Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo akizungumza machache wakati wa maadhimisho hayo ambapo pia alisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon kuwa leo tunatoa heshima kwa Walinda Amani zaidi ya 2900 ambao wamepoteza maisha wakiwa kazini katika miaka iliyopita na kuahidi kuendeleza kazi yo kurejesha Amani katika nchi zenye vita.
Amesema katika siku hii ya Umoja wa Mataifa ya Walinda Amani tuitumie kukumbuka jinsi watu walivyojitolea maisha yao, na tuahidi kuimarisha ushirikiano wa kidunia ambao unawafanya hawa wavaa kofia za Bluu waonekane kama alama ya Amani duniani kote.
Mgeni rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya Siku ya Walinda Amani Duniani 2012 ambapo amesema Kauli mbiu ya Mwaka huu imelenga kuunganisha majeshi yote ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha bara la Afrika linakuwa na Amani na Utulivu.
Mgeni rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa.
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa. 

kwa picha zaidi 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...