ULIMSUKUMA,LABDA HUKUJUA KAMA MAUTI YANGEMFIKA,MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU,HATA UKISHINDA KESI LAKINI UJUE HICHO KITENDO KITAKUZUNGUKA KICHWANI,

    ReplyDelete
  15. Masikini namuonea huruma sana huyu binti,i hope ukweli utajulikana na haki itatendeka.

    ReplyDelete
  16. Kweli Tnzania hakuna haki hata kidogo,huyo Michael Jackson alivyokufa docta wake hakukamatwa hapo hapo hadi uchunguzi ulipokamilika,serikali hii na mfumo wake ni aibu tupu

    ReplyDelete
  17. Mungu, yupo pamoja nawe usijali ni sehemu tu ya maisha. Kama ulifanya kwa kudhamilia basi mbivu an mbichi zitajulikana.

    ReplyDelete
  18. Mwenyezi Mungu...!! atamrehemu na ndiye ajuaye mwenye makosa...na wanasheria wamsaidie kuona makovu alivyopigwa na Marehemu...na nasiki ana uja uzito wake ni vema binti akafunguka na DNA zikafanywa mapema...!!

    ReplyDelete
  19. POLE LULU. NI BAHATI MBAYA HATA KAMA ULIMSUKUMA AU ALIJIKWAA HUKUWA NA NIA YA KUMUUA. MLIKUWA WAPENZI. HAKI ITUMIKE NATEGEMEA VYOMBO VYA DOLA VISIFATE MEDI AU USHABIKI WA KUWA TULIMPENDA KANUMBA. HAKI ITUMIKE

    ReplyDelete
  20. Ankali hivi huyu kicheche lulu mbona haeleweki walipoulizwa na kile kipindi cha mkasi cha salama jabir kuhusu umri wake alisema kuwa ana miaka 18

    salama jabir alimuuliza ikiwa ana miaka 18 na ameanza kuenda disco kumbi za starehe miaka minne 4 nyuma ina maana alianza akiwa na miaka 14

    sasa leo hii anasema kuwa ana miaka 17 na hivi kweli jamani hawa watoto wana haraka gani ya maisha na kuanza starehe miaka 14?
    hawataki elimu?
    ndio faida ya ulezi mbovu.

    ReplyDelete
  21. Elizabeth michael pole sana mdogo wangu,mimi sina uwezo ila jamani mwenye uwezo baada ya kesi yake amchukue aende nje ya nchi walau apumzike jamani,hatujua anajutia kiasi gani maana anaweza fanya maamuzi magumu hasa akijichukia mwenyewe,wasamaria msaidieni lulu apumzike,namuonea huruma sana sasa hapo kichwani sijui anawaza nini,siajabu anajuta sanaa,mahakama imsamehe tu kwani wangapi wanafanya makosa?hata ikimbana kiasi gani uhai wa kanumba utarudi?lulu mama omba hata kimoyo moyo mungu atasikia sala zako,nasi tunakuombea,nakupenda sana lulu,single parent ni tatizo sana.

    ReplyDelete
  22. we are all with her at this time the only mistake why did she run!!!!!!!! angebaki kusaidia isingeonekana vibaya kabisa, kitendo cha kukumbia kimemponza mdogo wangu

    ReplyDelete
  23. Tunaomba hukumu ya haki ipite. Kama hakuhusika aachiwe lakini kama kaua apewe hukumu stahiki. Haki itendeke

    ReplyDelete
  24. msichana mzuri ndio kwanza una miaka 17 rudi kwenye dini yako ya kuzaliwa ambayo ni islam achana na dini ya ubatizo

    anza kusali kumuomba Allah na Allah atakusaidia kesi itaisha na utaishi maisha ya amani.

    ReplyDelete
  25. hivi huyu si ndio yule aloact filamu anamuua baba ake mzazi Ambae anakua baba ni muuaji?
    hizi filamu za kwetu hazifai kuwahusisha watoto wa underage na hayo ndio yanayotokea ulaya na marekani watoto wanacheza game za kivita kisha wanaigiza katika ma collage yao.AAAMA KWELII- lakini we never know labda haya mambo wenye nchi wameyapanga au vipi.

