WAREMBO wanaotaka kushindana katika shindano dogo la kumsaka mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Dunia (Miss World 2012) wameombwa kuendelea kuchukua fomu za kushindana katika kinyang’anyiro hicho na kuzirudisha kabla ya Juni 4.

Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga amesema kuwa wanatarajia kufanya mchujo wa washiriki Juni 5 kwa ajili ya kubakiza warembo 10 kwa ajili ya kuwania nafasi ya kushiriki katika mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika Agosti 18 kwenye ukumbi wa Dongsheng Fitness Center Stadium, mjini Ordos, Inner Mongolia, China.

Lundenga alisema kuwa zoezi hilo lilisimamishwa kutokana na zuio la Serikali na wakati huo, jumla ya warembo 12 walikuwa wamekwisha chukua fomu za kushiriki. Alisema kuwa muda wa kufanya mashindano hayo umekaribia na wanatarajia kuitangaza tarehe mpya hivi karibuni.

Alisema kuwa amefurahishwa na kasi ya kuchukua na kurejesha fomu, hata hivyo wanahitaji warembo wengi zaidi ili kuweza kupata wigo mpana kwa ajili ya kumsaka mrembo atakayewania taji la Dunia ambalo kwa sasa lina mikononi mwa mrembo kutoka Venezuela, Ivian Sarcos.

“Tunakaribia kufanya mashindano madogo hivi karibuni, hivyo ni wajibu wetu kuwakumbusha warembo wanaotaka kuwania taji hilo kufanya hivyo kabla ya Juni 4 ili kuweza kuingia katika zoezi la mchujo,” alisema Lundenga.

Alisema kuwa mpaka sasa jumla ya nchi 84 zimekwisha pata wawakilishi wao kwa ajili ya mashindano hayo. Nchi 32 pamoja na Tanzania bado hazija chagua wawakilishi wao katika mashindano hayo.

Fomu za kuomba kushiriki zinapatikana katika ofisi za Miss Tanzania za jijini na mawakala wote wa mashindano hayo katika mikoa ya Tanzania Bara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2012

    MH!!!!ATI NI KWELI HUYU NI MZEE WA KUONJA?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...