NDUGU MICHUZI NAKUOMBA UNIWEKEE  HILI LIFUATALO KUSUDI WADAU WA BLOG YETU PENDWA  WAPATE KUNISHAURI. 

MIMI NIMEFANIKIWA KUPATA UFADHILI WA KWENDA KUSOMA NCHINI ITALIA SHAHADA YA KWANZA (FIRST DEGREE). NDUGU WADAU NI SOME MASOMO GANI HUKO ITALIA AMBAYO MITAALA YAKE INASHABIHIANA NA YA KWETU? {MFANO NILITAMANI SHERIA, WENGI WAKASEMA SISI HAPA TZ TUNATUMIA MFUMO WA KIINGEREZA AMBAO NI TOFAUTI NA WAKIITALIANO}. 

SHAHADA YA PILI  (MASTERS) NATEGEMEA KUSOMA HAPA NYUMBANI; SITOPENDA NITAKAPORUDI HAPA NIAMBIWE NIMESOMA KITU TOFAUTI NA HAPA.

WADAU NISAIDIENI MDOGO WENU KWANI NAKARIBIA KUONDOKA KUELEKEA HUKO.

MTANZANIA MWENZENU
DAR ES SALAAM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 54 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 15, 2012

    somea mapishi, yako sawa huko na hapa.

    form six mzima hujui kuangalia mbele.

    unafikiri hawa wabongo walioko italia wamesoma.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 15, 2012

    Acha uzushi kwani wakati unaomba ulipanga ukasome nini?Ungeomba ushauri kabla ya kuomba.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 15, 2012

    Hongera kwa kupata scholarship, huko Italy waweza soma journalism ambayo internationally misingi haitofautiani kuliko sheria itakusumbua kidogo. Fani ya journalism nchini bado inakua taratibu kwahyo hutotaabika sana kupata kazi. Kama chaguo lako moyoni ni sheria waweza isoma hapo baadae hata Tanzania kikubwa ni nia tu pia huwezi jua hao waliokupatai scholarship bdae unaweza kuwaomba scholarship ya masters ufanye media law. Kila lakheri

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 15, 2012

    Safi sana kwa kuwa na mwamko wa kusoma hasa nje ya nchi. Kiukweli sidhani kusoma sheria nje ya nchi ni vizuri, hapana kabisa. Sababu moja ni kwamba kama unataka kuja kufanya kazi Tz we tafuta chuo hapahapa nyumbani kwani kuna vyuo vingi vinatoa degree ya sheria. Ila unaweza soma mambo ya International Relations hata nje ya nchi na ukawin. Please usikimbilie nje kumbuka kuna TCU.

    Goodluck...

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 15, 2012

    Mdau hapo juu si amesema alitaka kusoma sheria ila amaembiwa itakula kwake akirudi nyumbani. Wewe ndo inaonyesha hujaenda shule unashindwa hata kusoma meseji na kuelewa. Mimi sina cha kukushauri mdogo wangu. Ngoja waje wadau wengine

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 15, 2012

    Ama bingo dogo, ufadhili bila kujua usomacho? Ngoja waitaliano waje wakushauri wengine born here die here...

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 15, 2012

    kijana hujasema a-level ulisomea masomo gani. jee ulisomea sayansi? au sanaa? masomo yako ya a-level ndio yatakayoamua ni kozi gani uchukue. lkn nachukulia umesomea sayansi na hivyo kukushauri kama ifuatavyo:

    soma uhasibu ndugu. dunia nzima uhasibu upo sawa hakuna cha italy wala marekani wala uingereza. masuala ya kifedha ni sawa tu.

    pia unaweza kusomea udaktari ambao pia dunia nzima ni sawa bila ya kujali nchi na nchi.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 15, 2012

    Hiyo University unayokwenda wanaoffer masomo gani kwanza? Somea Human Resource ambayo itakupa uwezo wakujiendeleza kusomea Masters ya sheria baadaye.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 15, 2012

    soma technology iwe coz yeyote ya Tech.