    ReplyDelete
  26. Lulu Omba Mungu wako.Nina imani hukutarajia hayo.Wewe sio muuwaji.Binaadam tunakuhukumu tunasahau kuwa ni kazi ya Mungu na serikali.Vyombo vinavyohusika viko wapi kutoa msaada kwako na faaji milia yako.(proffessional help-physchology nk)Huyu binti anahitaji sana msaada.Kina mama mko wapi?Maneno ni mengi kwani tuangalie nyuma je yeye ni wa kwanza kuwa binti machachari?Na huyo kanumba pia hakuwa msafi ilikuwaje baba wa 28 kuwa na mahusiano na kitoto alichokielea kwenye ulimwengu wa maigizo.Jamani muwe wakweli mtende haki sawa.

    ReplyDelete
  27. Liwe fundisho kwa mabinti wadogo wenye mambo yanayowazidi umri. SIna maana kuwa namuhukumu kuwa ameua; ila kwa umri wake hakupaswa kuwa nyumbani kwa wanaume muda mbaya hivyo. Nina imani wazazi wake walishamshindwa wakaacha dunia imfunza na ndo funzo lenyewe hilo.

    ReplyDelete
  28. Eeeeeh wewe luluh umezidi kuparamia mambo ya wakubwa ukiwa umri mdogo! Wasanii lazima muwe vioo kwa jamii!

    Mara kibao ukiwa under 18 (luluh) nimekuona sana maisha, bills!
    Kila uliposhauriwa hukusikiaaa! Ukijitetea ooh me star maneno lazima

    Haya uko wapi sasa? Ungetulia yote yasingekukuta! Ulitakiwa uwe shule now maana hata 4m6 hujafika degree huna! Ulitakiwa uwe navyo hivi coz nafasi ulikua nayo!

    Mdogo wangu dunia hadaa ulimwengu shujaaa!

    Ukipona kwenye hii case utajitamba saana bt please liwe fundisho mtoto eeeh! You are too young 4this! Jus like the way steve was to die!

    Manslaughter itakuhusu! Be smart utachomoka

    ReplyDelete
  29. Hapa tuombe mungu haki itendeke. maana kama kawaida yetu hapa bongo, Lulu alikamatwa na polisi na kuswekwa kupango, hakuwa na access ya Mwanasheria, polisi wamemuhoji na kuchukua maandishi yake bila ya yeye Lulu kupata ushauri kutoka kwa mwanasheria huru. Kesi hii ni kubwa na kutokuwa na upeo wa kisheria kwa mtuhumiwa Lulu na kukosa mssada wa kisheria mapema kunaweza kuweka dosari katika madhumuni ya kuhakikisha haki inatendeka.

    ReplyDelete
  30. Kwa africa hata kama hajaua huyu dada atasukumiziwa tu sababu yeye ndio chanzo.... huruma inakuja kuwa bado mdogo ila bado tunarudi pale pale kafanya kosa na akitaka kuishi kwa raha akubali adhabu lakini sio kifungo cha maisha wala kuuwawa.

    Kwa wale ambao mnajiona ni mastaa huko bongo kaeni chonjo leo huyu kesho wewe...

    RIP SK

    ReplyDelete
  31. lulu dada, najua una wakati mgumu sana na unapata maswali magumu sana yasiyokuwa na majibu. Mwombe Mungu akupe ujasiri na akuongoze kwa kila neno litakalo toka ndani ya kinywa chako.
    mdau kutoka dar es salaam

    ReplyDelete
  32. Mungu amtangulie huyu mtoto haki itendeke

    ReplyDelete
  33. wao a lot of comment here,pregnancy, mtoto mdogo,aachiwe huru, akakae kwa police. what can i say. It happens that I like to watch this unsolved mysteries(http://www.cbsnews.com/video/48hours/). Guys go on this website mtajifunza mengi.

    ReplyDelete
  34. Hahahaha hapa ndio "foreseability Principle" inapopata umaana.

    ReplyDelete
  35. MBONA MAJIBU YA BABU WA LOLIONDO KAMA ILE DAWA INAPONYA AMA HAIPONYI MAELFU WAMEKUFA HAJAKAMATWA AU WALISUBILI ILI MAREHEMU KANUMBA AENDE NDIYO BABU AKAMATWE. HUYO MKEMIA AMA MEDICAL EXAMINER YUKO WAPI KUTUPA TAALIFA YA KIKOMBE KAMA KINA TIBU AMA BABU TAPELI? WATU KIBAO WAMEKUFA MBONA ISSUE YA LULU IMEKUWA FASTER FASTER?

    ReplyDelete
  36. Kaka hapo juu mie binafsi kiatu cha baba yake hakinitoshi na cha mamayake lazima kidogo.binfasi namuonea huruma sana naamini atashinda kesi ila atakuwa amejifunya nini katika maisha yake yaliyobakia na kusamehewa kwake ni kitu kimoja tu kubadilisha mwelekeo wa maisha yake na jamii ijue kweli amebadilika basi watamsamehe mbona ni mwanadamu tu

    ReplyDelete
  37. MIMI NI MAMA KWAKWELI KTK NAFASI ZOTE MBILI NIKIWA KM MAMA WA MAREHEMU AU MAMA WA MTUHUMIWA NAJARIBU KUPATA FEELINGS PANDE ZOTE MBILI IWAPO KM MAMA, INAUMA MAMA WA MAREHEMU KUMPOTEZA MTOTO WAKE KIPENZI KWAKWELI NIMEUMIA SANA MBALI NA USHABIKI NIMEUMIA KM MZAZI, NA VILEVILE UPANDE WA PILI WA SHILINGI, NIKICHUKUA NAFASI KM MZAZI WA MTUHUMIWA ANAJISIKIAJE? JAMII INAMUONAJE NA NINI HATIMA YA MWANAE HAPO BAADAE... TUNACHUKULIA MZAHA MZAHA, KUAMBIWA UMEUA SI KITU KIDOGO, NA KWA UMRI WAKE NI ISSUE NZITO KUKABILIANA NAYO KISAIKOLOJIA, LAKINI KIKUBWA SIMLAUMU MTUHUMIWA NAMLAUMU MZAZI WAKE MALEZI YALIKUWA HAYANA MAADILI NIMEFATILIA KWA KARIBU HISTORIA YA MALEZI YA MTUHUMIWA, NIMEGUNDUA MAMA AMECHANGIA KWAKIASI KIKUBWA MTOTO HUYU KUWA HAPO LEO,NANI ANAJUA LULU ANALALA NJE? MBALI NA NYUMBANI NA MAMA YAKE HAONI AJABU? UMRI ULE, NA IWEJE MTOTO MDOGO WA UMRI ULE FAMILIA IMTEGEMEE? WAKATI MAMA YAKE ANAFANYA BIASHARA NDOGONDOGO, NA MAREHEMU ALIKUWA AKIENDA KWAKINA LULU KUMCHUKUA MAMA YAKE ALIKUWA ANAJUA? IWAPO MAMA UNAKAA BAR ASUBUHI UKINYWA UNATEGEMEA MTOTO ATAJIFUNZA NINI? MTUHUMIWA ALIPOFUKUZWA SHULE MAMA ULITAKIWA UKABILIANE NALO KUMRUDISHA MTOTO KWENYE MSTARI NA SI KUMUAMISHA UKAONA UMEMSAIDIA BILA KUMKANYA? NINA MENGI YA KUANDIKA AMBAYO SI SAWA..LULU NI MTOTO AMBAE BADO ANAHITAJI KUSOMA BADO, ASILEWE USANII AKAONA AMEMALIZA KILA KITU, LEO MAMA ANFURAHIA MTOTO ANARUDI NA BURUNGUTU KESHO ATARUDI NA UKIMWI USO WAKO UTAINAMISHIA WAPI? MRS. SARAKIKYA.