    ReplyDelete
  10. Ewe Kijana kasome pale Tursia University, Viterbo. Ukisomea hapa Engeniere (Engineering) au Forestale miaka Minne unapewa Degree ya Udokta au Dr. Italy Economia husomewa kwa Kiingerezakwa mfumo wa UK nayo poa. Kwa mtanao wa sasa utakubalika kufanya kazi za Kimataifa au hukohuko kama Dr. Tanzania ukirudi wameze wateme utakubalika kwenye Ma NGOS nk. Ciao e Auguri. Richardo Mazingira

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 15, 2012

    mmmmh we umemaliza f6 kweli? hujui whats happening now? then hujasema una combination gani ya masomo,kasome wildife management haina tofauti dunia nzima

    ReplyDelete
  12. soma udakitari. utapeta sana sana popote pale!!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 15, 2012

    wewe shule ni interest yako, ukiambiwa ufanye Engineering utaweza!! unasomea kitu ambacho una interest nacho na unaweza kuperfom vizuri, sio unauliza nisome nini. Naanza kuwa na wasiwasi na hata hiyo form six yako, maana mtu na akili zake hawezi uliza swali kama hilo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 15, 2012

    Kasomee ubunge au uwaziri, na make sure with specialsation of Tanzania. Ukirude utakuwa tajiri kabisa maana utakula hii nchi, kama kutakuwa kumebaki kitu cha kula!!! Nakutakia kila la heri.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 15, 2012

    Kasome Engineering au medicine uje usaidie nchi,wanasheria tunao wengi wa kutosha

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 15, 2012

    Nafikiri ni vizuri ukaenda kusomea INTERNATIONAL LAW. ni nzuri sana, coz itapanua upatikanaji wa ajira kwako. ukiwa na hiyo nahisi unaweza kufanya kazi sehemu yoyote ile duniani. Good luck!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 15, 2012

    kajifunze namna ya kuishi Tanzania au kuendesha taxi ughaibuni au kufagia vyoo

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 15, 2012

    Nafikiri ni vizuri ukaenda lusome INTERNATIONAL LAW. coz itapanua upatikanaji wa ajira kwako baadaye, ukiwa na iyo nahc unaweza kupata/kufanya kazi sehemu yoyote ile duniani. Good luck!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 15, 2012

    Mfadhili gani huyo yuko tayari kutoa hela yake bila kujua unaenda kusomea nini!? Angalia kama ni ufadhili wa kujuana through intrenet utapigwa changa la macho! Kama ni mzazi kwa nini asikupeleke nchi nyingine zaidi ya Italia!

    Kukushauri ni ngumu maana hatujui a-level umesomea nini! lakini pia wewe interest yako ni nini?

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 15, 2012

    Wewe ulivyoomba sponsership hukujua unaenda kusomea nini?

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 15, 2012

    Kwa ushauri wangu ni bora ungesomea hapo hapo nyumbani bongo kuliko kukimbilia huku. Italy ni ubabaishaji mtupu na jamaa ni wasanii ile mbaya. Huku ni kiitaliano kila kona. Maprofesa hawajui kiingereza ni zero kabisa halafu jamaa ni wabaguzi sana wanaona hii ngozi nyeusi haijui kitu kwa hiyo hapo pia ni shughuli nyingine. Kwa hiyo ndugu kama uko serious unataka kusoma shule ya uhakika bora au usome hapo hapo bongo au upate shule nyingine Nothern Europe kuliko hapa Italy. Ni ushauri wangu tu maana na mimi niko huku joto ya jiwe naipata. Usifikiri nakukatisha tamaa ila nakupa hali halisi ili ufanye informed decision. Halafu kama una ndoto za kuja huku na kufanya hiyo usahau kabisa maana kazi hazipatikani kwa urahisi na kama zipo priority ni kwa weupe wenzao. Hii ni tofauti na Northern Europe ambapo kazi zipo nje nje. Kwa hiyo usishangae unakuja huku unasoma unamaliza unnarudi bila chochote mfukoni. Kila la heri.

    ReplyDelete
  22. Consult TCU you will get what you need and will give you a variety of choices for more help TCU offices are located near Rose Garden Mikocheni.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 15, 2012

    Wewe Mtanzania vipi bwana..Weka unachofikiria kwenda kusoma halafu uliza kama kinashabihiana na ya kwetu....lakini umeficha..Kama unatutega vile?.Ni Kushabihiana au kutambulika na vyuo vikuu vyetu?Kila la kheri.