    ReplyDelete
  38. Mungu ndio anaejua ukweli wa janga hili. Sitaki niwe hakimu kwenye kesi ya haka katoto! Ila ukiponyoka kwenye hili! basi badilika! Huyu sisi twamwita mtoto, ila huyu si mtoto mbona ni mzee mwenzetu! Binti mzuri wenda paramiwa hovyooo na wazee wa kukuzaa!Mola atakujalia inshalla utatoka, ila ukitoka achana na ustaa koko au mbuzi!! Pengine Mungu ametaka ujifunze kitu kwenye hili! si kukimbia sana mbio ndio kufika. Kanumba alifanya movies 40 na bado alikuwa akaa machokoroni! wewe tokea ulipokata kamba, umeshakuwa na nini cha ajabu! nakuombea Mola akuepushie janga hili.

    ReplyDelete
  39. Ni vizuri kuona wasomaji wa hii Blog wanestaarabika vya kutosha kutokuanza kutuo hukumu kabla ya Mahakama. kesi bado changa hii, na sheris inasems mtu ni innocent till proven Guilty. kama wenzangu wengi walivyosema hapo juu, tusubiri vyombo vya sheria vitoe Haki.
    Mtowe

    ReplyDelete
  40. Kwanza kabisa ni masikitiko makubwa kumpoteza Marehemu Kanumba kwetu wote tuliobakia duniani na hasa kwa familia yake, na nina toa salam zangu za rambirambi. Pili, ndio nakubali pia kuwa tusimhukumu Lulu ila tuiachie mahakam ifanye hivyo.Lakini haki lazima itendeke ipasavyo kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu.Mimi si mtaalam wa sheria na nadhani kama ni bahati mbaya huwa ina adhabu yake na kama ni kusudi pia ina adhabu yake. Kilichobaki ni kuwaombea wote marehemu, familia ya marehemu, Lulu na familia ya Lulu pia katika wakati huu mgumu.

    ReplyDelete
  41. Hata kama hakukusudia kumuua kuna principle inaitwa "The egg shell skull" inayotaka umuache mtu kama ulivomkuta, inayomaanisha kwamba, hata kama utasema labda alikuwa na ugonjwa wa moyo ama na presha sijui why umsukume? simhukumu lulu bali naelimisha. Ni kweli kwamba lulu atakuwa na defence ya self defence ama ni accident itakayomtoa. Na kama miaka naona ishageuzwa sasa make nilipoona kipindi cha mkasi tayari alisema ana miaka 18. Sawa it might have been done purposely to save her kuwa ni mtoto so asifungwe. Kikubwa ni kwamba hata akiachiwa guilty consciousness will always hunt her no matter the place she might live, hata aende ulaya atamuona Kanumba and she wont have peace of mind. Nini cha kufanya sasa?
    Kwanza anatakiwa akaombe msamaha wazazi wa kanumba.
    Pili Ajisamehe yeye mwenyewe, yaweza chukua muda lakini akipata counselling na kumfundisha jinsi gani mtu anaweza kujisamehe.
    Tatu aombe msamaha kwa watanzania wote kwani ni midomo mingi inayosikitika, kumbuka maneno huumba hasa ukizingatia kuwa kilichotokea ni kweli hukusingiziwa. Make hata wanaokutetea kuwa hukuhusika labda ni moyo still you are the cause of it, kama usingepokea hizo simu zako asingestuka.
    Nne, Utubu na kumrudia Mungu, kuna aliyesema kuwa urudi uislam kuwa ndo bora zaidi ya ubatizo, hyo ni maoni yake ana uhuru wa kuongea, wewe ni mtu mzima utajua wapi panakufaa zaidi.
    La mwisho,akiomba msamaha watanzania tumsamehe tu kwani kila siku wakristo huwa tunasali kuwa Mungu atusamehe kama nasi tunavyowasamehe wengine, tusipomsamehe na Mungu hatatusamehe sisi.
    Asanteni

    ReplyDelete
  42. Lulu pole mdogo mdogo wangu! Mwenyezi Mungu anakila sababu yakile leo kilichotokea inakupasa kutafakari mapema mitihani hii yakimaisha juu yako! kwanza umshukuru Mungu uko mikononi mwa sheria salama naona pia Mungu anakupenda kwani ule umati wa jana ingekuwa bahati mbaya ukapata fursa ya kuja makaburini cjui nini kingetokea jinc ambavyo wanadamu kila mtu anauelewa tofauti juu ya hiki kilichotokea! Cjui wewe ni dhehebu gani lakini naamini una imani kuwa Mungu yupo na ukiomba anajibu...Umumuombe mwenyezi Mungu kwanza akusamehe na pili akuongoze km una imani kwahili atakusimamia haki itatendeka utatoka uendelee na maisha mengine,
    Ushauri wangu kwako "UBADILIKE! LULU UWE LULU KWELI, UACHANE NA ANASA ZA KIDUNIA WEWE NI MZURI SANA UNAKILA HAJA YAKUJIVUNIA UZURI WAKO! NENDA SHULE...UJIENDELEZE SANAA IPO LAKINI UKIWA MSOMI UTAKUWA JUUZAIDI...MAGAZETI HAYAKUPI UMAARUFU MZURI YANAKUHARIBIA, MTOTO MDOGO AT THAT AGE MAMBO YAKURUKARUKA UYAACHE, TAFUTA MARAFIKI SAIZI YAKO HAO WALIOPOTEA WASIKUANGAMIZE, MIMI NAUMIA SANA KWANI WATAUFUJA UZURI WAKO THEN WATAKUACHA VIBAYA. WEWE NI MZURI YANI NATAMANI NIPATE FURSA YAKUONGEA NA WEWE UNIELEWE "Ngoma ivumayo....."

    ReplyDelete
  43. Hi all. Nafikiri watu wengi wana miss big picture juu ya jamii yetu ya kitanzania ilivyo hivi sasa. Lulu ana represent a true picture ya jinsi maadili yetu ya kibongo yalivyo potea, na yanavyo potea. Watoto wanaanza kupotea mapema. Why? kuna mengi tunayo weza kujiuliza lakini kwangu mimi, naamini maisha yamekua magumu, hivyo familia nyingi zina jikuta katika wakati mgumu wa kua pamoja. Watu wana zaa hovyo, ndoa zina vunjika na kuparaganyika. Hapo ndipo uzuri au jinsia inatumika kusaka mlo na mahali pa kulala. Pia, Je tumtumie lulu kama kesi ya kuadabisha sehemu zetu za starehe zinazo haribu ujana wa watoto? kwa nini watoto wadogo mpaka umri wa miaka kumi na sita wana ruhusiwa kuingia club na kunywa mpaka kuharibikiwa. Watoto wanatakiwa kulindwa. Lulu si mtoto; ahukumiwe kama wengine wote wa umri wake wanavyo hukumiwa. Jinsia isiwe kigezo. Haki itendeke.

    ReplyDelete
  44. Pole sana lulu. I don't know know what kanumba was doing with a girl her age anyway. All those people on tv talking too much about kanumba are fakes after fame, most of them probably barely knew him. People are so quick to vilify her that they are forgetting all the bad things kanumba was also doing. I hope the media coverage doesn't destroy her case and the police properly investigate instead of following the whims of gossips that want a quick decision so they can sell more gazzette.

    ReplyDelete
  45. Mh.Halima Mdee angalia usipoteze kura zako kwa kushabikia usichokijua.Nimesoma msg zako toka twit unasema kuwa Lulu anamajeraha aliopigwa na maremu, Unauhakika gani na hilo? ukiwa kama mwanasheria unapaswa ujiulize Lulu alipokimbia sehemu ya tukio alienda wapi?Je kama alienda kwa huyo bwana aliyekuwa anampigia simu na akamchapa au kafanya hivyo kutengeneza story? unajua Lulu ni muigizaji hivyo anaupeo wa kutosha kabisaa kuwa ninini kinafuata baada ya hilo tukio. Kuhusu umri wa Lulu mimi naona ni utata mtupu,upande wa upelelezi nawashauri wafuatilie uhalali wa cheti chake na ikiwezekana wapate record za hospital aliyozaliwa. nahisi atakuwa 18 and over and not under 18 jamani,mbona mambo ya kikubwa kaanza zamani sana? Halima Mdee chunga sana huo mdomo wako usifikirie na hizo ni kampeni.Swali la kujiuliza?Lulu anamiliki driving licence toka lini?je inaruhusiwa kwa mtu wa chini ya 18yrs kuwa nayo? huyo mtoto atakuwa na vyeti tofauti na vinatumika mazingira tofauti kutokana na mahitaji. Sheria ifuate mkondo wake.