    David V

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 15, 2012

    Mdau usihangaike bureeee,

    Italia ndio Makao Makuu ya Ukatoliki, pia kulingana na mabadiliko ya kimaisha Sekta tatu (3) hizi, yaani Michezo, Siasa na Dini ndio SACCOS za kisasa hivyo usipoteze muda kufikiri Engineering, Business,Management, Law na mengine, kwanza inaonyesha Udhamini huo umepewa na Kanisa sasa unataka kuwageuka mapema(Dunia imefilisika ni vigumu kwa zama hizi kupata Sponsor) kwa namna ulivyopata wewe hata aina ya Masomo usijue?.

    Italia nenda kasomee DINI YA KIKRISTO ili UPIGE BAO!

    ReplyDelete
  25. Nenda ofisi za TCU kwamsaada zaidi, ndio pekee wanaoweza kukupa muongozo mzuri ahsante.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 15, 2012

    Ungeuliza mapema ningekwambia kwamba fanya bachelor nyumbani halafu ndo uende kwa masters na PhD nje. Huwa si vizuri sana kuanzia bachelor nje ukaja kufanya master TZ utakuwa frustrated na system ya elimu ya juu ya Bongo. Pia hujasema ni masomo gani ulifanya A-level. Pengine ungesema baadhi ya kozi unazotaka ukiondoa hiyo sheria ili ushauriwe kirahisi.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 15, 2012

    Somea photo editing

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 15, 2012

    NENDA TU KAKA KITAELEWEKA HUKO HUKO.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 15, 2012

    somea umafia. ukirudi ukachanganya na ufisadi degree ya pili utatisha mwanangu

    ReplyDelete
  30. soma engineering like electrical, n.k kwa experience yangu ukimaliza vizuri unaweza pata ajira popote i.e duniani

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 15, 2012

    Kasomee ukocha wa mpira wa miguu

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 15, 2012

    acha ushamba wewe!! umepataje scholarship hata hujitambui!! ndio mambo ya kuletewa driving licence kama zawadi ya birthday.unatakiwa kujitambua unataka uwe nani ufanye nn ndo uamue usome nn. umemuabisha sana hata aliekupa scholarship

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 15, 2012

    Ndugu yangu sijui ni ipi nikupe kwanza pole au hongera. Hongera kwa kupata ufadhili wa kusoma nje ya nchi, pole kwa kuwa hadi umemaliza form six hujui ni aina gani ya kazi ungelipenda kufanya/kusomea. Nashangazwa kuwa kuna mtu au kampuni imeweza kukupa ufadhili bila ya hata kujua ni fani gani ya masomo unataka kuchukua, au wewe ni moja katika watoto wa vigogo?

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 15, 2012

    Somea udaktari.

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 15, 2012

    Mambo vipi?
    mimi ningeweza kukushauri, kwanza kabla ya kukushauri naomba nikuulize ulisoma masomo gani A-level? na pia nisingekushauri ukasome sheria as ulivyosema sisi tuko tofauti sheria yetu na hao Italy.
    Pia ningekushauri kama ulisoma hesabu fanya accounting, finance, management au economics
    au computer science au IT.
    kama ulisoma Arts A-level,
    Kuna environment field, its a coming field now all over the world and its very good, geology pia its good.
    Napia kama ulisoma science kafanye science na usome chemistry, physics etc.engineering we need this people in TZ a lot.
    Good luck.
    Good luck.

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 15, 2012

    Kasomee fani unayoimudu, then think beyond the nation borders. Si lazima ufanye kazi Tanzania. Nenda ukajenge skills zitakazokuwezesha kucompete internationally. Think of East Africa Community and beyond that! Kama hapa Tz watasema haimatch and so & so...bac skills zako zikuwezeshe kefanya kazi zako Sudan, Uganda, Zambia n.k. Nakutakia masomo mema

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 15, 2012

    mtoa maoni wa kwanza , wewe kiboko, nakupa 5 bila kupigwa . Yaani huyu jamaa bogasi kichizi, sijui na huyo aliyemlipia nauli kwenda Italia, hiyo pesa bora angelikaa kwa macheni akanywa bia. yaani watu kama hawa na vicheti vyao ndo wanaoshika madaraka hapa bongo ,na kutuvurundia kila wizara wanakopelekwa, hata hayo mapishi !!!! mmmm!!! sidhani asije akaua watu huko Kebbys hotel. Mimi naona abaki tu bongo au akienda basi asirudi. Zebedayo mna Nasa.

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 15, 2012

    Hivi kweli mpaka sasa hivi huna muelekeo wa maisha tu? Yaani inamaanisha mpaka sasa hujui unataka nini hii ni aibu kubwa sana mpaka unaanza chuo huna muelekeo. Usisome unachoambiwa na jua wewe unataka nini. Sasa Kama ukipokea ushauri zaidi ya tano si ndio tutakuchanganya kabisa. Acha hizo wewe hata ukipewa uongozi wa taifa utalipeleka kijingajinga hivyohivyo

    ReplyDelete
  39. Watu wengine bwana mwenzenu kaomba mssada mnatukana..
    Technology ni sawa kote Duniani
    IT, Computer, Engineering, Economics, Finance etc

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 15, 2012

    Ningekushauri kama unapenda lugha usomee communication aidha international communications au international relations. Itakusaidia hata utakapo tafuta stashahada ya pili kupata mambo ya relations au hiyo hiyo communications au ukiona vyote haviko sawa malizia na HR (Human Resources).Angalia mbali utaweza jikuta unachukuliwa hata na UN ukimaliza masomo kama hayo,au hata mashirika makubwa au ya kimarekani au italia hasa kwamba utakuwa umesoma kwao...Mdau

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 15, 2012

    Degree ya law ambayo inajulikana kama LLM ninadhani kua ni moja dunian kwa maana ukisoma sheria popote basi umesoma sheria kitu labda cha kuwa na wasiwasi ni lugha inayotumiwa ktk masomo. I think if language problem is solved you shoul be fin, giv it try. thanks

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 15, 2012

    Dunia imegawanyika kwa fani kulingana na Taifa husika,

    Mifano ya nchi chache ikiwemo Italia unazoweza pata taaluma ikakusaidia ukiwa hapa Tanzania ukirudi:

    1.Italia:-
    Somea kati ya fani hizi:
    -Udobi (kufua na kupiga pasi)
    -Ukinyozi
    -Uhudumu wa Baa au Migahawa
    -Uchomaji wa Pizza (aina ya Chapati)
    -Unenguaji ktk Klabu za Srarehe za Usiku (Kazi ambayo hata Waziri Mkuu Mstaafu wa Italia Bilionea Silvio Berlusconi aliwahi kuifanya kabla ya kupata Fedha, Madaraka na Umaarufu, tena yeye alifanya ktk Meli za Kifahari za Watalii matajiri)

    2.Ujerumani:-
    Somea kati ya fani hizi:
    -Ufinyanzi (Hii ukiwa hodari itakupelekea hadi kuwa mbunifu ktk Viwanda vikubwa vya Mitambo na Magari kama Mecredes Benz,Audi,Opel,BMW n.k
    -Uchoraji na Sanaa
    -Ufundi wa mashine ndogondogo na matengenezo (micro mechanics)

    3.Uholanzi:-
    Somea kati ya fani hizi:
    -Ukulima wa mbogamboga na matunda
    -Biashara ndogo ndogo (kama Magenge)
    -Usindikaji wa vyakula
    -Utayarishaji wa Maziwa ya ng'ombe na mazao yake, Siagi,Jibini n.k

    Ila kwa baadhi ya taaluma hapo ktk nchi hizo (3) utaona kama ninakubeza isipokuwa hiyo ni kweli.

    Kazi kwako !

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 15, 2012

    Hiyo "scholarship" uliipataje au ndio undugu?

    Nenda kasomee theolojia inalipa, uje kugombea urais na wewe

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 15, 2012

    Ahhh,

    Wewe nenda kalitumike Kanisa tu!

    Angalieni huyu jamaa, unapewa Udhamini kwa Masomo ya Dini unataka kuchomoka usomee mambo ya Kimaslahi sio?