    ReplyDelete
  46. They were together in the middle of the night nyumbani/chumbani kwa Kanumba,hawa ni watu waliokuwa karibu sana!Lulu young as she is owes so much to Kanumba,whether walikuwa wapenzi or not.Kanumba ndiye aliyemlea na kumfikisha kisanii hapo alipo sasa Lulu.There is no way(unthinkable)Lulu could have done what most pessimists are predicting!And there is no way Kanumba could have done similar harm to Lulu,his Treasure (in Movie Industry)!Hatui,we love Kanumba,but the truth is Dead Men Tell No Stories,the saying goes....!But,the truth and nothing but the truth will always prevail at the end of the day!Lulu will walk out innocent!Ulikuwa usiku mnene sana,past midnite!Kuna ile Whisky iliyokutwa chumbani!Kuna simu iliyopokelewa na Lulu inasemekana,but nobody can be sure of this except Lulu herself!Yeye kama Movie Star anaweza kupigiwa simu na mtu yoyote wakati wowote kikazi na sio lazima iwe kimapenzi!Kuzozana baina ya Lovers au Partners (particularly movie stars) ni kawaida kabisa duniani kote!Lulu to the best of my imagination hana ubavu wa kumsukuma Kanumba with such Impact kiasi cha kusababisha yaliyotokea!Inaelekea mdogomtu alikuwepo karibu sana na lazima lingekuwepo jambo baya la kutisha angefahamu mapema na kuchukua tahadhari mapema!But it appears this was strictly an affair between the two lovely couples!very unfortunate,kilichotokea kimetokea!Its only Lulu who can tell the world exactly what happened,tell the exact and whole truth! Ile ni ajali ambayo hakuna aliyeitarajia!Our only hope left are the findings from the Govt Chemist,on whether poisoning was any such possibility!Otherwise,jamani tumrejee Mungu,this poor girl could be innocent,and this is what it is! Jambo moja tu,katika kipindi hichi kigumu Lulu asiachwe peke yake,asije akanywa sumu,lazima pawepo na uangalizi wa karibu sana na apewe kila aina ya msaada wa Kisaikolojia na neno la Mungu ili akili yake iweze kutulia.She is still too young to be left alone! Being a movie star,especially for the actresses,has dire consequences,hilo kina dada lazima walijue!Ni kazi nzuri,ina heshima kubwana inalipa sana,lakini machungu yake ndiyo hayooo!usumbufu kila mahali!hakuna atakyekuacha utulie hata kama umeshampata wakwako!Tusali Mungu amuepushe Lulu na dhahama inayomkabili.Tutamtendea haki hata mpendwa wetu Kanumba kwa kufanya hivyo!wote mbarikiwe!

    ReplyDelete
  47. Wote tunaochangia hapa ni wazazi tunamaumivu ya pande zote, but ukweli ni kwamba Lulu hata hiyo miaka 17 hana na kama amefika 16 labda iwe mwaka huu, hii ni Tz na watoto wa kike/kiume kwenye facebook huku wazazi wakifurahia mtoto wangu amekuwa. Wazazi tuacheni tamaa za kutaka hela/zawadi kutoka kwa watoto. Lulu ni mdogo sana hata kuwa na boyfriend na huyo boyfriend angejua kuwa it was wrong to approach her. Anyway ndo hivyo tusijaji zaidi. Ila ninhofu Lulu akiachiwa huru atajiua