    Kila kitu kinaonyesha ya kuwa hiyo Sponsorship ni ya Kanisa,(Kwa sasa ni nadra sana mtu ukapata Udhamini kwa Mazingira haya labda uwe GENIUS (mwenye akili za ziada),au BABA YAKO AWE NI TAJIRI PIA),,,MARA NYINGI UDHAMINI WA AINA HII UNALENGA WATU WA TAALUMA YA DINI SIO TAALUMA ZA KIMASLAHI,,,sasa wewe huku pembeni unawatoka Maaskofu na Mapadri unataka kuchagua Kozi ya Fedha!

    Ohoooo acha hizo!

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 15, 2012

    Mpendwa mchangiaji wa kwanza unadhani usingechangia kungeharibika neno? Siyo kwamba hawezi bali ninadhani anahitaji kupewa mwelekeo na ndo maana kaomba kusaidiwa kumamanua hili.

    Kama umeshapata udahiri, jaribu kutembelea website ya chuo husika uchagua degree programme uipendayo au uwezayo kuimudu vizuri zaidi.

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 15, 2012

    Engineering
    Biashara
    Mimi naona ukisoma masomo ya sayansi au biashara yanakubalika kila mahali.

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 15, 2012

    Ungetuambia umesoma "combination" gani tungekuwa katika nafasi nzuri ya kukushauri.Kama umesoma sayansi ni vizuri ukasoma course za engineering(zipo nyingi),Geomatics(surveying)au zinazohusiana na afya kama umefanya PCM,PGM,PCB au CBG kwa sbabu zote zipo world wide.Kama umesoma arts ni bora ukasoma mambo ya utawala au internatinal relations kwa sababu hizo huwa zinashabihiana nchi zote.Sheria utaingia chaka manake sidhani kama mitaala ya Italy inafanana na hapa kwetu

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 15, 2012

    Mdau,
    Ushauri wangu ni kama ifuatavyo: Shahada ya kwanza inahitaji uwe na background ya masomo fulani ili ufanye vyema. Kwa mfano, shahada ya kwanza ya Uhandisi(Engineering) inahitaji umesoma A-level(Physics, Chemistry na Maths) au shahada ya Social science pengine itahitaji umesomea history, lugha au geography ili uweze kufanya vyema. Kwahiyo ni muhimu ujue umesomea A-level kitu gani ndipo uendeleze hiyo field shahada ya kwanza ama sivyo masomo yatakuwa magumu kwako.
    Pili, ni muhimu ujue job market ya Tanzania inahitaji zaidi taaluma gani kwa sasa? Je wahandisi, Quantity Surveyors, Architects au Marketers n.k ili ukimaliza upate kazi kwa wepesi.
    Haya mawili ni muhimu kuzingatia.

    ReplyDelete
  49. Brightony TumainiMay 15, 2012

    Kwanza ningependa kufahamu mtu uyo kasomea masomo gani A-level.Kama ni Arts ni vyema akasomea mambo ya International Relatioship(IR).Nahisi ni course itakayomfaa.Na kama amesoma science,basi ni vyema akisoma mambo ya ICT,atakubalika

    ReplyDelete
  50. ungesema umesomea mambo gani huko labda mtu angepata picha akushauri nini...specify hiyo degree ya nini unakaribia kuipata...

    ReplyDelete
  51. AnonymousMay 16, 2012

    kuhusu sheria sikushauri kila nchi wanamfumo wao kama mimi nasoma uingereza nafanya business ila kunakitengo cha law as subject nimesoma ambapo tunafuata sheria za uk , waweza fanya business, science na vinginevyo

    ReplyDelete
  52. Huu ni mfano halisi ya watanzania wengi. Jitu linafika hatua ya kusoma chuo halijajua linataka kufanya nini huku duniani. Badala yake litakurupuka na kitu halafu likiirudi linabaki misifa ya kusoma italy tu huku haliwezi fanya chochote. Watanzania bwanaa!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 16, 2012

    Jim, hilo ni tatizo la mfumo wa nchi yetu. Na tunawaza kuajiriwa zaidi. Ndo maana watu wanakimbia taalama zao na kukimbilia kwenye siasa!

    ReplyDelete
  54. kapige book kaka hao wasikuzingue.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...