    ReplyDelete
  48. POLE SANA MDOGO WANGU LULU, NAAMINI KWA UWEZO WAKE MWENYEEZ MUNGU, NAKUOMBEA AKUVUWE JANGA HILI KWA SALAMA NA AMANI, KWANI KUFA NI KWA KILA MTU NA KILA MTU NA AHADI YAKE, SEMA TU SABABU HUWA HAZIKOSEKANI, NDIO TUNASIKITIKA KWA KIFO CHA MAREHEM KANUMBA, LAKINI PIA HUENDA NDIYO AHADI YAKE ILIKUWA IMESHAPANGWA ITOKEE NA APANGALO MWENYEZ MUNGU, MJA HAWEZI KULIPANGUWA, TUENDELEE KUVUTA SUBIRA, NAAMINI MBIVU NA MBICHI ZITABAINIKA, KAMA UMKOSA UTASTAHILI ADHABU NA KAMA HUNA HATIA, BASI UTASTAHILI UHURU WAKO, NAKUHURUMIA SANA MDOGO WANGU. ILA USIJALIA NA NAAMINI ASIYEKUWA NA MTU, BASI ANA MUNGU. MWENYEEZ MUNGU AWE NAWE NA AKUVUWE HILI NA JINGINE, INSHA ALLAH - AMEEN.

    ReplyDelete
  49. KILA MTU HUFA KWA SIKU YAKE,WEWE IKIFIKA TIME YAKO UTAKWENDA TU,UKIUMWA USIUMWE,HAIZIDI DAKIKA.M/MUNGU AMESHAANDIKA KILA MMOJA ATAISHI UMRI GANI HIYO NI SIRI YA ALLAH,YEYE PEKE YAKE NDIE AJUAYE.MIMI BABA ANGU ALIANGUKA CHINI
    TULIPOMUANGALIA AMEKWISHA KUFA,WALA HAKUKERWA,AU KUGOMBANA NA MTU.HUYO KANUMBA AMEKUFA SABABU SIKU YAKE IMESHAFIKA,HATA HUYO LULU ASINGEENDA BASI ENGEKUFA TU,LAKINI VIFO VYENGINE HUWA NA SABABU,KAMA HAYO YALIYOMTOKEA LULU,INSHAALA M/MUNGU ATAKUSAIDIAYA LULU,POLE SASA LULU

    ReplyDelete
  50. Mimi nafikiri Lulu anaweza kutumia utetezi wa "self defence" kuweza kujinasua, ila tatizo nilionalo na polisi wetu ni katika kuandika maelezo "statement", kuna muda wanachomeka stories ambazo hukuongea na ambazo kesi ikianza kusikilizwa unaweza kushangaa unapata wakati mgumu katika madodoso "cross examination", kwa hiyo ni vema kama unahojiwa na polisi omba wakili au mwanasheria wako awepo ili aupate "guidance" nini cha kuongea, kesi yako ya mahakamani unaweza kuijenga au kuibomoa kwa maelezo yako pale polisi. Ila cha msingi bado nasistiza na ningependa kushauri kuwa kwa kuwa kifo hakina muda maalum ni vizuri kuandika wosia mapema hata kama bado wewe ni kijana, hii itasaidia kujua mali zako na mambo yako mengine yakaeje baada ya kifo chako. Kama unataka kufanya hivo na unakosa msaada tuwasiliane kupitia katerero73@gmail.com

    ReplyDelete
  51. Poleni ndugu zangu. Huyu LuLu sio mtoto ni mtu mzima ambaye amekwishaota sugu. Utoto unatoka wapi? huyu alikuwa ni mpenzi wake, mtoto mdogo kwa sheria zetu anaruhusiwa kuwa kahaba. Enyi madaktari mnaodai eti mmekwisha kamilisha uchunguzi, kweli kwa muda mfupi kama huo. Hata Ulaya kwenye vifaa ambavyo vinafanyakazi sawasawa na sio vya Mchina na kama vya kichina specification ni za EU. Hutumia muda. SASA NAANZA KUWA NA MASHAKA NA MADAKTARI WETU

    ReplyDelete
  52. Kila mtu kwa imani yake naombeni tumkumbuke kwa sala zetu Binti huyu. ni wakati mgumu kwake na tujue hakuna binadamu aliye msafi mbele za Mungu na sio wote waendao gerezani ni wahalifu kweli.

    ReplyDelete
  53. Dah, cjui vile mwaka jana binti ali celebrate birthday yake ya 18 years kwa mbwembwe zote!
    ghafla leo amerudi kuwa 17!
    mambo ya hivi yanaweza kuwafanya watu kuwa suspicious.
    under 18 driving a car? where are the authorities!

    ReplyDelete
  54. Wengi hapa wanasema Lulu, lulu, je ilikuwa halali kwa mwenzio kumchukua mtoto mdogo hivyo? Totally wrong, Wasanii wa Tz wakishapata hela mapenzi yanakuwa ni kama chakula kila kona anataka. Waone sasa wajifunze kuwa hela is good but when you belong to it the consequences are always bad. Make sure money is just money and control it never allow money to control you.

    ReplyDelete
  55. "
    1. Leseni ya kuendeshea gari amepewa na nani?
    2. Ucku mtoto anatoka kila wikenda mama yupo wapi?
    3. Kuna kesi ya kudanganya umri ili apate leseni kwa makusudi akijua wazi kua hilo ni kosa kisheria
    4. Angalieni kwenye mitandao hizo picha za huyo mnaesema ni mtoto
    5. Ameanza kwenda maDISKO mwaka gani?
    6. Nani alimtoa BIKIRA? Na alimtoa akiwa na umri gani? 7. Aliemtoa bikira anatakiwa akamatwe afunguliwe mashataka ya ubakaji 8. Tukija kwa wazazi, wanawezaje kumtegemea mtoto, hajasoma, hajaajiriwa? Katika umri mdogo, eti mtoto anajenga nyumba imefikia kwenye linta, ametoa muvi yake binafsi? Ameuza nakala ngapi? 9. Pesa amepata wapi? 10. Na hao wazee waliotembea na huyu mtoto wawekwe wazi ili iwe fundisho kwa jamii
    11. Wazazi wamevuna walichokipanda, mtoto ameish maisha ya kuiga! Wazazi wa lulu WAMEFELI kwenye MALEZI"

    ReplyDelete
  56. So sorry about present predicaments as i hope that you have to count seriously on God Almighty who can take out of this bondage and set you free.

    Pole Sana!

    ReplyDelete
  57. Wadau mmesema mengi, issue ni kumsaidia Lulu kisaikolojia. She is sick. Acheni ujinga wa kusema ni mtoto, kuna video ya party yake ya birthday ya miaka 18. Chonde chonde asifundishwe uongo wa kijinga, awe mkweli na Mungu atamsaidia. Lulu kwenye picha haoneshi kama anasikitika au kuwa ana mawazo kama walivyandika au ana uchungu wa kuua bila kukusudia au ataenda kulala segerea!! Ameweza hata kukumbuka kupaka wanja uliokolea wakati anepelekwa Mahakama ya kisutu. Ni mgonjwa huyo bint anahitaji msaada wa kisaikolojia! Wanaume wamemuharibu tangu akiwa na umri mdogo sana. Tumwombee kwa mwenyezi Mungu, awe na hofu ya Mungu na utu ambavyo hana kabisa. Angalia picha zake zote zinazotoka magazetini, always nusu uchi!!!

    ReplyDelete
  58. Sasa mbona yamekuwa mengine?
    Huyu anayesema kuwa huenda wenye nchi wamepanga haya mambo anamaanisha nini?
    Tunafaa tufikilie kabla ya kutoa maoni yetu mtandaoni. pia tujaribu kutumia kauli stahiki.

    Kila mtu anayo makosa yake, kuna na wengine ni zaidi ya wauaji lakini hawalitambui hilo. Hakuna aliyekuwepo tofauti na marehemu(Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake) a Lulu. Lulu huenda alikimbia kwa sababu ya hofu. hata kama ni wewe utakimbia!

    ReplyDelete
  59. Hi citizens! i am a girl of the same age as lulu so i guess i probably know what she feels ryt naw. I believe that she has learnt a lesson from this and surerly she will make a better life out of here so the society should give her a second chance for her to see her mistakes and correct them. I hope she knows wat she's supposed to do.

    ReplyDelete
  60. Mdau wa 55 kutoka juu mwenye Pointi 11 kuhusu malezi ametoa maoni yenye Faida kubwa kwa WAZAZI NA WALEZI WA WATOTO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...